ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 22, 2024

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUACHA ULEVI ILI KUMLINDA MTOTO

Afisa Tarafa ya Idodi, Makala Mapesah J.J  akiongea na wananchi juu ya malezi na makuzi ya watoto ili kujenga taifa lenye watu imara
Afisa Tarafa ya Idodi, Makala Mapesah J.J  akiongea na wananchi juu ya malezi na makuzi ya watoto ili kujenga taifa lenye watu imara

Na Fredy Mgunda, Iringa.

WAZAZI na Walezi wa Kijiji cha Tungamalenga Tarafa ya Idodi Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa wametakiwa kuacha Tabia ya ulevi na kutotekeleza majukumu yao ya malezi kwa watoto ili kuhakikisha uliinzi na usalama wa watoto wao.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho Afisa Tarafa ya Idodi, Makala Mapesah J.J alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto wa kijiji cha Tungamalenga.


Mapessah alisema kuwa matukio ya ukatili kwa watoto katika Kijiji hicho yanachangiwa na wazazi na walezi kutumia muda mwingi kwenye kilimo cha Mpunga na Kuwaacha Watoto kwenye mazingira hatarishi kwa usalama Wao.

Alisema kuwa tatizo la Ulevi kwa wazazi na walezi Linatajwa Kuchangia Watoto Kutelekezwa na kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo kwa kiasi kikumbwa vitendo hivyo huishia ngazi ya familia.

Mapessah alisema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatakiwa kutolewa taarifa kwa mamlaka zinazohusika ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.

Alimalizia kwa kusema Kuwa Mkakati wa Serikali ya Tarafa na Kijiji cha Tungamalenga ni kuendelea kutoa elimu ya Malezi, Makuzi, Ulinzi na Usalama kwa Watoto Wenyewe, Wazazi na Walezi Pamoja na Jamii kwa ujumla.

Watoto Wakisoma Risala yao Kwenye Maadhimisho hayo wameitaka jamii na hasa Wazazi kutopoka haki yao ya malezi na kuwaacha wakijilea wenyewe huku pia wakitaka hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wanaotenda ukatili.

Friday, June 21, 2024

ROYAL TOUR YA RAIS DKT SAMIA SULUHU YAPAISHA IDADI YA WATALII HIFADHI YA MAZINGIRA ASILI YA MAGAMBA

 



MKUU wa wilaya ya Lushoto Jaffay Kubecha akizungumza mara baada ya kutembelea Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba wilayani humo

Mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba Vyokuta akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya huyo

 Na Oscar Assenga, LUSHOTO.

KAMPENI ya Rais Dkt Samia Suluhu ya kuhamasisha utalii hapa nchini kupitia Filamu ya Royal Tour imeonyesha mafanikio makubwa kwenye Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba baada ya kupandisha idadi ya watalii kutoka 500 mpaka kufikia watalii zaidi ya 4300.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba Vyokuta wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Lushoto Jafari Kubecha akiwa na kamati ya ulinzi na usalama lengo likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani.

Katika ziara hiyo kiongozi huyo wa wilaya alitembelea eneo la kivutio la Maporomoko makubwa ya maji ya Mkuzi Water Falls ambalo limekuwa likitembelewa na wageni wa ndani na nje.

Alisema kwamba kutokana na uwepo wa hamasa hiyo ya Mkuu wa nchi kuhamaisha utalii idadi imekuwa ikipaa sana na mwaka wa fedha 2022/2023 walikuwa na watalii zaidi ya 500 na sasa huu mwezi wa tano wana watalii zaidi ya 4300 .

Alisema hiyo inaonyesha ni jinsi gani utalii unaimarika na tija ya Rais Dkt Samia Suluhu aliyoianzisha inaonyesha jinsi watu walivyoiitikia na wananchi kuitikia kutembelea vivutio vya utalii.

