ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 4, 2016

CHEKA UPATE AFYA NA JAMBO NA VIJAMBO

Cheka uapate na vichekesho vya mambo na vijimambo. Vichekesho ambao vimewavuta wengi kwa kipindi fulani na sasa kurudi Live hivi karibuni.

SHULE YAKOSA MADARASA MTWARA.

 Ukosefu wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Sengenya iliopo wilaya ya Nanyumbu umesababisha wanafunzi kurundikana katika madarasa machache yaliyopo shuleni hapo.

JERRY JULIAN + GHUSTLER - YOU ARE THE ONE.

Its a new song with G.hustler and  Jerry Julian. I hope u like it. Have a blessed night. Stay blessed. 

BOFYA PLAY.

JEMBE FM KUNA KITU USIKU HUU.....

.... Weekend is here ARee time zake soma LEBO, wadau wako mtamboni @mbabavc + @johnjackson_jj na JEMBE DjZ wakuitwa @djmike_beatz_ Ukithubutu kusikiliza @jembefm #HUTOBanDuKa yaani fULL kunasa kwani #VyumaVimekaza Kama uko mbali na mkoa wa Mwanza basi 'Tupate popote ulimwenguni kupitia Google play store kwa kusachi JEMBE Fm HD kisha sikiliza LIVE kupitia simu yako ya mkononi AU nenda kwenye TUNe in search JEMBE FM HD kisha sikiliza LIVE'

AIRTEL YATANGAZA WASHINDI WA SHINDANO LA VIDEO BORA IJULIKANAYO KAMA “JICHO LA KITAA”

Jaji wa shindano la jicho la kitaa na mmiliki na mkurugenzi mkuu wa studio ya picha ya I-View,  Raqey Mohamed (katikati) pamoja na jaji na mtayarishaji wa video Hance  Richard (kulia) na Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde, wakiangalia filamu za  washindi wawili kabla ya kutangazwa kuwa washindi.
Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiwapongeza majaji wa shindano la Jicho la Kitaa Raqey Mohamed na Hance  Richard mara baada ya kutangaza washindi wa shindano hilo ambao ni Santos Hillary na Elly EMD

Airtel yatangaza washindi wa shindano la video bora  lijulikanalo kama “Jicho la Kitaa”

·       Washindi wawili wapatikana kila mmoja kajishindia shilingi millioni tano na nafasi ya kwenda kwenye mashindano ya kimataifa nchini Singapore

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza washindi  wawili wa shindano la Jicho la kitaa lililokuwa likiendeshwa kupitia mitandao yake ya kijamii ya faceebook na Instagram na kuwapa nafasi watanzania wenye vipaji vya kutengeneza filamu ya dakika 5 yenye maudhui ya connecting life  yaani kuunganisha jamii kushiriki na kujishindia zawadi nono.

Akitangaza washindi wa jicho la kitaa,  Jaji wa shindano hilo na mmiliki na mkurugenzi mkuu wa studio ya picha ya I-View,  Raqey Mohamed alisema “ shindano la jicho la kitaa limekuwa na ushindani mkubwa,  zaidi ya filamu fupi 120 zimetumwa na tumezipigia zote  na hatimae kupata washindi wawili .  napenda kuwapongeza sana kwa kazi zao nzuri kwa maani huu ndio mwanzo mzuri wa kuinua kazi zao na kuzifikia ndoto zao

Raque aliwataja washindi hao na kusema “ninayofuraha kutangaza washindi wetu ambao ni  Santos Hillary mwenye filamu yake ijulikanayo kama “  uliza kiatu “ na  mshindi wa pili ni  Elly EMD filamu yake inaitwa “Day by Day” nawapongeza sana washindi wetu na wote walioshiriki.”

Kwa upande wake Afisa uhusiano wa Airtel , Bi Jane Matinde alisema “ kila mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 5 pesa taslimu pamoja na kupata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa yanayotegemea kufanyika tarehe 21 mwenzi huu nchni Singapore.

Nawashukuru vijana wenye vipaji walioshiriki katika shindano hili na kuwahasa kuendelea kuchangamkia fursa kama hizi kupitia program zetu mbalimbali kwani ndio mwanzo mzuri wa kuinua vipaji vyao na kuzifikia ndoto zao.

WANAWAKE WAWILI WAKAMATWA LEO JIJINI ARUSHA WAKIIBA KWENYE DUKA LA NGUO.

Picha ikionyesha wamama wawili ambao ni wezi waliokamatwa katika mtaa wa koni Eletronic uliopo  jijini Arusha wakiwa wanaiba katika duka moja la mfanyabiashara wa nguo ambaye akutaka kutajwa jina lake gazetini wakiwa wamezingirwa na wananchi mara baada ya kukutwa wakiwa wanajidai wanataka kununua nguo kumbe wanachagua nguo na kuziweka katika mapochi yao 
makubwa waliobeba, wamama hawa waliambulia kipigo nusu wa chomwe moto lakini walibahatika kusaidiwa na polisi mara baada ya polisi kufika eneo latukio na kuwachukuwa kisha kuwapeleka katika kituo cha polisi.

