Moja ya picha ya uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura. |
NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza
WAFANYAKAZI wa umma na sekta binafsi jijini Mwanza wameshauriwa kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la wapigakura ili waweze kuwachagua viongozi bora katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Chama cha Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Yusuph Simbaulanga, alisema kura ni nyenzo muhimu inayoweza kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima yanayoweza kujitokeza baada ya uchaguzi.
“Idadi ya watu wanaojiandikisha imeongezeka, hivyo kwa fursa hii ni vyema pia wafanyakazi kujiandikisha kwa wingi kwani wengi ni vijana wanaofanya kazi katika sekta binafsi na za umma,” alisema Simbaulanga.
Aidha, alisema kujiandikisha kwa wafanyakazi kutawafanya kuoana thamani ya kura zao katika kufanya uamuzi sahihi wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
“Kupitia sanduku la kura mfanyakazi ataweza kujikomboa kwa kuchagua viongozi watakaoleta tija kwenye utendaji, lakini pia kuboresha maslahi yao,” aliongeza Simbaulanga.
Alitumia nafasi hiyo pia kuwahimiza wafanyakazi kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka huu itakayofanyika kitaifa jijini Mwanza ili kushiriki pia kupima afya zao kuhusu magonjwa ya kisukari, shinikizo la damu na ukimwi, ambapo wataalamu wa afya watatoa vipimo hivyo bila malipo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yanayoratibiwa na chama cha wafanyakzi wa migodini, nishati na ujenzi (Tamico) chini ya Tucta ni Rais Jakaya Kikwete.
ZIFUATAZO NI PICHA ZA MATUKIO YA UFUNGUZI WA MICHEZO MBALIMBALI YA MEI MOSI INAYOSHIRIKISHA MASHIRIKA, MAKAMPUNI NA IDARA MBALIMBALI ZA KISERIKALI NDANI YA UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.