ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 31, 2023

'MWANZA INAKWENDA KUVUNJA REKODI'

 

 

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA Ni katika zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Chuo Cha Ualimu Butimba kupitia kampeni endelevu inayoratibiwa na Bank ya #NMB pamoja na wakala wa usimamizi wa misitu #Tanzania #TFS lengo likiwa ni kutunza mazingira nchini. #Ofisiyamakamuwakwanzawaraismazingira #samiasuluhuhassan #mazingira

NCHI KUMI AMBAZO RAIA WAKE WANA SILAHA NYINGI ZAIDI


United States: 120.5% ya Wamarekani anamiliki bunduki

Yemen: Watu 100 wanamiliki bunduki 52.8

Serbia: Watu 100 wanamiliki bunduki 39-1

Montenegro: watu 100 wanamiliki bunduki 39-1

Uruguay: 34.7% wanamiliki bunduki

Canada: 34.7% wanamiliki bunduki

Cyprus: 34% wanamiliki bunduki

Finland: 32.4% wanamiliki bunduki

Lebanon: watu 100 wanamilikini bunduki 31.9

Iceland: 31.7% wanamiliki bunduki


MWANAMUME AUA WATOTO WAKE WAWILI KISA KUACHWA NA MWANAMKE


Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 28 amekiri kuwaua wanawe wawili baada ya mke wake kuondoka nyumbani kufuatia mgomvi mkali wa kinyumbani katika kaunti ya Bomet.

Hillary Kibet Rono anaripotiwa kuwaua watoto wake wavulana wenye umri wa miaka miwili na mitatu kutumia upanga kabla ya kujaribu kujiua kwa kunywa sumu.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Bomet ya Kati Musa Omar anasema mshukiwa anakisiwa kulewa kulipiza kisasi baada ya mke wake kuondoka nyumbani Jumapili

Babake aliwaambia majirani ambao walikimbia na kumkamata mshukiwa kabla ya polisi kufika.

Polisi waliondoa miili ya watoto hao na kupata kichupa kilichokuwa na sumu inayoaminika kunywewa na mshukiwa.

Alipewa matibabu ya dharura katika kituo cha afya cha karibu kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Longisa ambako anaendelea kupata matibabu.

Polisi wamesema kuwa mke wa mshukiwa aliondoka nyumbani wiki mbili zilizopita akihofia kuuawa na mumewe kutokana na mizozo ya nyumbani ambayo haikuwa ikiisha.

Aliacha wanawe wawili chini ya uangalizi wa baba yao ambaye sasa amewaangamiza.

WATU 35 WAFARIKI BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA INDIA

 


Takriban watu 35 wamefariki baada ya kutumbukia kwenye kisima walipokuwa wakisali katika hekalu moja katika jimbo la kati la India la Madhya Pradesh.

Wengine 14 wameokolewa na mtu mmoja bado hajapatikana katika ajali hiyo iliyotokea katika mji wa Indore.

Polisi wanasema waathiriwa walikuwa wamesimama kwenye slab ya zege juu ya kisima kilipoporomoka chini ya uzani wao.

Kisa hicho kilitokea siku ya Alhamisi wakati wa hafla ya maombi iliyoandaliwa katika hekalu la Beleshwar Mahadev Jhulelal kwenye hafla ya sherehe ya Kihindu ya Ram Navami.

Umati mkubwa wa waumini walikuwa wamesimama kwenye slab ya zege iliyofunika kisima ambacho kiliporomoka kwa uzito wao, na kuwatumbukiza watu wengi kwenye kisima chenye kina cha futi 40 (12m).

Vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti kwamba hekalu hilo lilijengwa baada ya kisima hicho kufunikwa takriban miongo minne iliyopita.

Afisa mkuu Illayaraja T amesema kuwa watu 18 walilazwamekatika hospitali hiyo baada ya kuokolewa na watu wawili wameruhusiwa .

Aliongeza kuwa msako bado unaendelea ili kumpata mtu aliyetoweka.

Timu ya wafanyakazi 75, ikiwa ni pamoja na wale wa serikali na vikosi vya kitaifa vya kukabiliana na maafa wanashiriki katika juhudi za uokoaji.

Waziri Mkuu Shivraj Singh Chouhan ametangaza fidia ya rupia 500,000 ambayo ni sawa na shilingi shilingi 13,978,185kwa jamaa wa marehemu na rupia 50,000 ambayo ni sawa na shikingi za kitanzania 1,421,998 kwa waliojeruhiwa.

