ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 22, 2015

KIMENUKA TOTO AFRICANS WANACHAMA WACHACHAMAA.

Wachezaji na mashabiki wa Toto African ya Mwanza wakishangilia kwa kumbeba juu kocha wa timu hiyo John Tegete, baada ya kuiwezesha timu hiyo kupanda Ligi Kuu soka Tanzania Bara 2015. Je shangwe hizi zitadumu?
WANACHAMA WA TOTO AFRICANS WACHACHAMAA WAWASILISHA BARUA NA SAINI 54 KUUTAKA UONGOZI UITISHE MKUTANO MKUU WA DHARURA

BAADHI ya wanachama wa Toto Africans ya jijini Mwanza wameorodhesha majina na kuweka saini wakiambatanisha na barua na kuupelekea uongozi wa klabu hiyo wakimtaka Mwenyekiti kwa kushirikiana na kamati ya utendaji waitishe mkutano mkuu wa dharula ufanyike tarehe 3/05/2015 kujadili masuala ya msingi yanayoitatiza klabu hiyo.

Ajenda zinazotajwa ndani ya barua hiyo ni pamoja na Taaarifa ya fedha msimu wa ligi hatua ya pili ya ligi msimu 2013-2014 na msimu wa 2014-2015.

Mkataba wa kisheria na mdhamini (Nsejjere)

Kujiuzuru kwa viongozi muhimu wa Klabu (Mwenyekiti na wajumbe wawili)

Ukiukwaji wa Mamlaka ya Utendaji na kupelekea uvunjwaji wa katiba ya Toto African, pia sekretarieti kushindwa kusimamia majukumu yao kwa kipindi chote.

Mpango mkakati wa ushiriki ligi kuu pamoja na kuunda kamati za kufanikisha malengo ya ushiriki na kadhalika. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA ALICHOSEMA MMOJA WA WANACHAMA MWASILISHA BARUA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.