ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 14, 2026

MAHUNDI : SAYANSI NI SULUHUSHO LA AJIRA KWA WASICHANA


Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mhandisi Maryprisca Mahundi, amewahimiza wanafunzi wa kike nchini kuwekeza juhudi katika masomo ya Sayansi, akisisitiza kuwa kusoma masomo hayo ni njia muhimu ya kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira.


Naibu Waziri Mahundi ameyasema hayo leo, Februari 11, 2026, wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana Katika Sayansi, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

“Watoto wa kike, ninawaambia kusoma Sayansi inawezekana. Ukifaulu vizuri, itakuwa msaada mkubwa katika mapambano ya kujenga taifa,” amesema Naibu Waziri Mahundi.


Ameongeza kuwa jukumu kuu la wizara ni kuhakikisha wanawake na wasichana wanahamasishwa na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Sayansi, kupitia maboresho ya sera na miongozo inayowarahisishia kushiriki ipasavyo katika fursa za maendeleo ya Sayansi.


Aidha, Naibu Waziri Mahundi amesisitiza kuwa wanapowahimiza wasichana kusoma Sayansi, wizara haimuachii nyuma mtoto wa kiume, ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza za kutowapa fursa sawa watoto wa kiume katika nyanja za elimu na Sayansi.




RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WA UMOJA WA AFRIKA MJINI ADDIS ABABA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika ambao unaongozwa na Kaulimbiu ya Mwaka 2026 inayosema: “Kuhakikisha Upatikanaji Endelevu wa Maji na Huduma Salama za Usafi wa Mazingira ili Kufikia Malengo ya Ajenda 2063.” Kaulimbiu hiyo inalenga kuhimiza hatua za pamoja za bara katika kuhakikisha usalama wa rasilimali maji, afya ya jamii, na maendeleo endelevu.

NA ALBERT G.SENGO

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kwa mwaka 2026 umeongozwa na kaulimbiu isemayo, “Kuhakikisha Upatikanaji Endelevu wa Maji na Huduma Salama za Usafi wa Mazingira ili Kufikia Malengo ya Ajenda 2063"


Kaulimbiu hiyo inalenga kuhimiza hatua za pamoja barani Afrika katika kulinda rasilimali maji, kuboresha afya za wananchi na kuhakikisha maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Kwa Tanzania, ajenda hii inaleta manufaa makubwa katika nyanja mbalimbali.

Kidiplomasia, ushiriki wa Tanzania katika utekelezaji wa ajenda ya maji na usafi wa mazingira unaimarisha nafasi ya nchi katika majukwaa ya kikanda na kimataifa. Pia unatoa fursa ya kupanua ushirikiano kupitia jumuiya za kikanda kama Jumuiya ya Afrika Mashariki, hususan katika usimamizi wa vyanzo vya maji vya pamoja.

Kiuchumi, uwekezaji katika miundombinu ya maji unachochea ajira, unaimarisha sekta ya kilimo kwa kuongeza umwagiliaji, pamoja na kukuza viwanda vinavyotegemea upatikanaji wa maji ya uhakika. Hali hiyo pia huchochea ukuaji wa pato la taifa.

Katika sekta ya afya, upatikanaji wa maji safi na huduma bora za usafi wa mazingira unapunguza magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na kuhara, hivyo kupunguza gharama za matibabu kwa familia na serikali kwa ujumla.

Kwa upande wa maendeleo endelevu, ajenda hiyo inalinda mazingira, inaongeza usawa wa kijinsia kwa kupunguza muda unaotumika kutafuta maji, na kusaidia kufikia malengo ya muda mrefu ya maendeleo ya bara la Afrika.