TASAC YATUMIA MAONESHO YA BIASHARA,UWEKEZAJI NA FURSA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

 

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa elimu kwa wananchi kuhusu namna linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria wakati wa maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Fursa yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mashujaa kuanzia tarehe 19 hadi 31 Machi, 2023 Mkoani Mtwara. 

Akizungumza na vyombo ya habari wakati wa maonesho hayo Kaimu Afisa Mfawidhi wa Mkoa wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania Mkoa wa Mtwara,Joseph Myaka amesema kuwa katika kutekeleza majukumu yao shirika hilo limejikita katika kutoa elimu kwa wananchi kufahamu shirika hilo linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria. 

Amesema kuwa licha ya majukumu makubwa waliyonayo waliamua kushiriki maonesho hayo ili kuwapa elimu wananchi kuhusu fursa za biashara zilizopo katika Sekta ya Usafiri kwa njia ya Maji sambamba na elimu kuhusu Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa mazingira majini jukumu linalotekelezwa na Shirika hilo. 


“TASAC tunashiriki maonesho haya ya Biashara Uwekezaji na Fursa mkoani Mtwara ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yanayotekezwa Kisheria. kama mdhibiti wa shughuli za usafiri kwa njia ya maji tunasimamia huduma zinazotolewa na Bandari, tunadhibiti na kusimamia ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira na kuratibu shughuli za uokoaji na utafutaji pale panapotokea dhoruba majini” 


“Pia tunatoa elimu kwa wananchi wa Mtwara na wadau wa usafiri kwa njia ya maji katika jukumu letu la Udhibiti wa Safari kwa njia ya Maji na udhibiti Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira majini, wanaweza kufanya shughuli zao kwa usalama na kupata maendeleo na kuongeza pato la Taifa.” Ameeleza Joseph. 

Kwa mujibu wa Sheria, TASAC ina wajibu wa kusimamia kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhimiza usimizi na shughuli za uwakala wa meli wenye ufanisi, kuhimiza shughuli za bandari na huduma za meli zenye ufanisi, kuhakikisha kunakuwepo usalama na ulinzi wa shehena, kuhimiza na kutunza mazingira, usalama na ulinzi wa bahari, maziwa na mito. 


Maonesho hayo ya Biashara, Uwekezaji na Fursa ni maonesho ya Kwanza kufanyika Mkoani Mtwara yakiwa na lengo la kuwaleta pamoja wadau mbalimbali katika Sekta hiyo ili kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kujifunza biashara na uwekezaji wa kisasa pamoja na fursa zilizopo katika sekta hiyo na Mkoa wa Mtwara kwa ujumla. 

Thursday, March 30, 2023

NMB WAJA NA 'BONGE LA MPANGO MOTO ULE ULE'

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Msimu wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka akiba na benki ya NMB Bonge la Mpango umezinduliwa rasmi na mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Paula Chacha. Chacha amezindua kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima, ambako zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 180 zikiwemo pesa tasmlimu, bodaboda, pikipiki za mizigo za matairi matatu na vifaa vya nyumbani vuya kielektoniki zitatolewa katika kipindi cha wiki 12.

UNALIONA WAPI SOKA LA TANZANIA MIAKA MITANO AU KUMI IJAYO?

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Mchambuzi wa masuala ya michezo kutoka Jembe Fm Madanya Jr anasema, mafanikio ya uhakika yanaandaliwa.

BENKI YA CRDB YAANDAA FUTARI KWA WATEJA WAKE

 


Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally (katikati) akiwa ameambatana na Kaimu Sheikh wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, wakiongozana na Mwenyeji wako, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakati walipowasili kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 1,000. Picha zote na Othman Michuzi.

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally (watano kulia) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (watatu kulia) wakikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa watoto wawakilishi wa moja ya kituo cha kuwalea watoto yatima, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Hussein Laay akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Kaimu Sheikh wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al-Baraq, Rashid Rashid akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.


























MHE. RAIS SAMIA NA MHE. KAMALA HARRIS WAKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI IKULU-DAR

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea Mhe. Kamala Harris, Makamu wa Rais wa Marekani Ikulu jijini Dar es Salaam na kuzungumza na vyombo vya habari leo tarehe 30 Machi, 2023

Wednesday, March 29, 2023

NMB NA LVRLAC KUBORESHA MAZINGIRA BONDE LA ZIWA VICTORIA


 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Katika kuhakikisha wakazi wanaoishi katika bonde la ziwa Victoria wanakuwa salama Benki ya NMB kwa kushirikiana na Jumuiya ya Serikali za Mitaa zinazozunguka bonde hilo kutoka nchi za Tanzania , Kenya na Uganda zimeanzisha mkakati wa pamoja wa kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi katika kulinda na kuhifadhi mazingira.

TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA UGANDA DAR

 WENYEJI Tanzania wamechapwa bao 1-0 na Uganda katika mchezo wa Kundi F Kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la The Cranes lililoizamisha Taifa Stars jana lilifungwa na winga wa KCCA ya nyumbani, Kampala, Rogers Mato Kassim dakika ya 90 na ushei akimalizia kazi nzuri ya Farouk Miya wa Rizespor ya Uturuki.

Matokeo hayo yanazidi kuliweka pagumu Kundi F kuelekea mechi mbili za mwisho, kwani sasa ukiondoa Algeria ambayo imekwishafuzu kwa pointi zake 12, Tanzania na Uganda zenye pointi nne kila na Niger yenye pointi mbili moja wapo unaweza kufuzu pia.

MHE. RAIS SAMIA AKIPOKEA TAARIFA YA CAG NA TAKUKURU - IKULU, DAR ES SALAAM

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka 2021/2022 kutoka kwa Ndugu Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Ripoti ya TAKUKURU ya Mwaka 2021/2022 kutoka kwa CP. Salum R. Hamduni, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 29 Machi, 2023

Tuesday, March 28, 2023

UJENZI WA SGR MWANZA-ISAKA WAFIKIA ASILIMIA 28% 'WANANCHI CHONDE CHONDE MSILALE' - KAMATI YA BUNGE

 NA ALBERT G. SENGO/SIMIYU

Kamati ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma leo imetembelea Kiwanda cha uzalishaji Mataluma kwaajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha Mwanza - Isaka chenye urefu wa kilometa 341 kilichopo Seke wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni mbunge wa Ukonga Jerry Slaa








MVUA YALETA ADHA KWA WATUMIAJI WA BARABARA MALINYI

Mvua za masika ambazo zimeanza kunyesha hivi karibuni Wilayani Malinyi leo Machi 28 imesababisha adha kwa watumiaji wa Barabara Kuu kutoka Malinyi kuelekea wilaya jirani za Kilombero na Ulanga.

Maji yamezingira Barabara kwa TAKRIBANI masaa sita ambapo watumiaji wa Barabara hiyo ikibidi kuchukua tahadhari kubwa kutokana na maji kukatiza Barabara ambayo inamilikiwa na wakala wa barabara nchini TANROADS.


Eneo la Madumba lenye makazi ya watu pia limeathiriwa na Mvua ambayo ilinyesha usiku wa Machi 27 ambapo kujaa kwa mto Furua ulisababisha kumwaga maji katika maeneo mbalimbali ya eneo la Madumba.




Mkuu wa wilaya ya Malinyi Sebastian Waryuba amezuru eneo hilo na kushuhudia baadhi ya nyumba zikiwa zimezungukwa na maji ambapo pia kanisa katoliki Malinyi ambalo kuna shule ya wavulana ya Myakatifu Pio iliathiriwa na maji ambayo yalizingira shule na kanisa hilo.

Monday, March 27, 2023

WANAUME WANNE WAMPIGA NA KUMUUA DADA YAO KISA SHAMBA LA URITHI.


Polisi nchini Uganda wanachunguza kisa ambapo wanaume wanne wanadaiwa kumuua dada yao kwa kumpiga katika Wilaya ya Rukiga, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.

Christine Kiconco mwenye umri wa miaka 41 anaripotiwa kuuawa na kaka zake - Innocent Tumwekwase, Samuel Atuhirwe, Christopher Bikorwomuhangi na Justus Mayumba - kufuatia mzozo wa ardhi.

Msemaji wa polisi wa eneo la Kigezi Elly Maate anasema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa familia hiyo ilikuwa na mzozo mrefu kuhusu shamba walilorithi kutoka kwa mababu.

Kwa mujibu wa polisi, kaka hao wanne walipewa vipande vyao vya ardhi lakini wakavipiga mnada punde tu vilipofika katika umiliki wao.

Polisi wanasema kuwa wanne hao walianza kuwaandama dada zao wakitaka ardhi waliyopewa wasichana wa familia hiyo na sasa hilo limeishia katika mauti.