“Lakini pia tunawashukuru viongzi wa wilaya na mikoa na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ambao wamekuwa wakihamasisha watanzania kuja kutembelea huku akiwakaribisha watalii wa ndani na nje kuweza kufika lushoto

Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Lushoto Jaffary Kubecha alisema kwamba katika wilaya hiyo wameanzisha kampeni ya kuhamasisha vivutio vya utalii kutokana na uwepo wa maeneo mengi ya vivutio vya utalii unaosisimua.

Kubecha alisema kwamba watu wengi walikuwa wakisikia Lushoto wanafikiria ni sehemu ambayo ni maarufu kwa Kilimo cha Mbogamboga ikiwemo Kabichi kumbe ni sehemu ya mkakati wa kuvutia watalii.

Alisema kwamba baada ya kutembelea vivutio hivyo ameona namna utalii unavyosisimua kwenye wilaya hiyo lakini bado hawajapata jukwaa rasmi la kutangaza vivutio hivyo kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama na Maafisa utalii wa Halmashauri ya Bumbuli na Lushoto wamejipanga kuanza kutangaza vivutio vya utalii.

Alisema pia kampeni hiyo ya kutangaza vivutio vya utalii inaelekea kwenye shamrashamra za Tamasha kubwa la Lushoto Utalii Festival ambalo litafanyika Julai mwaka huu .

“Lakini hapo katikati kutafuatiwa na Marathon, Water falls tunataka kuiuonyesha dunia na watanzania kwamba Lushoto kuna vivutio vingi hicho ni kimojawapo kwa maana Water falls tulizonazo hapa Lushoto si chini ya tano hii ni mojawapo na misitu ya asili zi chini ya 10”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Aliongeza kuwa pia wana vivutuo vya malikale maeneo ya geographiaya milima,hali ya hewa na majengo ya kale,hotel si chini ya 50 zenye hadhi ya kimataifa dunia na watanzania watambue hilo

“Tupo makini kumuunga mkono Rais Samia Suluhu ambaye wana Lushoto wanamtambuka kama Championi wa Utalii na muda ukifika watampa tuzo ili dunia ijue kwamba lushoto wanatambua kazi nzuri aliyofanya kupitia Royal Tour na namna anavyotembea duniani kutangaza vivutio vya hapa nchini”Alisema DC huyo

Hata hivyo aliwataka watanzania kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii hasa Lushoto kwa sababu wanapokwenda huku wanapata utulivu kwa maana ni sehemu salama ya kumpumzika.

“Lakini bei ni rafiki kwa wazawa badala ya kufikiria msongo wa kutaka kwenda kujinyonga tunaweza kufika Lushoto kwa ajili ya kwenda kupata utulivu wa mwili na akili lushoto ni sehemu salama”Alisema

MBUNGE KOKA ACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI KWA UWT KIBAHA MJI UJENZI WA NYUMBA



NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka katika kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo ametoa mifuko 100 ya sarufi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya kuishi katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha mji.

Koka ametoa ahadi hiyo wakati wa kikao cha baraza kuu UWT Wilaya ya Kibaha ambacho kilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na viongozi wengine wa jumuiya za chama.
Koka alibainisha kwamba lengo lake kubwa ni kushirikiana bega kwa bega na jumuiya zote za chama ili kuweza kuweka mipango ya  kuleta maendeleo kwa wananchi.

"Mimi kama Mbunge wa Jimbo hili kwanza nawashukuru sana wanawake wa UWT,kwa kuwez kunialika katika baraza hili na nimeguswa na mm ktk ujenzi wa wa nyumba ya mtumishi nitachangia mifuko 100 ya Saruji,"alisema Mbunge Koka.
Mbunge huyo aliwahimiza wanawaje hao kuendelea kumpa ushirikiano wa hali na mali katika kutekeleza shughuli mbali mbali za kimaendeleo na kuwatumikia wananchi.

