ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 25, 2015

WALIMU KAHAMA WANASWA NA MTIHANI.

Na Emmanuel Mlelekwa, 
Novemba 25,2015 
KAHAMA 

Jeshi la polisi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga linawashikilia walimu watatu wa shule binafsi ya sekondari Andaleck kwa kosa la kukutwa na mtihani wa Historia wa kidato cha nne kabla ya kufunguliwa. 

Kaimu Mkuu wa jeshi la polisi wilayani humo George Bagyemu amesema kuwa walimu hao wanashikiliwa tangu juzi kwa mahojiano kutokana na kuvujisha mtihani wa somo hilo kwa baadhi ya wanafunzi wanaoendelea na mtihani wa kumaliza kidato cha nne. 

Amesema kuwa walimu hao ambao hakutaka kuwataja majina kwa sababu za kiusalama walikutwa na mtihani huo siku moja kabla ya kufanyika kwa mtihani huo na kusema kuwa jeshi la polisi linasubili maelekezo ya kina kuhusu walimu hao.

Aidha amesema kuwa kukamatwa kwa walimu hao hakukuathiri mitihani mingine kuendelea na kwamba kuvujisha mtihani ni kosa la jinai hivyo sheria itachukua mkondo wake baada ya uchunguzi kukamilika. 

Hata hivyo mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Alexander Kasmil akiongea kwa njia ya simu amesema kwa sasa yuko safarini akifika atalitolea ufafanuzi zaidi suala hilo jumatatu ijayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.