ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 28, 2011

KWAHERI RAFIKI..

Tangu 1975 hadi 2011 Ni siku za maisha yako na hatimaye siku ya jana (jumapili) ndugu jamaa na marafiki tulielekea katika kijiji cha Masanzakona wilayani Magu mkoani Mwanza, mahala ulipojenga nyumba yako kwa ajili ya mazishi. Namzungumzia Paul Kabara rafiki mcheshi aliyekuwa akisimamia jambo na kuhakikisha kuwa anapigana nalo mpaka mwisho wa matokeo. Mpendwa huyu alifariki siku ya ijumaa katika hospitali ya rufaa Bugando baada ya kuugua kwa muda.

Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba yao.

Marafiki wa marehemu wakiongozwa na Mr. Bruno kulia wakiweka kwa pamoja wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Paul Kabara.

Sehemu ya umati msibani nyumbani kwa marehemu. Shukurani kwa wote walioshiriki kwa hali na mali kufanikisha safari ya mwisho ya mpendwa wetu Paul Kabara, Mwenyezi mungu twakuomba ilaze mahala pema peponi roho ya marehemu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.