Saturday, April 25, 2015
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI WA UANDISHI WA HABARI (EJAT) JIJINI DAR ES SALAAM.
MIKOA MITANO KUSHIRIKI DARTS TAIFA.
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakipasha kabla ya kuanza kwa mashindano hayo yaliyofunguliwa jana Moshi Hoteli Manzese jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakipasha kabla ya kuanza kwa mashindano hayo yaliyofunguliwa jana Moshi Hoteli Manzese jijini Dar es Salaam. |
Washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayo fanyika Moshi Hotel Manzese jijini Dar es Salaam. |
Washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayo fanyika Moshi Hotel Manzese jijini Dar es Salaam. |
Na Mwandishi Wetu.
MASHINDANO ya mchezo wa Darts Taifa yamezinduliwa jana jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Moshi iliyopo Manzese kwa kushirikisha mikoa mitano ya Tanzania.
Akizindua mashindano hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya kinondoni, Selestine Onditi ”kwanza aliwapongeza viongozi wa chama hicho kwa juhudi za pekee za kufanya mashindano hayo yafanyike kwa mwaka wa 2015,lakini zaidi aliwashukuru wachezaji kwa moyo wa kupenda mchezo kujigarimia kuacha kazi zao kutoka mikoani ikiwa pamoja na wenyeji Dar es Salaam kuja kushiriki mashindano hayo ya Taifa kwa kujilipia gharama zote za ushiriki hiyo inatia moyo sana kuwa ni dhahiri mnaopenda mchezo”.
Alisema Onditi michezo ni afya,michezo ni furaha na michezo ni kufahamiana basi aliwataka washiriki wote watumie nafasi hii ya kukutana katika kuyafanikisha haya yote.
Onditi alitoa wito kwa wafadhili kuwa wasiegemee kwenye mpira wa miguu tu kuna michezo mingi kama Darts na mingine wajitokeze wadhamini kwani kwa kutumia wapenda michezo kama hawa waliojitolea kutoka mikoani kwa gharama zao kuja kushiriki mashindano ya Taifa ni nafasi ya pekee wewe mfanyabishara kutangaza biashara yako.
Mwisho aliwatakia mashiondano mema yenye amani kuwa waanze salama na wamalize salama na mwisho warejee majumbani salama salimini.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama alizitaja zawadi kuwa ni Vikombe na Pesa taslimu kwa mfumo wa mashindano utakaotumika ni wa Singles(mmoja mmoja),
Doubles(wawili wawili) na Timu.
Mwisho Katibu wa Chama cha Darts Taifa, Kalley Mgonja aliitaja mikoa iliyofanikiwa kufika jijini Dar es Salaam kwa ushiriki wa mashindano ya Taifa kuwa ni Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha na wenyeji Dar es Salaam.
Friday, April 24, 2015
DROO UEFA:BARCELONA KUCHUANA NA BAYERN MUNICH
Klabu ya Barcelona Itakutana na mabingwa wa kombe la kilabu bingwa Ulaya Bayern Munchen katika nusu fainali ya kwanza ya kombe hilo.
Nusu fainali ya pili itazikutanisha timu za Real madrid dhidi ya Juventus ikiwa ni mkutano wa kwanza kati ya klabu hizo mbili tangu mwaka 2003.
Nusu fainali hizo zitachezwa tarehe tano na sita ya mwezi Mei huku mechi ya marudio ikichezwa wiki moja baadaye.
katika ligi ya Yuropa,mabingwa watetezi Seville kutoka Uhispania watakabiliana na Fiorentina huku Napoli wakikabiliana na Dnipro kutoka Ukraine.
NAPE AMVUTA SHATI DK SILAA
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Taifa, kimesema kwamba hakijachelewa mchakato wa kumtoa na kumtangaza mgombea wake wa Urais kutokana na kuwa na muda wa kutosha wa kufanyakazi hiyo.
Pia kimemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demkorasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrlod Silaa, kuacha kuwapotosha watanzania juu ya zoezi la uwandikishaji wa daftari la kudumu litakalotumika na Tume ya Uchaguzi (NEC) katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu ni vyma “Babu” huyo ameanza kuchoka hata kufikiri ni vyema akapumzika siasa.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika uwanja wa ndege wa Mwanza, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM taifa, Nape Nnauye, alisema kwamba kuanzia mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 Chama hakikuwahi wala kuchelewa, kiliweza kumpata mgombea ndani ya wakati na muda sahihi na atapimwa na watanzania kabla ya kumchagua.
“Ni kweli kumekuwa na presha kwa watu wengi ambao wamekuwa wakisema hivyo kuwa tumechelewa kufanya mchakato na kumtangaza mapema mgombea wao, tunacho wahahidi watanzania kuwa hatutachelewa na tutawaletea mgombea ambaye akitangazwa na CCM pale Mjini Dodoma ndiye Rais wa awamu ya tano hivyo wavute subila muda si mrefu vikao vitafanya kazi hiyo,”alisisitiza.
Nnauye alisema kwamba Dk. Silaa hana budi kujitazama upya juu ya mwenendo na matamko yake na kuiachia jukumu la uandikishaji wa daftari la kudumu NEC kwani tume hiyo ni9 huru kufanya kazi yake hiyo , ikiwemo kuanzia mikoa yoyote ya Tanzania ambayo itaona inafaa kutokana na ratiba iliyojiwekea bila kufuata kupangiwa na vyama vya siasa ikiwemo CCM.
“Kabla ya tume kuanza zoezi hilo vyama vyote vya siasa vilikaa na tume na kuelezwa kuanza kwa zoezi hilo na halikuwaeleza kuanzia mikoa ipi, bali vyama viliomba kila raia mwenye sifa ni vyema akaandikishwa katika daftari hilo, sasa inashangazwa na kauli za Dk Silaa kuanza kuilaumu na kuingilia kazi za tume,”alisema.
Katibu huyo alisema kwamba kutokana na wingi wa vijana waliishauri tume kuweka utaratibu mzuri ili vijana wengi wajiandikishe na kuhakikisha inaondosha mizengwe ya kutowapa nafasi katika zoezi linaloendelea katika mikoa ya Rukwa, Njombe na Iringa.
“Kwenye hili CCM tulisema hakuna njia ya mkato watu wote waandikishwe na katika daftari hilo ili kuwawezesha kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu na huo si msimamo wa CCM tu bali vyama vyote vya siasa viliomba kwa NEC, sasa inashangazwa kauli za Dk. Silaa kuwa tume imeanzia zoezi hilo kwenye mikoa ambayo ni ngome yake ili kuudhoofishwa upinzani, si kweli huko ni kuweweseka,”alisema.
Nnauye alisema kuwa CCM haiku kuipangia tume utaratibu na kuingilia zoezi hilo na badala yake inawasisitiza wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari hilo la kudumu na hakuna njia ya mkato juu ya kujiandikisha, ni vyema pia watanzania wakaepuka poropoganda za viongozi wa kisiasa wanazotumia kuwahadaa.
Aliongeza kuwa Dk. Silaa awaeleze ukweli watanzania juu ya kukaa kwao yeye, Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na wengine wanaotoka mikoa ya Kaskazini na kuwatenga Mwenyekiti wa CUF, Porfesa Haruna Lipumba na Mwenyekiti wa NRD, Emanueli Makaidi walio kwenye muungano wa Ukawa.
“Waache kuwachochea wananchi na kuwahadaa, CCM itawashinda tu, hivyo ni vyema wakaaacha kuwagawa watanzania kwa uroho wa madaraka wanachotakiwa kujua ni nini watanzania wanataka kupitia sera za vyama vyao na kuacha kuwajaza hasira wananchi kwa madai ya NEC kupendelea maeneo fulani hii si sawa, badala pia kuwajengea hofu,”lisisitiza.
Nnauye pia amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu na vyombo vya vingine vya Ulinzi na Usalama kuvishughulikia vyama vya siasa vinavyoanzisha vikundi kwa kutumia vijana kwa ulaghai wa kuanzisha vikundi hivyo kwa lengo la kujilinda, kwamba CCM inaendelea kurahani vyama vinavyoanzisha vikundi hivyo na vya kiharakati vinalengo la kufanya ugaidi na fujo ni vyema vikadhibitiwa mapema kabla ya kuleta machafuko.
“Isifananishwe Chipukizi na Green Gard wa Chama hicho na vikundi vyao vya kigaidi kwani CCM inao utaratibu mzuri na unaokubalika kwa kuwalea vijana wakiwa wadogo na kuwatumia katika haraiki na gwalidea kwenye sherehe zake na ieleweke kuwa haiandai vikundi vya kupambana na kujilinda kwani kazi hiyo itafanywa na vyombo vya ulinzi na usalama,”alisisitiza.
