ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 4, 2017

MISA TANZANIA YAWAKUTANISHA WABUNGE NA WANAHABARI KUJADILI NAMNA NZURI YA KUSHIRIKIANA

“Tunapongeza kitendo hicho cha viongozi wetu kufikia hatua ya kuyataja hadharani majina ya wauzaji wa dawa za kulevya kwasababu jambo hili siyo rahisi na haikuwezekana huko nyuma kwahiyo kutokana na hili ni vyema wakuu wa  mikoa mingine waanze kuchukua tahadhari ya kupambana na watu watakaohamia mikoani baada ya kutangaziwa vita jijini Dar es Salaam, kwahiyo Mwanza, Tanga, Arusha nao wajipange kupambana na wafanyabiashara hawa,” alisema.

Akizungumzia kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini, Soko alisema hali siyo nzuri kwani kuna ongezeko kubwa la matumizi ya dawa za hizo na kuitaka jamii kushiriki kwa kuwaumbua wauzaji na wasambazaji kwasababu wanaishi katika jamii na siyo suala hilo kuiachia serikali pekee.

“Matumizi ya Bangi yameongezeka kwa asilimia 6.5  kwa mwaka 2015/16  ambapo watumiaji 247 walishikiliwa kwa tuhuma hizo na matumizi ya dawa za viwandani aina ya Heroine na Cocaine nayo yameongezeka,” alisema.

 OJADACT wanasisitiza kwamba ni muhimu haki itendeke katika kuwashughulikia  watakaopatikana  na hatia katika sakata hilo na biashara ya dawa za kulevya kiujumla kadri  sheria  ya kuthibiti   dawa za kulevya  ya mwaka 2015 inavyosema.

MISA TANZANIA YAWAKUTANISHA WABUNGE NA WANAHABARI KUJADILI NAMNA NZURI YA KUSHIRIKIANA


Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akiwasilisha mada kuhusu namna ya kufanya mahusiano ya kikazi kati ya bunge na wanahabari kwa baadhi ya wabunge, wahariri na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na Geofrey Adroph

 Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo mbele ya baadhi ya  wabunge pamoja na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waliofika katika semina ili kujadili jinsi ya kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Bunge na wanahabari yatakayoleta ukaribu kwa pande zote.




Baadhi ya wabunge wakichangia mada kuhusu kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Bunge(wabunge) na wanahabari pamoja na kutoa maoni yao ili kuboresha utoaji wa habari kwa wananchi boila kujali itikadiza kivyama.

Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akijibu maswali kutoka kwa wabunge katika mkutano uliowakutanisha wabunge, wahariri na waabdishi wa habari katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo.
 Mhariri mtendaji wa Jamhuri Media, Deodatus Balile akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi pamoja na wabunge walioudhuria mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma. 
 Mmoja wa waandishi wa habari akitoa changamoto anazozipata kwenye kazi zake za kila siku za kuripoti habari mbalimbali

Baadhi ya wabunge, wahariri na waandishi wa habari wakiwakwenye mkutano 


Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakfu wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamewakutanisha  wabunge pamoja na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Mkutano huu ulikuwa na lengo la kuwajengea Wabunge na Wanahabari uhusiano mzuri katika utendaji wao wa kazi. Bunge na Vyombo vya Habari ni Mihimili miwili ya dola (Mmoja ukiwa Rasmi na mwingine usio Rasmi) inayotegemeana sana katika utendaji wake wa kazi.

Kutokana na kazi kubwa ya Bunge ambayo ni kutunga sheria na kuwakilisha Umma katika mijadala mbalimbali ya maendeleo katika ngazi za Taifa na Jimbo lazima kutumia vyombo vya Habari kwenye kazi ya kutafsiri mipango na mikakati mbalimbali inayofanywa na Bunge katika lugha ambayo mpiga kura/mwananchi wa kawaida anaweza kuelewa. Lengo kuu likiwa ni kuharakisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima.

Katika siku za karibuni kumetokea changamoto mbalimbali katika utendaji kazi wa muhimili huu rasmi na muhimili huu usiokuwa rasmi, na hasa kutoaminiana na kushutumiana kwa namna moja ama nyingine. Kutokana na changamoto hizo hakuna budi kwawaandishi wa habari paamoja ili kujadili changamoto na kuja na suluhisho la changamoto hizo.



