ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 14, 2011

ROCK CITY NA BARABARA ZAKE ZA MAWE.

Maajabu hayaishi ndani ya jiji la miamba nazungumzia Rock City, Mwanza, Thamani za miamba zimeendelea kutumika inavyopaswa katika kunakshi maandhari ya jiji.

Mawe hayaja tumika tu katika kutengeneza misingi ya nyumba, kujenga nyumba juu mpaka chini au pengine kujenga visima, Eh bana eee! kwa sasa mawe haya ya Rock City yamekuwa mbadala wa lami na yanatumika kutengeneza barabara,

Katika hili mawe makubwa makubwa toka katika miamba huvunjwa vunjwa na kuwa vipande vidogo, yakapangwa kwa ustadi kuanzia mwanzo wa barabara hadi mwisho yakakamilisha ujenzi wa barabara imara kufanya mwonekano nadhivu wa barabara unaorahisisha shughuli za usafirishaji.



Katika ujenzi wa barabara aina hii hutumii simenti labda katika kingo na mifereji yake pembezoni kwaajili ya kupitisha maji, ila barabara yenyewe pale kati ni kuyapanga tu mawe kisha ukajaza udongo kidogo kuyafanya yakae sawia.

Zoezi kama hili kwa kila mpango unapoanzishwa na halmashauri ya jiji la Mwanza limekuwa ajira kwa vikundi mbalimbali hasa vya akinamama wale walio mafundi wa kuponda mawe kwani tenda zikitoka wao na vikundi vyao hunufaika kwa kupata posho ya malipo kwa ukusanyaji mawe hivyo kupunguza makali ya maisha.

Kwa upande wa wananchi wao wanasema kuwa wanaishukuru serikali ya mkoa kwa ubunifu huo, kuwanusuru na makorongo na madimbwi ya maji yaliyokuwa yakisababishwa na maji kutuama yakizua urahisi wa usafiri, usafirishaji na usambazaji huduma hivyo watumie changamoto hiyo kuboresha maisha ya wananchi wake sambamba na maadhari ya jiji.

Barabara ambazo zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia hii rahisi inayotumia nguvu shirikishi ya wananchi jijini Mwanza ni pamoja na Kitangiri makaburi, Butimba na Igogo.

NAWAOMBA RADHI WASOMAJI WANGU.

Habari zenyu wasomaji wa blog ya G Sengo.

Napenda kuwaomba radhi kwa matatizo ambayo yametokea ya kufutika kwa post zote nilizoziweka tarehe 12 na 13 kwa siku nzima ya jana, na hata kushindikana kutundika habari yoyote mtandaoni kwa siku nzima.

Tatizo kubwa lililosababisha kutokea kwa yote hayo ni suala la marekebisho yaliyokuwa yakifanywa na wenzetu wa google.com ambao wao ndiyo wanatupa huduma hii.


NAO WALITUPA TAARIFA KAMA IFUATAVYO:-
Blogger Status
Friday, May 13, 2011
To get Blogger back to normal, all posts since 7:37am PDT on Weds, 5/11 have been temporarily removed. We expect everything to be back to normal soon. Sorry for the delay.
Posted by at 04:25 PDT


Asante sana,
Imetolewa na Albert G.Sengo.
Mmiliki wa: www.gsengo.blogspot.com

Thursday, May 12, 2011

HAFLA YA KUWAPONGEZA WAANDISHI WA MKOA WA MWANZA WALIOPATA TUZO 2010 MAY 11/2011 ILIVYOFANA.

Emmanuel Chacha wa ITV - Aliyeshinda Tuzo ya Habari Bora ya Biashara kupitia gazeti la Raia Mwema.

Sheilla Sezzy wa Mwananchi - Tuzo ya Habari Bora ya Afya 2010.

Cosmas Makongo wa ITV - Tuzo ya Habari bora ya Biashara 2010-2011 Tuzo anayoishikilia mwaka wa pili mfululizo.