Koka alisema pia wanawake hao wanapaswa kuwa na mshikamano kuamzia katika ngazi za chini na kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ili kuweza kushinda kwa kishindo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja amemshukuru kwa dhati Mbunge Koka kwa kuwasapoti mifuko hiyo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo.
Mngoja alifafanua kwamba pamoja na kumshukuru Mbunge amewashukuru baadhi ya wabunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuchangia misaada mbali mbali ya ujenzi wa nyumba hiyo ya mtumishi.

Katika hatua nyingine Mngoja alisema kwamba walifanya harambee kwa ajili ya ujenzi huo ambapo wamefanikiwa kupata matofali zaidi ya 2500,pamoja na mifuko ya saruji.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM)  Mwalimu Mwajuma Nyamka amewataka wanawake kujikita zaidi ya kushinda katika chaguzi mbali mbali.

"Jukumu la UWT ni  kushinda katika chaguzi mbali mbali ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025,"alisema Nyamka.

Kikao cha baraza kuu la umoja wa wanawake wa (UWT) kimekutana na kujadili mambo mbali mbali ikiwemo kupatiwa mafunzo ya utunzaji wa fedha pamoja na umuhimu ya kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali.

Thursday, June 20, 2024

UWT KIBAHA MJI YAMPA KONGOLE MBUNGE KOKA NA MKEWE SELINA KUSAPOTI JENGO LA KITEGA UCHUMI

 


NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

 
Umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mji umempongeza kwa dhati Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka pamoja na mke wake Mama Selina Koka kwa juhudi na sapoti yao kubwa ya kuwakomboa wanawake kiuchumi kwa kuwawezesha  mradi wa ujenzi wa jengo la kitega uchumi ambalo litakuwa ni mkombozi mkubwa katika kutimiza ndoto zao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalumu Mwenyekiti wa UWT Kibaha mji Elina Mgonja alisema kwamba   Mbunge Koka amekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia  kwa hali na mali wanawake pamoja na jamii kwa ujumla katika mambo mbali mbali ya uwezeshaji wanawake kiuchumi.

Mgonja alisema kwamba kwa sasa UWT Wilaya ya Kibaha mjini imeweka mikakati kabambe ya kuaznisha miradi mbali mbali mabayo itakuwa ni moja ya mkombozi mkubwa katika kuwasaidia wanawake kuondokana na wimbi la umasikini na hatimaye kuweza kujikwamua kiuchumi.

"Kwa kweli sisi kama wanawake wa UWT Kibaha mji tunasema kwamba tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha Silvestry Koka pamoja na mke wake Mama selina Koka kwa moyo wao wa kujitoa kwa hali na mali katika kutusaidia sisi umoja wetu kwani kwa sasa tunamalizika kukamilisha mradi wa ujenzi wa jengo letu la kitega uchumi ambalo kwa sasa lipo tayari isipokuwa tunamalizia kukamilisha  baaadhi ya vitu kadhaa,"alisema Mwenyekiti Mgonja.

Aliongeza kuwa  Mbunge Koka amekuwa akitekeleza Ilani ya chama kwa vitendo na ndio maana ameweza kuwasaidia wanawake hao kuwa na mradi wa jengo lao kwa ajili ya kitega uchumi ambapo wameshirikiana bega kwa bega na mke wake ili kuhakikisha kwamba wanawawezesha wanawake hao kutimiza malengo yao waliyojiwekea.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa lengo kubwa la UWT ni kuweka misingi imara ambayo itaweza kumkomboa mwanamke  na mtoto hivyo mradi huo wa kitega uchumi  pindi utakapokamilika wataanzisha miradi  mbali mbali ambayo itaweza kutoa hata fursa za ajili kwa wanawake wa UWT.

