ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 30, 2011

WACHUNGAJI MWANZA WAAHIDI KUWALINDA ALBINO.

Wachungaji jijini Mwanza leo wamepata fursa ya kuitazama filamu ya mauaji ya waafrika wenye ulemavu wa ngozi inayoitwa WHITE & BLACK nao kwa kauli moja kuahidi kuendelea kutoa elimu sambamba na kuwalinda albino dhidi ya vitendo vya mauaji na ukatili dhidi yao.Kiongozi wa mpango huo wa utoaji elimu na usaidizi kwa walemavu wa ngozi 'Under the same sun' bwana Peter Ash na Mchungaji kiongozi wakiwa wameshikilia moja ya machapisho wakati kiongozi huyo akitoa maelezo kwa washiriki juu ya mikakati iliyopo ili kuleta mabadiliko.

Ili kudhihirisha kuwa bado sakata la mauaji dhidi ya ndugu zetu albino bado linaendelea ndani ya jamii yetu, huko wilayani Ukerewe mkoani Mwanza mama Sabina wa mtoto huyu mwenye ulemavu wa ngozi aitwae Mei mosi, ndani ya mwezi mmoja uliopita amenusurika mara mbili kuuawa na watu waliokuwa wakitaka kumkatakata mwanae ili wachukuwe viungo vyake.

Mara baada ya kuitizama filamu hiyo viongozi hao wa dini walipata fursa kuuliza maswali uongozi wa UTSS pamoja na kuchangia mawazo juu ya nini kifanyike kuondoa fikra za imani potofu dhidi ya albino, zilizoganda kwenye vichwa vya baadhi ya watanzania.

Mratibu wa shirika hilo Vicky Ntetema aliwazawadia DVD za lugha mbalimbali pamoja na kalenda kwa kila kiongozi wa dini aliyehudhuria kusanyiko hilo.

Under The Same Sun (UTSS) imeanzishwa ili kuinua hali ya maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kuwapa fursa ya elimu wale wasio na uwezo na ambao hawapewi hadhi wanayostahili.

Mie na dada Vicky.
Tunaongozwa na imani kwamba watu wote tumeumbwa kwa mfano wa mungu na kwamba tunayo thamani inayolingana na tunastahili kupendwa na kusaidiwa.Together we can change the mindset of society on albinism.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.