ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 19, 2011

TWANGA PEPETA 50th Tanzania INDEPENDENCE TOUR

African stars Entertainment Tanzania wanakuletea Bendi nzima ya Twanga Peteta ili iweze kufanya nao Makamuzi Live ndani ya Nchi ya Uingereza.Hii si yakukosa mazee kwani inatokea mara moja moja tuuuu!!! Safari hii ni Terehe 26.05.2011, Usikose mwanawane!!

MASHINDANO YA NGUMI YA KOVA CUP YAMALIZIKA

Bondia Mussa Mohamedi (kulia) akimfulumusha makonde mfululizo, Fadhili Hassani wakati wa mpambano wa mashindano ya Kova Cup yaliyomalizika, Dar es salaam jana Mussa alishinda kwa K,O ya raundi ya tatu.Eh bana duh!!!!....!!!!

Mabondia wa kike Mariamu Edwer (kushoto) na Matha George wakipambana wakati wa mashindano ya Kova Cup yaliyomalizika, Dar es salaam, jana Matha alishinda kwa ponti.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

BREAKING NEWS: MTOTO WA GADDAFI AKAMATWA

Serikali ya muda ya Libya inasema kuwa Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, amekamatwa.

Waziri wa Sheria wa serikali ya mpito, Mohammed al-Allagi, alisema kuwa Saif al-Islam amezuwiliwa karibu na mji wa Ubari, kwenye jangwa la kusini-magharibi mwa nchi.

Ripoti moja ilieleza kuwa hivi sasa amechukuliwa kwa helikopta kupelekwa Zintan, kaskazini mwa nchi.

Amekuwa akijificha tangu wapiganaji wa serikali ya mpito kuuteka mji mkuu, Tripoli, mwezi Agosti, na anasakwa na Mahakama ya Uhaini ya Kimataifa, kwa mashtaka ya uhalifu wa kivita.

CHANZO: bbc swahili.

WAHITIMU CHUO KIKUU CHA KANISA KATOLIKI CHA SAYANSI ZA AFYA BUGANDO WAPOKEA NONDO ZAO LEO

"Anayetimiza wajibu wake hupata furaha ya moyoni" Kauli ya Mgeni rasmi Mhasham Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SAUTI Agustin Shayo.

Meza kuu.

Licha ya juhudi za nchi kupata wataalamu wake kwenye sekta ya afya imeanza zamani lakini mpaka sasa idadi ya wataalamu kwenye sekta hiyo hairidhishi hivyo jitihada za dhati zinahitajika kukidhi mahitaji ya hospitali zetu.

Takwimu zinaonyesha kwamba karibu 60% ya wafanyakazi wanaohitajika kwenye sekta hii hawapo hivyo maamuzi ya kuanzishwa kwa chuo hiki cha kufundisha madaktari yalilenga kuchangia kupunguza pengo hilo. Big up kwa BUGANDO.

Rais wa Touch Foundation Mr Bryan Lowell akisema machache kwenye mahafali hayo. Ni mfuko ulio wawezesha wahitimu wengi kulipia ada za masomo.

Since the establishment of this medical school a total of 556 students have graduated, 337 in Diploma Programmes, 144 in the MD Course, 33 in Masters programmes and one in PhD programme.

Sehemu waliyo keti Wahitimu 33 kwenye shahada ya uzamili na mhitimu mmoja kwenye shahada ya uzamivu Stephen Mshana (mbele).

Kwaya ya kanisa katoliki kigango cha Bugando iliweka nakshi katika siku hii nzuri ya kumbukumbu.

Derick David, Magdalena Denis, Mamwanda Jebby, na Veronica Lyandala ni kati ya wahitimu 144 wa shahada ya udaktari (MD) waliotunukiwa shahada zao leo katika viwanja vya Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Picha maalum ya meza kuu na Dr. Stephen Mshana (wa tatu toka kulia) mhitimu pekee aliyetunukiwa shahada ya uzamivu (PhD) toka Chuo cha Sayansi za Afya Bugando.