Shughuli ya kuwapongeza ilifanyika jana usiku katika moja ya kumbi nzuri za Lakairo Hotel ambapo waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali walipata fursa ya kujumuika ktk hili.Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mh.Said Amanzi na washindi
“Nawashukuru sana kwa kuwa mmeisaidia Halmashauri ya jiji la Mwanza kupata heshima katika utumishi sekta mbalimbali na pia kuchangia kuleta amani katika jiji la Mwanza kwa kuwasaidia watendaji wa serikali ngazi zote kufikisha ujumbe wa kile kilichonuwiwa kwa wananchi.” Kauli ya mgeni rasmi.

Kama ilivyo ada kwa kila familia huwa ina kichwa kimoja ambacho kisipoonekana kusanyikoni pana boooa!! basi familia ya habari Mwanza akikosekana kamanda huyu shughuli hainogi. Ni John Maduhu 'Zagamba' ambapo yeye alitupia kitu cha zawadi kwa washindi huku akitanguliza maneno yake 'Ungependa nisemeee!' Ni zawadi gani chekshia picha inayofuata..Kale kawimbo ketu "FU-NGU-A, TU-O-NE yaliyomo"

Sheilla Sezzy wa Mwananchi akifungua zawadi yake aliyo zawadiwa na kamati.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Fredrick Katulanda, Sambamba na kuwapongeza washindi hao kwa kuleta changamoto pia amewaomba MPCT kuona mpango katika zama zijazo Tuzo zitolewe mikoani, tofauti na sasa kwa Tuzo hizo kufanyika jijini Dar es salaam pekee na kisha akasema “Mwanza kuna waandishi wengi wazuri na katika hili tungepata Tuzo nyingi sana zaidi ya hizi ila tatizo wengi sie ni wavivu kushiriki-TUAMKE!”

Mkurugenzi wa UTPC
“Rais hivi majuzi kasema viongozi wa serikali watoe ushirikiano kwa waandishi wa habari ili kusaidia watanzania kujua mafanikio, matatizo yao na mapungufu nao wapate kushiriki au kuchangia katika harakati za utatuzi, Wito kwa mkurugenzi wa jiji la Mwanza aondoe urasimu uliopo wa kutoa habari kwa kutenga siku maalum kwa waandishi kupata habari ili jamii itambue nini kinafanywa na Halmashiauri zake”

Tabasamu la ukweli Sheilla na Asia.

Crew ya Mwananchi Communication Mwanza kutoka kushoto ni Fredrick Katulanda, Sheilla Sezzy na Ray Naluyaga ambaye ni Lake Zone Bureau Chief wa Mwananchi.

Mie in the house'

Marry Misoji na braza Katulanda ndani ya mitegozzZ.

Kuchangamana muhimu.

KWAHERI DA-JETRUDA MACHIBYA.

Ilikuwa ni asubuhi ya jumapili ya tarehe 8/05/2011 ndipo mwenzetu ndugu yetu, dada yetu, maarufu kwa kifupisho cha jina la 'JETU' alipotutoka, huu ni msiba, hakika umeacha simanzi kwa familia yako na marafiki kwani utakumbukwa kwa ushiriki wako katika shida na raha, ucheshi na uchangamfu kwa kila aliyekusogelea. Pumzika kwa amani. Kutoka kushoto ni Lucy Donard, John Katalambula, Francis Kaseko, Mrs. J.Katalambula, Modekai, Vailet Kaseko, Victor Kaseko, ...sis, Eva Kiyuga na Albert Sengo.
Picha ya familia mara baada ya mazishi ya dada yetu 'JETU' yaliyofanyika jana tarehe 11/05/2011 katika makaburi ya Kitangiri, Bwiru jijini Mwanza.

RAIS MUSEVENI KUAPISHWA LEO

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni,anatarajiwa kuapishwa kwa muhula mwengine hii leo siku ya Alhamisi. Anaapishwa huku kukiwa na wingu la shutma kwa utawala wake kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya upinzani.

