ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 28, 2015

Rais Magufuli Amsimamisha Kazi Kamishina Mkuu wa TRA

Rasi Magufuli amsimamisha kazi kamishina mkuu wa TRA na kutaka uchunguzi juu yake kufuatia upotevu wa makontena bandarini.

Friday, November 27, 2015

KITUO CHA KILIMO N AUFUGAJI KUJENGWA WILAYANI KIBAHA KUUNGA JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA SEKTA YA KILIMO.

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza sekta ya kilimo Chama cha wakinamama wataalamu katika sekta za kilimo mifugo  pamoja na mazingira Tanzania (TAWLAE) wamejiwekea mikakati ya kujenga kituo maalumu  cha kilimo na ufugaji  katika kata ya Pangani iliyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa TAWLE Dr. Sophia Mlote katika ufunguzi wa  mkutano wa siku tatu  uliowakutanisha wadau mbali mbali wa maendelea  pamoja na wataalamu katika sekta ya kilimo na ugugaji kwa lengo la kuweza kujadili changamoto zilizopo pamoja na kuweka mpango mkakati wa kuimarisha kilimo cha kisasa pamoja na ufugaji.

Dr.Sophia alisema kwamba nia wameamua kukutana wataalamu  wa kilimo na mazingira ili kuweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya kilimo sambamba na kujenga kituo hicho maalumu ambacho kitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi  wa Wilaya ya Kibaha  na Taifa kwa ujumla kutokana na kituo hicho kitakuwa kinajihusisha na kutoa mafunzo  ya kilimo pamoja na masuala mbali mbali ya ufugaji.

“kitu kikubwa katika mkutano wetu huu ambao umeshirikisha wakinamama ambao ni wataalamu katika sekta ya kilimo, mazingira pamoja na uvuvi ni kujadili masuala mabli mbali ambayo yanayohusiana na utafiti ya kilimo ili kuweza kuweka mipango mizuri ambayo itaweza kuleta mabadiliko chanya katika kuwasaidia wakinamama kupitia kilimo,”alisema Dr Sophia.

Aidha alisema kwamba kwa sasa tayari wameshapata eneo kwa ajili ya kujenga kituo hicho katika Wilaya ya Kibaha ambacho maandalizi yake yameshaanza kufayika na kwamba hati imepatikana hivyo ana imani kukamilika kwa kituo hicho cha kilimo na ufugaji kitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa kibaha na maeneo mengine.

Kwa upande  wake Katibu mkuu mtendaji wa  jukwaa la wadau wa sekta ya kilimo linaloitwa (ANSAF) Audax Rukonge amesema kuwa sekta ya kilimo pamoja na mazingira ina umuhimu mkubwa katika jamii inayotuzunguka ya watanzania hivyo serikali inapaswa kutilia mkazo suala hilo kuanzia ngazi zote za kuanzia uzalishaji mpka hatua ya utunzaji  wa chakula.
Awali akitoa hotuba yake wakati alipokuwa anafungua mkutano huo katibu mku u wa Wizara ya maendeleo ya mifugo  na uvuvi  Dr.Yohana Budeba amesema kwamba serikali itahakikisha inapambana vilivyo katika kuboresha sekta ya kilimo, mifugo pamoja na uvuvi ili kuweza kuwapa fursa wananchi waweze kupata ajira na kuondokana na janga la umasikini.

Katibu huyo mkuu alisema kwamba anatambua kilimo katika nchi ya Tanzania kina umuhimu sana hivyo atahakikisha anashirikina bega kwa bega na wakinamama hao ili waweze kutimiz amalengo waliyojiwekea katika kuendeleza kufanya utafiti wa kina katika mambo mbai mbali amabyo yataweza kuwasaidia wananchi katika upatikanaji wa ajira.

Katika hatua nyingine Katibu huyo alisema alengo kubwa la serikali ni kuweka utaratibu mzuri wa kuwajengea uwezo  watumishi wa umma pamoja na vikundi mbali mbali katika ili kuvipa ujuzi ambao utaweza kuisaidia sekta hiyo ya kilimo kutokana na mafunzo mbali mbali ambayo yatakuwa yanatolewa.