Jumla ya wahitimu 149 wametunukiwa stashahada na shahada mbalimbali, kati ya wahitimu hao wahitimu 51 ni wanawake.

Mtunukiwa Stashahada ya Udaktari wa magonjwa ya binadamu Dr. Mwandu Makani akiwa na ndugu zake waliokuja kumpa tafu la chereko kwenye maafali hayo.

Friday, November 18, 2011

ROCK CITY IS RAINING...

Take one.

Take two.



Finito.

MING'ARO KUELEKEA WIKIENDI.....

Usimchukulie powa!! Ni Mwanahabari mahiri katika uandishi wa makala na habari, long time katika gemu anaitwa Selemani Bitala, katoka ki-kadzyo aka simple kwaajili ya wekeend, anaronga kuwa aamevaa kizungu kuikaribisha wikiendi.

Wakibariz mdogo-mdogo pichani ni Mr. Vodacom Fred Fidelis aka 'Freduor' (fredwaaa) akiwa na Mr. Big Brother wa Radio Free Afrika Mwanza. Swali: Jeh! hapo mezani ni maji tu na vyoda au mixa?

LIFE GOES ON NA KITAA CHETU.....

Ni ubunifu tu katika biashara kwani dukani hapa bidhaa zilizopo ni mifagio, koroboi, tambi za majiko ya mchina, chemli na koroboi, majiko, miko size zote, matenga kwaajili ya nyanya na kuhifadhia kuku, nyungo, makarai, vikaangio kwa vitumbua, chapati na maandazi, vinu, mitwangio, mipini ya majembe na visu.

Wakati makanisa mengi yakizidi kuongezeka kujengwa, madhehebu mapya yakisajiliwa, huku wengine wakikodisha kumbi mbalimbali kwaajili ya kufanya ibada (hadi zile za viti virefu jioni); Najiuliza kunani hata watu wadiriki kuyakacha makanisa yao ya zamani waliyoyajenga kwa bloku na kuyanakshi kwa malumalu yakiwa matupu bila waumini na kuja huku..?..!

Taswira ya soko la Kimataifa la Mwaloni, toka majini ndani ya Ziwa Victoria.

Ni biashara ya majiko ambapo miaka ya sasa nyenzo za ndani ni udongo na siyo chuma au bati kama zamani...kunani?

Msusi.

Vitunguu tatu tatu, bania na-na-na-na na-nini...!!!

Kibiashara zaidi..

Thursday, November 17, 2011

RAIS WA FIFA AJICHANGANYA KUHUSU UBAGUZI

Mlinzi wa England na Manchester United Rio Ferdinand amesema ameshangazwa na madai ya Sepp Blatter kwamba hakuna tatizo la ubaguzi katika mchezo wa kandanda uwanjani.

Rais wa Fifa amesema matukio ya uwanjani yanaweza kutatuliwa kwa kupeana mikono, ingawa baadae alidai ameeleweka vibaya.

"Nieleze nimesoma matamshi ya Blatter vibaya... iwapo sijakosea basi nimeshangazwa," alisema Ferdinand kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Ferdinand baadae alimtumia ujumbe kwa Blatter. Katika ujumbe huo aliandika: "Matamshi yako kuhusiana na ubaguzi yanashangaza na kwa kweli yanachekesha. Iwapo mashabiki watapaza sauti zao kwa maneno ya kibaguzi jee kushikana mikono hapo ni sawa?"

Matamshi ya Blatter yamekuja wakati nahodha wa Chelsea John Terry akichunguzwa na polisi pamoja na Chama cha Soka cha England juu ya tuhuma za kumtamkia maneno ya kibaguzi mlinzi wa QPR Anton Ferdinand, ambaye ni mdogo wake Rio.

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez naye ameshtakiwa na FA kwa tuhuma za kutoa maneno ya kibaguzi dhidi ya mchezaji mwenzake Ferdinand katika Manchester United, Patrice Evra.

