Fainali ya michuano hiyo itapigwa katika uwanja jijini Lisbon wa Estadio da Luz tarehe 24 mwezi Mei.Mechi zao za mzunguko wa kwanza zitaanza tarehe 1 mpaka 2 mwezi Aprili na marudiano yatakuwa tarehe 8-9 Aprili.
Mabingwa wa ligi ya Uhispania, Barcelona watapambana na Atletico Madrid, huku Real Madrid ikipangwa kukutana na Borussia Dortmund.Chelsea inayoongoza kwenye msimamo wa ligi itaifuata PSG nchini Ufaransa katika mzunguko wa kwanza.
Manchester na Bayern wanakutana tena tangu mwaka 1999 kwenye fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, ambapo Ole Gunnar Solkjaer na Teddy Sheringham waliiwezesha Manchester kutwaa kikombe chini ya Kocha wao Alex Ferguson.
Mara baada ya kupangwa kwa timu hizo nchini Switzerland, kiungo mshambuliaji wa Bayern, Philipp Lahm amesema kuwa hawawezi kutetereshwa na nafasi waliyonayo United kwa sasa katika ligi kuu na kusema kuwa watasafiri mpaka Manchester kwa kazi moja tu, nayo ni kufunga magoli. THANX 2 BBC SWAHILI.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.