 MKUTANO huo   wa 19 kufanyika kwa wakinamama hao umefadhiliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Agriculture non state Actor forum (ANSAF)limewashirikisha washiriki zaidi ya 100  ambao ni wataalamu  katika sekta ya  kilimo, pamoja na mazingira kwa lengo la kujadili masuala mbali mbali ambayo yataweza kusaidia kuleta mabadiliko makubwa  hususan kwa wakinamama  kuweza kujikwamua  kiuchumi bila ya kuwa tegemezi pamoja na kutengeneza ajira kwa watu mbali mbali.

KAMPENI YA ABIRIA PAZA SAUTI YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Abel Swai (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo, kuhusu kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyozinduliwa Dar es Salaam leo asubuhi.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga amesema kila mwananchi anawajibu kuzuia ajali za barabarani badala ya kudhani kazi hiyo ni ya polisi pekee.

Mpinga alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyozinduliwa Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam leo asubuhi, ambao ulikwenda sanjari na mabalozi wa Usalama barabarani  (RSA) ambao walitoa elimu  kwa abiria kuhusu usalama barabarani.

"Abiria pazeni sauti pale mtakapoona dereva anaendesha gari lake ndivyo sivyo na kama mtapaza sauti itasaidia kupunguza ajali hapa nchini" alisema Kamanda Mpinga.

Mwakilishi  wa Mwenyekiti wa Usalama Barabarani ambaye ni Mratibu wa kampeni hiyo , Jackson Kalikuntima, alisema kampeni hiyo itaendelea nchini kote kwa njia ya kutoa elimu, haki na wajibu wa raia wanapokuwa safarini.

Alisema abiria wanaowajibu wa kuzuia ajali wakishirikiana na mabalozi watakao kuwa ndani ya mabasi kuhimiza abiria kupaza sauti.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Abel Swai alisema kumekuwa na changamoto kubwa kwa baadhi ya madereva kukiuka sheria na kusababisha ajali kwa makusudi.

Alisema kampeni hiyo inalengo la kutoa elimu kwa abiria waweze kujiamini na kutoa taarifa pale wanapoona dereva anakwenda kinyume na sheria kwa kutumia namba za kutoa taarifa kwa polisi na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ambazo ni 0800110019 au 0800110020.

Swai alisema madereva wanapaswa kutii sheria bila shuruti na kuwa wana amini kila mmoja atakuwa makini na kuzingatia sheria ajali zitapungua kama sio kuisha kabisa.


MKURUGENZI WA AMANA BANK AFUNGA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA TAWI LA MWANZA.

Mkurugenzi wa benki ya Amana  Dk Muhsin Masoud  akimkabidhi  zawadi mteja Yasmin Ismail Mussa kwa utunzaji bora wa fedha katika tawi la Mwanza.


Benki ya Amana leo hii imehitimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo katika tawi la Mwanza mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud alitoa zawadi mbali mbali kwa wateja wenye sifa tofauti tofauti kama ioneshavyo pichani. 

Mkurugenzi huyo alikutana na wateja mbali mbali tawini  hapo ili kubadilishana nao mawazo na pia kupokea maoni toka kwao katika kuboresha huduma kwa wateja wa benki hiyo pekee ya Ki Islamu nchini. 

Kilele hicho cha wiki ya huduma kwa wateja kimefanyika katika matawi yote ya benki hiyo ambayo kwa Dar es Salaam ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na Main, vile vile Arusha na Mwanza.
Mkurugenzi wa Amana Bank Dk Muhsin Masoud akimzawadia Bw Juma Kivuruga kwa kuwa mfanyakazi bora kwa tawi la Mwanza, Kivuruga alipigiwa kura na wafanyakazi wenziye wa tawi hilo.
Daud Lweno akizawadiwa na Mkurugenzi wa Amana Bank kama mteja mzuri kulipia miamala ya TRA katika tawi la Mwanza.
Mteja Yasmin Ismail akikata keki ya kuadhimisha miaka minne tangu kufunguliwa kwa benki hiyo, huku wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wao wakifuatilia tukio hilo kwa umakini.
Bw Juma Msabaha meneja huduma kwa wateja wa Amana bank akijibu baadhi ya maswali kuhusu benki hiyo toka kwa waandishi wa habari.
Meneja wa tawi la Mwanza Saleh Awadh akiongea na mteja wa benki hiyo.
Hawa Maftah wa Amana Bank akimhudumia mteja mapema leo katika tawi.
Mkurugenzi Dk Muhsin Masoud akiongea na mmoja wa mamia ya wateja aliokutana nao leo katika tawi la jijini Mwanza ambako alikuja rasmi kwa shughuli ya ufungaji wa wiki ya huduma kwa wateja.
Picha ya pamoja wafanyakazi wa benki hiyo na mkurugenzi wao.
Zainab Barker ambaye ni meneja huduma kwa wateja wa tawi la Mwanza.
Ibtisam Akrabi akimhudumia mteja katika tawi la Mwanza.
Mahmoud Maimu akimhudumia mteja.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AVAMIA BANDARI LEO, AAMRISHA KUKAMATWA KWA MAAFISA KIBAO WA TRA

