ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 15, 2025

RATIBA NZITO YA SOKA HII LEO: MANCHESTER UNITED, ROMA, FENERBAHCE VITANI

 

Leo hii kuna mechi kibao sana ambazo zitapigwa  kule Uingereza pia kuna mechi kali ya Derby Country atakiwasha dhidi ya Sheffield Wednesday kule ugenini huku tofauti yao kwenye msimamo ukiwa ni pointi 16. 

Vilevile ligi nyingine ya  SERIE A ambapo AS Roma atamenyana dhidi ya Como 1907 ambao wananolewa na Fabregas huku wakiwa ni moja ya timu ngumu kabisa msimu huu. Roma wao wamekuwa na mwendelezo mzuri, hivyo hii ni mechi ya kibabe haswa. Nani kushinda mechi hii?. .

EPL kuna mechi ya kibabe kati ya Manchester United vs AFC Bournemouth ambapo mara ya mwisho kukutana hawa wawili walitoa sare, hivyo leo hii kila timu inagitaji ushindi huu. 

LALIGA pia kuna kivumbi kati ya Rayo Vallecano vs Real Betis ambapo tofauti ya pointi kati yao hadi sasa ni 7, huku msimu uliopita kwenye mechi zote mbili za ligi walizokutana walitoa sare. Je kwenye mechi hii ya kwanza ya mzunguko huu, nani anaenda kuibuka mbabe?. 

Uturuki kule sasa, SUPER LIG itaendelea kwa mechi moja kati ya Fenerbahce atakipiga dhidi ya Konyaspor ambao mpaka sasa wameshinda mechi 4 kwenye michezo 14 waliyocheza huku wenyeji yeye akishinda 9. Kila timu inahitaji ushindi huu asogee mbele zaidi. Je nani kushinda leo?. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment