ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 14, 2025

R.I.P CHIKO USHINDI WAKUBANZA

 

R.I.P CHIKO USHINDI WAKUBANZA
"Ni huzuni kubwa katika tasnia ya soka barani Afrika baada ya kuthibitishwa kifo cha aliyekuwa mshambuliaji wa klabu za TP Mazembe, YANGA na AS Vita Club (VClub), Chico Ushindi, amefariki dunia JANA Jumamosi, ya December 13".

KUMBUKUMBU:
Chico Ushindi anakumbukwa kama mmoja wa mawinga mahiri waliowahi kuichezea klabu hizo kubwa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, pamoja na Young Africans ya Tanzania akitoa mchango mkubwa katika mafanikio yao kwenye mashindano ya ndani na ya kimataifa.

Akiwa mshambuliaji aliyetoa kila alichokuwa nacho uwanjani, Chico ameacha kumbukumbu za ari, kujituma na nyakati zilizowasisimua mashabiki wa soka la Kongo.

Mchango wake kwa klabu mbili kubwa zaidi nchini humo hautasahaulika kamwe.

Atakumbukwa milele kwa kufunga bao la kwanza rasmi katika Uwanja wa Japoma, Douala, mwezi Januari 2021 — tukio la kihistoria katika soka la Afrika.

Kifo chake kimeacha pengo kubwa kwa familia yake, marafiki, pamoja na jamii nzima ya michezo, hususan mashabiki wa TP Mazembe na AS Vita Club.

Familia ya michezo na wadau mbalimbali wameendelea kutoa salamu za rambirambi, wakimtaja marehemu kama mchezaji aliyekuwa na nidhamu, kipaji na mchango mkubwa katika maendeleo ya soka la ushindani.