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa watano na watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.
Akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Bandari pamoja na viongozi wa TRA katika ziara ya kushtukiza leo mchana (Ijumaa, Novemba 27, 2015), Waziri Mkuu amewataka Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Rished Bade na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Lusekelo Mwaseba wahahakikishe wanashirikiana na polisi kufuatilia upotevu huo na kwamba fedha hizo zinapatikana na zinarudi Serikalini.
Akitangaza uamuzi huo baada ya kufanya kikao na baadhi ya viongozi wa Serikali bandarini hapo, Waziri Mkuu aliwataja maafisa waliosimamishwa kazi kuwa ni Kamishna wa Forodha, Bw. Tiagi Masamaki na Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja, Bw. Habibu Mponezya.
“Hawa wanasimamishwa kazi. IGP ninaagiza hawa watu wakamatwe na kuisaidia polisi. Hati zao za kusafiria zikamatwe na mali zao zikaguliwe kama zinaendana na utumishi wa umma,” alisema Waziri Mkuu.
Maafisa wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Bw. Haruni Mpande, Bw. Hamisi Ali Omari (hakutaja ni wa idara gani), na Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu (ICD In-Charge), Bw. Eliachi Mrema. “Hawa wanasimamishwa kazi hadi uchunguzi utakapokamilika na pia wawe mikononi mwa polisi,” alisema.
Pia aliagiza watumishi watatu wa mamlaka hiyo wahamishwe kutoka Dar es Salaam na kupelekwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Katibu Mkuu wa Hazina, Dk. Servacius Likwelile ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho, kuhakikisha kuwa anapeleka wataalamu kutoka Wakala wa Serikali Mtandao (e-Govt) haraka iwezekanavyo ili wakakague mifumo ya taarifa na kubaini jinsi ambavyo wizi huo unafanyika.
“Ninataka uchunguzi uanze kufanyika mara moja, tafuteni njia ambazo zinatumika kama mianya ya wizi kutokea hapa bandarini hadi kwenye ICDs. Nataka hayo makontena yatafutwe hadi yajulikane yako wapi, na fedha hiyo ihakikishwe inarudi serikalini,” alisema.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Bw. Ernest Mangu, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Suleiman Kova, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Bw. Awadh Massawe na viongozi mbalimbali kutoka TRA na TPA.
Mapema akijibu maswali ya Waziri Mkuu, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Bade alikiri kwamba kuna upotevu wa makontena ambao huwa unafanyika kati ya bandarini na ICDs na hasa ICD ya Ubungo. Akitoa ufafanuzi, alisema kwamba walifanya ukaguzi kwenye ICD moja na kukuta makontena 54 yamepotea kwa njia za wizi. “Hata hivyo, tulipoendelea na ukaguzi, namba iliongezeka na kufikia 327. Tunaendelea kufuatilia kwa kushirikiana na TAKUKURU. Mmiliki wa ICD ametakiwa kulipa faini sh. bilioni 12.6/- na ameshalipa sh. bilioni 2.4/-,” alifafanua.
Alipoulizwa na Waziri Mkuu kama ana majina ya watumishi wanaohusika na wizi huo, Bw. Bade akakiri kwamba anayo lakini siyo kwa wakati huo labda ayapate kutoka kwa wasaidizi wake. Ndipo Waziri Mkuu akamuonyesha orodha ya makontena 349 yenye taarifa zote hadi namba za magari yaliyobeba mizigo hiyo na Bw. Bade akakiri kwamba orodha hiyo ni ya kweli.
“Kwa utaratibu huo hatuwezi kufika, labda baadhi ya watu waondolewe kazini”. Ndipo akaanza kutaja majina ya maafisa hao waliosimamishwa

MWILI WA MAWAZO SASA KUAGWA RASMI KESHO JUMAMOSI MWANZA

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Salum Mwalimu.
Wanachama wa Chadema mkoani Mwanza wanatarajia kuuaga mwili wa marehemu Alphonce Mawazo siku ya kesho Jumamosi kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Geita;
Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Geita Alphonce Mawazo kesho utaagwa katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza na Baadaye kusafirishwa kupelekwa mkoani Geita kwa maandalizi ya mazishi.

