SERIKALI imesimamisha mauzo ya korosho hadi tarehe 30 mwezi huu itakapo tangaza tarehe mpya ya kuanza mauzo ya zao hilo kwa msimu wa 2018/2019.
Agizo hilo limetolewa leo na waziri mkuu waJamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa katika manispaa ya Lindi alipozungumza na viongozi wa vyama vya ushirika,wakuu wa mikoa,warajisi wasaidizi,mameneja wa vyama vikuu ya ushirika wa mikoa ya Lindi,Pwani,Mtwara na Ruvuma.
Waziri mkuu Majaliwa ambaye alifikia uamuzi huo kwaniaba ya serikali kufuatia sintofahamu iliyojitokeza kutokana na mwenendo wa mauzo wa zao hilo ambao umesababisha wakulima kugomea kuuza korosho zao kwa bei zinazopangwa na wanunuzi katika minada yote iliyofanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Aliwaomba wananchi wawe watulivu kwani nia ya serikali kusimamisha ununuzi huo ni njema.Kwahiyo wavute subira hadi tarehe 30 mwezi huu itakapo watakapotangaziwa tarehe ya kuanza upya ununuzi.Kwani katika kipindi ambacho minada haitafanyika,serikali itakuwa inafanya utafiti kuhusu masoko na utaratibu utakaotumika kununua zao hilo.
Majaliwa alisema awali zao hilo lilikumbwa na matatizo mengi yaliyohusu utaratibu wa mauzo.Ambayo yalitoa mianya kwa wanunuzi kuwadhulumu wakulima.Hata hivyo serikali iliyafanyia kazi.Hali ambayo ilisababisha mwenendo wa mauzo yake kuwa mzuri na wakulima walianza kunufaika na jasho lao.
Alisema serikali ilibaini matatizo ambayo yalisababisha wakulima wengi kuanza kuacha kulima na kuzalisha zao hilo.Hivyo ilifanya marekebisho makubwa.Yakiwamo ya mwaka 2014 ambayo yalisababisha kiwango cha uzalishaji na bei ya zao hilo kuongezeka kila msimu.
Waziri mkuu Majaliwa aliweka wazi kwamba misimu ya 2016/2017 na 2017/2018 bei ya korosho ilikuwa mzuri.Hata hivyo alianza kupata mashaka kwa msimu wa 2018/2019.Kwani hata bei iliyotangazwa na bodi ya korosho ya shilingi 1550 ilikuwa ndogo ikilinganishwa na bei ya juu ya sokoni ya msimu uliopita.Ambapo kilo moja ilifikia kununuliwa kwa shilingi 4000.
Majaliwa alihoji sababu zilizosababisha bodi ya korosho kwa kushirikiana na wizara yenye dhamana ya kilimo kuweka bei elekezi ndogo ambayo imetoa mwanya kwa wanunuzi kununua kwa bei ndogo zao hilo tofauti na msimu uliopita.Akiweka wazi kwamba walifanya hivyo kwa nia isiyo njema kwa wakulima kama inavyotokea sasa.
Waziri mkuu alishangazwa na kimya cha wizara ya kilimo kwakitendo cha kutoonesha jitihada zozote za kutafuta na kuwapa majawabu sahihi wakulima ambao nikama wamekosa mtetezi.Kiasi cha kujitetea wenyewe kwa kugoma kuuza korosho zao.Hivyo aliitaka wizara hiyo ijitathimini kuhusiana na yanayoendelea sasa.
Katika hali ya masikitiko waziri mkuu Majaliwa alishangaa kuona mfumo na utaratibu wa ununuzi wa zao hilo nitofauti na misimu iliyopita.Japokuwa yeye alipokutana na wadau wa zao hilo,akiwemo waziri wa kilimo,Charles Tizeba mjini Mtwara walikubaliana utumike mfumo na utaratibu ulitumika msimu uliopita.
"Lakini nimesikia kwamba waziri na nyinyi watu wabodi mlisema mfumo mpya ambao umeleta matatizo umeridhiwa na mheshimiwa Rais nakwamba hakuna anaweza kupinga agizo la Rais.Huko nikumchafua mheshimiwa Rais,makamo wa Rais na hata mimi msaidizi wao,"alisema Majaliwa.
