ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 30, 2011

WACHUNGAJI MWANZA WAAHIDI KUWALINDA ALBINO.

Wachungaji jijini Mwanza leo wamepata fursa ya kuitazama filamu ya mauaji ya waafrika wenye ulemavu wa ngozi inayoitwa WHITE & BLACK nao kwa kauli moja kuahidi kuendelea kutoa elimu sambamba na kuwalinda albino dhidi ya vitendo vya mauaji na ukatili dhidi yao.Kiongozi wa mpango huo wa utoaji elimu na usaidizi kwa walemavu wa ngozi 'Under the same sun' bwana Peter Ash na Mchungaji kiongozi wakiwa wameshikilia moja ya machapisho wakati kiongozi huyo akitoa maelezo kwa washiriki juu ya mikakati iliyopo ili kuleta mabadiliko.

Ili kudhihirisha kuwa bado sakata la mauaji dhidi ya ndugu zetu albino bado linaendelea ndani ya jamii yetu, huko wilayani Ukerewe mkoani Mwanza mama Sabina wa mtoto huyu mwenye ulemavu wa ngozi aitwae Mei mosi, ndani ya mwezi mmoja uliopita amenusurika mara mbili kuuawa na watu waliokuwa wakitaka kumkatakata mwanae ili wachukuwe viungo vyake.

Mara baada ya kuitizama filamu hiyo viongozi hao wa dini walipata fursa kuuliza maswali uongozi wa UTSS pamoja na kuchangia mawazo juu ya nini kifanyike kuondoa fikra za imani potofu dhidi ya albino, zilizoganda kwenye vichwa vya baadhi ya watanzania.

Mratibu wa shirika hilo Vicky Ntetema aliwazawadia DVD za lugha mbalimbali pamoja na kalenda kwa kila kiongozi wa dini aliyehudhuria kusanyiko hilo.

Under The Same Sun (UTSS) imeanzishwa ili kuinua hali ya maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kuwapa fursa ya elimu wale wasio na uwezo na ambao hawapewi hadhi wanayostahili.

Mie na dada Vicky.
Tunaongozwa na imani kwamba watu wote tumeumbwa kwa mfano wa mungu na kwamba tunayo thamani inayolingana na tunastahili kupendwa na kusaidiwa.Together we can change the mindset of society on albinism.

VODACOM MISS TANZANIA YAZINDULIWA RASMI

Mkurugenzi wa Miss Tanzania Hashimu Lundenga akipiga makofi kushangilia uzinduzi rasmi ya Nembo mpya ya Vodacom Miss Tanzania pamoja na uzinduzi wa mashindano hayo kwa mwaka 2011, shughuli iliyofanyika katika Hotel Kempnisky jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wanakamati wa Vodacom Miss Tanzania pamoja na wadhamini wa wakuu wa shindano hilo na warembo walioshiriki mashindano hayo miaka ya nyuma katika picha ya pamoja.

Picha zote kwa hisani ya JIACHIE.

WATANZANIA LEO KAZI NI MOJA TU!

Leo kazi ni moja tu. Kila Mtanzania atakayekwenda Uwanja wa Taifa, anataka kuona Waganda, The Cobs wakitoka uwanjani vichwa chini kama ilivyokuwa Cameroon, katika mchezo wa marudiano wa kuwania kucheza Michezo ya Afrika itakayofanyika baadaye Septemba, Maputo Msumbiji.

Mchezaji wa timu ya Vijana ya Manyara Stars Mbwana Samata (kushoto) akimpiga chenga Idrisa Abdulahim, kwenye mazoezi.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Kampala, Uganda ilishinda mabao 2-1, hivyo vijana wa Tanzania leo wanahitaji ushindi wa bao 1-0 waweze kusonga mbele.

Kocha wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo 'Julio' alisema jana kuwa hana cha zaidi ya kuona timu hiyo inafanya vizuri katika mchezo huo. "Unajua mimi kawaida yangu namalizia nyumbani wao wanatambia kwao na mimi nikija kwangu natamba, sasa bora aliyeanza kwake," alisema Kihwelo.