Mwili huo ulitakiwa kuagwa jumamosi iliyopita zoezi ambalo lilikwama baada ya zuio la Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza kabla ya Mahakama kuu kutengua Pingamizi hilo mapema jana. BOFYA PLAYA KUSIKILIZA RATIBA.

Thursday, November 26, 2015

TAMASHA KUBWA LA BURUDANI LA INSTAGRAM PARTY KUFANYIKA JUMAMOSI VIWANJA VYA ESCAPE ONE MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi wa Freconic ideaz, Fred Ngimba.
 Mkurugenzi wa Freconic ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la burudani la Instagram party litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya Escape One Mikocheni likiwa na kauli mbiu Bongo Throw Back. Kulia ni Meneja Mawasiliano, Krantz Mwantepele.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Freconic Ideaz, imeandaa tamasha la burudani la 'Instagram party' litakalofanyika kesho kutwa kwenye Ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini  Dar es Salaam likiwa na lengo la kuwakumbusha wapenzi wa muziki, mavazi na misemo ya kizamani.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa  Freconic Ideaz, Fred Ngimba alisema pia tamasha hilo litahusisha watu wenye ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii na wasanii mbalimbali wa muziki na filamu.

Alisema wadau na marafiki mbalimbali wanaotumia mitandao ya kijamii watakutana siku hiyo kuweza kufahamiana na kubadilishana mawazo huku wakipata burudani mbalimbali.

"Kiingilio katika tamasha hili kitakuwa ni sh. 50,000 kwa viti maalumu na vile vya kawaida ni sh. 10,000, ambapo halitaishia hapa ila litaendelea katika Mikoa ya Mwanza, Morogoro, Tanga, Dodoma na Iringa," alisema Ngimba.

Alitoa mwito kwa wadau wa muziki wa mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani itakayotolewa siku hiyo.

RATIBA YA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO NA MAZISHI YA KAMANDA MAWAZO.

Mahakama kuu Kanda ya Mwanza imeamuru mwili wa marehemu Alphonce Mawazo uagwe jijini Mwanza, hukumuimetoka hii leo majira ya saa 16:15.

KESI ya msingi imemelizika kwa Mahakama hiyo kupitia Jaji Lameck Mlacha kuamua kwamba; 

Agizo la polisi la kuzuia kuagwa Kamanda Mawazo limefutwa na Mahakama Kuu.

Wafiwa wameruhusiwa na Mahakama kumwaga Kamanda Mawazo kwa kujadiliana na polisi sehemu ya kuagia.

Polisi watoe ulinzi kama ilivyo wajibu wao.



Ratiba ya shughuli ya utoaji heshima za mwisho na mazishi ya Kamanda Mawazo
Kesho Siku ya Ijumaa, Novemba 27 saa 2 asubuhi, mwili wa Mpiganaji na Kiongozi wetu Alphonce Mawazo utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo, eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, wabunge wa UKAWA, wataongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mawazo.
Baada ya Viwanja vya Furahisha, mwili wa Mpiganaji Mawazo utasafirishwa kuelekea Geita kwa ajili ya kuwapatia nafasi wakazi wa Mkoa wa Geita kumuaga Kiongozi wao siku ya Jumamosi, Novemba 28 kuanzia asubuhi mapema ambapo baadae mchana mwili huo utapelekwa Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, ambapo pia wananchi watapata fursa ya kumpatia heshima za mwisho na kumuaga Mawazo ambaye alikuwa ni Mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Busanda.
Baada ya wakazi wa Katoro kushiriki tukio hilo, mwili wa Kamanda Mawazo utapelekwa nyumbani kwao kijijini Chikobe tayari kumhifadhi kwenye nyumba ya milele shambani kwake, siku a Jumapili, Novemba 29, baada ya familia, ndugu, jamaa na wakazi wa kijiji hicho kutoa heshima zao za mwisho.
Makene Tumaini Afisa Habari Chadema

TIGO YADHAMINI ONESHO LA MWANAMUZIKI MOUSSA DIALLO KUTOKA NCHINI MALI LITANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO

Meneja wa Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kampuni hiyo kudhamini onesho la mwanamuziki Mousa Diallo kutoka nchini Mali litakalofanyika kesho katika Mgahawa wa Chakula na Vinywaji wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert na katikati ni Mwanamuziki, Moussa Diallo.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja (kushoto), akizungumza na Mwanamuziki, Moussa Diallo (kulia). Katikati ni Mmiliki wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Carlos Bastos.
Mwanamuziki Moussa Diallo wa nchini Mali anayeishi Denmark (katikati), akiimba mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akijitambulisha ambapo leo atafanya onesho lake Ukumbi wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Slaam. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja ambao wamewezesha ujio wa mwanamuziki huyo na kushoto ni Ofisa  Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert.
Ofisa Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert (kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu onesho hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Warembo wa Samaki Samaki wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

MWANAMUZIKI maarufu toka Afrika Magharibi anayeishi Denmark, Moussa Diallo, leo anatarajia kufanya onesho lake hilo leo (Novemba 26) katika Mgahawa wa Chakula na Vinywaji wa  Samaki Samaki uliopopo Masaki jijijini Dar es Salaam ambapo litaenda sanjari na ziara ya kutembelea  miradi mbalimbali ya kijamii hapa nchini.

Onesho hilo lililodhaminiwa na Kampuni  ya simu za mikononi ya Tigo ikishirikiana na Mgahawa huo wa  Samaki Samaki litafanywa na Mwanamuziki huyo toka nchini Mali mwenye asili ya Denmark, ambaye amewasili nchini leo.

 Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi kwenye mkutano wa waandishi wa habari, Ofisa Mkuu wa Masoko wa Samaki Samaki, Saum Wengert, alisema mwanamuziki huyo anapiga muziki wa aina ya soul iliyochanganywa na vionjo vya kiafrika na muziki wa Magharibi unaopendwa ulimwenguni kote.

 Alisema onesho hilo pia linatarajiwa kufanyika kesho kutwa (Novemba 27) katika Hoteli ya Melia jijini Zanzibar na baadae watafanya Full Moon Party kwenye Hotel ya Kendwa Rocks iliyopo jijini Zanzibar. 

Moussa alizaliwa jijini Paris nchini Ufaransa na kukulia Bamako nchini Mali ambapo hivi sasa anamakazi yake Copenhagen nchini Denmark.

Katika juhudi za kukuza utamaduni, Diallo anachanganya muziki wake kwa kushirikisha vikundi mbalimbali vya utamaduni ikiwemo; Dawda Jobarten (Kora, Mwimbaji), Preben Carlsen (gitaa), Salieu Dibba (Percussions, Sauti), na Marco Diallo (Ngoma).

Kwa upande wake, Meneja uhusiano wa Tigo, John Wanyacha alisema kampuni hiyo na wadhamini wengine wamekubali Diallo kufanya onesho nchini ikiwa ni pamoja na kuweka mahusiano mazuri yaliyopo na maonesho yanayokuja.

Alisema kuwa wanafahamu wanachopenda wateja wao kwenye muziki na kwamba wana eneo ambalo linaweza kuwawezesha kuzuia miziki wasioyoipenda hivyo ujio wa Diallo nchini utaendeleza makubaliano mazuri kati ya kampuni hizo kwa kuwapa wateja wanachokihitaji ikiwa ni pamoja na vionjo. 


Wengine waliodhamini ziara hiyo ni pamoja ni; Johnnie Walker, French Kiss, Heineken na Ledger Plaza Bahari Beach.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

S MIAH ft YOUNG RAFA MANENGO & AMP, ALLY KIJO - AMSHA POPO


S Miah ft Young Rafa Manengo & Ally Kijo - Amsha Popo (Official Music Video)

Ni safari nyingine hii katika game ya muziki hapa Bongo, and this time toka Rock City ni video mpya kutoka kwa Smiah akiwa amemshirikisha Young Rafa na Ally Kijo wimbo unaitwa Amsha Popo ikiwa audio yake imefanywa na producer anaejulikana kwa jina la King Fenya Ze Beat na video ikiwa imeandaliwa na kuongozwa na Kenny Ukiyz.

Wednesday, November 25, 2015

WALIMU KAHAMA WANASWA NA MTIHANI.

Na Emmanuel Mlelekwa, 
Novemba 25,2015 
KAHAMA 

Jeshi la polisi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga linawashikilia walimu watatu wa shule binafsi ya sekondari Andaleck kwa kosa la kukutwa na mtihani wa Historia wa kidato cha nne kabla ya kufunguliwa. 