Katika siku za hivi karibuni serikali imelaumiwa kwa namna walivyokabiliana na maandamano ya upinzani na kusababishwa kulazwa hospitali kwa mwanasiasa wa upinzani, Dk Kizza Besigye pia kumezua shutma kali.

Wakati atakapoapishwa kwa muhula mwengine,Yoweri Museveni atakuwa amejiongezea muda wa kukaa madarakani kwa takriban miaka thelathini na alipoingia madarakani mwaka 1986 alisema tatizo la viongozi wa Afrika ni kukaa kwenye utawala kwa muda mrefu sana. Kwa miaka mingi amefanya juhudi kuijenga upya nchi ya Uganda baada ya nchi hio kuwa kwenye vita na utawala mbaya.


Bado anaungwa mkono na wengi lakini wadadisi wanaona kuendelea kutegemea jeshi kunaweka nchi hiyo katika mazingira magumu. Kiongozi wa upinzani, Dokta Kizza Besigye,bado yuko nchini Kenya baada ya kupata matibabu kufwatia kushambulia kwake na polisi.

Mapema siku ya Jumatano,Besigye alisema kuwa alizuiwa kupanda ndege kutoka Nairobi kwenda Uganda, baada ya kupatiwa matibabu nchini Kenya na haijulikana kama atajaribu kusafiri hii leo kwenda nyumbani wakati Rais Museveni anaapishwa - hatua ambayo italeta aibu kwa serikali. Baadhi ya viongozi walioalikwa kwa sherehe za kuapishwa kwa Rais Museveni waliwasili Kampala siku ya Jumatano huku wengine wakitarajiwa hii leo siku ya Alhamisi.
PICHA Rais Kikwete akipokewa kwa maua muda mfupi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Entebbe nchini Uganda tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa Yoweri Kaguta Museveni.

KONA YA MATUKIO: LIBENEKE JIPYAAaaaa hewani!

Tunapenda kulitambulisha wadau wote libeneke jipya la KONA YA MATUKIO ambapo nia na lengo kubwa ni kuleta matukio yanayotokea kila siku katika Jamii yetu na Duniani kwa Ujumla.. pia kutakuwa na Matukio ya papo kwa hapo yani Breaking News Endelea kuwepo kila muda kujua nini kitatokea.

TEMBELEA www.konayamatukio.blogspot.com

Wednesday, May 11, 2011

MAADHIMISHO YA SIKU YA MALARIA HATIMAYE YAFANYIKA LEO MWANZA / SABABU ZATAJWA

Kutoka mkoani Mwanza inatajwa kuwa kwa mwaka uliopita 2010 takribani watu wapatao 309,163 wameugua malaria, huku idadi ya watu 1,063 wakiwemo watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakitajwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.Mganga mkuu Dr.Mmasi.
Hayo yamebainishwa leo katika Taarifa fupi ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani yaliyokwenda sambamba na upimaji bure wa malaria uliyofanyika kwenye viwanja vya Ghand Hall jijini Mwanza nakusomwa na Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dr. Meshack Massi.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa wakazi wa Mwanza wako katika hatari kubwa kupata malaria kutokana na kuwa katika ukanda wa mazalio ya mbu waenezao ugonjwa wa malaria kwa vile sehemu kubwa ya ardhi inatuamisha maji kwa muda mrefu, kupata mvua za vuli na masika kwa mwaka sambamba na eneo lake kubwa la ardhi kuzungukwa na mwambao wa ziwa Victoria.

Wananchi kwa zamu wasubiri kupima malaria ndani ya Ghand hall Mwanza.
Jamii imepata athari kubwa kutokana na ugonjwa wa malaria ikiwa ni pamoja na kudhoofu kwa afya ambayo ni nguvu kazi kwa watu wake ambayo imesababisha wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo na kuwa chanzo cha umasikini ikiwa ni zao la kushindwa kutekeleza majukumu ya shughuli za kila siku za maendeleo.