Kihwelu alisisitiza kuwa kikosi chake kiko fiti kisaikolojia na kila mchezaji amejiandaa kwa ushindi na zaidi aliwaomba mashabiki kuishangilia kwa nguvu timu hiyo kama ilivyokuwa mchezo wake na Cameroon kuwania kucheza Michezo ya Olimpiki mwakani jijini London.

Friday, April 29, 2011

'STONE CLUB' MWANZA WIKI HII.. EH BANA DAH!!

Wiki hii nDANi ya sTONe cLUb mWANZa ni full cAlAz zA The 'UTAMU' pANa sHINe hAINa kWIKWi yAANi ni sOOo kUDADADEKi nI dISCo la mWISHo wA mWEZi*** kIINGILIo ni kILEKILe kAMa kWa bABu Loliondo sHILINGi 500 ongeza sIFURi mBELe, uKIVUNGa hUJAIONa hII sIKIDOGo iMEKULa kWAKo jOMBAa.

PRINCE WILLIAM NA KATE SASA NI WANA NDOA KAMILI

Tabasamu la ukweli limetawala kwa wapenzi wawili Prince William na Kate Middleton mara baada ya ndoa yao takatifu kufungwa katika kanisa la Westminster Abbey, mjini London ikiwa ni mbele ya mashuhuda waalikwa wapatao 1,900 na watu takribani bilioni 2 walioshuhudia tukio hilo sehemu mbalimbali duniani kupitia luninga zao.

Maharusi hao walishangiliwa na maelfu ya watu waliojipanga barabarani kuelekea kasri ya Buckingham Palace ambako Malkia amewaandalia karamu wageni 650.


Mwana mfalme William akifungishwa ndoa na Aksofu Rowan William katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.

Wana ndoa hao wapya walitumia gari liliovutwa na farasi la muundo wa mwaka 1902 ambalo lilitumiwa na wazazi wake Prince William wakati wa ndoa yao mwaka 1981 ambapo baadae maharusi hao walijitokeza kwenye roshani ya kasri ya Buckingham na kuwasalimu maelfu ya watu waliokwenda kuwasherehekea.

Si wawili tena bali ni mwili mmoja.
Baada ya kulishana viapo vya ndoa Askofu mkuu wa Canterbury, Rowan Williams, aliwanadi rasmi kuwa "mume na mke". Kuanzia sasa maharusi hawa watajulikana rasmi kama Duke na Duchess wa Cambridge.

KATIKA KUELEKEA KILI TAIFA CUP TBL WACHANGIA MAANDALIZI YA MWANZA HEROUS.

Meneja wa mauzo wa kampuni ya bia Tanzania TBL tawi la Mwanza bw. Maliki Sitaki akikabidhi fedha taslimu shilingi milioni 1.5 kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Abass Kandoro kama sehemu ya mchango wa kampuni yake kusaidia maandalizi ya awali kwa timu ya mkoa wa Mwanza (Mwanza Herous) itakayoshiriki michuano ya ligi ya Taifa inayotaraji kuanza kutimua vumbi may 7/2011.

Meneja wa mauzo na usambazaji TBL kanda ya ziwa Malaki Sitaki (aliyesimama), pembeni yake ni Special Event Manager wa kampuni hiyo Erick Mwayela na mwisho kabisa ni Katibu tawala mkoa wa Mwanza Bi. Dorothy Mwanyika. Jumla ya timu 23 za mikoa mbalimbali hapa nchini zimepangwa kushiriki michuano ya Kili Taifa Cup 2011 kwa makundi sita ambapo kila mkoa umetengewa fungu lake kwa ajili ya maandalizi ya awali.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mchango huo na kisha kuuwasilisha papo hapo kwa mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mwanza (MZFA) Jackson Songora, mkuu wa mkoa wa Mwanza Abass Kandoro amesema ofisi yake itatoa shilingi milioni moja kuchangia maandalizi hayo ambapo mpaka sasa jumla ya shilingi milioni 3.8 zinahitajika kwenye bajeti ya shilingi milioni 7 iliyowekwa.

Pia mkuu huyo ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo, mashirika binafsi na wafanyabiashara wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi kuisaidia timu hiyo ili ishiriki vyema kwenye mashindano hayo na hatimaye ipate ushindi.