Semina hiyo imeshirikisha watu 55 ikiwa ni pamoja na wabunge mbalimbali toka vyama vyote, Wahariri wa vyombo Habari vilivyoko Dodoma na Bureau Chiefs wa vyombo vya Umma na Binafsi vilivyopo Dodoma.

AUDIO | K STAR FT DAYNA NYANGE - NITULIZE


BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Friday, February 3, 2017

'CHAKUWA' YABAINISHA CHANGAMOTO ZILIZOPO KWA WASAFIRI NA SEKTA YA USAFIRI MWANZA.

Familia ya Bi. Ashura Mohamed wa kwanza kulia mwenye tiketi akionyeshoa tiketi ya awali waliyopewa na kukatazwa kupanda basi kwaajili ya safari yake mara baada ya Polisi kwa kushirikiana na Chama Cha Kutetea haki za Wasafiri (CHAKUWA) na kituo cha radio Jembe Fm kumsaidia kupata haki zake na sasa ataweza kusafiri kuelekea jijini Dar es salaam.
Licha ya mizigo yao kuondoka na Basi walilopaswa kusafiria wasijue usalama wake huko mbele ya safari au hata ikifika jijini Dar es salaam, Familia ya Bi. Ashura Mohamed alishindwa kusafiri na kuishi maisha ya kuungaunga kutokana na kuzuiwa na wahusika wa basi la Princess Shabaha wakimweleza kuwa amezidisha mtoto mmoja. 
 MAMA huyo ambaye tangu juzi tarehe 1 mwezi Februari alipaswa kusafiri yeye, watoto wawili na bibi mmoja kutoka Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam lakini mpaka leo tarehe 3 alikwama kusafiri, lakini Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Chama Cha Kutetea Haki za Wasafiri (CHAKUWA) wamefanikisha safari yake leo asubuhi na mama huyo kulipwa stahiki zake za usumbufu alioupata.  BOFYA PLAY KUSIKILIZA ALICHOSEMA SIKU YA KWANZA

Mapema leo alfajiri Gsengo BLOG ilifika kituo cha mabasi yaendayo mikoani kwenye eneo la Nyegezi na kushuhudia mama huyo akiwa unafuu mara baada ya kupata stahiki zake ikiwa ni pamoja na kupata tiketi za kusafiri yeye na familia yake kuelekea mkoani Dar es salaam.
Elimu kwa madereva kutoka CHAKUWA.
CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WASAFIRI TANZANIA WAISHANGAA MWANZA KUTOKUWA NA UTARATIBU WA KUTOA TIKETI.
Mkurugenzi wa CHAKUWA Kanda ya Mashariki Wilson Sylvester amesema kuwa moja kati ya changamoto walizokuja kuzibainisha kwa wananchi kupitiaelimu wanayoitoa ni pamoja na abiria kujua wajibu wao pale panapotokea upandishwaji holela wa nauli, namba za simu na TIN namba kutokuwepo kwenye tiketi za abiria na pale ajali inapotokea nini haki za abiria.   BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Moja ya mabasi mkoani Mwanza na siti ya dereva.
Mazingira ya mbele kwa dereva.
Ndani.
Uchakavu wa viti vya basi na mzingira.
Air Jordan


MAJIBU:- SUALA LA MELI YA MV BUTIAMA.

Ni lini serikali itaitengeneza meli ya MV Butiama.? Haya hapa ni majibu ya serikali kutoka kwa naibu waziri Mhandisi Ngoyani;

BARAZA LA TATU LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA.

MOI1
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MOI Prof, Bakari Lembariti akihutubia wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi wa Kikao cha Tatu cha Baraza Hilo, kutoka kulia ni Naibu Katibu Baraza la Wafanyakazi hilo, Mwenyekiti wa Tughe na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt, Othman Kiloloma
MOI2
Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt Othman Kiloloma akiwasilisha ripoti ya Utendaji ya Mwaka 2015/2016, 
MOI3
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Prof, Bakari Lembariti
MOI4
Makamu mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi MOI Prof , Bakari Lembariti akimkabidhi cheti Mfanyakazi bora wa Taasisi ya  MOI kwa  Mwaka 2015/2016 Rbert Ojock na pesa TSH. mil. 4(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).