Kwa ujumla, kaulimbiu ya mwaka 2026 si tu wito wa kisera, bali ni fursa kwa Tanzania kuimarisha diplomasia, kukuza uchumi, kuboresha afya za wananchi na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo endelevu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika ambao unaongozwa na Kaulimbiu ya Mwaka 2026 inayosema: “Kuhakikisha Upatikanaji Endelevu wa Maji na Huduma Salama za Usafi wa Mazingira ili Kufikia Malengo ya Ajenda 2063.” Kaulimbiu hiyo inalenga kuhimiza hatua za pamoja za bara katika kuhakikisha usalama wa rasilimali maji, afya ya jamii, na maendeleo endelevu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika ambao unaongozwa na Kaulimbiu ya Mwaka 2026 inayosema: “Kuhakikisha Upatikanaji Endelevu wa Maji na Huduma Salama za Usafi wa Mazingira ili Kufikia Malengo ya Ajenda 2063.” Kaulimbiu hiyo inalenga kuhimiza hatua za pamoja za bara katika kuhakikisha usalama wa rasilimali maji, afya ya jamii, na maendeleo endelevu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mheshimiwa Abiy Ahmed huku waandamizi wake wakifuatilia maelekezo hatua pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika, tarehe 14 Februari, 2026 jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mheshimiwa Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika, tarehe 14 Februari, 2026 jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mheshimiwa Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika, tarehe 14 Februari, 2026 jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mheshimiwa Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika, tarehe 14 Februari, 2026 jijini Addis Ababa, Ethiopia.

HOTUBA NZIMA YA NAIBU WAZIRI WA HABARI AKITOA TAMKO LA SERIKALI KUSHUSHA GHARAMA ZA USAJILI MITANDAO

 NA ALBERT G.SENGO/DODOMA

SERIKALI imechukua hatua ya kihistoria ya kuchochea ukuaji wa sekta ya habari za kidijitali nchini kwa kupunguza kwa kiwango kikubwa ada za leseni kwa wanablogu na wakusanyaji wa maudhui mtandaoni, hatua inayolenga kuondoa vikwazo vya gharama na kufungua fursa zaidi kwa wabunifu wa maudhui. Hatua hiyo imetangazwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji (ABC) Februari 12, 2026 jijini Dodoma. Kwa mujibu wa tangazo hilo, ada ya leseni kwa wakusanyaji wa maudhui mtandaoni imepunguzwa kutoka Shilingi 1,000,000 hadi Shilingi 100,000 kwa mwaka, huku ada ya fomu ya usajili ikishuka kutoka Shilingi 100,000 hadi Shilingi 20,000. Aidha, ada ya leseni kwa blogu imepungua kutoka Shilingi 500,000 hadi Shilingi 50,000 kwa mwaka, na fomu ya usajili kushuka kutoka Shilingi 50,000 hadi Shilingi 10,000.

SEKTA YA HABARI YASISITA ITHIBATI KUIMARISHA UWAJIBIKAJI.

 

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imesema utekelezaji wa mfumo wa ithibati kwa waandishi na watangazaji wa habari nchini ni hatua ya kimkakati ya kuimarisha uaminifu, weledi na ushindani wa sekta ya habari katika uchumi wa kisasa unaotegemea taarifa sahihi na zenye kuaminika.


Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji (ABC) uliofanyika Februari 13, 2026 jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, amesema ithibati inalenga kujenga taaluma yenye misingi imara ya kitaaluma, maadili na uwajibikaji kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229.

Kwa mujibu wa Wakili Kipangula, ithibati si chombo cha kudhibiti maudhui, bali ni utaratibu wa kuweka viwango vinavyolinda hadhi ya taaluma na kuimarisha imani ya umma kwa vyombo vya habari na kwamba katika mazingira ya sasa ya ushindani wa kidijitali, uaminifu wa chanzo cha habari ndiyo mtaji mkubwa wa chombo husika.

Ameongeza kuwa vyombo vya utangazaji vinavyowekeza katika weledi wa rasilimali watu wake vinajiweka katika nafasi bora ya kuvutia wawekezaji, matangazo na ushirikiano wa kimataifa, kwa kuwa soko la habari linazidi kuthamini ubora na uwajibikaji.