"Jambo kubwa amelifanya Mhe. Mbunge kwa ajili yetu sisi kina mama pamoja na mlezi wetu ambaye ni Mama Selina Koka kwa hivyo mimi nasema kwamba sio kwamba tunajipendkeza bali tunaongea ukweli na kwa sasa siasa ni uchumi  na siku hizi tunasema mnyonge anyong'wi na haki yake anapewa maana jengo letu linapendeza,"alisema Mwenyekiti Mgonja.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini   Cesilia Ndalu hakusita kumpongeza mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka ambaye pia ni mlezi wa UWT kwa kuwa bega kwa bega na jumuiya ya umoja wa   wanawake  katika kuwasapoti mambo mbali mbali ya kimaendeleo.

Katika hatua nyingine Katibu huyo alitumia fursa hiyo ya kuwakaribisha wajumbe wote katika mkutano wa baraza la UWT ambalo linatarajiwa kufanyika siku ya kesho Ijumaa katika ukumbi wa jengo la Halmashauri na kuwahimiza kuwahi mapema lengo ikiwa ni kushiriki kikamilifu katika baraza hilo.

Wednesday, June 19, 2024

KAMA UNAHITAJI WATOTO MAPACHA KUPITIA DAWA ZA ASILI FANYA HIVI...

 NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA

Dr Mossi, ni Bingwa wa Tiba asili, Ajali za moto, Vidonda vya tumbo, Utumbo kuoza, Ganzi mwilini, Uzazi kwa kina dada , Chango la kuchoma na Kuhariibu mimba, Uvimbe tumboni na Walio vimba matumbo , Kusafisha Figo ghalama ni nafuu sana kwa atakae hitaji huduma ya kuonana na daktari. Dr. Mossi atakufuata popote ulipo kwa huduma maalum, pia kwa wale wanaosumbuliwa na Bawasili au Mang'ondi daktari anatibu ndani ya wiki moja tu, Matatizo ya ngozi au Mapele yanayo toa maji maji tiba ipo ambapo ngozi yako itarudi vizuri kama awali. Kwa maelezo na ushauli tembelea TikTok ya Dr. Mossi, au Whatsapp 0764219747 na utahudumiwa popote pale ulipo. Nawatakia afya njema na Mungu awabariki. #samiasuluhuhassan #mwanza #Ukerewe #tibaasili

DC MAGOTI AUNGURUMA AFANYA ZIARA NA WATAALAM YA KUTEMBELEA MRADI WA UWEKEZAJI VISEGESE




NA VICTOR MASANGU,KISARAWE 

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mhe.Petro Magoti  amefanya kikao kazi na   wataalam wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyi pamoja na Kamati ya Usalama Wilaya kwa ajili ya kujadili maendeleo ya Mradi wa viwanja vya Uwekezaji wa Viwanda. 

Mkuu wa Wilaya hiyo pia katika kikao hicho ameweza kuongozana na  Viongozi mbali mbali  wa Halmashauri ya Kisarawe pamoja na Timu ya Watalaam na kupata fursa ya kutembelea  eneo la Mradi wa upangaji wa Upimaji wa Eneo la Viwanda lililopo Visegese kata ya Kazimzumbwi.

Mhe.Magoti alisema kwamba mradi wa Upangaji wa upimaji  ulibuniwa kwa ajili ya kutenga viwanja kwa ajili ya Viwanda na Maeneo mbali mbali  ya Makazi ya watu.

Magoti alifafanua kuwa utekelezaji wa Mradi huo ulianza kutekelezwa.mnamo  mwaka 2014 na kufanikiwa kuzalisha Viwanja 291 hivyo eneo hilo litakuwa Maalum kwa ajili ya Viwanda vya aina mbali mbali.

"Utekelezaji wa Mradi huu ulifanyika kwa ubia kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na Wananchi wenye Maeneo katika Eneo lililopendekezwa kwa lengo la uwelezaji huo,"alisema Mhe.Magoti

Mkuu huyo alieleza kuwa muda  si Mrefu Wananchi wote  wenye nia yakutaka kuwekeza nakujenga Viwanda Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa pwani karibuni sana sana.Huduma za Maji zipo na barabara tupo mbioni kuzishughulikia ili kupanua wigo wa usafirishaji.