Kuhusu CCM kukisaidia Chama cha ACT Wazalendo, Katibu huyo aling’aka na kusema kwamba Chama hicho kisihusishwe na migogoro na uchu wa madaraka katika vyama vya upinzani vinavyofarakana wakati huu, lakini pia viache kutumia mbinu ya kujimaliza kwa kutumia mgongo wa Chama kilichopewa dhamana na watanzania kuongoza nchi.
“Wasituhusishe na siasa zao ambazo karibu vyama vyote vya siasa vilivyo kwenye muungano wa Ukawa na vilivyo kwenye usajili, kugombana na kufukuzana kutokana na uchu wa madaraka hivyo ni vyema pia watanzania wakavipima na mwisho kuvinyima kura kwa kuwa haviko tayari kuwatumikia zaidi ya viongozi wake walio wengi kusaka tonge tu,”alisisitiza.
Wito wangu kwa watanzania tudumishe muungano na umoja wa taifa letu bila kubaguana kwa Itkadi zetu za vyama vya siasa na tuhakikishe kila mtanzania awe ni mlinzi, kuwa na taifa lenye machafuko ni kuwafanya watu wawe wakimbizi kudadumaza ustawi wa taifa chini ya mfumo wa vyama vingi na wanaotaka kuwagawa kwa manufaa ya kupata madaraka tusiwaunge mkono kamwe.
Thursday, April 23, 2015
BASATA WAMPONGEZA MAYUNGA KWA KUWAKILISHA VYEMA TANZANIA.
BASATA wampongeza Mayunga kwa kuwakilisha vyema Tanzania
· Kufatia ushindi wake katika mashindano ya Airtel Trace Africa
Baraza la sanaa Tanzania BASATA leo limempongeza mwakiliwa wa Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace kufatia ushindi alioupata katika mashindano ya muziki yaliyoshirikisha washiriki 13 toka nchi za Afrika .
Mwisho mwa mwezi wa tatu BASATA ilimkabidh bendera Mayunga na kumpa kibali cha kwenda kushiriki mashindano hayo yaliyokuwa yanafanyika nchini Kenya na kumtakia kila laheri katika mashindano hayo ambapo mwakilishi huyu aliweza kufanya vizuri na kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Star wa Afrika
Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua katika halfa fupi ya pongezi kwa Nalimi Mayunga katika ofisi za BASATA alisema” Ushindi huu ni furaha kubwa kwetu sisi Baraza la Sanaa la Tanzania kwani tunayo dhamana ya kuhakikisha tunaendeleza sanaa nchini kwa tunashirikiana na wadau mbalimbali nchini katika kuwawezesha vijana wenye vipaji kukuza sanaa zao ndani na nje ya nchi.
Nachukua fulsa hii kwa niaba ya BASATA kumpongeza Mwakilishi wetu Nalimi Mayunga kwa kufanya vizuri na kushinda mashindano haya.
Nawashukuru sana Airtel kwa kufata taratibu stahiki na kushirikisha BASATA tangu mashindano haya yaanze ikiwa ni kusajili kampuni yao na kupata hati ya kufanya shughuli za sanaa na pia kutushirikisha katika mchakato mzima wa mashindano haya na kumleta mshindi huyu kuchukua hati maalumu ya kusafiri na kuagwa rasmi wakati wa kuondoka kwenda kwenye mashindano ya Afrika. Kwakweli huu ni mfano wa kuigwa na wadau wengi na wasanii kwa ujumla, kufata taratibu na kupata vibali maalumu pindi wanapoenda nje ya nchi kufanya shughuli za sanaa na kuwakilsisha nchi yetu.
Natoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi pindi awamu ya msimu wa pili wa mashindano haya ya Airtel Trace yatakapotangazwa ili nao waweze kupata nafasi ya kushiriki na kuinua vipaji vyao. Aliongea Shalua
Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando alisema Tunawashukuru watanzania wote walioshiriki katika shindano hili tangu tulipolizindua. tunampongeza sana mayunga kwa ushindi huu. Nalimi Mayunga ameweza kujishindia dili la kwenda marekani na kupata mafunzo chini ya usimamizi wa Akon,na pia kuweza kurekodi wimbo na video yake ya kwanza vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekai 500,000/= Tunategemea baada ya mafunzo hayo na kutoa wimbo wake na Akon basi mayunga ataendelea kufanya vizuri na hatimae kuweza kuzifikia ndoto zake.