Kwa upande wa wadau wa mkutano huo ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeelezwa kuwa ushirikiano kati ya msimamizi wa maudhui na wadau wa tasnia ni nguzo muhimu katika kujenga sekta imara, inayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Hatua ya kuimarisha ithibati inaonekana kuwa sehemu ya mkakati mpana wa Serikali wa kukuza taaluma za ubunifu na mawasiliano kwa viwango vinavyokidhi mahitaji ya kitaifa na kimataifa, huku ikihakikisha kuwa sekta ya habari inabaki kuwa mhimili wa uwazi, uwajibikaji na maendeleo endelevu.

Waandishi zaidi ya 3,200 kati ya 3,900 walioomba vitambulisho vya uandishi wa habari (Press Card) wamethibitishwa baada ya kukidhi vigezo vya kisheria, hali inayoonesha mwitikio chanya wa wadau na utayari wa sekta kujiimarisha kitaaluma.


Friday, February 13, 2026

SERIKALI YATOA NAFUU KWA WAWEKEZAJI WA MAUDHUI YA HABARI MTANDAONI

 

SERIKALI imechukua hatua ya kihistoria ya kuchochea ukuaji wa sekta ya habari za kidijitali nchini kwa kupunguza kwa kiwango kikubwa ada za leseni kwa wanablogu na wakusanyaji wa maudhui mtandaoni, hatua inayolenga kuondoa vikwazo vya gharama na kufungua fursa zaidi kwa wabunifu wa maudhui.

Hatua hiyo imetangazwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji (ABC) Februari 12, 2026 jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, ada ya leseni kwa wakusanyaji wa maudhui mtandaoni imepunguzwa kutoka Shilingi 1,000,000 hadi Shilingi 100,000 kwa mwaka, huku ada ya fomu ya usajili ikishuka kutoka Shilingi 100,000 hadi Shilingi 20,000.

Aidha, ada ya leseni kwa blogu imepungua kutoka Shilingi 500,000 hadi Shilingi 50,000 kwa mwaka, na fomu ya usajili kushuka kutoka Shilingi 50,000 hadi Shilingi 10,000.


Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Waziri Mwinjuma amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya utafiti wa kina na majadiliano ya kimkakati yaliyodumu kwa takribani mwaka mmoja kati ya Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN) na Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), yakilenga kuondoa changamoto za gharama zilizokuwa zikikwaza ukuaji wa uandishi wa habari za kidijitali nchini.


Katika hatua nyingine, Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA, Andrew Kisaka, alitangaza msamaha wa ada ya leseni kwa mwaka mmoja kwa waandishi wa habari wanaoanzisha mitandao ya habari watakaotambulika kama “amateur”, ili kuwapa nafasi ya kujitambulisha rasmi na kukuza vipaji vyao bila mzigo wa kifedha.

Awali, mwombaji wa kuanzisha mtandao wa habari alitakiwa kulipa ada ya maombi ya Shilingi 50,000 na ada ya leseni ya Shilingi 500,000 kwa mwaka.

Tangazo hilo limepokelewa kwa furaha kubwa na wamiliki wa mitandao waliohudhuria mkutano huo wa siku mbili, ambapo baada ya kutangazwa rasmi walishangilia na kupiga makofi kuonyesha kuunga mkono hatua hiyo.


Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni wanachama wa Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN), Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), MOAT, NIBA, Wakongwe RTD, Baraza la Habari Tanzania (MCT), MISA Tanzania na EACO.


Thursday, February 12, 2026

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI WABAINISHA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI KATIKA UTANGAZAJI VIJIJIN

Meneja Kitengo cha Utangazaji Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akiwasilisha mada kwenye mkutano huo.

Changamoto za Uwekezaji katika Utangazaji Vijijini Zabainishwa.