KAIMU Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MOI Profesa Bakari Lembariti jana amezindua kikao cha Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa MOI katika ukumbi wa IDDI NYUNDO katika halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam. kikao  kimehudhuriwa na zaidi ya wajumbe 50 kutoka katika kila idara, vitengo na chama cha wafanyakazi wa MOI (TUGHE) na wajumbe wa TUGHE mkoa.

Akizindua Baraza hilo Profesa, Lembariti alisema anampongeza Mh, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Alisema ” Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini MOI Mh. Zakia Meghji natumia Fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli kwa uongozi wake uliotukuka na jitihada zake za kuboresha huduma za afya hapa nchini, sote ni mashahidi“.

Aidha, Profesa Lembariti aliwakumbusha wafanyakazi wa MOI kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma ili kujenga imani kwa watanzania walio wengi ambao wanaitegemea MOI kama Taasisi pekee inayotoa Tiba ya kiwango cha juu cha rufaa kwenye Tiba ya Mifupa, upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.

Pia Profesa, Lembariti alisema ni vyema wajumbe wa Baraza la MOI wakatumia vikao vya Baraza kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili Taasisi ya MOI na kutafuta muarobaini  ili Taasisi ya MOI iendelee kutoa huduma bora,

Kwa upande mwingine Profesa,  Lembariti aliwakabidhi zawadi wafanyakazi Bora wa MOI kwa mwaka 2015/2016 ambapo, Robert Ojock na pesa TSH. mil. 4 aliibuka kidedea na kuwa mfanyakazi Bora wa MOI na kujipatia cheti na fedha taslimu kiasi cha Tshs Milioni 4, nafasi ya pili ikishikwa na Bwana Lucas Machage akijipatia cheti na kiasi cha Tshs Milioni 2 na nafasi ya tatu ikishikwa na Bi Betty Shila ambaye alijipatia  cheti na kiasi cha Tshs Milioni 1.5

Kwa upande wake ,akiwasilisha ripoti ya utendaji wa Taasisi ya Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt. Othman Kiloloma alisema kutokana na ongezeko kubwa la ajali ambazo zimepelekea ongezeko kubwa la wagonjwa MOI, Taasisi ya MOI iko kwenye mpango mkakati kabambe wa kushirikiana na baadhi ya hospitali za rufaa za pembezoni kwa kuwapeleka wataalamu kutoa huduma katika hospitali hizo na kupunguza kama si kuondoa kabisa wimbi la wagonjwa wanaopokelewa MOI.

Dkt, Kiloloma alisema kwamba Taasisi ya MOI imeendelea kuwa Kitovu cha Weledi katika matibabu ya Mifupa , Ajali , Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati ambapo mwaka 2015 MOI ilitoa utafiti bora wa mfupa mrefu wa paja duniani ,ambapo utafiti uliwasilishwa katika Taasisi ya kimataifa ya upasuaji wa mifupa duniani  ya Marekani (AOTA)
Vilevile, Dkt. Kiloloma aliwaomba wajumbe wa Baraza la MOI kutoa michango yenye tija ili kupata matibabu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Taasisi ili Taasisi iendelee kutoa huduma bora kwa watanzania

MALAIKA: NINAFANYA MPANGO WA KUMSHIRIKISHA DAVIDO, PIA KUKUTANA NA JUSTIN BIEBER.

HITMAKER wa Zogo, wakuitwa Malaika amedai kuwa tayari ameshafanya collabo na msanii mkubwa wa Sierra Leone. Kama hiyo haitoshi, Davido na Justin Bieber nao wapo kwenye menu.

“Mpaka sasa hivi nimefanya kazi na msanii mkubwa kutoka Sierra Leone na pia amenilink-up pamoja na Davido so nafikiri tutafanya kazi,” amesema Malaika.

“Na sasa hivi tunafanya kazi ya kukutana na Justin Bieber pia, sababu nimepewa ndani ya siku 10 ndio nitaweza kumuona, yupo kwenye ratiba zake zingine,” ameongeza muimbaji huyo.