WAZIRI MKUU WA TANZANIA AVUTIWA NA KASI UJENZI WA SGR MWANZA-ISAKA

 


Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa mwishoni mwa juma tarehe 26 Machi 2023 amekagua Mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa SGR Mwanza-Isaka, Kipande cha Tano cha Ujenzi wa reli awamu ya kwanza Dar es Salaam Mwanza.


Kipande hiki cha Mwanza-Isaka kina jumla ya kilometa 341, hadi kukamilika kwake kitagharimu shilingi Trilioni 3.062.



Kipande hicho kitakuwa na jumla ya vituo vya abiria 10 na vituo viwili vya mizigo vya Fela na Isaka.



Maendeleo ya ujenzi huo umefikia asilimia 28.03 na ujenzi wa tuta ni asilimia 58.4 sawa na kilometa 136 kati ya kilometa 249 za njia kuu.


Mradi huo umetoa ajira zaidi ya 6,720 na kandarasi ndogo zenye thamani ya shilingi bilioni 80 hadi sasa.


Baada ya kukagua mradi huo Mheshimiwa Majaliwa amesema amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo huku akitoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kuwa walinzi wa vifaa na mitambo inayotumika katika ujenzi huo.

MAAFISA HABARI SERIKALINI ONGEZENI UBUNIFU - MAJALIWA


Awataka wahakikishe wananchi wanapata elimu na taarifa sahihi


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini waongeze ubunifu wa kusukuma ajenda za Serikali kwa umma na si kusubiri kazi zifanywe na waandishi wa habari wengine.


“Mnapofanya kazi ongezeni ubunifu wa kusukuma ajenda za Serikali kwa umma na msisubiri kazi zifanywe na wanahabari wengine. Hakikisheni kila mwananchi anapata elimu na taaarifa sahihi kuhusu faida na umuhimu wa miradi na mipango au shughuli zinazotekelezwa na Serikali,” amesema.


Ametoa wito huo leo asubuhi (Jumatatu, Machi 27, 2023) wakati akifungua kikao kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kilichoanza leo katika Kituo Cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu amesema: “Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini mnao wajibu wa kuhakikisha kuwa yale yote yanayopangwa na kutekelezwa na Serikali yanafahamika kwa umma wa Watanzania kwa usahihi, kwa wakati na kwa tija.”


Amesema wanapofanya mawasiliano hasa ya kimkakati, wahakikishe wanafahamu lengo la mawasiliano wanayotaka kufanya, faida na matarajio ya kutekeleza mawasiliano husika, nani mlengwa wa mawasiliano hayo pamoja na kuchagua njia sahihi za mawasiliano.


“Nimeona nisisitize hayo kwa kutambua kuwa mafanikio ya Serikali hayana budi kufahamika kwa wananchi wote na ni wajibu wa kila taasisi kuhakikisha mawasiliano hayo yanakuwa ya kimkakati ili yaweze kuleta tija na kufikia malengo yaliyokusudiwa.”

 

Ili kuwawezesha maafisa hao kutekeleza majukumu yao, Waziri Mkuu amewaagiza Makatibu Wakuu wote, Wakurugenzi wa Halmashauri na taasisi zote za umma watenge bajeti ya kutosha kugharamia shughuli za utoaji wa taarifa pamoja na elimu kwa umma na kuhakikisha jukumu hilo linatekelezwa kwa tija na ufanisi uliokusudiwa.

Pia amewataka viongozi wa wizara na wakuu wa taasisi waweke kipaumbele cha kuwashirikisha maafisa habari kwenye vikao mbalimbali ikiwemo vikao vya menejimenti ili waweze kwenda na wakati na kupata ufahamu wa kutosha wa taasisi na mipango ya Serikali.


Mapema, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari alisema wizara hiyo ipo katika hatua za mwisho kukamilisha utayarishaji wa Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano kwa Umma (The National Communications Strategy) ambao ukikamilika utaainisha na kufafanua utaratibu wa upatikanaji na usambazaji wa taarifa za Serikali kwa umma.


“Pamoja na mkakati huo, tuko kwenye hatua za mwisho za uandaaji wa Mkakati wa Mawasiliano Serikalini wakati wa Majanga (Risk Communication Strategy) na Mkakati wa Taifa wa Kujitangaza (National Branding Strategy).”


Pia alimkabidhi tuzo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua na kuthamini mchango wake katika kuimarisha sekta ya habari, demokrasia, uwazi, uhuru wa kutoa maoni na kupata taarifa nchini.