Ili kupata dozi kwa tiba ya malaria, vipimo vya uzito muhimu.
Dr. Massi amezitaja baadhi ya changamoto zinazojitokeza katika mapambano dhidi uganjwa wa Malaria kuwa ni pamoja na jamii kuchelewa kwenda kwenye vituo vya tiba kupatiwa matibabu pindi wanapougua (delay in health seeking behavior), baadhi ya wagonjwa kutozingatia ushauri wa matibabu sahihi ya malaria unaotolewa na wataalam wa afya na imani potofu ya matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu.

Kujiandikisha.
Aidha halmashauri ya jiji la Mwanza imejiwekea malengo kupunguza maambukizo ya ugonjwa wa malaria toka asilimia 36.1 hadi 25 na kupunguza kiwango cha vifo vya watoto chini ya miaka 5 vinavyotokana na malaria kutoka 8/1000 hadi 5/1000 kwa mwaka.

Upimaji.
Shughuli zitakazo fanyika kufikia malengo hayo ni pamoja na kuhamasisha matumizi endelevu ya vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu vilivyogawiwa ngazi ya kaya, kuhamasisha usafi wa mazingira, kuhamasisha jamii kuwahi kwenye vituo vya tiba ili kupata matibabu sahihi ya ugonjwa wa malaria na kuwahimiza wanawake wajawazito kuwahi kliniki ili kupata kwa wakati dawa ya SP inayowakinga dhidi ya maambukizo ya malaria.

SABABU YA JIJI LA MWANZA KUFANYA MAADHIMISHO HAYO LEO
Siku ya malaria duniani huadhimishwa tarehe 25 April ya kila mwaka ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo yalifanyika kitaifa tarehe 29 April mkoani Arusha baada ya kuahirishwa kutokana na kuangukia siku ya jumatatu ya pasaka na katika jiji la Mwanza maadhimisho hayo yamefanyika leo tarehe 11/05/2011 kutokana na sababu zilizotajwa.

WHAT NEXT AFTER KIKOMBE CHA BABU?

Babu anakula vichwa like crazy.

Tangu habari za “Babu” wa Loliondo ziingie mitaani, mchungaji mstaafu huyu Ambilikile Mwasapila amekuwa akipata wateja wa kumwaga na waliopo kwenye “waiting list” yake si chini ya 25,000.

Mtaalamu huyu wa miti shamba anaaminika kuwa na “magical cure” kwa magonjwa yote sugu ikiwa ni pamoja na gonjwa la UKIMWI. Sijajua kwa hakika ni kiasi gani anauza dawa zake ila kwa kifupi babu huyu kama hakika dawa zake zinatibu pumu, kisukari, ukimwi n.k basi once foleni inapungua huko Loliondo blog hii itamtafutia sponsors na kumleta kiwanja kufanya kweli.
Ni wakati muafaka wa serikali ya Tanzania kuangalia na kufanya utafiti wa hali ya juu kuhusu dawa za retired pastor huyu ili kumuweka kwenye mazingira mazuri ya kufanya kazi yake ya kutibu watu.Taifa linajengwa na watu wenye afya njema,just tazama viongozi wangapi wa serikali waliokwenda Loliondo kupata tiba.

Formula yake inaweza kuwa ni big deal internationally na kuiweka Tanzania kwenye ramani ya moja ya nchi zenye watafiti wa hali ya juu,japo ni ishu ya miti shamba.Nina imani babu huyu na dawa zake ni msaada mkubwa kwa watanzania.Who would have thought tiba ya “ngoma” itagunduliwa na mtanzania?

Ngorongoro hapaingiliki sasa maana kuna foleni kubwa ya magari yenye wagonjwa na wateja wanaosubiri huduma za Mchungaji Ambilikile. Watu toka kona zote za Tanzania plus Kenya na Uganda wanamiminika Loliondo kila kukicha.Big up to “Babu” Ambilikile kwa kuja na tiba hizi.


