ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 27, 2024

MSIMAMIZI WA UCHAGUZI TANGA JIJINI MHANDISI JUMA AMESEMA WATAZINGATIA 4R ZA RAIS DKT SAMIA SULUHU KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

 

Na Oscar Assenga,Tanga.

MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Mhandisi Juma Hamsini amesema kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu utazingatia 4R za Rais Dkt Samia Suluhu.

Mhandisi Hamsini aliyasema hayo leo wakati akizungumza waandishi wa habari ofisini kwake kuelekea kwenye uchaguzi huo ambapo alisema kwa Jiji la Tanga kuna mitaa 181 na kata 27 huku akiwataka wananchi kujitokeza kwenye uchaguzi hizo.

Alisema kwamba katika uchaguzi ni lazima uangalia tathimini za chaguzi zilizopita lakini wa mwaka huu utakuwa huru ,Haki na Amani .

“Lakini niwaambie kwamba Rais Dkt Samia Suluhu amehakikisha bajeti yetu tulioomba tumepatiwa kama ilivyokusudiwa hii inaonyesha uchaguzi huo ni huru na haki “Alisema

Aidha alisema kwa sababu mpaka leo hakuna mdau yoyote wa uchaguzi aliyesema anajitoa kwenye uchaguzi tofauti na ilivyokuwa mwaka 2019 kwenye uchaguzi kama huo.

“Lakini niseme kwamba kuelekea kwenye uchaguzi huo kutakuwa na vikao vya nje vya hamasa kuwahamisha wananchi kujitoeza kwenye uchaguzi pamoja ana viongozi wa Serikali na wanasiasa kuwahamisha wananchi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali,kujitokea kupiga kura”Alisema Mkurugenzi huyo

Alisema ili uchaguzi uweze kuwa mzuri lazima kuwe na uwiano sawa kwa wadau wote wanaoshiriki uchaguzi kupitia vyama vyote kuanzia kwenye ngazi ya Mtaa,Kata mpaka Halmashauri washirikishwe kikamilifu nao wanafanya hivyo.

Hata hivyo aliwaeleza wananchi kwamba uchaguzi huo unasimamiwa na Tamisemi hivyo ni muhimu kila mkazi ajiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura huku akieleza kila mgombea kwenye mtaa lazima kuwepo na nafasi za wajumbe ili mwenyekiti awe kamilifu lazima awe na wajumbe wake na Katibu wake ni Mtendaji wa Mtaa.

MAMA KOKA KUCHELE ACHANGIA MATOFALI 1300 SHULE YA MSINGI ZEGERENI


 VICTOR  MASANGU, KIBAHA

Mke wa Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka katika  kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu ya msingi ameamua kuchangia  matofali 1300 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili likiwemo  darasa la awali pamoja na ujenzi wa darasa moja kwa ajili ya mradi katika shule ya msingi Zegereni iliyopo Kata ya Visiga.

Mama Koka ameamua kuchangia matofali hayo kutokana na kubaini kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa  madarasa hivyo amebainisha kuwa kujengwa kwa madarasa mapya kutaweza kusaidia kwa kiasi  kikubwa wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki na kuondokana na adha ya kusoma kwa mlundikano.

Mama Koka amebainisha  kwamba anatambua umuhimu mkubwa wa elimu hasa katika wanafunzi wa madarasa ya awali pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi ndio maana akaamua kujikita na kusapoti matofali hayo ambayo matofali 800 yatakwenda kutekeleza mradi wa shule ya awali pamoja na matofali 500  ambayo aliyatoa hapo awali yatatekeleza ujenzi wa darasa moja katika shule hiyo ya msingi Zegereni.

"Katika kuboresha sekta ya elimu mimi kama mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini nimechangia matofali 1300 katika shule ya msingi Zegereni ambapo matofali 800 ambayo yatakwenda kujenga darasa moja la awali na yale mengine matofali 500 yatakwenda kusaidia ujenzi wa darasa moja katika shule ya msingi Zegereni likiwemo la awali ambalo nimechangia matofali 800.



Kadhalika Mama Koka amebaissha kwamba pamoja na kuweza kuchangia matofali pia atahakikisha anasaidia kwa hali na mali  katika  kuboresha elimu katika shule hiyo ikiwa sambamba na kuahidi kuchangia vitabu mbali mbali  hasa katika vitabu vya kiingereza  pamoja na hisabati ili kuongeza uwezo zaidi wa wanafunzi kujifunza  na kufaulu masomo yao.


Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Visiga Kambi Legeza amempongeza kwa dhati mke wa Mbunge la Jimbo la Kibaha mjini kwa juhudi zake za kuweza kuchochea na kuchangia matofali katika shule hiyo ya Zegereni na kwamba kukamilika kwa miradi hiyo ya ujenzi wa madarasa kutasaidia zaidi wanafunzi kupata fursa zaidi ya kusoma katika mazingira rafiki na kuongeza kiwango cha ufaulu.

Naye Katibu wa kikundi cha wajasiriamali cha Malkia wa nguvu Bhoke Nyamonge amesema kwamba wao wamesapoti kuchangia matofali 1000 kwa ajili ya kusapoti mradi wa ujenzi kwa wanafunzi wa shule ya awali Zegereni lengo ikiwa ni kuendelea kuunga juhudi za serikali katika kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka amesema kwamba lengo kubwa ni kuhakikisha wanatekeleza Ilana ya chama kwa vitendo hivyo walichokifanya kikundi hicho cha Malkia wa nguvu kinafaa kuigwa na kwamba mke wa Mbunge atawasaidia kwa hali na mali kwa kuwa na yeye ni mjasiriamali.