Alipoulizwa iwapo anadhani ubaguzi uwanjani ni tatizo katika soka ya kisasa, Blatter aliiambia televisheni ya CNN kipindi cha michezo: "Nakanusha hilo. Hakuna ubaguzi.

"Huenda kuna tatizo la mchezaji mmoja kwa wengine - anakuwa anasema kitu ambacho kinakuwa si sahihi.

"Lakini yule ambaye anaathirika na hilo, hana budi kusema ndio mchezo. Tumo katika mchezo na mwishoni mwa mchezo, tunapeana mikono na hili linawezekana, kwa sababu tumefanya kazi kubwa kupambana na ubaguzi."

CHANZO: bbc swahili.

KUSHEREKEA MIAKA 40 YA KONYAGI KAMPUNI YA TDL YATOA MISAADA YA VIFAA VYA USAFI KWA JIJI LA MWANZA.

Mike Mrema ambaye ni Meneja wa Mauzo na Usambazaji kanda ya Ziwa toka kampuni ya TANZANIA DISTILLERIES LIMITED (TDL) akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa kaimu mkurugenzi wa jiji la Mwanza Fransis Mkabenga(left) ili viwasilishwe kwa makundi mbalimbali yaliyosajiliwa na ofisi za jiji hilo.

Kwa upande wake Afisa afya wa jiji mazingira na usafi bw. Dontora Kamenya ameishukuru kampuni ya Konyagi kwa msaada huo kwani uhaba wa vifaa na vitendea kazi imekuwa changamoto kuu inayovikabili vikundi vingi vya kufanya usafi vilivyo chini ya Halmashauri ya jiji hivyo ofisi yake imeahidi kuvipa uangalizi mzuri.

Nia ya msaada huo ni kuchangia juhudi za kuimarisha usafi katika majiji ya Mwanza, Arusha na Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kuchangia maendeleo ya jamii ambapo TDL imeahidi kuhamasisha kampeni za usafi wa mazingira katika kuendeleza usafi na maandari safi ya majiji.

Sekta ya habari waalikwa Mr. Deus (Tanzania Daima), Abdalah Tilata (Star Tv), Sheila Sezzy (Mwananchi), John Maduhu (Mtanzania) na Grace Chilongola (Habari Leo).

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Matoroli 20, Vest zenye reflectors 50, Gloves 50, Marsk 50, Kofia za usalama 50, Miwani ya kuzuia vumbi na jua 50, Gum boots 50, Mifagio 50, Jembe 50 na Reki 50 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni kumi.

Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mwanza Fransis Mkabengwa ametoa wito kwa wafanyausafi wa jiji kuvitumia kwa uangalifu vifaa hivyo bila kuvifuja ili vitumike kwa muda mrefu katika suala la kutunza mazingira.

Wito pia umetolewa kwa mashirika mengine kuiga mfano huo wa TANZANIA DISTILLERIES LIMITED kuunga mkono juhudi za serikali kwenye harakati mbalimbali za kuihudumia jamii hasa suala la usafi na utunzaji wa mazingira.

Pamoja na msaada huu Konyagi imeahidi kwa siku za baadaye kutoa mapipa makubwa ya kuhifadhia taka.

Katibu wa Usafi Wafagizi jiji la Mwanza bi Fatma Ramadhani- "Tatizo la kutapisha vyoo hasa kwa watu waishio milimani ni sugu, tunakutana na taka za vinyesi, nyingine za siri hazija hifadhiwa kiusalama, wafanya usafi wamekuwa wakikumbwa na magonjwa mengi hivyo nawaomba maafisa afya, wenyeviti wa vitongoji kuhamasisha jamii nyumba hadi nyumba kuchimba vyoo vya kudumu"

Kwa kauli moja Jumuiya ya wafanya usafi jijini Mwanza imeimba jamii kuithamini na kuiheshimu kazi hiyo muhimu katika suala zima la utunzaji wa mazingira kwani bila ya kufanya usafi sote tutaangamia kwa magonjwa.

