ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 14, 2026

HOTUBA NZIMA YA NAIBU WAZIRI WA HABARI AKITOA TAMKO LA SERIKALI KUSHUSHA GHARAMA ZA USAJILI MITANDAO

 NA ALBERT G.SENGO/DODOMA

SERIKALI imechukua hatua ya kihistoria ya kuchochea ukuaji wa sekta ya habari za kidijitali nchini kwa kupunguza kwa kiwango kikubwa ada za leseni kwa wanablogu na wakusanyaji wa maudhui mtandaoni, hatua inayolenga kuondoa vikwazo vya gharama na kufungua fursa zaidi kwa wabunifu wa maudhui. Hatua hiyo imetangazwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji (ABC) Februari 12, 2026 jijini Dodoma. Kwa mujibu wa tangazo hilo, ada ya leseni kwa wakusanyaji wa maudhui mtandaoni imepunguzwa kutoka Shilingi 1,000,000 hadi Shilingi 100,000 kwa mwaka, huku ada ya fomu ya usajili ikishuka kutoka Shilingi 100,000 hadi Shilingi 20,000. Aidha, ada ya leseni kwa blogu imepungua kutoka Shilingi 500,000 hadi Shilingi 50,000 kwa mwaka, na fomu ya usajili kushuka kutoka Shilingi 50,000 hadi Shilingi 10,000.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment