ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 23, 2018

TUNISIA LAKUVUNDA HALINA UBANI, YADUNGULIWA MKONO NA BELGIUM




Lukaku na Hazard kila mmoja karudi mara mbili kusalimiana na nyavu za Tunisia.

GSENGOtV:- Romelu Lukaku na Eden Hazard walifunga mabao mawili kila mmoja na kuimarisha uongozi wa Ubelgiji dhidi ya England katika Kundi G kwa ushindi wa 5-2 dhidi ya Tunisia Jumamosi.
Kundi hilo linalowajumuisha pia Panama ambao watakutana na England Nizhny Novgorod Jumapili.
Bao la tano la Ubelgiji lilifungwa na Michy Batshuayi.
Tunisia walifungiwa na Dylan Bronn na Wahbi Khazri.
Tunisia wanatarajia Panama wawashinde England ndipo waweze kusalia katika michuano hiyo.
Hilo lisipofanyika basi Afrika itasalia na mataifa mawili pekee katika michuano hiyo - Nigeria na Senegal.
Lukaku amfikia Ronaldo kwa mabao
Lukaku sasa ana mabao manne katika Kombe la Dunia, sawa na Cristiano Ronaldo wa Ureno katika kinyang'anyiro cha kushinda Kiatu cha Dhahabu.
hazard alikuwa amemkosoa mchezaji huyo mwenzake, waliyecheza pamoja Chelsea wakati mmoja, kwa kutoweka wakati wa kipindi cha kwanza mechi dhidi ya Panama.

Lakini leo alitamba mechi yote hadi alipoondolewa uwanjani na nafasi yake akaingia Marouane Fellaini dakika ya 59.

MPOGORO AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 281 SENETI YA VYUO NA VYUO VIKUU NA KUVUNA WANACHAMA WA CHADEMA MKOANI IRINGA LEO.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick Mpogoro akizungumza  katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
 Wahitimu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa Wakiimba nyimbo Mbali mbali za Chama mara baada ya Mgeni rasmi kuzungungumza katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC) Bi Theresia Mtewele akiongoza meza kuu kuimba nyimbo Mbali mbali za Chama mara baada ya Mgeni rasmi kuzungungumza katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Viongozi na wahitimu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa wakiburudika kwa pamoja kwa nyimbo Mbali mbali za Chama mara baada ya Mgeni rasmikuzungungumza katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Mwl Raymond Mwangwala akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
Mwenyekiti wa Chama cha Mapindui Mkoa wa Iringa Ndg.Albert Chalamila akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo 
Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg.Rodrick Mpogolo akimkabidhi cheti cha pongezi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndg.Kenani kiongosi katika sherehe ya Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
 Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg.Rodrick Mpogolo akitoa vyeti kwa wahitimu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogolo akipokea baadhi ya bendera na jezi za chadema wakati akimkaribisha ndg Godfrey Maiko aliojiunga rasmi na CCM Leo  katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogolo akimvisha kofia ya CCM ndg Godfrey Maiko aliojiunga rasmi na CCM Leo  katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza akipeana Mkono na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini Ndg Damalo aliporejesha kadi ya Chadema na Kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi Leo katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogoro akifurahi pamoja na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini Ndg Damalo aliporejesha kadi ya Chadema na Kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi Leo katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo. 

PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI CCM BLOG

RAIS WA ZIMBABWE ANUSURIKA KIFO AKIWA KATIKA MKUTANO BULAWAYO

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amenusurika baada ya mlipuko kutokea mkutano aliokuwa anauhudhuria Bulawayo.

