ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 31, 2023

MWANAMUME AUA WATOTO WAKE WAWILI KISA KUACHWA NA MWANAMKE


Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 28 amekiri kuwaua wanawe wawili baada ya mke wake kuondoka nyumbani kufuatia mgomvi mkali wa kinyumbani katika kaunti ya Bomet.

Hillary Kibet Rono anaripotiwa kuwaua watoto wake wavulana wenye umri wa miaka miwili na mitatu kutumia upanga kabla ya kujaribu kujiua kwa kunywa sumu.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Bomet ya Kati Musa Omar anasema mshukiwa anakisiwa kulewa kulipiza kisasi baada ya mke wake kuondoka nyumbani Jumapili

Babake aliwaambia majirani ambao walikimbia na kumkamata mshukiwa kabla ya polisi kufika.

Polisi waliondoa miili ya watoto hao na kupata kichupa kilichokuwa na sumu inayoaminika kunywewa na mshukiwa.

Alipewa matibabu ya dharura katika kituo cha afya cha karibu kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Longisa ambako anaendelea kupata matibabu.

Polisi wamesema kuwa mke wa mshukiwa aliondoka nyumbani wiki mbili zilizopita akihofia kuuawa na mumewe kutokana na mizozo ya nyumbani ambayo haikuwa ikiisha.

Aliacha wanawe wawili chini ya uangalizi wa baba yao ambaye sasa amewaangamiza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.