ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 9, 2014

KHADIJA KOPA NA ABDUL MISAMBANO WATUA MWANZA ASUBUHI HII KWAAJILI YA SHOW YA BUZURUGA PLAZA HII LEO.M

SIKIA MPANGO MZIMA LEO PALE BUZURUGA PLAZA MWANZA. 
Malkia wa Taarab nchini Tanzania Khadija Omar Kopa akiwasili katika uwanja wa ndege wa jijini Mwanza asubuhi ya leo kwaajili ya kutoa burudani kwa wakazi wa Mwanza hii leo (Ijumaa) katika ukumbi wa Buzuruga Plaza Nyakato.
The Super Roxx Abdul Misambano akiwasili katika uwanja wa ndege wa jijii Mwanza asubuhi ya leo kwaajili ya kutoa burudani kwa wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake kwenye usiku wa Mitikisiko ya Pwani katika ukumbi wa Buzuruga Plaza Nyakato jijini Mwanza.Kiingilio ni shilingi 10,000/=.
Vaa, Nukia, Pendeza kwani langoni kuna Red carpet kwaajili yako hivyo twataka picha za kunukia!!!

HABARI KATIKA PICHA, SSRA WAENDELEA NA SEMINA MWANZA, SAFARI HII ILIKUWA NI VIONGOZI WA WAFANYAKAZI KUPATA KOZI.

Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mawasilano wa SSRA), Sarah Kibonde Msika, katibu wa TUCTA Taifa,  Nicolaus Mgaya Mwenyekiti wa TUCTA (M) Mwanza Yusuph Simbaulanga, na Katibu wa TUCTA Mkoa wa Mwanza,  Evarist Mwalongo, wakiimba wimbo wa Mshikamano wakati wa Semina ya Viongozi wa Vyama vya wafanyakazi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa CWT Mkoa wa Mwanza.
Viongozi wa Wafanyakazi wakiimba Wimbo wa Mshikamano wakati wa Semina hiyo.
Katibu wa TUCTA Taifa Nicolaus Mugaya akifungua Semina kwa Viongozi hao wa Wafanyakazi.
Hapa Nicolaus Mugaya akiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi hao.
 Nicolaus Mugaya Katibu Mkuu wa TUCTA Nchini akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari.
Bibi Sarah Kibonde  Mkuu wa Mawasiliano wa SSRA, akiwa anawasilisha mada katika Semina hiyo.
 Semina inaendelea hapa na Washiriki wakiwa wametulia tuliii.
Darasa limekolea na sasa Ishara zinabidi zitumike zaidi.
Maswali haya kukosekana, Pichani ni Bw. Samweli Mkama aliye simama katikati aliyetaka kufahamu hatima ya wafanya kazi 260 ambao hadi sasa tatizo lao halijapatiwa ufumbuzi kutokana na kuchangia mifuko tofauti tofauti.

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AWASILI WILAYANI IGUNGA MKOANI TABORA JANA JIONI KUANZA ZIARA WILAYANI HUMO.

 Pichani Kulia ni  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora,Ndugu Hassani Wakasubi akimpokea mgeni wake,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake alipowasili jioni ya leo katika kijiji cha Makomelo wilayani Igunga mkoani Tabora kwa ziara ya siku 10,ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi. 

 Ndugu Kinana akisalimiana na Wananchi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Makomelo mapema leo jioni.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama ngoma ya kiasili iliondaliwa wilayani Igunga wakati wa mapokezi ya Ndugu Kinana, ambaye ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye na viongozi mbalimbali wa chama hicho,mara baada ku kuwasili kijiji cha Makomelo Wilayani hummo jioni ya leo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kijiji cha Makomelo Wilayani Igunga mkoani humo tayari kwa kuanza ziara ya siku 10 ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi. 
 Ndugu Kinana akipokelewa na vijana wa Green Gard tayari kwa kuvalishwa skafu na kukaribishwa wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akiwa sambamba na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya na Mkoa wakisubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Makomelo Wilayani Igunga mkoani humo tayari kwa kuanza ziara ya siku 10 ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.
  Baadhi ya wananchi mbalimbali waliojitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake alipowasili jioni ya leo Wilayani Igunga mkoani Tabora.
 Sehemu ya magari ya Wenyeji waliofika kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana jioni ya leo katika kijiji cha Makomelo,wilayani Igunga mkoani Tabora jioni ya leo.
 Ndugu Kinana akivalishwa skafu
 Ndugu Kinana na Ujumbe wakiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wilayani humo,kwa ajili ya kikao kupata taarifa ya maendeleo ya wilaya na mkoa sambamba na hali ya siasa.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Kamati ya Siasa na Mkoa wakiwa kwenye kikao hicho,ambapo Ndugu Kinana pia alizungumza nao.
PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA-IGUNGA TABORA

Thursday, May 8, 2014

MNARA WA KUPINGA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI WAZINDULIWA WILAYANI SENGEREMA MKOANI MWANZA.