Malaika ambaye usiku wa leo mnamo saa 3 kamili atasikika kwenye mahojiano na Jembe Fm Mwanza katika kipindi cha CLUB JEMBE akiwa na @mmbabaVC & @JohnJackson_jj along side @djmike_beatz_  amepanga kumshirikisha Bieber, Malaika amesema, “Oh Yeah, sasa hivi ndio ipo inafanyiwa kazi soon nafikiri itakavyokuwa tayari watatuona tukiwa studio. Lakini pia naweza kusema kuwa nimefanya kazi na producer ambaye ametengeneza ngoma ya Beyonce, Drunk in Love, kwahiyo kazi ipo tayari, na tunasubiria mixing, itakapokuwa tayari tutaitoa.”

Pamoja na kwamba Bieber ni miongoni mwa mastaa vipenzi vya watoto wa kike, Malaika amedai kuwa akipata nafasi hiyo hatokuwa na wazo lolote zaidi ya kazi.

“Actually nilivyosikia kwamba anaweza kupatikana Bieber mimi kufanya naye kazi na akawa ametoa hizo siku 10, mawazo yangu hayakuwa kuanzisha mahusiano, mawazo yangu yalikuwa kazi, kwahiyo nategemea kazi sana kwa Bieber kuliko vitu vingine.”

NI CAMEROON SASA USO KWA USO KWENYE FAINALI DHIDI YA EIGYPT

Dakika ya 72 Michael Ngadeu-Ngadjui anafungua milango migumu ya Ghana kwa kuiandikia Cameroon bao la kwanza.
Cameroon wataumana na Misri katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika 2017 baada ya magoli mawili ya kipindi cha pili kuiondosha Ghana katika mashindano hayo.
Timu zote mbili zilicheza mchezo wa kuvutia huku ikishuhudiwa kipindi cha kwanza zikimaliza kwa sare ya bila kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo milango ya kila timu iliendelea kuwa migumu mpaka dakika ya 72 Michael Ngadeu-Ngadjui alipofunga goli la kwanza kwa Cameroon.
Zikiwa zimesalia sekunde chache huku Ghana wakijaribu kusawazisha Christian Bassogog alifunga goli la pili na kuzamisha kabisa matumaini ya Ghana kwa mwaka huu.
Matumanini ya Ghana kuchukua kikombe hicho ambacho kwa mara ya mwisho walikibeba mwaka 1982 sasa yamefikia mwisho katika michuano ya mwaka huu.
Mara ya mwisho kwa Cameroon kuingia fainali ilikuwa mwaka 2008 walipofungwa na Misri ambao ndio wanakutana nao tena katika fainali ya mwaka huu.
"It is a real dream for us to get to the final," said the Belgian coach.
"Ghana have more experience than us - look at what they have done in recent tournaments. But since the start of this tournament we have shown we keep going right to the end in every game.
"I am very happy, especially for the team. They are an exemplary group on and off the field and they deserve to be in the final."
Cameroon have won the competition on four previous occasions

Their build-up to the match was clouded by a dispute between the team and the national association over pay, but on Gabon's Franceville stadium pitch their focus rarely wavered from the task in hand.
Cameroon defended brilliantly, nullifying the threat of Andre Ayew and brother Jordan - and, later on, substitute Asamoah Gyan.
They also caused Ghana several problems at the other end.
Slavia Prague defender Ngadeu-Ngadjui was both a rock in defence and a menace on set-pieces in attack, highlighted when he fired in from the angle to give his side the lead.
A free-kick was swung into the area and both Ghana defender John Boye and keeper Razah Brimah flapped at the delivery, allowing Ngadeu-Ngadjui to thrash home.
As Ghana, coached by former Chelsea boss Avram Grant, searched for the equaliser they left space at the back, which was exploited in the third minute of stoppage time when Aalborg forward Bassogog sprinted into the area and poked in past the reach of Razak.
"I am more than unhappy. We wanted so much to be in the final," said Grant.
"We did everything to be there and in the second half we completely dominated. Congratulations to Cameroon of course but we were the better side and we lost."
The Black Stars will meet Burkina Faso in Saturday's third place play-off in Port Gentil.

CHANZO: BBC

• POLISI WAKAMATA MASHAMBA MAWILI YA BHANGI YENYE UKUBWA WA EKARI 4, WILAYANI SENGEREMA.


TAREHE 01.02.2017 MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI KATIKA ENEO LA MSITU WA HIFADHI YA SERIKALI WA BUHINDI ULIPO KIJIJI CHA ILYAMCHELE TARAFA YA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA PAMOJA NA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU WA SERIKALI YA BUHINDI WALIFANIKIWA KUTEKETEZA SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA EKARI MBILI NA NUSU AMBALO LILIKUWA NDANI YA HIFADHI HIYO.

