BRAD GOLDAN – Afisa mtendaji mkuu African Barrick Gold Mining. |
KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya dhahabu
African Barrick Gold Mining (ABG), mwaka
huu inatarajia kuwapunguza kazi wataalamu kadhaa wa kigeni kutoka mataifa
mbalimbali Duniani ili kufungua milango ya ajira kwa watanzania hususani vijana.
Kampuni hiyo imetangaza uamuzi huo Jijini
Mwanza katika mkutano wa wadau wa sekta ya madini, baada ya takwimu za Wizara
ya kazi na ajira kuonyesha kuwa zaidi ya asilimia 11% ya vijana, waliohitimu
katika vyuo mbalimbali hapa nchini hawana ajira za uhakika.
Katika mkutano huo Afisa mtendaji mkuu
wa (ABG) Brad Goldan amewaambia wadau hao kuwa kutokana na uzito wa tatizo hilo
tayari kampuni hiyo imeshawapunguza kazi wataalamu 121 kati ya 411 ili kutoa
nafasi za ajira kwa watanzania.
Hadi sasa Takwimu zinaonyesha kuwa vijana walioajiriwa wenye umri kati ya miaka 15 hadi 34 ni 9,056,217 wakati idadi ya vijana wasiokuwa na ajira ikionyesha kuwa 1,398,677 na kusababisha ongezeko la watu wasiokuwa na ajira Duniani kufikia million 74.6.

Ni sehemu ya kusanyiko la wadau wa sekta ya madini walio jitokeza katika mkutano huu ulio fanyika hii leo mchana ukumbi wa Hotel malaika jijini Mwanza. |
Wadau wakichukuwa data. |
ANTONY DIALO – Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza. |
Ushauri WA WADAU HAO umefuata baada ya taarifa ya Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni hiyo Brad Goldan kueleza kuwa Kampuni hiyo imeshindwa kulipa kodi katika kipindi cha mwaka 2002 hadi 2006 baada ya serikali kuchelewa kuwasilisha notisi ya madai.
Mikakati ya Kampuni ya African Barrick Gold Mining kuwekeza kwa wafanyakazi wazalendo zaidi imekuja wakati Kampuni hiyo ikiwa bado inasuasua katika suala la ulipaji kodi, hivyo kuikosesha serikali mapato ambayo yangeinufaisha katika mikakati yake ya kuboresha huduma za jamii. Nao wadau wa mkutano wa sekta ya madini hawakubaki nyuma kutumia fursa hiyo kuishauri (ABG) kujikita katika shughuli za kijamii na kuzingatia ulipaji wa kodi kwa wakati.

Naye blooger wa blogu ya Maarufu ya Kanda ya ziwa inayojulikana kwa jina la Kijukuu Blog (kulia) naye alikuwa sehemu ya wadau na hapa kwa umakiiiiini akichukuwa data na taarifa mbalimbali. |
Meza kuu wadau wa ABG. |
ATHUMANI AKARAMA – Mkurugenzi halmashauri ya Manispaa ya Tarime akichangia . |
PATRICK KALANGWA – Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Msalala mkoani Shinyanga. |
DEO MWANYIKA – Makamu wa Rais African Barrick Gold Mining. |
Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Deo Mwanyika anasema katika kutekeleza azma hiyo tayari asilimia 60% ya watanzania wapo katika mataifa mbalimbali Duniani wakisoma masomo maalumu ya ufundi ili waweze kuziba nafasi hizo. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.