Changamoto mbalimbali zimeibuliwa kuhusu hali ya uwekezaji katika sekta ya utangazaji vijijini, huku ikielezwa kuwa bado kuna pengo kubwa kati ya maendeleo ya teknolojia mijini na hali ilivyo katika maeneo ya vijijini.


Akizungumza katika mjadala kuhusu Hali ya Uwekezaji wa Utangazaji Vijijini, mchangia mada alieleza kuwa licha ya teknolojia kukua kwa kasi katika miji mikubwa, vijijini maendeleo hayo bado ni hafifu. Hali hiyo imechangia kuwepo kwa changamoto nyingi kuliko fursa katika sekta ya habari vijijini.

Imeelezwa kuwa uwekezaji umekuwa ukikwama mara kwa mara kutokana na ukosefu wa wataalamu. Vijana wengi wenye elimu na ujuzi wamekuwa hawako tayari kubaki vijijini, wakihamia mijini wakivutiwa na kasi ya maendeleo na fursa zinazoonekana kuwa nyingi zaidi.


Aidha, changamoto ya nishati ya umeme pamoja na gharama na upatikanaji wa matengenezo ya vifaa vya utangazaji imeelezwa kuwa kikwazo kikubwa. Vilevile, taasisi nyingi zinakabiliwa na tatizo la wafanyakazi kutokubali kupangiwa vituo vya kazi vijijini.


Licha ya ukweli kwamba vijijini kuna maudhui muhimu yanayochangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa taifa, kasi ya uwekezaji kutoka kwa wadau wa habari bado ipo chini. Takwimu zinaonesha vijana wengi wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 wanahama vijijini kwenda mijini.


Kwa mfano, takwimu za sensa zinaonesha kuwa Dar es Salaam imeendelea kupokea idadi kubwa ya wahamiaji. Kutoka takribani watu milioni 2 katika sensa ya awali, hadi kufikia zaidi ya milioni 5.3 katika Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022. Inakadiriwa kuwa karibu asilimia 50 ya vijana wanaohamia jijini humo wanatoka vijijini, wakivutiwa na taswira ya Dar es Salaam kuonekana kama kitovu cha fursa na mafanikio.

Sehemu ya Washiriki katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa vyombo vya Utangazaji (ABC 2026) ulioanza leo tarehe 12 na kutarajiwa kutamatika kesho 13 Februari 2025, Jijini, Dodoma.

Mapendekezo ya Maboresho

Ili kukabiliana na changamoto hizo, imependekezwa kuwa:


Kila kituo cha utangazaji kiunde mkakati maalum wa kutambua, kuibua na kuanisha fursa zilizopo vijijini.


Vijana wapewe elimu ya kujitambua inayozingatia mazingira halisi ya sasa.


Maboresho ya sera za sekta ya utangazaji yafanyike ili kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji vijijini.


Miundombinu ya nishati na mawasiliano ya mtandao iboreshwe.


Serikali itoe ruzuku kwa vituo vya habari vinavyofanya kazi vijijini ili kuviwezesha kujiendesha kwa ufanisi.


Imeelezwa kuwa utekelezaji wa mapendekezo hayo unawezekana kwa kuwa jamii sasa imepata uelewa mpana wa aina ya elimu na maendeleo inayoyahitaji.

Sehemu ya Washiriki katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa vyombo vya Utangazaji (ABC 2026) ulioanza leo tarehe 12 na kutarajiwa kutamatika kesho 13 Februari 2025, Jijini, Dodoma.

Mkutano Mkuu wa Vyombo vya Utangazaji

Hoja hizo zimejadiliwa katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji, unaofanyika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka Februari 13.


Kitaifa, maadhimisho hayo yanafanyika katika makao makuu ya nchi, Dodoma, yakiwa na kauli mbiu: “Matumizi ya Teknolojia katika Kupanua na Kuboresha Huduma za Utangazaji Vijijini".