Kaimu Mkuu wa jeshi la polisi wilayani humo George Bagyemu amesema kuwa walimu hao wanashikiliwa tangu juzi kwa mahojiano kutokana na kuvujisha mtihani wa somo hilo kwa baadhi ya wanafunzi wanaoendelea na mtihani wa kumaliza kidato cha nne. 

Amesema kuwa walimu hao ambao hakutaka kuwataja majina kwa sababu za kiusalama walikutwa na mtihani huo siku moja kabla ya kufanyika kwa mtihani huo na kusema kuwa jeshi la polisi linasubili maelekezo ya kina kuhusu walimu hao.

Aidha amesema kuwa kukamatwa kwa walimu hao hakukuathiri mitihani mingine kuendelea na kwamba kuvujisha mtihani ni kosa la jinai hivyo sheria itachukua mkondo wake baada ya uchunguzi kukamilika. 

Hata hivyo mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Alexander Kasmil akiongea kwa njia ya simu amesema kwa sasa yuko safarini akifika atalitolea ufafanuzi zaidi suala hilo jumatatu ijayo.

HAKIELIMU YAZINDUA JOPO LA WASHAURI MABINGWA

Timu ya Menejimenti ya HakiElimu ikiwa katika picha na Mwenyekiti wa Bodi ya HakiElimu na Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa jopo la washauri bingwa
Wafanyakazi wa Shirika la HakiElimu waliohudhuria uzinduzi katika picha ya pamoja na jopo la washauri bingwa
Waliosimama ni Prof. J. Galabawa (kushoto) Prof. Kitila Mkumbo (katikati) na Prof. Elias Jengo (kulia) Waliokaa ni John Kalage (Mkurugenzi wa HakiElimu) Prof. G.Mmari (katikati) na Prof. Prof. Martha Qorro (Kulia).
Mgeni rasmi Prof. Geofrey Mmari,akizungumza jambo katika hafla fupi ya uzinduzi wa jopo la washauri mabingwa akitoa neno la ufunguzi.
Prof. Kitila Mkumbo mmoja wa wajumbe wa ThinkTank akitoa neno kwa niaba ya jopo la washauri bingwa wa HakiElimu.
Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu Bi, Joyce Sekimanga kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akiwasilisha ujumbe kutoka serikali katika uzinduzi wa jopo la washauri wa HakiElimu
Prof. Martha Qorro mmoja wa wajumbe wa jopo la washauri mabingwa akipokea mpango mkakati wa HakiElimu kutoka kwa mgeni Rasmi Prof Geofrey Mmari
Prof. J. Galabawa mmoja wa wajumbe wa jopo la washauri mabingwa akipokea mpango mkakati wa HakiElimu
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu John Kalage akielezea lengo la kuanzishwa kwa Think Tank
Washiriki katika uzinduzi wa jopo la washauri mabingwa wa HakiElimu





Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

SHIRIKA la HakiElimu  limezindua Jopo la Washauri Mabingwa  linaloundwa na maprofesa 10 waliobobea katika fani ya elimu ili  kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa watoto kupata elimu bora.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu , John Kalage amesema kazi ya jopo hilo itakuwa kutoa ushauri wa kitaalam juu ya masuala ya elimu kadri litakavyoombwa na  HakiElimu.

Amesema jopo hilo litatatoa ushaufri juu ya mikakati ,taratibu na mbinu za kuhakikisha ushiriki madhubuti katika kukuza na kutetea ubora wa elimu nchini.

Kalage aliwataja maprofesa wanaounda jopo hilo kuwa ni Abel Ishumi,Herme Mosha,Justinian Galabawa,Kitila Mkumbo,Suleiman Sumra,Martha  Qorro, Mwajabu Possi,Akundaeli Mbise, Masalukulangwa pamoja na Elias Jengo.

Amesema kuanzishwa kwa jopo hilo litasaidia shirika kupata mawazo mapana zaidi ya kitafiti na uchambuzi wa changamoto za sekta ya elimu.

Kalage amesema kuwa jopo hilo litakwenda sambamba na jitihada za serikali kuwa na mikakati mingi ya kuboresha elimu na azma ya serikali kutekeleza maazimio mbalimbali ya kimataifa kama  Malengo Maendeleo Endelevu (SDGs)na Incheon ya uboreshaji wa elimu.