Airtel ilimkabithi Mayunga zawadi ya shilingi million 50 za kitanzania kufatia ushindi wake hapa nchini na sasa anajiandaa kwenda marekani na kufanya kazi na msaani nguli Akon.
Akiongelea ushindi wake Mayunga alisema, nawashukuru sana watanzania kwa kunipigia kura toka mashindano haya yaanze, najisikia furaha kupata nafasi hii ya pekee na naamini safari yangu nchini marekani itakuwa ya mafanikio makubwa na mwanzo wa mafanikio katika kuzifika ndoto zangu za kuwa mwanamuziki nyota ndani na nje ya nchi.
Nawashukuru Airtel kwa kuanzisha mashindano haya na BASATA kwa kunipa ushirikiano wakati wote wa mashindano. Natoa wito kwa watanzania na vijana wenzangu kuchangamkia fulsa hii pindi msimu wa pili wa mashindano haya yatakapotangazwa na kuanza .
Mashindano ya Afrika yalimalizika kwa mtanzania kushika nafasi ya kwanza , Nigeria nafasi ya pili na Congo Brazavile nafasi ya tatu.
Wednesday, April 22, 2015
KIMENUKA TOTO AFRICANS WANACHAMA WACHACHAMAA.
BAADHI ya wanachama wa Toto Africans ya jijini Mwanza wameorodhesha majina na kuweka saini wakiambatanisha na barua na kuupelekea uongozi wa klabu hiyo wakimtaka Mwenyekiti kwa kushirikiana na kamati ya utendaji waitishe mkutano mkuu wa dharula ufanyike tarehe 3/05/2015 kujadili masuala ya msingi yanayoitatiza klabu hiyo.
Ajenda zinazotajwa ndani ya barua hiyo ni pamoja na Taaarifa ya fedha msimu wa ligi hatua ya pili ya ligi msimu 2013-2014 na msimu wa 2014-2015.
Mkataba wa kisheria na mdhamini (Nsejjere)
Kujiuzuru kwa viongozi muhimu wa Klabu (Mwenyekiti na wajumbe wawili)
Ukiukwaji wa Mamlaka ya Utendaji na kupelekea uvunjwaji wa katiba ya Toto African, pia sekretarieti kushindwa kusimamia majukumu yao kwa kipindi chote.
Mpango mkakati wa ushiriki ligi kuu pamoja na kuunda kamati za kufanikisha malengo ya ushiriki na kadhalika. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA ALICHOSEMA MMOJA WA WANACHAMA MWASILISHA BARUA.
TUCTA YAHAMASISHA UCHAGUZI MKUU
Moja ya picha ya uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura. |
NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza
WAFANYAKAZI wa umma na sekta binafsi jijini Mwanza wameshauriwa kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la wapigakura ili waweze kuwachagua viongozi bora katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Chama cha Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Yusuph Simbaulanga, alisema kura ni nyenzo muhimu inayoweza kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima yanayoweza kujitokeza baada ya uchaguzi.
“Idadi ya watu wanaojiandikisha imeongezeka, hivyo kwa fursa hii ni vyema pia wafanyakazi kujiandikisha kwa wingi kwani wengi ni vijana wanaofanya kazi katika sekta binafsi na za umma,” alisema Simbaulanga.
Aidha, alisema kujiandikisha kwa wafanyakazi kutawafanya kuoana thamani ya kura zao katika kufanya uamuzi sahihi wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
“Kupitia sanduku la kura mfanyakazi ataweza kujikomboa kwa kuchagua viongozi watakaoleta tija kwenye utendaji, lakini pia kuboresha maslahi yao,” aliongeza Simbaulanga.
Alitumia nafasi hiyo pia kuwahimiza wafanyakazi kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka huu itakayofanyika kitaifa jijini Mwanza ili kushiriki pia kupima afya zao kuhusu magonjwa ya kisukari, shinikizo la damu na ukimwi, ambapo wataalamu wa afya watatoa vipimo hivyo bila malipo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yanayoratibiwa na chama cha wafanyakzi wa migodini, nishati na ujenzi (Tamico) chini ya Tucta ni Rais Jakaya Kikwete.
ZIFUATAZO NI PICHA ZA MATUKIO YA UFUNGUZI WA MICHEZO MBALIMBALI YA MEI MOSI INAYOSHIRIKISHA MASHIRIKA, MAKAMPUNI NA IDARA MBALIMBALI ZA KISERIKALI NDANI YA UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA.
WAJASILIAMALI WA RUZUKU ZA SAFARI LAGER MWANZA WAPEWA MAFUNZO
LENGO NA MANUFAA YA CHANGAMOTO MSIKILIZE MTAALAMU.
Majina ya wajasiliamali waliofuzu kupewa ruzuku za programu ya Safari Lager Wezeshwa kwa msimu wa nne kwa mkoa wa Mwanza ni kama ifuatavyo kwenye orodha.
Mshauri wa biashara kutoka TAPBDS Theresia Kato alifafanua kuwa, baada ya mafunzo hayo patafuatiwa na makabidhiano ya vifaa vyao walivyoomba kwa nyakati tofauti ambapo; |
Baadhi ya washiriki hao kwa mkoa wa Mwanza wakiwa darasani wakati wa kupatiwa mafunzo. |
Darasa linaponoga. |
Mshauri wa biashara kutoka TAPBDS Theresia Kato akipitia wakufunzi wake kuona utendaji wao. |
Happiness Mabula Mandula ambaye ni mbunifu wa mavazi sambamba na utengenezaji batiki anaamini kuwa kupitia Safari wezeshwa biashara yake itakuwa. BOFYA PLAY. |
Jemes Edward Mwandefu mjasiliamali kutoka Bariadi anajishughulisha na utoaji wa huduma za Sekretari. BOFYA PLAY. |
Khadija Liganga mbunifu wa mavazi na fundi wa nguo za vitenge mafunzo yamembadilisha, wafanyabia shara wengi wanawekeza katika ubora wakisahau kujitangaza na kusaka masoko. BOFYA PLAY. |
Zebedayo Lazaro Kingi mjasiliamali kutoka Bariadi anasema mahusiano ndiyo silaha, jeh ni kipi kingine alichojifunza? BOFYA PLAY |
Majina ya wajasiliamali waliofuzu kupewa ruzuku za programu ya Safari Lager Wezeshwa kwa msimu wa nne kwa mkoa wa Mwanza ni kama ifuatavyo kwenye orodha.
MWANZA
1.Bagaile Shaban Barabara
2.Dastan Mutayoba Amon
3.David Awasi
4.Godlove Charles Muro
5.Happiness Mabula Mandula
6.Jemes Edward Mwandefu
7.Khadija Liganga
8.Raymond Emmanuel Kamisha
9.Zebedayo Lazaro Kingi
10. Zeda Lucas Magomola
Mafunzo yanayotolewa ni chachu kwa biashara zao na kwa wafanya biashara wengine wanao wazunguka kwani licha ya kuwawezesha katika suala la mitaji na vitendea kazi pia yamelenga katika kuwakuza kielimu kujua jinsi ya kuboresha bidhaa zao, utanuzi na usakaji masoko.
Zoezi hili la utoaji mafunzo limehusisha wataalamu wenye uwezo na uzoefu mkubwa katika kushauri na kusaidia ukuzaji wa sekta ya biashara ndogo dogo na kubwa.
Mafunzo yanayotolewa ni chachu kwa biashara zao na kwa wafanya biashara wengine wanao wazunguka kwani licha ya kuwawezesha katika suala la mitaji na vitendea kazi pia yamelenga katika kuwakuza kielimu kujua jinsi ya kuboresha bidhaa zao, utanuzi na usakaji masoko.
Zoezi hili la utoaji mafunzo limehusisha wataalamu wenye uwezo na uzoefu mkubwa katika kushauri na kusaidia ukuzaji wa sekta ya biashara ndogo dogo na kubwa.
Kabla ya washiriki kupatikana toka mikoa mbalimbali nchini mchakato ambao ulikuwa mzito, jumla ya fomu za maombi zilizoifikia kamati toka mikoa yote shiriki nchini zilikuwa ni 3,613. Wajasiliamali walifuzu vigezo ni 55 kutoka kanda tatu tofauti.
Subscribe to:
Posts (Atom)