Rais wa Shirika linalohudumia watu wenye ulemavu wa ngozi duniani liitwalo Under the Same Sun, Peter Ash (wa pili kushoto) pamoja na mratibu wa shirika hilo nchini Vick Ntetema, wakiwa na Mkuu wa wilaya ya Sengerema (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa wilaya ya Sengerema Alfred Kapole (kulia) wakishikana mkono mara baada ya rais huyo kuzindua Mnara wa kwanza wa kipekee wa kumbukumbu ya watu waliouawa nchini Tanzania katika matukio mbalimbali yaliyo husisha imani potofu za kishirikina na suala la albinism.  
Mnara huu wa kwanza wa kihistoria dunia umesimikwa katika kipita shoto kikuu kinachounganisha barabara zinazoelekea mkoa wa Geita, Kahama, Bukoba mkoani Kagera na Kamanga mkoani Mwanza, ukiwa umeorodheshwa majina takribani 72 ya watu wenye albinism waliouawa.
Kabla ya uzinduzi huo maandamano yalifanyika yakihusisha wageni pamoja na wananchi wa wilaya ya Sengerema walio hamasika na mpango huo ulionuia kutokomeza kabisa mauaji hayo ya kinyama. 
Viongozi wa kada mbalimbali wilayani Sengerema wakiwa na Rais wa Under the Same Sun Bw. Peter Ash wakisoma majina ya watu wenye albinism waliouawa kwa matukio ya ushirikina.
Mnara uliozinduliwa unamwonyesha baba asiye na ulemavu wa ngozi akiwa amembeba mabegani mtoto wake mwenye albinism huku mama ambaye pia hana ulemavu wa ngozi akisaidia kumvika kofia mwanaye. Kumbe sasa hata baba na mama wasio na albinism katika mwonekano wa ngozi ya kawaida wanaweza kuzaa mtotomwenye albinism.
Pia Shirika hilo la Kimataifa la kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngoziduniani kupitia Taasisi yake ya Under the Same Sun limetoa tuzo ya kwanza duniani kwa vyombo vya habari 127 hapa nchini ikiwemo kampuni ya IPP MEDIA ambayo imejinyakulia ushindi mkubwa wa tuzo 5. Pichani Mwakilishi wa ITV Cosmas Makongo akitoka kupokea moja kati ya tuzo.
Ni tuzo ya kwanza duniani kwa vyombo habari na waandishi wake ambao wameibuka washindi kwa kuhamasika kufuatilia kwa ukaribu matukio mbalimbali yaliyojitokeza na kuyawasilisha kwa jamii.
Mwakilishi wa ITV Cosmas Makongo akipata mkono wa pongezi kutoka kwa Katibu Tawala wilaya ya Sengerema Alfred Kapole mara baada ya kupokea Tuzo kwa Kampuni yake ya IPP kupitia ITV kwa kutangaza bure habari na vipindi vilivyokuwa vikihamasisha kupungua kwa mauaji ya kinyama dhidi ya albinism hapa nchini.
Rais wa Under the Same Sun Peter Ash akitoa hotuba yake kwa jamii iliyofurika katika viwanja vya Telecenter mjini Sengerema. Huku akiwa na baadhi ya watu walioathirika  na matukio ya kinyama walio nusurika kuuawa wakipoteza baadhi ya viungo vyao. Kutoka kushoto ni Bi. Mariam ambaye alipoteza mikono yake kwa kukatwa mapanga na watu waliokuwa wakihitaji viungo vya albino kwaajili ya masuala ya ushirikina, mtoto Festo aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na kukatwa kabisa mkono wake wa kushoto huku aking'olewa meno pamoja na Said Abdalah mkulima mkata mkaa aliyekatwa mkono wake wa kushoto kwa imani hizo hizo. Inasikitisha.
Wadau wa Taasisi ya Under the Same Sun Vick Ntetema (L) na Gamariel mboya (R).
Nao wazazi wenye watoto wenye albinism walifika eneo la tukio kupata elimu. Kutoka kushoto ni Daudi Nzila akiwa na mwanae Elikana na Mathayo Felician akiwa amempakata mwanae Faustin.
Mahudhurio yalikuwa makubwa huku huzuni ikitawala.
Wanahabari mstari wa mbele kunasa matukio.
Eneo lilifurika watu kiasi cha wengine kujikita pembezoni mwa barabara.
Mwanadada Mariam aliyekatwa mikono yake yote na wavamizi, aliwatoa machozi wengi kwa simulizi ya mkasa wake. BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Mwalimu Peter akisoma risala ya Kikundi cha albinism Sengerema kwa mgeni rasmi.
Wananchi wakigawiwa vipeperushi na majarida ya Taasisi inayopambana na ukatili dhidi ya watu wenye albinism ya Under the Same Sun.
Elimu toka kwa majarida.
Wageni wadau wa Taasisi ya Under the Same Sun, ambapo kulia ni Bi. Maphordens Soto ambaye ni Mfamasia Bingwa wa kutengeneza losheni za kuwakinga albinism dhidi ya miale mikali ya mwanga wa jua inayo athiri ngozi zao.
Blogger G. Sengo.
Mnara huu wa kwanza wa kihistoria dunia umesimikwa katika kipita shoto kikuu kinachounganisha barabara zinazoelekea mkoa wa Geita, Kahama, Bukoba mkoani Kagera na Kamanga mkoani Mwanza, ukiwa umeorodheshwa majina takribani 72 ya watu wenye albinism waliouawa.

KKKT WATOA TAMKO MLIPUKO WA BOMU KANISA LA MWANZA.


KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria (DMZV), limeitaka Serikali kuhakikisha inawatafuta watu waliohusika na tukio la bomu lililolipuka kanisani hapo juzi.
Pia, limewataka Wakristo kuwa watulivu, wasiogope wala wasitishwe na mashambulizi hayo na kwamba wasilipize kisasi.
Akizungumza kwenye Kanisa la Imani Makongoro Misheni jana, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria, Andrew Gulle alisema wanaamini shambulio hilo ni la kigaidi na kwamba, Serikali inapaswa kuchukua hatua ya kuwasaka wanaohusika.
“Kanisa tunaamini tukio hili linahusiana na ugaidi, umefika wakati Serikali ikachukua hatua za kuwasaka waliohusika ili sheria ifuate mkondo wake,” alisema Gulle.
Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya dini wanasema huenda tukio hilo linatokana na migogoro inayoendelea kanisani hapo kwa sababu tayari kuna baadhi ya waumini wamejitenga kwa kuanzisha kanisa lingine.
“Wasikwepe matatizo yao ya ndani, kuna askofu aliuawa kwa kupigwa tofali kutokana na migogoro, hivyo hata hili (tukio) litakuwa ni migogoro inayoendelea,” alisema mmoja wa waumini ambaye hakutaka kutajwa jina lake.
Askofu Gulle alikanusha kuwapo kwa migogoro kanisani hapo na kwamba, tukio hilo halihusiani na mgogoro wowote ndani ya Kanisa bali ni ugaidi.
Hali ya majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea kanisani hapo, Benadeta Alfred, imeelezwa kuendelea vizuri katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikolazwa. “Hali ya mgonjwa ni nzuri ukilinganisha na tulivyompokea kwani hata kuongea alikuwa hawezi, lakini hivi sasa anaweza kuongea japo kwa shida,” alisema Lema.

KWA WASANII NA WADAU WOTE WA MUZIKI HAPA BONGO


TATIZO = FURSA

UKIIJUA hiyo hesabu vizuri maisha kwako yatakuwa bam bam.
Wasanii wengi kwa kipindi kirefu tumekuwa tunalalamika kuwa tunabaniwa kwenye MEDIA bila kuelewa kwa kifupi tu ukweli wa mambo.

Kwa Uchunguzi nilioufanya kwa kipindi cha miaka mitatu hivi nimegundua haya, Watayarishaji au watangazaji wa vipindi kwa siku wanapokea zaidi ya nyimbo 30 kutoka kwenye studio mbalimbali hapa nchini, kwao inakuwa ni vigumu kucheza nyimbo zote kutokana either muda kuwa mdogo wa vipindi vyao au kuwa na request nyingi za nyimbo ambazo wamekuwa wanazicheza sana.

Swali likaja kwangu nyimbo au video ambazo hazichezwi na ni nzuri tufanye nazo nini ili na hawa wasanii wapate airtime?

SULUHISHO LA TATIZO
Baada ya kuliona tatizo nikapata idea ya kuzunguka kwanza Manispaa zote ILALA, KINONDONI na TEMEKE kuangalia usajili wa vituo vya bodaboda na bajaj zilizosajiriwa kwenye vituo ambazo pia wameweka radio ambazo zinatumia flash na memory cards, Huku nikapata idea ya kuanzisha KITAA RADIO FM ambayo itahusika na
kuwasambazia watu hapa muziki ule ambao ulishindwa kupenya radioni muziki wa aina yeyote wa Kitanzania ambao mzuri kusikika na watu wakaupenda.