By tunyfish.

DK SLAA ALIPO CHAFUA HEWA KWA PINDA.

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa amechafua hali ya hewa katika Jimbo la Katavi lililopo Mkoa mpya wa Katavi ambalo Mbunge wake ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya kuwaambia wananchi kuwa: "Kiongozi huyo anafurahia anasa za uwaziri mkuu."Dk Slaa alifanya mikutano mitatu ya hadhara jimboni humo juzi katika vijiji vya Majimoto, Mbende na Usevya, alikozaliwa Pinda ikiwa ni mfululizo wa maandamano na mikutano inayofanywa na chama hicho katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

"Nikiangalia hali ya maisha yenu wananchi wa jimbo hili, Mkoa wa Rukwa na Katavi si haki ninyi kuendelea kuishi kwenye nyumba za udongo na nyasi wakati kodi zinafujwa kila kukicha kwa matumizi ya anasa ya Serikali hii," alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema mbali na anasa hiyo, semina elekezi kwa mawaziri inayoendelea mkoani Dodoma imegharimu fedha nyingi na kwamba iwapo serikali ingekuwa inawajali wananchi wake, ingeweza kujenga shule za sekondari katika jimbo zima la Waziri Mkuu kwa kutumia fedha zinazotumika katika semina hiyo.


Rais akiongea wakati wa ufunguzi wa semina elekezi.
"Kikwete amewateua mawaziri kisha anawaandalia semina za kazi gani? Kama hawana uwezo wa kuongoza si angeteua wabunge wengine? Alisema mawaziri walioshindwa kufanya kazi wajiondoe wenyewe. Kwani anajua mawaziri wake hawafai, lakini badala ya kuwafukuza anawapa ruksa wajiondoe wenyewe!"

Kutoka kushoto waziri mkuu Mh.Pinda, waziri mkuu mstaafu Msuya na Mh.Rais Jk.
"Pinda, kwa siku moja akiwa kule bungeni hupata posho ya Sh200,000 ambayo inazidi mshahara wa mwezi mmoja wa mwalimu, hata polisi anayelinda usalama wenu. Lakini magari anayotumia kwenye msafara wake yasiyopungua 30 gharama yake haipungui Sh600 bilioni. Gharama ya gari analotembelea mbunge wenu ni sawa na kujenga vituo vitano vya afya."

Dk Slaa aliyekuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka jana alisema, inasikitisha kuona Mbunge wa Katavi anakuwa mbinafsi kwa kujiwekea umeme wa jua kwenye nyumba yake pekee katika Kijiji cha Usevya badala ya kuupeleka kwa wananchi wote.


Habari :Edwin Mjwahuzi, Mpanda na Boniface Meena Sumbawanga
Habari zaidi tembelea www.mwananchi.co.tz

Tuesday, May 10, 2011

WAHARIRI WA GAZETI LA DER TZITUNG WAZUA BALAA! WAVUNJA SHERIA WAIEDIT PICHA YA HILLARY CLINTON AKISHUHUDIA MAUAJI YA OSAMA WHITE HOUSE.

Hillary Clinton's expression, right hand clasped over her mouth in astonishment, is largely responsible for making the above photo iconic--and, to at least one newspaper, sexually suggestive.In the photo, President Obama and his national security team are huddled around a conference table in the White House Situation Room, watching CIA director Leon Panetta narrate last Sunday's raid on Osama bin Laden's compound. The mood is clearly tense.

When Women's Wear Daily consulted a coterie of photo editors and designers about why the image is "destined to be one for the history books," Clinton was foremost in their responses. "The Hillary Clinton expression is the one that holds the photograph fully," Time's photo director told the magazine.

