NA ALBERT G SENGO/MWANZA
Wajumbe wa halmashauri shauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa kutoka Mkoa wa Mwanza Mh.Dkt Angelina Mabuba na Hellen Bogohe wamesema kuwa wapo tayari kwa mikutano ya hadhara ambayo imeridhiwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hivi karibuni. Wajumbe hao wametoa kauli hiyo wakati wa mapokezi yao Mkoani Mwanza ambapo wakisema kuwa wapo tayari kuzinadi kazi nzuri zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na Rais wa awamu ya sita Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ilichukuwa dakika kadhaa Jiji la Mwanza kusimama kutokana na Wajumbe hao kupata mapokezi ya kishindo yaliyo ambatana na maandamano ya msafara wa magari na watembeao kwa miguu kuanzia viwanja vya Furahisha hadi makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi yaliyopo katikati ya jiji hilo.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.