Bw Mnangagwa amesema kitu "kililipuka inchi kama kutoka pahala nilipokuwa - lakini wakati wangu haujafika".
Video kutoka uwanja wa michezo wa White City unaonesha Bw Mnangagwa akiondoka kwenye jukwaa baada ya kutoa hotuba, mlipuko unapotokea.
Msemaji wake amesema rais huyo alinusurika bila majeraha.
Msemaji wa rais George Charamba ametoa taarifa akisema: "Kumekuwa na majaribio kadha ya kumuua rais miaka mitano iliyopita."
Gazeti la serikali la Herald limeripoti kuwa makamu wa rais Kembo Mohadi ameumia miguuni wakati wa mlipuko huo unaodhaniwa kutokana na bomu, lakini taarifa hizo hazijathibitishwa.
Maafisa wengine wakuu serikali pia wanadaiwa kujeruhiwa, sawa na walinzi wao.
Runinga ya taifa imesema Makamu wa Rais Kembo Mohadi aliumia mguuni.
Bw Mnangagwa amesema amewazuru waliojeruhiwa hospitalini na kushutumu shambulio hilo.
Ametoa wito kwa raia kudumisha umoja.
Makamu wa Rais wa kwanza wa Zimbabwe Constantino Chiwenga pia alipata majeraha madogo, shirika la habari la Reuters limeripoti.
Mke wake Marry pia ameumia na picha zake akitembelewa na Rais Mnangagwa hospitalini zimesambaa sana mtandaoni.
Gazeti la Herald limetaja mlipuko huo kama jaribio la kumuua rais.
Runinga ya taifa ZBC pia imesema mwenyekiti wa kitaifa wa Zanu PF Oppah Muchinguri-Kashiri, na afisa mkuu wa kisiasa Engelbert Rugeje pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa ZBC walijeruhiwa

Ubalozi wa Marekani mjini Harare umeshutumu shambulio hilo.
Rais Mnangagwa aliingia madarakani Novemba mwaka jana baada ya kuondolewa madarakani kwa Robert Mugabe aliyekuwa ameliongoza taifa hilo kwa miaka 37.
Bw Mnangagwa amekuwa akifanya kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika 30 Julai ambao utakuwa wa kwanza tangu kuondolewa madarakani kwa Bw Mugabe.

RATIBA YA REO WORIDI KAPU

Ratiba ya Leo 23/6/2018

👉Ubelgiji na Tunísia, Saa 9 Alasiri

👉Korea na Mexico, saa 12 jioni

👉Ujerumani na Sweden, saa 3 usiku

Tunakumbushana tu

PADRE ALIYEMZABA KIBAO MTOTO ALIYEKUWA AKIMBATIZA AVUNJA UKIMYA KWA KUJIFUTA UTUMISHI.

GSENGOtV

Padre aliyempiga kibao mtoto kwa sababu ya kulia wakati wa ubatizo amevunja ukimya baada ya kujitokeza na kutamka bayana kuwa sasa amestaafu rasmi kutoa huduma na kudai kuwa "umri wake umechangia kujitokeza kwa tukio hilo baya"

Baba Jacques Lacroix, mwenye umri wa miaka 89, alisema alimtaka mtoto huyo kuwa mtulivu wakati wa sherehe huko Champeaux, karibu na Melun, katika vitongoji vya kusini-mashariki mwa Paris nchini Ufaransa lakini haikuwa hivyo, mtoto huyo aliendelea kulia na kupiga kelele. Kanisa la Katoliki limesema limelazimika kumsihi mtumishi huyo kustaafu baada ya kumlamba kibao mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka miwili wakati akimbatiza. Baba Jacques Lacroix, mwenye umri wa miaka 89, alisema: "Ninaimaliza huduma yangu sasa ... kuna mwisho kwa kila kitu." Alifanya shambulio la ajabu wakati wa sherehe katika Kanisa la Collegiate huko Champeaux, karibu na Melun, katika vitongoji kusini-mashariki mwa Paris, Jumapili iliyopita. Katika video ya tukio ambalo limeshika kasi kunako mitandao ya kijamii (hususani YouTube), Baba Jacques anaonekana akipiga kelele kwa kijana na kisha kumlamba kibao. "Chula chini, utulivu, lazima utulivu," anasema, akiongeza "utulivu" kabla ya kufuta uso wa kivulana hicho mikononi mwake. Kisha kuhani hutazama kijana huyo machoni na kumtia kibao cha nguvu kwenye shavu na mkono wake wa kushoto. Tendo hilo la ukatili lilisababisha maamuzi ya haraka kutoka kwa wazazi waliogopa juu ya hatma ya mtoto wao pamoja na wajumbe wengine wa familia ambao waliambatana kwenye tukio hilo, ambapo ilimlazimu baba wa kivulana hivho kumchomoa mwanae toka kwenye mikono ya Padre. Akihojiwa na kituo cha Radio Info Ufaransa, Baba Jacques akikataa kuwa shambulio hilo lilikuwa kali sana, "Ilikuwa mahali fulani kati ya kumuweka sawa na nilitumia mbinu hiyo kama kumtuliza, sikujua nini cha kufanya. "Mtoto alikuwa akipiga kelele sana na nilibidi kugeuza kichwa chake ili kumwagilia maji juu yake. "Nilimwambia 'atulie, awe mtulivu' lakini hakuwa na utulivu. Nilijaribu kumfunga kinywa na nilitaka awe na utulivu. "Ninaomba msamaha kwa ajili ya kwa yale niliyoyafanya mbele ya familia. Nimeimaliza huduma yangu sasa, ilikuwa ni ubatizo wangu wa mwisho, Naam ninaamini kuna mwisho wa kila kitu." Jean-Yves, ambaye ni Askofu wa Meaux, amesema kuwa amechukua hatua na kuhani amesimamishwa kutoa huduma kwenye sherehe zote za ubatizo na ndoa. Askofu alisema Baba Jacques ataruhusiwa kusherehekea masuala wakati ujao kama hii ilifafanuliwa kabla. Alisema Baba Jacques alikuwa na hatia ya "Hii ishara ni zaidi ya kusikitisha kwa sababu ubatizo unafanywa kuwa wakati wa furaha, lakini uchovu na umri mkubwa wazi alicheza sehemu yake na kusababisha mambo kwenda mrama. " Wazazi wamekubali msamaha wa kuhani na walifurahi kuona mtoto wao akibatizwa, Askofu aliongeza.

DKT TIZEBA ATOA SIKU 4 WAKULIMA WA MKONGE MKOANI TANGA KULIPWA FEDHA ZAO

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba akitoa maelekezo ya serikali wakati wa kikao cha pamoja na wadau wa Kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO) kabla ya mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela akizungumza jambo kabla ya kumaribisha mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba kuongoza mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.
Viongozi mbalimbali Mkoani Tanga wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela wakiagana na Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.
Wadau wa zao la Mkonge wakichangia mada wakati wa mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.

Na Mathias Canal-WK, Tanga

Wakulima wa Mkonge Mkoani Tanga wamempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba kupitia agizo lake alilolitoa kwa Kampuni ya Katani Limited kuhusu kulipa madeni ya wakulima ndani ya siku nne kuanzia 21 Juni 2018 hadi 26 Juni 2018 Kwa madeni ya muda mrefu ya wakulima wa zao hilo jambo lililopelekea kupunguza ufanisi na tija ya Kilimo Kwa wakulima hao.

Dkt Tizeba ametoa agizo hilo leo 21 Juni 2018 akiwa kwenye mkutano na wadau wa Kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO) unaotekelezwa kwenye mashamba matano ya Hale, Magunga, Magoma, Mwelya na Ngombezi yaliyo chini ya miliki ya Bodi ya Mkonge Tanzania. 

Katika Mkutano huu uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Martin Shigela sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe, Msajili wa Hazina, Mtendaji wa BRELA, Muwakilishi wa mwanasheria Mkuu wa serikali, Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge na wataalamu wengine; Waziri wa Kilimo Mhe Tizeba ametoa agizo hilo Kwa Uongozi wa mfumo wa Kilimo cha wakulima wadogo wa kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO), Kampuni ya Katani ltd ambayo ndio mnunuzi pekee wa Mkonge wa mkulima na Bodi ya Mkonge Tanzania.

Sambamba na agizo hilo pia Mhe Waziri ameiagiza Bodi ya Mkonge Tanzania kupitia upya mikataba yote iliyopo Kwa kushirikisha Bodi yenyewe, Kampuni ya Katani na wadau wa zao hilo haraka iwezekanavyo ili kurekebisha makosa yaliyopo.

Aidha, ameitaka Bodi hiyo ya Mkonge Tanzania kuitisha kikao na wadau wote wa zao hilo ili kupitia upya utaratibu wa makato ya mgawanyo wa mapato katika kusindika zao la Mkonge.

Mhe Dkt Tizeba aliongeza kuwa hati za miliki ya mashamba zitapaswa kutolewa Kwa wahusika Mara baada ya kujiridhisha na mchakato utakapokamilika huku akiwataka wakulima kulipa malimbikizo ya kodi ya ardhi.

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemaliza ziara ya siku moja ya kikazi mkoani Tanga huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela Kwa umakini na uwajibikaji katika kusimamia sekta ya Kilimo hususani zao la Mkonge mkoani humo.

PALE SHERIA INAPOWANG'ATA WALIOITUNGA.


CHANZO/MWANANCHI
Katika mgawanyo wa madaraka ya utawala, Bunge ndicho chombo cha kutunga sheria, kuisimamia na kushauri Serikali, Serikali inatekeleza sheria hizo na kusimamia masuala ya utawala na kuleta maendeleo huku mhimili wa tatu wa Mahakama ukipewa jukumu la kutafsiri sheria hizo na kutoa haki.
Bunge likiwa mhimili mmojawapo wa utawala, ni chombo ambacho kimekuwa kikiheshimiwa katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, na hata inapotokea tatizo lolote, wabunge huchukuliwa tofauti na watu wa kada nyingine.
Na mara nyingi, watu mbalimbali kama wabunge, wamekuwa wakiitwa na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kwa tuhuma za kulidharau Bunge.
Bunge likiwa ndio chombo kilichopewa mamlaka ya kutunga sheria, limekuwa likitunga sheria zote zinazotumika nchini na kuridhia nyingine na mikataba ya kimataifa.
Miswada ya sheria iliyo nyingi huwasilishwa na Serikali na mingine na wabunge wenyewe. Miswada hiyo hujadiliwa kwa kina na hatimaye kuipitisha kuwa sheria baada ya marekebisho kadhaa, kama yapo, kisha kusainiwa na Rais na kuanza kutumika.
Sheria ya ‘kupima samaki’
Mwanzoni mwa wiki hii kulitokea sintofahamu ndani ya Bunge wakati watendaji wa Serikali walipokuwa wakitekelezaji moja ya sheria zilizotungwa na chombo hicho, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kuudharau mhimili huo.
Sakata hilo lilikuwa ni kukamata kwa samaki watatu waliokuwa wamepikwa katika mgahawa wa Bunge, kwa madai kwamba walivuliwa kinyume na sheria.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina aliagiza maofisa wake kuchunguza samaki wanaouzwa kwenye mgahawa huo. Maofisa hao walienda moja kwa moja kwenye mgahawa na kupima samaki kwa kutumia rula na kubaini samaki watatu waliokuwa hawajafikia kiwango cha kuvuliwa kwa mujibu wa sheria.
Suala hilo lilisambaa kila kona ya Bunge na hata katika mitandao huku kila kitu kikilinganishwa na upimaji kwa kutumia rula hata kama ni chakula.
Ilikuwa ni kama sinema, ingawa mitaani liligeuzwa masihara, maofisa wa Wizara ya Uvuvi walikunja nyuso zao na watu waliokuwapo wakaona jambo hilo si la mzaha.
Katika kuthibitisha kwamba jambo hilo si la utani, kila samaki mmoja aliyekamatwa kwenye mghahawa huo, alisababisha mwendeshaji mgahawa huo kulipa Sh100,000 na hivyo zilimtoka Sh300,000 bila suala hilo kufika mahakamani.
Waliotunga sheria wakerwa
Kitendo cha kuvamia mgahawa wa Bunge na kupima kitoweo, kiliwakera wabunge na kufikisha suala hilo ndani ya chombo hicho.
Ingawa suala la maofisa wa uvuvi kuwanyanyasa wavuvi na watu wengine wanaokamatwa na samaki limezungumzwa mara nyingi bungeni, safari hii lilipata mguso wa pekee na kutisha jamii.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba ndiye alikuwa wa kwanza kuhamisha mada hiyo kutoka mgahawani kwenda ndani ya ukumbi wa Bunge ambako wabunge ‘waliishambulia’ na kusababisha kiti cha Spika kuagiza Serikali itoe taarifa, tukio ambalo liliisha kwa Waziri Mpina kuomba radhi.
Mpina aomba radhi
Ilichukua siku moja kwa Mpina kuomba radhi baada ya kelele za wabunge kuongezeka na mizaha kujaa kwenye mitandao ya kijamii. Alikiri kuwa alikuwa ametumia vibaya sheria husika katika ukamataji wa samaki hao katika eneo ambalo lilipaswa kuombewa kibali kwanza.
Katika tamko lake, Mpima anasema watumishi wa wizara yake waliingia bila ya kibali maalumu na kumhoji mmiliki wa mgahawa huo na kuwapima samaki hao ambao walibaini kuwa walikuwa chini ya sentimeta 25 zinazotakiwa.
“Napenda kukiri kuwa, watumishi katika kutimiza wajibu wao, waliingia bila kibali, kupima chakula kilichopikwa na kwa taratibu hizo. Wizara inaliomba radhi Bunge lako tukufu na wewe Mheshimiwa Spika, na wizara haikuwa na nia mbaya katika jambo hilo,” alisema Mpina.
Pamoja na Spika Job Ndugai kutoa msamaha huo, alizungumza kwa njia ambayo ilionyesha kuwa jambo hilo halikuwa limefurahisha zaidi.
Ndugai alisema katika jambo hilo alikuwa amekasirishwa zaidi kwa kuwa lilikuwa limelidhalilisha Bunge na kwamba mabunge ya nchi nyingine yakisikia kuwa kuna jambo kama hilo limetokea Tanzania yatashangaa kwa kuwa yalipaswa kujifunza hapa.
Mpina akosa mtetezi
Kila mbunge aliyesimama kuzungumzia suala hilo alionyesha kukerwa na kitendo kilichofanywa na Mpina ambaye hata katika mjadala wa bajeti yake, wengine walienda mbali wakisema amejaa kiburi na majivuno.
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Msukuma) ambaye amewahi kueleza kuwa ni mwathirika wa operesheni ya kupambana na uvuvi haramu, alieleza kuwa Mpina ameshindwa kabisa kutumia elimu yake ya uchumi na akashauri kuwa iko haja ya kuangalia vyeti vyake.
Msukuma alikwenda mbali akieleza kuwa mambo hayo kufanyika kwake yanatokana na mbio za urais anazozitaka waziri huyo ambaye aliomba uteuzi wa CCM mwaka 2015.
Lakini, mbunge huyo alihitimisha kuwa Mpina hataweza kuipata nafasi hiyo ya juu katika nchi.
Sheria yawang’ata walioitunga
Pamoja na hoja zote ndani na nje ya Bunge, wabunge wengi wanaizungumzia sheria waliyotunga wao katika mitazamo tofauti, baadhi wakisema haina shida huku wengine wakisema ni mbovu.
Mbunge wa Monduli (Chadema), Julius Kalanga alisema sheria ya kupambana na uvuvi haramu ni mbovu na ilishapingwa na wabunge tangu muda mrefu, lakini kuna baadhi yao walilazimisha ipitishwe.
Kalanga anasema ugumu wa utekelezaji wa sheria hiyo waliuona mapema, lakini wengine hawakauona hadi walipotendewa kile walichoona kinawagusa wao.
Anasema kama ni udhalilishaji, wananchi walishalizwa kwa muda mrefu.
“Tuliipinga sheria hii kwa nguvu zote, ikapitishwa, leo hii imeligusa Bunge wameanza kulalamika. Lakini hawajui kuwa wananchi walishalizwa kwa muda mrefu na bado wanaendelea kulizwa,” alisema Kalanga.
“Naona hakuna haja kuibadili kwa pupa, badala yake tujifunze kuziangalia sheria zote kabla ya kupitishwa.”
Lakini, mbunge wa Mafia (CCM), Mbaraka Dau anamtaka Waziri Mpina kutambua kwamba kuna samaki ambao kimazingira hawawezi kufikia sentimita 25, hivyo kitendo cha kukamata kila samaki bila ya kujua wapi walikotoka hakitasaidia bali kuumiza wananchi.
Dau anasema sekta ya uvuvi ilishasaulika na hata katika bajeti imetengewa asilimia 0.01 ya fedha za maendeleo na kwamba kuna tatizo kubwa katika eneo hilo.
“Mimi ningeomba kule Mafia kuna kiwanda kikubwa cha kuchakata samaki, walikuwa wanafanyia kazi tani 20 hadi tani 30 kwa mwezi, lakini kwa matamko ya sasa yaliyokuja wanataka kukifunga,” alisema Dau.
“Kuna samaki hawezi kufikia sentimita 25, Waziri njooni mje muongee na wavuvi muwaeleze, kila samaki wakipelekwa wanakuwa ‘reject’ (hawafiki ukubwa), njooni kwani samaki wengine hawafikii sentimita hizo.”
Mbunge wa Babati Vijiji (CCM), Jitu Son alisema sheria ni nzuri lakini utekelezaji wake umekuwa ni kero na kumtaka Waziri Mpina kutafakari na kuangalia namna anavyoweza kutumia mamlaka yake katika kutekeleza sheria za Bunge bila kuwakera watu
Mbunge huyo alisema katika hali ya kawaida haiwezekani Waziri kuingia kwenye migahawa na kuanza kupima samaki waliopikwa wakati sheria inasema apambane na uvuvi haramu siyo upishi haramu.
Anataka jambo hilo liangaliwe kwa mapana na wizara itengewe fungu la kutosha kwa ajili ya kutoa elimu kwa Watanzania wote, vinginevyo wataumiza zaidi watu wa hali ya chini.
Mbunge wa Temeke (CUF), Abdallah Mtolea alisema sheria hiyo ina mapungufu makubwa na inapaswa kubadilishwa haraka kwa kuwa hata kanuni zikitungwa kwa hekima, bado kutakuwa na shida katika utekelezaji wake.
Mtolea alimshukia waziri kuwa angeweza kuifanya sheria iwe na unafuu kwani haisemi kuwa ashughulike na samaki wa jikoni badala yake anapaswa kushughulika na wavuvi haramu, hivyo angeweza kujipambanua katika utekelezaji lakini anatekeleza kwa kufuata mihemuko.
“Kuna samaki wengine hawakui na wengine ni wa kufugwa kwenye mabwawa, hivyo hawezi kulazimisha mfugaji atunze samaki wake hadi wafikie ukubwa wanaoutaka wao wakati si mali yao. Je, katika maeneo ambayo samaki hawakui nako hali ni hivyohivyo?” alihoji Mtolea.
Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatale, huku akimtaka Waziri Mpina ajitathmini, alisema sheria hiyo inalazimisha hata wavuvi wadogo kutembea na rula kupima kila samaki wanaomnasa.
Lwakatale anasema kama jambo hilo halitaangaliwa kwa mpana na kusimamiwa ipaswavyo, linaweza kupeleka kilio kikubwa kwa Watanzania wa hali ya chini na masikini wasiokuwa na hatia, hasa ambao uvuvi ni sehemu ya maisha yao.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, hakuna namna yoyote ambayo Bunge linaweza kujitetea katika maisha ya Watanzania kwa kuwa mfano ulioonyeshwa na Mpina ni maumivu na kilio kwa watu wa chini kama wafugaji na wajasiriamali.

BIRTHDAY YA CEDRIC A. SENGO

"What a cake..........WC2018"

GSENGOtV
Tarehe 20 mwezi Juni 2018 tunapata nafasi kumtembelea Cedric shuleni kwao Alliance Academy kwaajili ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Cedric (L) his Mom (C) and his friend Alan (R)
Happy birthday son stay happy, healthy and blessed on your special day...and every day of the year.
"Brother, don’t think too much about the past or where you are, because I believe you are destined to be great. On your birthday, I hope you reflect and understand that you are at a turning point in your life. Happy Birthday" says Cuthbert
Furahia utamu wake rafiki.

AaaauUuuu......you too.
We in na de area.
Birthday ting .....Yes sir.
'We are so luck to have you'
HAPPY BIRTHDAY CEDRIC.

USIDHARAU HUWENDA NGURUWE WA NIGERIA NI MSEMA KWELI.




Ahmed Musa anahitaji mabao matatu kuwa mfungaji bora wa Afrika Kombe la Dunia baada ya hii leo kuifungia timu yake mabao yote mawili ya ushindi dhidi ya Iceland
  • Asamoah Gyan(Ghana): Ana Mabao 6.
  • Roger Milla (Cameroon): Alikomea Mabao 5.
Usisahau  Jumanne ijayo itakuwa ni ya kuvutia kwani Nigeria itakwaruzana na Argentina

BRAZIL YATAKATA KOMBE LA DUNIA.


Timu ya Brazil, leo imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Costa Rica na kukaa kileleni mwa Kundi E katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi baada ya kufikisha point 4. Katika mchezo huo, mabao ya Brazil yamefungwa ndani ya dakika sita za nyongeza baada ya zile tisini kukamilika.

Friday, June 22, 2018

MAPEMA LEO RAIS SHEIN AMUAPISHA MRITHI WA JECHA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amemuapisha Mwenyekiti mpya wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Hamid Mahmoud huku Mwenyekiti huyo akiahidi kufuata katiba na sheria.

Hafla hiyo ya kuapishwa Mwenyekiti ilifanyika Ikulu na kuhudhuriwa na viongzoi wa juu wa Serikali akiwemo Makamu wa pili Balozi Seif Ali idi, Spika wa Baraza Mhe.Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Amkungu, wakuu wa vikosi vya SMZ na watendaji wengine.

Mbali ya Mwenyekiti mpya wa ZEC, Dkt. Shein pia aliwaapisha Makamishna wapya wa tume hiyo ambapo na Mabruki Jabu Makame na Fateh Saad Mgeni kutoka CCM, Makame Pandu wa CUF, Dkt. Kombo Khamis Hassan wa NLD,na wengine na jaji wa Mahakama kuu Khamis Ramadhan Shaabn na Bi.Jokha Khamis Makame ambaye alikuwa ni afisa mdhamni wa afisi ya Rais Pemba.

Mwenyekiti mpya wa tume hiyo Mhe.Hamid Mahmud ambaye pia ni Makamu Mwenyekti wa tume ya uchagzu ya taifa - NEC amesema atahakikisha anafanyaa kazi zake kwa uadilifu kwa kufuata katiba na sheria na kanuni bila upendeleo.