POLENI KWA UJENZI WA TAIFA NA NAAMINI MU WAZIMA WA AFYA TELE
STUDIO MPYA YA SEDUCTIVE RECORDS INAPENDA KUWAPA NAFASI WADAU, MARAFIKI NA WAPENZI WOTE WA MUZIKI WA BONGO FLEVA KUSIKILIZAA SINGLE YA PILI YA MSANII OCHU EDDY SHEGGY AU KWA JINA LA KISANII OCHU
SINGLE HIYO INAITWA "UMECHAKACHUWA" IMEREKODIWA NA PRODUCER JILLY BABY WA SEDUCTIVE RECORDS NA PIA IMESHAFANYIWA MUSIC VIDEO YAKE CHINI YA KAMPUNI YA EMPTYSOULZ PRODUCTION AMBAYO IMESHAANZA SAMBAZWA KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TV.
NATUMAINI MTAENJOY KAZI HII NZURI NA PIA KUMPA SUPPORT MSANII HUYU AMBAYE ANAJARIBU KUENDEREZA SANAA HII ALIYOKUWA AKIIFANYA MAREHEMU BABA YAKE MSANII WA MUZIKI WA DANCE EDDY SHEGGY.
PIA USISITE KUANDIKA KUTOA USHAURI PALE UTAPOSIKILIZA SINGLE HII YA "UMECHAKACHUWA"
ASANTENI NA TUWE PAMOJA!
Regards:
Solomon Lamba
For those who missed the concert on the 9th of february here is another chance to see a great collaboration of artists. Initially we were brought together through MDGFive.com and UNFPA's efforts to raise awareness about maternal health through music. This is an independent event organised by Caravan Records to challenge, renew and fuse two powerful youth cultures. Please spread the word. The concert will take place at Triniti on FRIDAY the 4th of March. 8PM-00AM
--
Kind Regards,
Caravan Records
MANAGEMENT
Tel: +255 763 822 022
E-mail: kichaamusic@gmail.com
www.myspace.com/mzungukichaa
www.reverbnation.com/mzungukichaa
www.youtube.com/nuttywhite
www.facebook.com/mzungukichaa
www.myspace.com/caravanrec
www.facebook.com/caravanrec
www.twitter.com/MzunguKichaa
Kutana na mtoto mwenye umri wa miaka saba raia wa serbia anayefahamika kwa jina la Bogdan ambaye ameufanya ulimwengu kujiuliza kulikoni kutokana na uwezo wa mwili wake usio wa kawaida.
Kulingana na taarifa za Shirika la habari la nchi hiyo mwili wa Borgan unanasa vyombo vya chuma kama vile vijiko, visu, uma, nyembe, funguo, misumari vyote katika hali ya kushangaza kabisa.
Wanasayansi wanaumiza vichwa, wasipate jibu la haraka kuwa hali hii ya mwili wa binadaamu ya kujitengenezea sumaku inatoka wapi? ni kama kiroja hivi! Na cha kushangaza zaidi hata sahani, vyombo vya kioo na hata kiendesha mbali ‘remote control’ vinanaswa na mwili wake, mama yyangu!!...
Baadhi ya vitu anavyovinasa vingine wala si vya vyuma kama vile glasi, alisema mwanahabari mmoja wa Serbia.
Mmmmmh! Chunguza mjomba utabaini. Source: in.yfittopostblog
Idadi ya ‘ ndoa bandia' zinazowahusisha raia wa kigeni ambazo zimefichuliwa na jeshi la Polisi kote nchini Japani kwa mwaka 2010 kuwa zilifikia 153 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.2 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Taifa la Polisi hapa Japani.
Polisi walichukua hatua malimbali ikiwa ni pamoja na kuuliza maswali, kukamata na kupeleka nyaraka kwa waendesha mashitaka dhidi ya watu 471 wakihusishwa na tuhuma hizo. Shirika hilo limesema kuwa Polisi wanafuatilia miendendo ya ndoa hizo ‘bandia ‘ zenye malengo mbalimbali kama vile kutengeneza mazingira ya kufanya uhalifu.Shirika hilo limesema kuwa baadhi ya raia wa kigeni walijihusisha na vitendo vya jinai baada ya kupata hati za vya ukaazi kwa hatua yao ya kufunga ndoa za raia wajapani huku vikundi vya kihalifu vikipata fedha kutokana nandoa hizi za kupanga.
Tuesday, March 01, 2011
SIASA
Tuesday, March 01, 2011
MSAADA
Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Filamu na wa Muziki wa kizazi kipya mara baada ya kupokea michango mbalimbali ya fedha na vitu vyenye thamani ya shilingi milioni 76 waliyoipata kutokana na tamasha walilolifanya mwishoni mwa wiki kuchangia waathirika wa mabomu wakatika eneo la Gongo la mboto jijini Dar es salaam. Kulia ni kaimu mkuu wa mkoa Mh. Sadik na kushoto ni Kamanda Kova, wa tatu kushoto ni mratibu mkuu wa tamasha hilo la soka kwa wasanii (GOLI) Bw. Ruge Mutahaba.
Picha ndogo msanii wa muziki wa kizazi kipya Mwana FA kwa niaba ya wasanii wote akiwasilisha hundi hiyo kwa mh. Waziri mkuu.
Monday, February 28, 2011
SIASA
Waziri mkuu wa Tunisia Mohammed Ghannouchi ametangaza kupitia televisheni ya taifa kuwa anajiuzulu- matakwa muhimu kutoka kwa waandamanaji.
Bw Ghannouchi mwenye umri wa miaka 69, anaonekana kuwa karibu sana na aliyekuwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali tangu mwaka 1989, aliyeondoshwa madarakani mwezi uliopita.
Alisema, " Baada ya kutafakari kwa zaidi ya wiki moja, nikaanza kushawishika, na familia yangu iliniunga mkono, na hivyo kuamua kujiuzulu. Si kwamba nakimbia majukumu yangu; nimekuwa nikitimiza wajibu wangu tangu Januari 14." " Siko tayari kuwa mtu anayechukua uamuzi utakaoishia kusababisha vifo." "Kujiuzulu huku kutasaidia Tunisa, mapinduzi pamoja na maendeleo ya siku za usoni za Tunisia." Alisema.
Baada ya saa kadhaa mbadala wa Bw Ghannouchi alitajwa- Beji Caid Essebsi, mwenye umri wa miaka 84, ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje katika serikali ya marehemu Rais Habib Bourguiba.
Awali, polisi mjini Tunis walirusha mabomu ya kutoa machozi na risasi za onyo kutawanya maandamano ya hivi karibuni wakitoa wito wa kutaka serikali mpya na katiba mpya katika siku ya tatu ya ghasia.