Awali mashindano hayo soka ya Taifa Cup ndani ya TBL yalikuwa yakidhaminiwa na bia ya Safari Lager ambapo kampuni hiyo baadae katika maamuzi yake na sababu maalum iliamua kuhamisha udhamini wa michuano hiyo kwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

FILAMU YA MAUAJI YA ALBINO YAZINDULIWA.

Filamu ya mauaji ya waafrika wenye ulemavu wa ngozi imezinduliwa rasmi jana katika ukumbi wa Nyumbani Hotel jijini Mwanza .Ni filamu iliyo katika muundo wa makala imetengenezwa kwa lengo la kuelimisha jamii kuziepuka mila potofu kwamba viungo vya albino ni dawa ya bahati sambamba na kupaza sauti kufichua ubaguzi uliopo juu ya watu wenye ulemavu huo.

Rais wa shirika la kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi linalofahamika kwa jina la UNDER THE SAME SUN, Peter Ash akiwa na mratibu wa shirika hilo hapa nchini Vick Ntetema wakizungumza na wadau toka makundi mbalimbali ya kijamii ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari walioalikwa kwenye kusanyiko hilo la kuitambulisha filamu hiyo sambamba na kuijadili elimu itokayo filamuni.

Mwenyekiti wa chama cha wenye ulemavu wa ngozi mkoani Mwanza akizungumza wakati wa ufanguzi wa kusanyiko hilo.

Kupitia mauaji ya albino yaliyozuka hivi karibuni na kuumiza ulimwengu, familia nyingi zimepoteza watoto wao na ndugu zao, mfano hai ni Babu na bibi Letisia (kushoto) wa kijiji cha Kashindaga ambao walimpoteza mjukuu wao aitwae Letisia, kulia ni Mama Manyashi na mumewe wa sasa ambaye mtoto wake aliuawa kwa kukatwa mapanga baada ya mumewe wa awali kushiriki kutimiza mauaji hayo kwa kulipwa kiasi cha shilingi laki mbili ili wauaji wachukuwe viungo vya mwanae Yunis.

Sehemu ya filamu hiyo ikimuonyesha babu yake Letisia akielekeza mahala alipomzika mjukuu wake chini ya kitanda chake, na amefanya hivyo kwani kulikuwa na mtindo wa watu kufukuwa makaburi ya albino na kuchukuwa viongo.

Katika sakata hili linalohusisha imani za kishirikina nao waganga wakienyeji wakitajwa kuwa ni kichocheo kikubwa, ni wengi wamepoteza maisha yao na wengi wamenusurika huku wengine wakibakiwa na ulemavu wa kudumu na makovu yasiyoisha.

Sehemu ya filamu...
"Tunataka mauaji yakomeshwe na haki itendeke kwa wavulana na wasichana waliopoteza maisha yao kwa kuchinjwa kinyama"

Mkutano ukiendelea.

M-blogishaji maarufu nchini kupitia blogu ya MTAA KWA MTAA anaitwa Othman Michuzi akihusika kikamilifu kupasha habari kwa umma kupitia mtandao wake.

Elimu ipanuliwe kwa watu, kisha akatumia na mistari ya biblia soma Yohana 10:10, Mathayo 11:28. Mwanachuo kutoka chuo cha SAUTI Mwanza Monalisa Juma wakati akichangia mawazo mara baada ya kuiona filamu.

Wakuu wa vikundi vya dini mbalimbali nao walikuwa sehemu ya waalikwa.

Picha ya pamoja nami.
Filamu hii imehusisha zaidi watu ambao maelezo yao ni ushuhuda wa ujasiri na ukakamavu wa mwanadamu ambaye anatumika kupaza sauti na kufichua undani wa yale maovu yanayotendeka kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi.