Wednesday, November 16, 2011

DUH - AISEEEEEEeeee!!!......

Kuwa makini ukiwa Hospitali ya wilaya wa Misungwi mkoani Mwanza kwani ukikalia mawe katika hospitali yetu utapigwa faini.

Goli la mpira wa miguu na vyandarua vyetu....
Vinatumika pia katika kutegea samaki,
Na Kingo za kufugia kuku hasa vifaranga
,


Moja moja nyiiiingi haijirudii - Never come twice.

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA KITUO CHA UPIMAJI WA RAMANI.

Na Anna Massao ,
Mkutano wa kimataifa kujadili masuala mbalimbali ya ardhi wenye jumla ya nchi wanachama kumi na nane kutoka Afrika unaendelea jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Double tree. Mkutano huo ulifunguliwa jana na katibu mkuu wa wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Patrick Rutabanzibwa ambao ni mkutano wa maandalizi wa makatibu wakuu utakaoanza 17 Novemba.

Lengo kuu la mkutano huo ni kusaidia nchi za Afrika katika masuala ya upimaji na ramani kwa ajili ya maendeleo ambapo mkutano huu ni wa 45 kufanyika baada ya ule wa Capetown, South Afrika na Tanzania ndio mwazilishi wa kituo hiki mwaka 1975 chenye makao yake makuu jijini Nairobi na unajumuisha nchi kumi na nane zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan, Ethiopia, Botswana ,Namibia , Zambia, Mauritius, Seychelles , Somalia, Comoros , South Africa, Rwanda, Burundi , Lesotho ,Malawi and Swaziland.

Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni mkurugenzi wa upimaji na ramani katika wizara ya ardhi Mr Silas Mayunga anasema, ‘tunafarijika kupata fursa ya kuaandaa mkutano huu, maazimio yatasaidia katika kuimarisha shughuli za upimaji ardhi, utunzaji wa mazingira na mafunzo kwa wataalamu na pia nchi yetu imejitangaza,’

Mr Mayunga aliongeza kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza barani Afrika kukamilisha mpango wa alama ya upimaji ardhi inayojulikana kitaalamu ‘geodetic network’ambazo ni 740 na kuweza kusimikwa nchi nzima na kuongeza kuwa 6 kati ya alama hizo zimepimwa kitaalamu kwa njia ya satelaiti na pia serikali ina mpango wa miaka mitano wa upimaji ardhi nchini na katika kutekeleza mpango huo serikali imekubali kuanzisha kituo cha kupokea picha za satelaiti kitakachojengwa mjini Dodoma.

Tarehe 16 Novemba wakurugenzi hao kutoka nchi kumi na nane za Africa watatembelea wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kujifunza na kuona mambo mbalimbali kama Mfumo wa Survey Registration System (SRC) katika idara ya Upimaji na Ramani vilevile kupata maelezo kuhusu mradi wa mji mpya wa Kigamboni.

ZAIDI YA WATOTO 3,000 TANZANIA WALIOCHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO HUPOTEZA MAISHA KILA SIKU KWA UGONJWA WA MARALIA.

Imeelezwa kwamba, ugonjwa wa malaria bado ni tishio kwa maisha ya Watanzania, ambapo hadi sasa zaidi ya watoto 3,000 hapa nchini waliochini ya umri wa miaka mitano, hupoteza maisha yao kila siku kwa ugonjwa huo.Abdul Salum.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Mwanza na Meneja wa Kanda ya Zanzibar, kutoka mradi wa kupambana na Malaria nchini (IRS), Bw. Abdulah Salum, wakati alipokuwa akiwasilisha mada kwenye semina ya siku tatu kuhusu athari za Malaria, iliyowashirikisha waandishi wa habari mbali mbali kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria, na kufanyika Midlend Hoteli jijini humo.

