ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Wakati Tanzania inaendelea na jitihada zake za kupanua soko na kuvutia watalii wengi, wakati ambao mchango wa sekta ya utalii katika uchumi wa Taifa unazidi kupaa kila mwaka, Wananchi wametakiwa kutambua umuhimu wa utalii wa ndani kwa kujenga desturi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Kulingana na takwimu za Wizara ya Maliasili na Utalii, sekta hiyo inachangia takriban asilimia 17.2 ya Pato la Taifa (GDP) na zaidi ya robo (asilimia 25) ya mapato yote ya fedha za kigeni. Pia inachangia zaidi ya asilimia 10 ya ajira zote nchini ambapo ajira za moja kwa moja ni 500,000 na ajira takribani millioni moja zisizo za moja kwa moja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.