Alibainisha kwamba Rais hakuagiza utumike mfumo na utaratibu mpya.Kwasababu haujui hata mfumo wa zamani na amekataa kuwa aliagiza.Hivyo jina lake linatumiwa vibaya.Tabia ambayo imeanza kushika kasi kwa watu wachini kutumia majina ya viongozi wa kuu wa nchi kwamba wanayofanya yanabaraka zao.
"Katika hilo mheshimiwa Rais ameniagiza kwamba mtu yeyote atayetumia jina lake kwamba anayofanya yametokana na magizo yake akamatwe.Kwasababu anataka kumchafua,"alisisitiza Majaliwa.
Alisema serikali ilibaini siku za nyuma kulikuwa na mchezo mchafu uliokuwa unafanywa na watu waliopewa dhamana ya kusimamia masilahi ya wakulima.Ndipo ilipoamua kuvunja bodi za mazao zilizokuwepo.Hali ambayo ilisababisha mafanikio ambayo yanataka kuvurugwa na baadhi ya watu waliopewa dhamana ya kusimamia masilahi ya wakulima.Kitendo ambacho hakikubaliki katika serikali ya awamu hii ya tano.
Waziri mkuu alisema sababu za kubadilisha mfumo na utaratibu wa ununuzi wa zao hilo ambao ulitumika misimu iliyopita hazikuwa na ukweli.Kwani miongoni mwa sababu zilizotolewa nikwamba ulikuwa unasababisha kufanyika rushwa baina ya viongozi wa vyama vikuu vya ushirika na wafanyabiashara.Wakati hakuna hata kiongozi mmoja aliyewahi kukamatwa kwa tuhuma hizo.
"Viongozi wanamgapi wa vyama walikamatwa.Wanakataa kuuza kwa bei ndogo mnawatisha kwa mitutu ya bunduki,mfumo mnaolazimisha tulicha kwasababu ulisababisha matatizo.Sasa mnataka kurudisha nyuma,"alisema kwa ukali Majaliwa.
Kaimu mkurugenzi wa bodi ya korosho yamkuta asiyo yatarajia.
Mbali na kutoa agizo hilo na mengine mengi nadani ya kikao hicho.Majaliwa akimgeukia kaimu mkurugenzi mkuu wa hbodi ya korosho(CBT),profesa Wakuru Magii ambae kabla kwenye mkutano huo alishushiwa tuhuma nyingi na wakuu wa mikoa ya Lindi na Mtwara(Godfrey Zambi na Glasious Byakanwa.
Majaliwa alimuuliza kaimu mkugenzi huyo sababu za wakulima kukubali kuuza korosho kwa being ya chini kwenye mnada uliofanyika jana wakati walikataa bei kubwa zaidi ya hizo za Jana.Huku akiwa amenyamaza kimya wakati mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika aliyekuwa kwenye mnada huo akilazimishwa na asikari asaini fomu kuridhia kwamba wakulima waliliridhika kuuza korosho zao.
Lakini pia waziri mkuu alimshangaa kaimu mkurugenzi huyo kwakitendo chake cha kumpigia simu katibu mkuu wa CCM,Dkt Bashiru Alli kwamba alisitisha minada kwasababu anakampuni zake.Lakini pia alimpigia simu mkuu wa jeshi la polisi nchini,Simon Siro nakumueleza tuhuma kama hizo.Jambo ambalo halina ukweli.Bali alifanya hivyo ilikutimiza wajibu wake wakuwasimamia masilahi y wakulima.Tena sio wakorosho peke yake bali wa mazao yote.
Kufuatia tuhuma mbalimbali zilizotolewa na wakuu hao wa mikoa na viongozi wa vyama vikuu vya ushirika vya TANECU na Lindi Mwambao ambazo kaimu mkurugenzi huyo alishindwa kukanusha.Waziri mkuu alifikia uamuzi wa kumrejesha wizarani.
Mkutano huo uliitishwa na waziri mkuu mwenyewe ili kutafuta suluhisho la kudumu kutokana na matatizo yaliyojitokeza katika msimu huu tangu kuanza ununuzi wa zao hilo.