Thursday, April 28, 2011

MAANDALIZI HARUSI YA KIFALME, UINGEREZA

Mapema leo mjini London kumepambazuka huku kukiwa na shamrashamra za kupindukia na ubize wa ajabu sambamba na matayarisho hayo vikosi vya jeshi la uingereza vilifanya mazoezi ya parade maalum kujiandaa na sherehe za harusi ya mwana wa mfalme.Maharusi.
Nchini Uingereza inshu kubwa inayopamba vinywa vya watu, magazeti na vyombo mbalimbali vya habari ni maandalizi ya harusi ya Kifalme kati ya Kate na William itakayofanyika kesho Aprili 29, 2011.

Organist and Master wa kwaya ya James O'Donnell akiongoza kwaya ya watoto walio mahiri katika uimbaji wa kanisa la Westminster Abbey inayotegemewa kutumika kwenye ibada ya kesho harusini, inatajwa kuwa Prince William ndiye aliyeichagua kwaya hii.

Sherehe hizo za harusi zimepambwa na maandalizi ya kufufuka mtu kwani kila kinachofanyika na kuhusishwa na tukio hilo kimegeuka dili.

Kwa ukakamavu wakipiga kwata nje ya Westminster Abbey ni jeshi la kikosi cha wanamaji.

Farasi.

As the horses walked through the parade ground at Horse Guards, clouds of dust kicked up covering the Welsh Guards, who were lining that part of the procession

Mtihani wa harusi.
Ili kuhakikisha kwamba kila jambo linakwenda kiuhakika zoezi linaendeshwa huku mkaguzi akichukuwa maelezo juu ya nini kibadilishwe kupitia kasoro zinazojitokeza na hata nini kiongezeke katika kuboresha nakuifanya harusi ya kiwango.

Mfanyabiashara John Loughrey (56) amekuwa mfanyabiashara wa kwanza kuweka kambi katika mji wa Westminster Abbey kuuza bidhaa zenye picha na maandiko ya maharusi pamoja na vitambaa na bendera maalum alivyobuni.

FANTASTIC MOMENTiZ

Fantastic pic.

Wasiwasi akiwa amekamatilia 'mdundo' bila wasiwasi...

"Habhari yako binafsi bhana!" Ni Chacha Kimori na Sis Kunda.

Ilikuwa ni sebene kwaito au kiduku? mdau kazi kwako kudadavua.

Mabeste' Kuanzia shoto Frank Pangani, Dj Cutter, Dizzo M, Daudi Tec, Wasiwasi Mwabulambo wa habari bila wasiwasi na Alex Luambano wa Sports Extra..

MRITHI WA TIDO TBC APATIKANA

RAIS Jakaya Kikwete amemteua Clement Mshana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Tido Mhando.Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema kwamba Mshana ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo). Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dunstan Tido Mhando ambaye amemaliza muda wake wa utumishi kwa mujibu wa mkataba wake.

Hata hivyo, Tido aliwahi kukaririwa akilalamika kwamba licha ya mkataba huo kumalizika, hakupewa fursa ya kujadiliana na mwajiri wake ili kuuongeza.

Mbali ya uteuzi huo, Rais Kikwete pia amewateua manaibu katibu wakuu 10 katika wizara mbalimbali. Miongoni mwa walioteuliwa ni Bashir Mrindoko ambaye sasa anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Kamishna wa Nishati na Mafuta ya Petroli.

Pia amemteua Mhandisi John Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi. Awali, alikuwa ni Mkurugenzi wa Ufundi na Umeme wizarani hapo.Wengine walioteuliwa na nafasi zao za zamani katika mabano ni Charles Pallangyo, Naibu

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Mkurugenzi wa Uratibu wa ofisi hiyo). Mhandisi Mwamini Malemi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Msaidizi wa Makamu wa Rais, Maendeleo ya Jamii na Uratibu wa Malalamiko ya Wananchi).

Mhandisi Musa Iyombe, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi (Mkurugenzi wa Miundombinu ya Usafiri, Wizara ya Ujenzi). James Mngodo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi (Mkurugenzi wa Uhakika wa Chakula), Anna Maembe, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (Mkurugenzi wa Mazingira na Habari wa Baraza la Taifa la Mazingira-NEMC).

