Lukaku na Hazard kila mmoja karudi mara mbili kusalimiana na nyavu za Tunisia.
GSENGOtV:- Romelu Lukaku na Eden Hazard walifunga mabao mawili kila mmoja na kuimarisha uongozi wa Ubelgiji dhidi ya England katika Kundi G kwa ushindi wa 5-2 dhidi ya Tunisia Jumamosi.
Kundi hilo linalowajumuisha pia Panama ambao watakutana na England Nizhny Novgorod Jumapili.
Bao la tano la Ubelgiji lilifungwa na Michy Batshuayi.
Tunisia walifungiwa na Dylan Bronn na Wahbi Khazri.
Tunisia wanatarajia Panama wawashinde England ndipo waweze kusalia katika michuano hiyo.
Hilo lisipofanyika basi Afrika itasalia na mataifa mawili pekee katika michuano hiyo - Nigeria na Senegal.
Lukaku amfikia Ronaldo kwa mabao
Lukaku sasa ana mabao manne katika Kombe la Dunia, sawa na Cristiano Ronaldo wa Ureno katika kinyang'anyiro cha kushinda Kiatu cha Dhahabu.
hazard alikuwa amemkosoa mchezaji huyo mwenzake, waliyecheza pamoja Chelsea wakati mmoja, kwa kutoweka wakati wa kipindi cha kwanza mechi dhidi ya Panama.
Lakini leo alitamba mechi yote hadi alipoondolewa uwanjani na nafasi yake akaingia Marouane Fellaini dakika ya 59.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.