"You can see 10 years of tension and heartache and anger in Hillary's face," Conde Nast's Scott Dadich agreed. Turns out she was probably just coughing during that crucial moment captured by White House photographer Pete Souza. But nevertheless, the image still proved a bit too racy for at least one of the many newspapers that printed it.

That would be the Ultra-Orthodox Hasidic broadsheet Der Tzitung, published in Brooklyn. The paper photoshopped Clinton, as well at the only other woman who could be seen in the room--Audrey Tomason, the national director of counterterrorism--out of the frame.

"Apparently the presence of a woman, any woman, being all womanly and sexy all over the United States' counterterrorism efforts was too much for the editors of Der Tzitung to handle," noted the prominent women's blog Jezebel.

Indeed, "The Hasidic newspaper will not intentionally include any images of women in the paper because it could be considered sexually suggestive," Rabbi Jason Miller explains in The Jewish Week. Though he notes that the publication's "fauxtograpphing" may in fact be a graver act against their religious tenets: "To my mind, this act of censorship is actually a violation of the Jewish legal principle of g'neivat da'at (deceit)."

Beyond that, Der Tzitung's editors apparently missed or blatantly ignored the guidelines stipulated on the official White House Flickr page, where the photo was released for use by news organizations: "The photograph may not be manipulated in any way."

The White House has not issued a response on the altered image.

UPDATE: The editors of Der Tzitung have apologized to the White House for altering the photo and responded to the Wasington Post with a comment clarifiying their position: "In accord with our religious beliefs, we do not publish photos of women, which in no way relegates them to a lower status... Because of laws of modesty, we are not allowed to publish pictures of women, and we regret if this gives an impression of disparaging to women, which is certainly never our intention. We apologize if this was seen as offensive."

SHULE ZA MSINGI ZATAKIWA KUANZISHA BENDI.

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika (mb) amezitaka kamati za shule za msingi kuhakikisha zinaansisha bendi za shule ili kuwavutia wanafunzi kupenda kuhudhuria masomo.

Uzoefu unaonyesha kuwa wanafunzi wengi wa shule za msingi hupenda kuungana na wenzao kwa mvuto wa bendi. mnamo mwaka 2002 Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ililitambulisha shirika lisilo la kiserikali la tanzania Environmental Health and Educational Services la Dar es Salaam kuwa linajishughulisha na ufufuaji wa vivutio mbalimbali vya watoto shuleni ikiwemo na usambazaji wa vifaa vya bendi vya bei nafuu.


Enzi hizo bendi ya shule ya msingi tumaini bukoba picha by Anthony Brown Masai.

Aidha, Shule za msingi hazina bendera ya Taifa katika maeneo yao. Moja katika mambo wanayofundishwa watoto ni uwepo wa Bendera ya taifa, rangi zake na maana ya rangi hizo. Wanafunzi wataelewa vizuri somo hili kwa kuiona bendera yenyewe. Wizara inasiositiza umuhimu wa shule zote kupeperusha bendera ya Taifa.

Mwisho, Ofisi ya waziri Mkuu - TAMISEMI inasisitiza kuwa michezo ni sehemu ya Elimu shuleni. Kila shule ni lazima kuwa na vifaa vya michezo na kuwashirikisha wanafunzi katika michezo. Mashindano ya michezo kwa wanafunzi katika ngazi mbalimbali yatafanyika hadi ngazi ya Taifa.

IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 09/05/2011.

14TH MAY NDANI YA SUN CIRO Adjha-djha-djhaaa!

MAJEMBE NA WENYE NCHI WOTE TUNAKUTANA SUN CIRO WEEKEND HII ...HAPA CODEREDTZ, HAPA TROOPS YA SO SO FRESH; DJ BULLAH NA NCHA KALIH...KWA BUKU 10 NA BUKU 15 VIP NJOO TUJIRUSHE NA SMIRNOFF IN THE MIX...KITU CHA SATO 14TH MAY 2011 KUANZIA MISHALE YA NNE USIKU HADI MAKUKUZ?!

sms by Ncha kali.