Sihaba Nkinga, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, (Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Uchukuzi.) Aphayo Kidawa, Naibu Katibu Mkuu, Ikulu (Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi). Habib Mkwizu, Naibu Katibu Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Karani katika Baraza la Mawaziri). Kwa mujibu wa taarifa hiyo. Uteuzi huo ulianza juzi Aprili 21, mwaka huu.

Wakati huohuo, Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa watu walioathirika na mafuriko mkoani Morogoro na kukosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao zaidi ya 200 kuharibiwa vibaya. Mvua hizo zilinyesha katika Milima ya Udzungwa na Mahenge kati ya Aprili 19 na 25, mwaka huu.

Wednesday, April 27, 2011

'UWASHAJI MOTO KWA KUTUMIA BIDHAA ZA PLASTIKI UNAZALISHA SUMU HATARI KWA BINADAMU' MKUTANO WA MAZINGIRA WABAINISHA.

Ni mkutano wa siku mbili uliolenga kuainisha mkataba wa Stockholm kuhusu kemikali zinazochukua muda mrefu kutoweka katika mazingira jinsi zilivyo na madhara kwa binadamu hasa zichomwapo sambamba na kujipanga kuwafikia wananchi kuwapatia elimu tosha kwa lengo la kulinda afya zao.Katibu tawala mkoa wa Mwanza Bi. Dorothy Mwanyika akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa mazingira uliofanyika Lakairo Hotel Mwanza, Pichani kushoto ni Profesa Jamidu katima, mhadhiri toka chuo kikuu cha Dar es salaam na kulia kwake ni Tutubi Mangazeni ambaye ni mkurugenzi wa utawala na raslimali watu ofisi ya makamu wa rais.
Bi. Mwanyika ameiasa jamii kuepuka vitendo vyote vinavyochangia kwa kasi uzalishwaji wa kemikali hizo zenye madhara kwa binadamu ambazo husababisha maradhi kama saratani katika maeneo mbalimbali mwilini mabadiliko katika mfumo wa kinga na madhara katika mfumo wa fahamu.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam Prof Jamidu Katima.
Polychlorinated dibenzo-p-dioxins (PCDD) kwa kifupi dioxin na polychrinated dibenzofurans (PCDF) kwa kifupi furans ni kemikali mbili miongoni mwa kemikali 12 zinazochukua muda mrefu kutoweka katika mazingira ambazo zinathibitiwa kwa lengo la kulinda afya ya binadamu.

Zaidi na zaidi mkutanoni.
Kemikali hizi huzalishwa bila kukusudia wakati wa mchakato wa shughuli za uzalishaji bidhaa viwandani na uchomaji taka. Shughuli nyingine ambazo zimetajwa kama sehemu ya uzalishaji sumu hatari kwa afya ya binadamu ni pamoja na uchomaji taka za hospitali kwa kutumia mitambo isiyo bora, uzalishaji wa bati na chuma, uzalishaji wa saruji, chokaa, matofali na vioo, mitambo ya kuzalisha nishati inayotumia mafuta, kuni au mabaki mengine ya wanyama na mimea.

Mratibu wa warsha Bi. Magdalena John.
Kwa upande wake ameiasa Jamii kuepuka kuchoma taka ngumu hata zile zenye dutu za sumu au kuwasha jiko la mkaa kwa kutumia bidhaa za plastiki na kwa wale wenye viwanda amewataka kujiunga na teknolijia bora zilizopo za utunzaji mazingira kwa kuzingatia miongozo iliyoandaliwa na Sekretarieti ya mkataba wa Stokholm ambapo serikali imedhamiria kuifikisha kwa kila kiwanda.

Wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Kigoma, Shinyanga na Mwanza katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo ya siku mbili kujadili kuhusu mazingira kufanyika.

Utunzaji mazingira si kwa kupanda miti pekee bali wahusisha hata hewa mwanadamu aivutayo ambayo ni muhimu zaidi.

Mipango kudhibiti imeundwa kubaini na kudhibiti uzalishaji wa kemikali hatarishi kwa mazingira kwa kutoa elimu ya madhara ya sumu hiyo hatari sambamba na kukuza upatikanaji wa njia mbadala wa kuzuia uteketezaji wa taka ngumu.

kwa msaada zaidi angalia tovuti www.pops.int