Pili, kwenye upande upande wa video napo nikajiuliza ni mabus mangapi yaendayo mikoani ambayo ndani hutoa burudani ya movies , music video nk nikakuta ni zaidi ya mabus 2000 ,ambapo kwa siku kila bus linasafirisha si chini ya abiria 50, Huku nako nikapata idea ya kuanzisha BODA 2 BODA Television ambayo itakuwa inatoa burudani ya music videos zile tu zilizokosa kupewa Airtime kwa namna moja au nyingine.

Kwa kusema hayo machache napenda kusema KITAA RADIO FM na BODA 2 BODA TELEVISION imezinduliwa rasmi now chini ya kampuni ya SHOWBIZ DEFINED MEDIA Co LTD

NB ; Huduma hii tutaitoa lakini kutakuwa na uchangiaji wa huduma kwa wale watakaokuwa tayari Aksanteni.

Mike Mwakatundu
Marketing Manager
ShowBiz Defined Media Co. Ltd
showbizdefined@gmail.com
+255 786 505 097

Wednesday, May 7, 2014

SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII NSSF LATOA SEMINA KWA WACHIMBAJI WADOGO WAMADINI MWANZA.

Naibu waziri wa wizara ya Nishati na Madini nchini Steven Masele ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi akizindua Mpango maalum na kufungua Semina kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.
Meneja kiongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii NSSF mkoa wa Mwanza akitoa maelezo ya awali na kutambulisha wadau mbalimbali walio hudhuria Semina kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza, ikiandaliwa na NSSF.
 "Mpango huu ni BIMA ambayo ukilipa utakusaidia katika huduma za matibabu wewe na familia yako lakini vilevile mwisho wa siku ukistaafu unachukuwa fedha kwaajili ya kuanza maisha mengine nje ya ajira, ikiwa ni sambamba na kukuwezesha katika suala la mikopo" Alisema Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la taifa la Hifadhi ya jamii NSSF Crescentius Magori.
Wadau wa NSSF wakinukuu pointi za msingi katika Semina ya wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.
"Serikali imetumia zaidi ya shilingi milioni 250 kuwakusanya wachimbaji wadogo ili waweze kuwa na vyama vyao, wapate kutambuliwa ili wapate kusaidiwa," kisha akaongeza  Rais wa Shirikisho la wachimbaji madini Chama cha wachimbaji TZ (FEMATA) John Bina kwa kusema "Napenda kuwahakikishienikuwa kwa sasa wachimbaji wadogo tumejipanga, Ile dhana ambayo watanzania wengi wamekuwa nayo kuwa siye wachimbaji wadogo ni watu wa kutangatanga au wakuzurura haipo!"  
Mameneja wa NSSF Makao Makuu Dar es salaam, Viongozi wa NSSF mikoa ya Mara, Geita, Shinyanga, Singida, Kahama na Mwanza pamoja na viongozi wa FEMATA na vyama mbalimbali vya wachimbaji wadogo wamekutana hapa.
Wadau NSSF.
Katika hotuba yake ya Ufunguzi kwa niaba ya Serikali na wizara Naibu waziri wa wizara ya Nishati na Madini nchini Steven Masele ameishukuru NSSF kwa kukubali kufanya kazi na wachimbaji wadogo.
Wanahabari wakisaka picha zenye mvuto za kutazamika.
"Niliamini kuwa itatuchukuwa muda mrefu kusafiri kuweza kujenga na kutengeneza kitu ambacho kitatambulika kitaifa kitakuwa na heshima inayostahili na kitatoa mchango unaostahili na kitashawishi wachimbaji wengine kuona kwamba hii ni Fursa ambayo hakuna yeyote yule anayeweza kuiacha ipite pembeni. Sasa wacha niwapongeze NSSF kwa kuwa wajanja kati ya mifuko mingine yote ya jamii na kuamua kuliangalia kundi hili ambalo nguvu yake ya baadaye italiongoza taifa kuwa na matajiri wake wa ndani nikimaanisha wawekezaji wa ndani wenye nguvu Mabilionea"  alisema Masele.
Engo ya wadau washiriki wa semina kwa umakini.
Meza ya baadhi ya waratibu wa semina ya NSSF kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.
Kutoka meza kuu hadi kwa wadau washiriki wa semina ya NSSF kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Serengeti, Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.
Naibu waziri Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Steven Masele, akipata picha ya pamoja na Viongozi wa NSSF  pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha wachimbaji wadogo wadogo wa madini (FEMATA).