POLISI WALIPOKEA TAARIFA ZA UWEPO WA SHAMBA HILO LA BHANGI KUTOKA KWA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU HUO, NA KWAMBA WANANCHI AMBAO WANAOISHI KARIBU NA MSITU NDIO WALIOPANDA BHANGI HIYO KATIKA ENEO HILO NA PINDI WANAPOKATAZWA WAACHE TABIA HIYO WAMEKUWA WAKIKAIDI NA KUWATISHIA KUWAPIGA KWA MAWE MAAFISA WA HIFADHI HIYO. ASKARI WALIKWENDA PAMOJA NA MAAFISA HAO HADI ENEO LA HIFADHI YA MSITU NA KUKUTA ENEO LA EKARI MBILI NA NUSU LIKIWA LIMEOTESHWA BHANGI, ASKARI KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU WALIFANIKIWA KUTEKETEZA SHAMBA HILO LA BHANGI LILILOKUWA NA JUMLA YA IDADI YA MICHE 7300 YA BHANGI. POLISI BADO WANAENDELEA NA UPELELEZI ILI KUWEZA KUWABAINI WATU AMBAO WALIHUSIKA NA KUOTESHA BHANGI KATIKA ENEO LA MSITU WA HIFADHI YA SERIKALI WA BUHINDI.

AIDHA KATIKA TUKIO LINGINE LA TAREHE 02.02.2017 MAJIRA YA SAA 06:00HRS ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA KAFUNZO KILICHOPO WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA,   ASKARI WAKIWA KWENYE MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA MKORO MSAMI MIAKA 74, MKAZI WA KIJIJI CHA MAFUNZO, KWA KOSA LA KUOTESHA MICHE 84 YA BHANGI KWENYE SHAMBA LENYE UKUBWA WA EKARI MOJA NA NUSU, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA MTU KATIKA KIJIJI TAJWA HAPO JUU ANAYEJIHUSISHA NA KILIMO CHA BHANGI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI JUU YA TAARIFA HIZO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA PAMOJA NA SHAMBA LAKE NA KUANZA ZOEZI LA  KUNG’OA MICHE YOTE YA BHANGI KATIKA SHAMBA HILO KISHA KUITEKETEZA KWA MOTO.

MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA ASKARI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIAKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, POLISI WANAENDELEA NA UPELELEZI PAMOJA  NA MISAKO KATIKA MAENEO YOTE ILI KUWEZA KUWAKAMATA NA KUWADHIBITI WATU WOTE WANAOJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA BHANGI.


KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI, ILI LIWEZE KUWAKAMATA NA KUDHIBITI WATU WOTE AMBAO WANAJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA BHANGI NA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

KOREA KASKAZINI YAONYA DHIDI YA CHOKOCHOKO ZA SERIKALI MPYA YA TRUMP


SERIKALI ya Korea Kaskazini imetoa onyo kali juu ya chokochoko za Marekani katika serikali mpya ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Pyongyang mapema leo sanjari na kuonya juu ya hatua za Washington kufanya maneva ya kijeshi kwa kuishirikisha Korea Kusini na ambayo hufanywa kila mwaka  imesema kuwa, Washington na Seoul zinaifanya hali ya mambo katika Peninsula ya Korea kuwa mbaya sana.

Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini
Aidha ripoti hiyo imesema kuwa, maneva hayo ya kijeshi ambayo yamepangwa kufanyika mwezi Machi mwaka huu, mbali na kuvuruga usalama, yanakusudia kurejesha upya silaha za nyuklia za Marekani katika eneo hilo. Radiamali ya Korea Kaskazini juu ya luteka ya pamoja baina ya Korea Kusini na Marekani imetolewa katika hali ambayo tayari Waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis amewasili mjini Seoul kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Korea Kusini kuhusiana na masuala ya kijeshi.

Moja ya silaha hatari za Korea Kaskazini zinazoitia tumbojoto Marekani

Taarifa iliyotolewa na serikali ya Seoul imesema kuwa, katika safari hiyo ya siku mbili, Mattis atajadiliana na viongozi wa nchi hiyo miradi ya nyuklia na makombora ya balestiki ya Korea Kaskazini na kadhalika suala la uwekaji ngao ya makombora ya Marekani ya THAD nchini humo. Ni vyema kuashiria kuwa, Korea Kusini na Kaskazini zimekuwa katika maandalizi ya kijeshi tangu kumalizika vita baina yao hapo mwaka 1953 huku nchi hizo zikishindwa kutia saini mkataba wa amani baina yao.

