ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 14, 2011

ROCK CITY NA BARABARA ZAKE ZA MAWE.

Maajabu hayaishi ndani ya jiji la miamba nazungumzia Rock City, Mwanza, Thamani za miamba zimeendelea kutumika inavyopaswa katika kunakshi maandhari ya jiji.

Mawe hayaja tumika tu katika kutengeneza misingi ya nyumba, kujenga nyumba juu mpaka chini au pengine kujenga visima, Eh bana eee! kwa sasa mawe haya ya Rock City yamekuwa mbadala wa lami na yanatumika kutengeneza barabara,

Katika hili mawe makubwa makubwa toka katika miamba huvunjwa vunjwa na kuwa vipande vidogo, yakapangwa kwa ustadi kuanzia mwanzo wa barabara hadi mwisho yakakamilisha ujenzi wa barabara imara kufanya mwonekano nadhivu wa barabara unaorahisisha shughuli za usafirishaji.



Katika ujenzi wa barabara aina hii hutumii simenti labda katika kingo na mifereji yake pembezoni kwaajili ya kupitisha maji, ila barabara yenyewe pale kati ni kuyapanga tu mawe kisha ukajaza udongo kidogo kuyafanya yakae sawia.

Zoezi kama hili kwa kila mpango unapoanzishwa na halmashauri ya jiji la Mwanza limekuwa ajira kwa vikundi mbalimbali hasa vya akinamama wale walio mafundi wa kuponda mawe kwani tenda zikitoka wao na vikundi vyao hunufaika kwa kupata posho ya malipo kwa ukusanyaji mawe hivyo kupunguza makali ya maisha.

Kwa upande wa wananchi wao wanasema kuwa wanaishukuru serikali ya mkoa kwa ubunifu huo, kuwanusuru na makorongo na madimbwi ya maji yaliyokuwa yakisababishwa na maji kutuama yakizua urahisi wa usafiri, usafirishaji na usambazaji huduma hivyo watumie changamoto hiyo kuboresha maisha ya wananchi wake sambamba na maadhari ya jiji.

Barabara ambazo zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia hii rahisi inayotumia nguvu shirikishi ya wananchi jijini Mwanza ni pamoja na Kitangiri makaburi, Butimba na Igogo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.