ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 19, 2012

WABUNGE KUMNG'OA WAZIRI MKUU KUFIKIA J3?

Deo Filikunjombe:- Ameliambia bunge kuwa Waziri wa Fedha Mkulo sio muaminifu anaitafuna nchi. Wabunge hawana imani na baadhi ya mawaziri wetu.
Awali alisema wengi wa mawaziri ni wezi na ushahidi anao atautoa ameongeza kuwa anashangazwa kwamba tangu jana hadi leo hakuna hata Waziri mmoja aliye jiuzuru na hii ni kutokana na malalamiko ya wabunge kuhusiana na kutokuwepo kwa usimamizi kutokuwepo kwa uwajibikaji mali za wananchi mali za umma zinapotea.

Vicent Nyerere:- Anashangazwa kwamba magari yananunuliwa na kufanyiwa ukaguzi kwa makampuni feki yanayotajwa kuwa ofisi zake ziko nje, kwa hali hii mawaziri wanaruka sarakasi na taulo watabaki uchi.Baada ya hapo wakafuata Wenyeviti wa Kamati

John Cheyo:- Alichoguswa zaidi ni kwa jinsi gani wabunge wameungana pamoja bila kujali itikadi zao katika kusimamia matumizi ya pesa za serikali nakuhakikisha kuwa fedha hazipotei kama ilivyo sasa.

Agustino Mrema:- Kuna haja sasa kuhakikisha kwamba kesi hizi zinazo husiana na watu waliotumia vibaya madaraka yao kwa kutafuna fedha za wananchi zinaharakishwa badala ya kusikilizwa kwa muda mrefu kama ilivyo hivi sasa.

Msumari wa Mwisho:Zitto Kabwe:- Yeye akasema huko huko TBS kumekuwa na matatizo mengi lakini bado viongozi wake wamekuwa kimya kunakosekana uwajibikaji akagusia kwamba kama kuna marekebisho mapya yanayopaswa kuwekwa katika katiba hii mpya ni uwajibikaji kwa wale ambao wamefanya vibaya, ambao wamelitia hasara taifa waweze kuwajibika kwa hili sasa akasema wao kama wabunge kuanzia kesho watakusanya saini 70 za wabunge watakaounga mkono hoja itakayoletwa Bungeni ya bunge kutokuwa na imani kwa Waziri mkuu ili jumatatu iwasilishwe. Lengo ni kukomesha ubadhirifu na wizi unaopewa baraka na mawaziri.

Ni kitu Live... leo leo tarehe 19/04/2012

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.