Amesema, ugonjwa wa malaria umekuwa tishio kwa maisha ya Watanzania, Afrika na dunia nzima, na kwamba, mradi huo wa IRS umedhamiria kupunguza kabisa mazalia ama ugonjwa huo ambao umekuwa ukiua watu wengi duniani.

Meneja huyo wa IRS Kanda ya Zanzibar, Bw. Salum amefafanua kwamba, mbali na idadi hiyo ya vifo kwa watoto, kati ya watu 80,000 wanaopoteza maisha mbali mbali, kati yake asilimia 40 wanakufa kwa ugonjwa huo wa Malaria.

Akizungumzia kuhusu vita hiyo ya kupambana na ugonjwa huo hatari, Bw. Salum ameitaja Zanzibar na viunga vyake kuwa imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kudhibiti maambukizo ya ugonjwa hatari wa Malaria, kutoka asilimia 40 mwaka 2008 hadi kufikia asilimia moja kwa sasa.

Kwa mujibu wa Meneja huyo wa IRS Kanda ya Zanzibar, Salum, upungua kwa maambukizi hayo, imetokana na mikakati thabiti ya kupambana na ugonjwa huo, hivyo Watanzania wote wanapaswa washirikiane na Serikali ukiwemo mradi wa kupambana na Malaria wa IRS ili kudhibiti kabisa ugonjwa huo.

Amewaomba Watanzania kushirikiana na mradi huo wa IRS katika kupambana na ugonjwa huo, na kwamba zoezi la kunyunyizia majumbani dawa ya ukoko linaloendelea nchini linapaswa kuungwa mkono na watu wote ili kufikia malengo ya kuwa na Tanzania siyo na malaria.
Dr Pius Tubet meneja mradi wa Kanda ya ziwa Victoria akiwasilisha taarifa ya kanda.

Tuesday, November 15, 2011

MKUU WA MKOA WA MWANZA ERENEST NDIKILO ATINGA OFISI ZA WANDISHI WA HABARI MWANZA, AHAIDI KUUNDA TUME KUFUATILIA MAUAJI YA MWANDISHI RICHARD MASATU

Mkuu wa mkoa wa Mwanza bwana Erenest Ndikilo ofisi yake imeahidi kuunda kamati ya kuchunguza kifo cha utata cha mwandishi wa habari kanda ya ziwa marehemu Richard Masatu aliyefariki dunia mnamo tarehe 10/08/2011 nakupatikana na tundu la jeraha lililoanzia chini ya kidevu hadi kwenye koromeo.

Hayo ameyasema leo kupitia ombi lililo ambatanishwa kwenye risala yao alipotembelea Ofisi za chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mwanza (MPC) kwa lengo la kuzungumza nao.

Mkuu huyo wa mkoa amewaasa wandishi waepuke kutumiwa na baadhi ya wanasiasa kuchafua wenzao kwa kuandika habari zinazo poteza amani, utulivu, mshikamano na wala wasitumike kuigawa nchi kikabila, kidini na kisiasa badala yake watumie taaluma zao kushauri, kukosoa, kutoa mapendekezo na kusifu pale viongozi wanapotenda stahiki kwa jamii.

Aidha Mh. Ndikilo amewaagiza wakuu wote wa halmashauri zote za wilaya mkoani Mwanza kutoa ushirikiano kwa wanahabari ili wananchi wapate taarifa zilizo sahihi na kwa wakati.

Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Wandishi wa Habari Mwanza (MPC) bi Flora Magabe akiwasilisha Risala kwa mh. mkuu wa mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo(kushoto) na aliyesimama katikati ni katibu wa MPC Edwin Soko.

Mwisho mkuu wa mkoa amewasihi wandishi wa habari kuwa na utaratibu wa kufika sehemu za vijijini kukusanya habari , taarifa na matukio kwa lengo la kuikwamua jamii hiyo muhimu.