Waziri mkuu Mizengo Pinda akiteta na wabunge John Mnyika (kushoto), Zitto Kabwe na Hamad Rashid mjini Dodoma april 21. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
LIVE KUPITIA BONGO FLEVA NEW SEASSON NA ADAM MCHOMVU sauti ya ripota wa clouds fm kutoka mkoani Dodoma imewasilisha kuwa waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda amkanusha taarifa zilizoripotiwa kupitia magazeti mbalimbali ya leo zikitaja mawaziri kadhaa kujiuzuru.Mh. Waziri mkuu (akisikika live yeye mwenyewe) amesema kuwa hakuna barua yoyote aliyoipokea kutoka kwa mawaziri kujiuzuru na taarifa kamili huenda ataitoa jumatatu na kama kuna wanaotaka kujiuzuru basi watawasilisha kwake barua nae atatanabaisha kwa waandishi wa habari, lakini mpaka hivi sasa hakuna barua yoyote aliyoipokea kuhusu hilo na wala hana taarifa zozote kuhusu mawaziri waliojiuzuru..
Kabla ya habari hizo
Mawaziri nane wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete walitajwa kujiuzulu baada ya wabunge kumkalia kooni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu ripoti chafu ya ubadhirifu wa fedha za umma zilizowasilishwa na wenyeviti wa kamati za tatu za Bunge.
Mawaziri waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Mkuchika, Waziri wa Maliasili na Utalii,Ezekiel Maige na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda.
Wengine waliotajwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami na Naibu wake, Lazaro Nyalandu.