MWANADIPLOMASIA WA SAUDIA APATIKANA NA HATIA YA KUBAKA, KULAWITI.


MAHAKAMA moja nchini Singapore imempata mwanadiplomasia wa Saudi Arabia, na hatia ya kubaka na kulawiti mhudumu mmoja wa hoteli kusini mwa nchi hiyo ya bara Asia.
Bander Yahya al-Zahrani, mwanadiplomasia wa Saudia mjini Beijing anakabiliwa na mashitaka matatu ya ubakaji, liwati na kumdhalilisha kijinsia mhudumu mmoja wa hoteli mwenye umri miaka 20, Agosti mwaka jana 2016.
Lee Poh Choo, Jaji wa Mahakama ya Wilaya aliyeisikiliza kesi hiyo jana Jumatano amekataa ombi la wakili wa mwanadiplomasia huyo, la kutaka kesi hiyo itupiliwe mbali kwa kuwa mteja wake anadai kuwa mhudumu huyo wa hoteli alishirikiana na wasimamizi wa hoteli hiyo ili kumhadaa ili kumpora pesa.
Mwanadiplomasia huyo wa Saudi Arabia anadaiwa kumnajisi na kumlawiti mhudumu huyo mnamo Agosti 14 mwaka jana, alipokuwa ameenda likizo katika kisiwa cha Sentosa, nchini Singapore.
Wanawake wakiandamana India kupinga kinga ya kisheria kwa mwanamfalme mbakaji wa Saudia

Hukumu dhidi ya mwanadiplomasia huyo wa utawala wa Aal-Saud inatazamiwa kutolewa kesho Ijumaa, na huenda akahukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela au faini ya dola 1,500 za Marekani kwa kumdhalilisha kijinsia binti huyo wa miaka 20, na pia kifungo cha miaka 10 kwa shitaka la kulawiti.
Oktoba mwaka jana, mwanadiplomasia mwengine wa Saudia alituhumiwa kuwabaka wanawake wawili wa Nepal waliokuwa wakifanya kazi katika makazi yake mjini New Delhi nchini India.
Aidha Oktoba mwaka 2015, wanawake watatu katika jimbo la Los Angeles nchini Marekani waliodhalilishwa kijinsia na mwanamfalme wa Saudia, Majid bin Abdulaziz Al Saud waliwasilisha mashtaka yao mahakamani nchini humo.

Thursday, February 2, 2017

MAMA ASEMA YUKO TAYARI KUFA LAKINI HAKI YAKE IPATIKANE.

Mjane ambaye jina lake halijafahamika amejitokeza katika sherehe za kuadhimisha siku ya Sheria nchini ikiwa imeudhuriwa na mgeni rasmi Rais Magufuli huku akiwa ameshika bango akiwa anaelekea kwenye meza kuu ambayo alikuwepo Rais Magufuli ndipo Usalama wa taifa walipo mvamia na kumtoa nje ndipo Rais Magufuli akataka aachiliwe ili aeleze yanayo msibu mama huyo..

MAKONDA AWATAJA ASKARI 9 WATUHUMIWA KUSHIRIKIANA NA MTANDAO WA MIHADARATI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataja Askari 9 wanaotuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.

1- Detective Koplo Noel (Kituo chake cha kazi ni Central Police Dar)

2- Dotto (Yuko Kituo cha Kijitonyama)

3- Mwingine anafahamika kama 'Makomeo' (Kituo cha Oyster-bay)

4- Glory (Yuko Kituo cha Kawe)

5- Inspector Fadhili (Yuko Kituo cha Kinondoni)

6- Steve (Kinondoni)

7- James (Kinondoni)

8- Ditective Koplo (Wille)
RC Makonda amewataja wanaotuhumiwa kutumiwa dawa za kulevya wakiwemo TID, Wema Sepetu, Chid Benz, Recho, amewataka kesho wakutane polisi