Na Woinde Shizza, Arusha

Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamama ,wadada kuwa na tabia ya kuingia madukani na kuibia wafanya biashara wanguo pamoja na vipodozi vitu mbalimbali 

hapa nyuma kumekuwepo na malalamiko mengi sana wanayotoa wafanyabiashara hawa kuwa wanakuwa wanaibiwa wengine ambao wamefunga kamera madukani mwao wamekuwa wakirusha picha zinazoonyesha  video za wadada hao wakiwa wanaiba 

hivi leo  kuna kina mama wawili wamekamatwa  katika mtaa wa  koni eltronic ulipo ndani ya jijini Arusha wakiwa wanaiba katika duka la dada mmoja mfanyabiashara wanguo ,na inasemekana hao wamama walikuwa wamezoea kuiba katika duka hilo naweza kusema kuwa walipafanya kama shamba la bibi sasa leo hii wamekamatwa nusu wachomwe

Mmiliki wa libeneke la kaskazini aliweza kuwashuhudia wamama hao wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi huku wakiwa wamezingirwa na wananchi wakiwa wanapigwa vibao na kuaambiwa wanazalilisha wanawake kwa kuwa wezi 

 Wadada hao mara baada ya kukamatwa awali walisema wametokea nchini kenya lakini baadae walibadilika na kusema wametokea mkoani hapa hapa Arusha 

Wananchi wanye asira kali waliwapiga huku wengine wakitaka wachomwe moto ili kukomesha tabia hiyo lakini kabla ya tukio la uchomaji moto kutokea ndipo askari polisi walitokea na kuwachukuwa kisha kuwapeleka kituo cha polisi

ASKWAMBIE MTU "HAUJAFIKA SINGIDA BILA KUFIKA REGENCY HOTEL & RESORT"





















BONUS:-
The prorate at the moment is TZS 80000 for single and TZS 100000 for double , anyone who books for this weekend from your GSENGO BLOG we will be selling at         TZS 70,000 single and TZS 90,000 for double they have to mention they got it from GSENGO blog Through 0769979191  /0672305551 or info@regencyresortsingida.co.tz.

BONASI:-
Bei ya sasa ni TZSh 80,000/= kwa single na TZSh 100,000 kwa double , yeyote atakaye weka booking mwishoni mwa juma hili kupitia blogu hii GSENGO BLOG atapewa punguzo la TZS 70,000 kwa single na TZS 90,000 kwa double kikubwa cha kufanya sema umepata ofa kupitia GSENGO BLOG kupitia simu namba 0769979191  /0672305551 au info@regencyresortsingida.co.tz.

Regency Hotel & Resort Singida

RAIS MAGUFULI ALIPOONGEA NA WANAHABARI.

Rais Magufuli akijibu swali la Dkt. Ayoub Ryoba kuhusu kujitathmini toka alipongia madarakani mwaka jana. 

Rais Magufuli Akijibu Swali Kuhusu Rushwa Na Ufisadi Nchini.
Rais Magufuli akifafanunua juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kupambana na rushwa na ufisadi nchini pamoja na madawa ya kulevya.
Tanzania Ya Viwanda.
Kauli Ya Rais Magufuli kuhusu serikali ya awamu ya tano kutimiza ndoto ya Tanzania ya viwanda kwa uchumi bora wa nchiFahamu kauli ya Rais John Magufuli kuhusu suala la ajira mpya wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Ikulu Dar es Salaam. 
Waandishi Watakiwa Kutumia Vizuri Kalamu Zao.
Rais Magufuli akiwataka wanahabari nchini kutumia vyema kalamu zao kuchagiza shughuli za kimandeleo nchini. 
Rais Magufuli Na Michezo Nchini.
Fahamu kauli ya Rais Magufuli kuhusu suala la michezo nchini wakati wa mkutano wake na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

MAHAKAMA KUU YAAMURU TUNDU LISSU AKAMATWE, KITIMTIM WABUNGE WAKITUHUMIANA RUSHWA BIL 2.7, MAGUFULI ARUKA KIUNZI KIGUMU.


Mahakama yaamuru Tundu Lissu akamatwe, Kitimtim wabunge wakituhumiana rushwa Bil. 2.7,  Rais Magufuli aruka kiunzi kigumu. Pata undani wa dondoo hizi za magazeti hapa; 


Wabunge CCM wahongwa, Utata mrembo Arusha alivyobakwa hadi kufa, Maalim akataza ziara za Lipumba, Mbowe azua taharuki. 


Kiwewe polisi kuondoka DCI, Lema akamatwa Dodoma awekwa rumande Arusha, Mbowe achafua hewa Bungeni. 

Thursday, November 3, 2016

BONUS NYINGINE YA HABARI ZA MICHEZO NDANI YA JEMBE FM.

