Mkutano wa kimataifa kujadili masuala mbalimbali ya ardhi wenye jumla ya nchi wanachama kumi na nane kutoka Afrika unaendelea jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Double tree. Mkutano huo ulifunguliwa jana na katibu mkuu wa wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Patrick Rutabanzibwa ambao ni mkutano wa maandalizi wa makatibu wakuu utakaoanza 17 Novemba.
Lengo kuu la mkutano huo ni kusaidia nchi za Afrika katika masuala ya upimaji na ramani kwa ajili ya maendeleo ambapo mkutano huu ni wa 45 kufanyika baada ya ule wa Capetown, South Afrika na Tanzania ndio mwazilishi wa kituo hiki mwaka 1975 chenye makao yake makuu jijini Nairobi na unajumuisha nchi kumi na nane zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan, Ethiopia, Botswana ,Namibia , Zambia, Mauritius, Seychelles , Somalia, Comoros , South Africa, Rwanda, Burundi , Lesotho ,Malawi and Swaziland.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni mkurugenzi wa upimaji na ramani katika wizara ya ardhi Mr Silas Mayunga anasema, ‘tunafarijika kupata fursa ya kuaandaa mkutano huu, maazimio yatasaidia katika kuimarisha shughuli za upimaji ardhi, utunzaji wa mazingira na mafunzo kwa wataalamu na pia nchi yetu imejitangaza,’
Mr Mayunga aliongeza kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza barani Afrika kukamilisha mpango wa alama ya upimaji ardhi inayojulikana kitaalamu ‘geodetic network’ambazo ni 740 na kuweza kusimikwa nchi nzima na kuongeza kuwa 6 kati ya alama hizo zimepimwa kitaalamu kwa njia ya satelaiti na pia serikali ina mpango wa miaka mitano wa upimaji ardhi nchini na katika kutekeleza mpango huo serikali imekubali kuanzisha kituo cha kupokea picha za satelaiti kitakachojengwa mjini Dodoma.
Tarehe 16 Novemba wakurugenzi hao kutoka nchi kumi na nane za Africa watatembelea wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kujifunza na kuona mambo mbalimbali kama Mfumo wa Survey Registration System (SRC) katika idara ya Upimaji na Ramani vilevile kupata maelezo kuhusu mradi wa mji mpya wa Kigamboni.
Tupe maoni yako
Kaka ili ni jambo zuri lakin angalia tulivyo wa bongo publicity ni hakuna kabisa na sana sana huwa hamna hata kdg. There is a lot to benefit from Kutokana na hili jambo. Thanks kwa tarifa.
ReplyDeleteNi kweli kabisa Jawad publicity hakuna ila leo kuna kikao cha makatibu wakuu wa ministry zinazohusiana na land so nadhani leo zitab published.thanks 4 comment
ReplyDelete