Kuna maeneo watu wanatuambia madawa ya kulevya wanayapata sehemu hizo, wamiliki wake kesho niwakute polisi, wasipokuja nitawafuata - RC Makonda

Kama unajua una eneo unafanya biashara za dawa za kulevya DSM natoa siku 7 biashara hii iishe, operesheni hii naiongoza mwenyewe - RC Makonda

Kama Kamishna Sirro na timu yake watashindwa kutokomeza dawa za kulevya DSM maana yake wamekosa sifa za kuendelea kuwa askari - RC Makonda

Watano tayari nimeshawakamata na wengine nimewakamata wakiwa na dawa za kulevya - RC Makonda

MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA NA TAIFA STARS GODFREY BONY YU HOI KITANDANI NA HAJITAMBUI.


KIUNGO wa zamani wa timu ya Yanga, Tanzania Prisons na Taifa Stars, Godfrey Bony, amelazwa katika Hospitali ya Rungwe mkoani Mbeya huku akiwa hana fahamu.

Akizungumza na Mwandishi wetu Dada wa mchezaji huyo aliyejulikna kwa jina la Neema Boniface, alisema kuwa Bony alianza kuumwa ugonjwa usiojulikana miezi mitatu iliyopita na mpaka sasa bado haijajulikana anaumwa ugonjwa gani.

"Alikua anaumwa lakini alikua na nguvu zake, alikua anatoka anaenda kwenye shughuli zake, wakati mwingine anaenda kuangalia mpira" Alisema dada huyo.

Neema aliendelea kueleza kwamba wiki mbili zilizopita hali ya Bony, ilibadilika ghafla na kuwa mbaya zaidi ambapo alikua akilalamika kuishiwa nguvu na wakati mwingine kupoteza fahamu hali iliyolazimu kupelekwa hospitali.

"Tulimleta hospitali ya Makandana, Hospitali ya wilaya ya Rungwe lakini vipimo havikuonesha ugonjwa wowote ndiyo juzi ikabidi apigwe X Ray ya kifua na vipimo tumeambiwa vimetoka jana lakini jioni wakati madaktari wameishaondoka kwa hiyo wamesema watatupatia leo".

Kwa mujibu wa maelezo ya dada huyo ni kwamba hali ya kaka yake si nzuri kwa sababu hana fahamu.

Wadau wa Soka popote nchini, TFF na wapendasoka wote kwa ujumla mnaombwa kujitokeza kumsaidia Godfrey Bony ili aweze kupata matibabu husika na kujua ugonjwa unaomsumbua ili nyota huyu wa taifa aliyetoa jasho lake kuipeperusha bendera ya taifa letu aweze kupata msaada wa matibabu na hatimaye kurejea katika hali yake ya kawaida.

Kwa yeyote mwenye nia njema ya kumsaidia Godfrey anaweza kuwasiliana na dada yake kwa simu namba 0765 359 290Chanzo: mtandao wa wapenda soka.

ZAIDI tega sikio Jembe Fm kipindi cha Sports Ripoti saa 3 kamili usiku.

SUALA LA OKWI KUTUA LIGI YA UGANDA NI GERESHA TU AMEPAKI AKISUBIRI USAFIRI BASI LA SIMBA...!!



HATUA ya mshambuliaji Emmanuel Okwi kuvunja mkataba na klabu ya SønderjyskE ya nchini Denmark, na kujiunga na klabu ya SC Villa ya Uganda inatajwa na wachunguzi wetu wa masuala ya soka kuwa ni geresha tu na kwamba ni kama anaitumia klabu hiyo kama kituo cha basi akisubiri safari yake kuelekea Msimbazi kujiunga na Klabu ya Simba ya Tanzania. 

Inasemekana Okwi anasubiri msimu mkuu wa usajili mwezi wa nane baada ya ligi kumalizika.

FUATILIA mazungumzo yafuatayo yaliyofanyika ndani ya Kipindi cha Sports Ripoti ya Jembe Fm kinachoruka kila siki usiku saa 3:00 hadi 4:00 chini ya mtangazaji Juma Ayoo na hapa alikuwa akizungumza na Hashim Mwesigwa kutoka Kampala nchini Uganda. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
 Zaidi ya hapo Okwi amejiunga na klabu yake ya zamani (SC Villa) kwa mkataba wa muda mfupi utakao muweka hadi mwishoni mwa msimu huu 2016/2017.