.......Baada ya kukushika vilivyo mdau wetu kupitia kipindi chako cha #SPORTSRIPOTI ya JEMBE FM kinachoruka saa 3 hadi 4 usiku. Sasa kamata nyongeza nyingine ya habari na uchambuzi wa kispoti toka kwetu. Kwa style mpyaaaa yenye mvuto wa kipekee. Kila jumamosi saa 2 kamili hadi 4 asubuhi, #SPORTSRIPOTI ikibaki pale pale Ungana na @jumaayoo + @elikanamathias featuring @gsengo

SHEHENA YA MBAO NA MAGOGO YANASWA TONGWE MASHARIKI.

Usiku wa kiasi cha saa 5 mwishoni mwa juma lililopita Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano akiambatana na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mhe. Salehe Mhando walikuwa kwenye oparesheni ya kukamata utoroshaji wa mbao na magogo ktk msitu wa mbao wa Tongwe Mashariki ambapo asubuhi yake ilithibitika kukamatwa kwa shehena kubwa ya Magogo pamoja na mbao.

Mhe Salehe Mhando Mkuu Wa wilaya ya Tanganyika akiwa na Waziri Wa Nchi ofisi ya makamu Wa Rais (mazingira na muungano) akimuonyesha njia za vichochoro ambazo hutumiwa na watoroshaji wakati akiwa ziarani wilayani hapo mwishoni mwa wiki.

PSehemu ya shehena ambayo ilikuwa imefichwa porini tayari kupakiwa na kusafirishwa.
Mhe Salehe Mhando Mkuu Wa wilaya ya Tanganyika akitia msisitizo juu ya katazo la serikali na suala la ulinzi shirikishi.
Pia tumekamata malori mawili kati ya matano yaliyopo msituni. Tunaendelea kuyasaka mpaka yapatikane. Kuna ufisadi wa kutisha ktk misitu yetu.

Watu wachache waliigeuza wilaya ya Tanganyika kama shamba la bibi! Sasa kazi tu!

"Kwa tathimini ya haraka huu mzigo tulioukamata unathamani ya zaidi ya sh.Mil 123"
"Unaweza kujiuliza kwa miaka miwili mitatu nyuma ni kiasi gani cha fedha kimenufaisha Mafisadi wachache na kuwaacha watanzania wenzao wakiendelea kukosa huduma za Jamii. Hapa hakuna namna naomba tuombeane sana ktk shughuli hii nzito!"

SIRI NZITO:- BINTI WA CHUO KIKUU ALIYEBAKWA HADI KUFA, ALIKUWA NA KIPAJI CHA SANAA HATARI.

INASIKITISHA SANA: Binti mmoja ambaye ni model na mwimbaji wa muziki aliyetambulika kwa jina la JULIANA ISAWAFO (pichani) ambaye picha yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia jana ikionyesha mwili wake ukiwa umetupwa eneo la Ndoro nje kidogo ya Chuo Kikuu cha Makumira, Arusha baada ya kudaiwa kubakwa na watu wasiojulikana.
Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, (jina lake halikufahamika mara moja) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa ameokotwa majira ya saa tano asubuhi jana akiwa amekufa na mwili wake kutelekezwa kwenye shamba la mpunga nje kidogo ya eneo la chuo hicho.
Mbali na kuthibitisha kifo hicho, kiongozi huyo ameeleza pia kuwa, msichana huyo ni mwanafamilia wa Chuo cha Makumira ila hakuwa mwanafunzi rasmi kama watu wanavyodai. 
Taarifa za awali zilieleza kwamba usiku wa kuamkia tarehe 2 Novemba, Juliana alikwenda kwenye “birthday party” katika Lodge moja maeneo ya mkabala na Chuo cha Tumaini Makumira pembezoni mwa barabara ya Moshi – Arusha, lakini asubuhi yake mwili wake ndipo ukakutwa katika mashamba hayo ya mpunga ambayo yapo kati ya barabara hiyo ya Moshi – Arusha na lodge ambayo birthday hiyo ilifanyika. Chini ni picha mbalimbali za Juliana enzi za uhai wake.
Juliana na hisia kutoka moyoni.

Ameongeza pia kuwa, msichana huyo alikuwa akiishi ndani ya eneo la chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja wa walimu wa Sanaa chuoni hapo.
Mwisho akaeleza hisia zake namna ambavyo familia ya chuo hicho ilivyoguswa na msiba huo kwani msichana huyo alikuwa kama dancer wa matamasha mbalimbali ya Chuo cha Makumira.

OLE MEDEYE AFUNGUKA JUU YA HALI YA UCHUMI SERIKALI YA MAGUFULI, VIPI HAMAHAMA YAKE VYAMA...?

🌀... Katibu Mkuu wa sasa UDP Goodluck Ole medeye hii leo amejibu maswali mawili ya kipindi cha #KAZINANGOMA

1.Anazungumziaje hali ya uchumi nchini Tanzania Jeh kuna ahueni, afadhali, tunapanda au tunashuka?
2.Vipi katabia kakE ka kuhamahama vyama toka CCM, majuzi kati CHADEMA na hatimaye UDP sasa.....!!?

#KAZINANGOMA ina majibu @mansourjumanne @gsengo na wakung'ata @djscopion

BOFYA PLAY KUMSIKILIZA

Wednesday, November 2, 2016