SPIKA BILA WAYA .....

Kampuni moja ya vifaa vya elektroniki nchini Japani ya Pioneer hivi sasa inauza Spika za aina mpya kabisa ambazo hazihitaji kufungwa waya zinazojulikana kama -Kai-Tele-kun VMS-700-K.

Wireless speakers hizo zinazopokea mawimbi ya sauti kutoka kwenye Televisheni moja kwa moja zina uwezo wa ufanya kazi hata zikiwa katika umbali wa mita 30.

Kampuni hiyo inasema kuwa spika hizo zitawasaidia akinamama wanaotaka kusikiliza matangazo ya Redio ama ya TV wakiwa jikoni bila kulazimika kutandaza waya.Spika hizo kwa sasa zinauzwa hapa apani Yeni Elfu 20 ambazo ni takriban Shilingi Laki tau na Elfu 60 kwa pesa za kitanzania. ( I Yen~Tsh.18.00). Mauzo hayo yameanza hivi karibuni tu…


KUHAKIKI TEMBEA
http://www.japantoday.com/category/new-products/view/wireless-speaker

KILA KUKICHA .... AJALI

Kila kukicha ajali zinaripotiwa kutokea, na nyingi kati ya hizo ni ajali zinazohusisha kwa namna moja au nyingine waendesha pikipiki hii nimeishuhudia muda mchache uliopita pale dreva wa pikipiki alipokuwa akijaribu kuovateki upande wa kushoto kwenye kona finyu ya kipitashoto cha barabara ya Kenyata karibu na jengo jipya la PPF Mwanza...dreva amepata michubuko kimtindo..

Kwa Mwanza imekuwa kawaida kwa madreva wa pikipiki kujichukulia sheria mkononi pindi inapotokea mmoja wao kapatwa ajali, hawatizami nani mkosaji wanachojua ni kumwadhibu dereva wa chombo kingine kwa kumpatia kichapo au kumdhuru kwa aina yoyote ile au hata pengine kumchomea moto chombo chake cha usafiri.

Lakini pamoja na hili pia kunatukio lililoripotiwa mwishoni mwa mwaka jana desemba 23 ambapo kibao kiligeuka pale mwendesha pikipiki mmoja alipouawa na wananchi katika wilaya ya Ukerewe, Mwanza baada ya kugongana na baiskeli na kusababisha kifo cha mmoja wa watu wawili waliokuwa wakisafari kwa baiskeli hiyo.


Mwendesha pikipiki aliyeuawa alikuwa Eric Elius [34] mkazi wa kijiji cha Buhima –Ukerewe,na aliyekufa baada ya baiskeli akisafiria kugongana na pikipiki hiyo ni Matha Kanyago [20] Mkazi wa Kijiji cha Chankamba – Ukerewe na mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Igombe – Ilemela Jijini Mwanza.
TUNA KAZI.

Monday, May 9, 2011

NI BIASHARA TU! NDANI NA NJE YA SOKO KUU LA MWANZA.

Muuza vitunguu na ubunifu wake katika kukabiliana na hali ya hewa eneo la nje ya soko kuu la Mwanza.

Watu toka sehemu na sehemu hufika sokoni hapa "Nianzie wapi?" anauliza Rooney.

Kwa wasomi.

Wale wa kitoweo.

Wauza ndizi, wauza viazi mviringo nao wamo kati ya wale walio kosa maeneo ya biashara kwa kupanga bidhaa zao chini nje pembezoni mwa soko. Je! Mradi mpya wa ujenzi wa Soko Kuu la Mwanza utawanusuru na kadhia hii?

Bidhaa aina mbalimbali hukutanishwa hapa, Soko kuu la jiji la Mwanza hali ni mbaya kipindi cha mvua.

Mchoro wa ramani kwa soko jipya litakalojengwa.
Mradi huu mpya wa ujenzi soko kuu la Mwanza utaanza lini?