Nyota huyo wa zamani wa Simba aliachana na SC Villa mwaka 2010 na kujiunga na Wekundu wa Msimbazi’ baada ya kuisaidia Jogoos kutwaa taji la Uganda mwaka 2009.

Mshambuliaji huyo mahiri wa Uganda amesema atahakikisha anaisaidia Villa iliyomkuza kufanya kweli.

“Dili tayari limekamilika,” Ivan Kakembo CEO wa SC Villa aliuambia mtandao wa Kawowo Sports wa Uganda.

Wednesday, February 1, 2017

KABANZA ATAMBULISHA NGOMA YAKE LEO.

Kabanza atambulisha Ngoma yake Mpya
Na James Timber, Mwanza
Msanii  chipukizi wa Kizazi kipya Bongo flava Kabanza kutoka jijini Mwanza, ametambulisha leo kibao chake kipya kiitwacho Digital alichomshirikisha Ydee kilichotengenezwa na  Adolf Beatz pamoja na  producer Doucher Master.

Kabanza itakuwa Track yake ya tatu baada ya kibao chake cha kwanza kilichomtambulisha kiitwacho  Money na cha pili Mdananda alichokifanya mwaka jana akishirikiana na Ydee ambacho kilikuwa hit kwenye media za jijini hapa kutokana na Ujumbe, uliokuwemo, Melody na Beatz 

Msanii huyo mwenye jina lake halisi  Kabanza Peter ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma anayechukua Degree ya Chemistry, alipenda mziki toka anasoma shule ya msingi na kujiingiza kwenye vikundi vya sanaa shuleni alipokuwa O’level pia na kufanya vizuri Shule ya Sekondari Bugogwa iliopo Ilemela jijini Mwanza.

Aidha aliomba watanzania wapenda mziki wa kizazi kipya bongo flava kumpa sapoti kadri wawezavyo ili kumfikisha sehemu anayostahili.
“Nimeachia Kibao changu kipya leo  February  1, 2017 kiitwacho Digital nilichomshirikisha Ydee, naomba washabiki na wapenda mziki wa kizazi kipya wakipokee wasikilize na pia naomba wadau wanisapoti ili nifike mbele zaidi,” alisema Kabanza.

Kwa upande wake Msanii huyo  anaamini heshima na nidhamu ndio nguzo bora katika kufanya vizuri na kupaa juu zaidi.

ALIYETEKELEZA MAUAJI MSIKINI CANADA NI MFUASI SUGU WA TRUMP.


MWANAFUNZI wa chuo kikuu aliyetekeleza mauaji dhidi ya waumini wa Kiislamu waliokuwa wakisali katika msikiti mmoja mjini Quebec nchini Canada siku chache zilizopita ni mtu mwenye misimamo ya mrengo wa kulia na mfuasi sugu wa Donald Trump, Rais wa Marekani.
Kwa mujibu wa machapisho kadhaa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Alexandre Bissonnette mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akitangaza wazi wazi kuwa anaunga mkono misimamo ya chuki dhidi ya Waislamu ya Trump, na pia vuguvugu linalotaka eneo la Quebec lijitenge na Canada la Parti Quebecois. 
Mwanachuo huyo amekuwa akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa, anafurahishwa sana na  misimamo ya Marine Le Pen, mwanasiasa wa mrengo wa kulia wa Ufaransa ambaye amekuwa akipigia debe sera za chuki dhidi ya Waislamu na wahamiaji nchini humo.

Aidha kijana huyo aliyetekeleza mauaji hayo ya kutisha anadaiwa kusema kuwa analipenda jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel ambalo kila uchao linaua shahidi wananchi madhulumu wa Palestina.
Alexandre Bissonnette ambaye anakabiliwa na mashtaka sita ya mauaji, alipandishwa kizimbani jana Jumatatu katika mji wa Quebec nchini Canada, ambapo mahakama imeagiza awekwe rumande hadi kesi dhidi yake itakaposikizwa tena Februari 21.
Kituo cha Kiutamaduni cha Kiislamu mjini Quebec kilisema waumini sita wa Kiislamu waliuawa walipokuwa wakisali Sala ya Ishaa Jumapili usiku, baada ya mwanachuo huyo na mwenzake aliyetoweka kuvamia msikiti huo na kuwamiminia risasi.