Pia alifafanua kwamba Mhe. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan  anapenda kuona Wananchi wake wanapata kipato kikubwa na kuinua uchumi wa kimaendeleo yenye kuleta mabadiliko na kuboresha  maisha yao kwa ujumla.

RAIS SAMIA AWASILI AFRIKA YA KUSINI KUHUDHURIA UAPISHO WA RAIS RAMAPHOSA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Waterkloof Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 18 Juni, 2024. Rais Samia anatarajia kuhudhuria hafla ya Uapisho wa Rais mteule wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa tarehe 19 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Waterkloof Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 18 Juni, 2024. Rais Samia anatarajia kuhudhuria hafla ya Uapisho wa Rais mteule wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa tarehe 19 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Dkt. Grace Naledi Pandor pamoja na Thembi Nkadimeng Waziri wa Utawala na Ushirika na Masuala ya Jadi. Rais Samia anatarajia kuhudhuria hafla ya Uapisho wa Rais mteule wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa tarehe 19 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Watanzania waishio Afrika Kusini mara baada ya kuwasili Pretoria tarehe 18 Juni, 2024. Rais Samia anatarajia kuhudhuria hafla ya Uapisho wa Rais mteule wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa tarehe 19 Juni, 2024.

Tuesday, June 18, 2024

SIKU MBILI ZA VIPIMO VYA SARATANI NA UCHUNGUZI BURE JIJINI MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

ZAIDI ya asilimia 40 ya wanawake nchini wanakabiriwa na tatizo la Saratani ya Matiti hali inayosababisha kujitokeza vifo vingi vinavyotokana na ugonjwa huo kutokana na wagonjwa wengi kufika hospitalini hatua za mwisho. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mradi wa Saratani ya matiti Dr. Mary Giattas katika warsha ya kuwajengea uwezo madaktari wa saratani waliopo katika Hospitali za mkoa wa Mwanza, namna ya uchunguzi wa ugonjwa huo. Tarehe 18 na 19 Juni 2024 Hospitali ya Makongoro na Buhongwa ndizo zitakazo husika na mradi huo ambapo wanawake watapata fursa ya kupata huduma ya uchunguzi wa saratani bure, ukiwa umelenga kuwafikia wanawake zaidi ya 500 katika mikoa mitatu nchini.

CCM TANGA YATAJA VIGEZO VITAKAVYOTUMIKA KUWAPATA WAGOMBEA WA UDIWANI, UBUNGE TANGA 2025

 Na Oscar Assenga, PANGANI

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimesema kuwa vigezo ambavyo vitatumika kuwapata wagombea kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka huu na ule Mkuu wa Wabunge na Madiwani wa mwakani 2025 kwamba ni wale ambao wanashiriki kwenye vikao kuanzia ngazi ya mashina.

Vigezo hivyo vilitangazwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman wakati aliposhiriki kwenye mkutano wa Shina namba 5 Mtaa wa Majengo Kata ya Pangani Mashariki ambapo pamoja na mambo mengine alihamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wakati utakapofika.




Katika mkutano huo wa Shina namba 5 Mwenyekiti huyo aligawa viti 100 ikiwa ni kuhakikisha wanakuwa na uchumi imara ambao utawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika shina hilo

Alisema kwamba wanahitaji wapate viongozi ngazi ya serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 wa Ubunge na Madiwani ambao wanakiheshimu chama cha Mapinduzi.

Alisema kwamba tafsiri ya kukiheshimu chama hicho ni kuhudhuria mikutano ya mashina yako na waanapokuwa hawaudhurii maanake bado haujaonyesha kukithamini na kukipenda chama cha mapinduzi.

