Wasichana zaidi ya 2300 kutoka shule 15 za sekondari za wilaya ya Kahama katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga wamepewa taulo takriani (pedi) 2300 na shirika la Amref health Afrika ,ikiwa na lengo la kuhamasisha wanafunzi hao kuhudhuria masomo pindi wawapo katika siku zao.
Katika semina iliyowahusisha taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo madawati ya jinsi,na idara ya ustawi ya jamii ya halmashauri hiyo ,mratibu wa mradi huo kutoka shirika la Amref health Africa Gaspery Misungwi amesema shirika hilo limelenga kutatua changamoto za Afya katika wilaya hiyo pamoja na kuboresha elimu ya wasichana hao kwa kuwapatia taulo hizo.
Hii ni miuongoni mwa jitihada za kuboresha sekta ya Afya katika mikoa ya Kanda ya ziwa hususani mkoa wa Shinyanga zinazofanywa na shirika la Amref Health Afrika Baada ya lile la BORESHA CHANJO mradi unaotumia teknolojia ya simu za mkononi na kompyuta katika kuratibu maswala ya chanjo katika wilaya mbalimbali za kanda ya ziwa.
Mratibu wa mradi huo kutoka shirika la Amref health Africa Gaspery Misungwi akiwasilisha dhumuni la kusanyiko, mipango ya baadaye pamoja na malengo ya mradi.
Kusanyiko la semina kutoka shirika la Amref health Africa.
Wadau washirika wakifuatilia kwa umakini yanyoendelea kujiri katika Semina hiyo.
Darasa na umakini.
Hatua kwa hatua wadau wa semina wakiendelea kuchukuwa pointi.
Wadau toka taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo madawati ya jinsi, na idara ya ustawi ya jamii ya halmashauri ya wilaya ya Misungwi wakiwa wamejumuika na wanafunzi kusikiliza na kuchangia yale yanayowasilishwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.