AZAM FC SASA RASMI MTEJA WA SIMBA.

 

MATAJIRI wa Dar Azam FC msimu wa 2024/25 wamepoteza mchezo wa kwanza wakiwa ndani ya Uwanja wa New Amaan Complex mbele ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Azam FC ilikuwa imecheza jumla ya mechi nne ambazo ni dakika 360 bila kuambulia kichapo kwenye mechi hizo ambapo ilipata ushindi kwenye mechi mbili na kuambulia sare kwenye mchezo mmoja.

Ilikuwa JKT Tanzania 0-0 Azam FC, Azam FC 0-0 Pamba Jiji kwenye mechi hizi ilitoshana nguvu na mpinzani wake na mchezo dhidi ya KMC 0-4 Azam FC, Azam FC 1-0 Coastal Union ilikomba pointi tatu hivyo kwenye mechi nne ni mabao matano ilifunga na kinara wa kutengeneza pasi za mwisho ni Feisal Salum mwenye pasi tatu  ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora dhidi ya KMC.

Mchezo wa kwanza kupoteza ilikuwa Septemba 26 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 0-2 Simba mabao yakifungwa na Leonel Ateba dakika ya 14 na Fabrince Ngoma dakika ya 47 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.

Simba imecheza jumla ya mechi tatu msimu wa 2024/25 ikikomba pointi zote tisa na safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 9 ambapo mchezo walioshinda mabao mengi ilikuwa dhidi ya Fountain Gate, Uwanja wa KMC, Complex wakishinda mabao 4-0.

Wednesday, September 25, 2024

RAIS DKT. SAMIA AKIWASALIMIA WANANCHI WA KIGONSERA MKOANI RUVUMA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akiwasalimia Wananchi wa Kigonsera Mkoani Ruvuma, leo tarehe 25 Septemba, 2024.

Tuesday, September 24, 2024

MBUNGE KOKA AFANYA KWELI KATA YA VISIGA KATIKA SEKTA YA ELIMU


 NA VICTOR MASANGU,KIBAHA


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka  katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu ametumia fedha za mfuko wa Jimbo kiasi cha shilingi milioni tano katika mradi wa ujenzi wa shule ya msingi shikizi ya Saini iliyopo kata ya Visiga ili kuondokana na changamoto ya wanafunzi wadogo kutembea umbari mrefu wa zaidi ya kilometa 12.

Hayo yamebainishwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mathias Alexanda wakati akitoa taarifa kwenye ziara ya kikazi ya  Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini ambaye alifika kwa  ajili ya kuweza  kutembelea   miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu pamoja na miundombinu ya barabara.

Mkuu huyo amebainisha kwamba shule hiyo ambayo imeanzishwa  mwaka huu imeweza kuwa ni msaada  mkubwa kwa watoto wadogo wenye umri wa kuanzia miaka mitano na kuendelea kwani  hapo awali  wanafunzi hao walikuwa na adha kubwa ya kutembea umbari mrefu kabla ya kuanzishwa kwa mradi huo wa shule mwaka huu.

Mkuu huyo  amempongeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni tano ambayo imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha miundombinu ya matundu ya vyoo pamoja na miundombinu mingine ya madarasa katika shule hiyo.

Mkuu huyo hakusita kuishukuru Halmashauri ya mji Kibaha kwa kuweza kuwa bega kwa bega katika kuchochea maendeleo ya elimu pamoja na Diwani wa Kata ya Visiga kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa shule.

Aliongoze kuwa katika mradi huo serikali imeweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 62  ambazo zimeweza kusaidia kwa kiwango kikubwa katika ujenzi wa kuanzishwa kwa shule hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amebainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuweka mikakati madhubuti ambayo itaweza kusaidia katika kuboresha sekta ya elimu hivyo ameamua kuchangia fedha hizo ili kuwaondolea wanafunzi hao kutembea umbari mrefu.

"Kikubwa nimefarijika kufanya ziaara ya kikazi katika kata ya Visiga na nimetembelea katika shule hii ya awali na darasa la kwanza na la pili la  Saini na nimeweza kujionea mradi huu umeanza utekelezaji wake na ujenzi wa  baahi ya madarasa na mimi  nimeweza kuchangia kiasi  cha shilingi milioni tano kwa ajili ya kuboresha   sekta ya elimu ikiwemo madarasa pamojana matundu ya vyoo.

Aidha Mbunge Koka amebainisha kwamba kipaumbele chake kikubwa katika mfuko wa Jimbo ni kuhakikisha kwamba anaboresha zaidi shule ambazo zipo pembezoni ikiwemo kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuweza kuboresha zaidi miundombinu ya madarasa pamoja na maboma ambayo miundombinu yake imechakaa.

Naye Afisa mtendaji wa Kata ya Visiga Aloise Nyello amesema kwamba serikali katika kutekeleza elimu bure malipo imetoa kiasi cha shilingi milioni 292 kwa ajili ya shule za msingi na sekondari.

Mbunge Koka yupo katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuweza kutembelea na kukagua miradi mbali mbali   ya maendeleo ikiwa pamoja na kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili  ili kuzitafutia ufumbuzi.