“Niwaambie kwamba sio hiari ni suala la lazima viongozi wa ngazi za mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa wilaya, Kata na Mitaa na Vitongoji kuhudhuria kwenye mikutano ya mashina na kwa sasa atakayechukua fomu na kujaza na kueleza mikutano ya shina amehudhuria mara tano wakati hajafanya hivyo tutafuatulia maana mikutasari ipo”Alisema

“Sio suala la Hiari ni lazima kuhakikisha viongozi wa ngazi za wilaya wahudhurie mikutano ya shine lake ,Mwenyekiti wa Kata, Mbunge,Diwani hilo ni jambo la msingi linahimizwa kwenye chama chetu lazima wahudhurie kufanya hivyo ndio kukitendea haki chama chetu ujumbe huo ni kwa viongozi wote wa mkoa wa Tanga kwa sababu ndi anadhama nao na wote”Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha alisema kwamba suala la viongozi hao kuhudhuria kwenye mikutano hiyo ya mashina yao sio suala la hiari ni suala la lazima na mtakumbuka wakati najaza fomu kwenye uchaguzi wa chama 2022 ile fomu inavipengelea vingi miongoni mwao ilitaka ueleza vikao ambavyo ulivyoshiriki vya CCM kwa nafasi yako.

“Kwa maana lazima ueleze mikutano ya shina umehudhuria mara ngani kwa maana vikao vya matawi na mikutano mashina umehudhuria mara ngapi hilo ni suala la lazima na mara nyingi tumekuwa tukifanya mazoea kuona jambo la kawaida kawaida”Alisema

“Niwahakikishie uchaguzi unaokuja wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji na Mkuu wa Mwakani 2025 wa uchaguzi wa kumchagua Rais, Ubunge na Madiwani kipaumbele cha kwanza cha watakaopewa kwenye kugombea ni wale wote ambao wanashiriki vikao na mikutano ya matawi na mashina ya CCM”Alisema

Aidha alisema kwamba atakayejaza fomu na kueleza mikutano ya shina amehudhuria mara tano na hajawahi kufanya hivyo watafuatilia maana mikutasari ipo kwa nafasi hiyo nyeti wanayotaka kumpa huyo mtu wanajua lazima akakiheshimu chama hivyo lazima wapate kumbukumbu zake kwa usahihi na kwa uhakika.

“Kwa hivyo wale wote wanaotarajia kugombea nafasi kwenye chama chao kwenye kura za maoni wajue kama kwenye mashina yao hawakuheshimu vikao vya mashina waliviona havina maana yoyote balozi balozi maana balozi kazi tuliomuachia ni kusuluhusha ndoa za watu”Alisema Mwenyekiti.

MBUNGE UMMY MWALIMU AUNGANA NA TAASISI YA SHITTA KUTOA SADAKA WAGONJWA BOMBO HOSPITALI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KUCHINJA

 






MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aungana na Umoja wa Taasisi za Kiislamu Mkoani Tanga (SHITTA) kutoa sadaka kwa wagonjwa waliolazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo) kusherehekea sikukuu ya Eid Al_Adha kwa ajili ya kuchinja.

Mbunge Ummy alisema kwamba kushiriki kwa pamoja kutoa chakula kwa wagonjwa, kwenye Hospital hiyo  ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Eid Al Adha kutawawezesha wagonjwa nao waweze kufurahia siku hiyo 

Akiwa Hospitalini hapo Mbunge Ummy alionyesha  furaha yake kutambulishwa shirikisho hilo  ambalo linaziunganisha Taasisi za dini ya kiislamu katika mkoa wa Tanga huku akiwatoa wito kwa taasisi nyengine kuona umuhimu wa kutoa sadaka kwa wahitaji ikiwemo wagonjwa.

"Kwa kweli nimefurahi sana kushirikiana na Taasisi hii,wakati mwingine mimi kama mbunge napata shida kuzungumza na taasisi moja moja ,lakini kama nataka kukutana na taasisi za kiislamu naweza kuitafuta SHITTA ambayo inaweza kuniletea taasisi zote",Alisema mbunge wa Jimbo hilo Ummy Mwalimu.