ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 3, 2013

WASIRA NAPE WAONGOZA KONGAMANO LA VIJANA KUJADILI RASIMU YA KATIBA MWANZA

Mjumbe wa Kamati kuu wa taifa ambaye pia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais mahusiano Uratibu wa sera  Mhe. Stephen Wasira amewaasa wajumbe wa Tume ya Katiba waache kuuza msimamo wao wa kutaka serikali tatu kwa wananchi wawaachie Wajumbe wa Mabaraza ya katiba na wananchi wajadili nakutoamaamuzi yaliyo sahihi. 

Eneo la washiriki kongamano hilo.

Nape amewataka vijana kutafakari kwa kina maamuzi yao na kuwasihi kupinga kwa kauli moja pendekezo la serikali tatu kwani ni kuwaumiza wananchi kutokana na gharama za uendeshaji.

Pia amependekeza vijana wachipue msimamo wa suala la mgombea wa nafasi ya ubunge kuwa 21 badala ya 25 kama ilivyopendekezwa kwenye rasimu ya katiba.

Mijadala ikiendelea na uchangiaji wake.

Kila mmoja alikuja na kipaumbele chake.

Viongozi wa CCM kada mbalimbali.

Wasira akizungumza na wadau wa kongamano.

Wananchi waliohudhuria.

Umakini zaidi ndani ya kongamano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa BOT Capri point Mwanza.

Shughuli imekwisha kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dk. Antony Diallo, Katibu wa CCM Ester Masunga na Katibu Mwenezi wa CCM nchini Nape Mnauye.

MDAHALO WA WADAU WA MAENDELEO YA MKOA WA MWANZA HIII LEO

Fanuel Yona akiongoza mada kuhusu fursa za uwekezaji mkoa wa Mwanza katika mdahalo wa wadau wa maendeleo ya mkoa wa Mwanza uliofanyika katika ukumbi wa Gold Crest. 

Mada kuhusu dhana na uzoefu wa Public private partnership na mipango ya muda mrefu nayo iliwasilishwa.

Wadau nao walipata fursa ya kuelezea uzoefu wao na kufanya uchambuzi wa sera za uwekezaji na biashara, juu ya nini hakikpsawa, nini si sahihi na nini tunaweza kufanya.

Wadau wa habari kwenye mdahalo huo.

Uchangiaji.

Wadau wakihifadhi masuala muhimu ya Mdahalo.

Safu ya waandishi wa habari kutoka kulia ni Flora Magabe, Grace Chilongola wa Habari Leo, George Ramadhan wa gazeti la Nipashe na Erika Elias wa RFA

Afisa habari wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Joseph Mlinzi akizibainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika jiji la Mwanza.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara Mwanza TTCIA Bwana Eribariki Mmary amesema kuwa bado hali ya ufanyaji biashara nchini si ya kuridhisha kwasababu watu wengi wamejitumbukiza katika ufanyaji biashara pasipo kujua taratibu za kufanya biashara kutokana na kuigana, wengi hawafanyi uchunguzi kwa biashara wanazo anzisha.



Wadau wakijishughulisha katika kunakili masuala muhimu.

Rais wa Klabu za waandishi wa Habari nchini Keneth Simbaya kwa upande wake alisema kuwa watanzania wengi kwa sasa wanatumia muda mwingi kujadili matatizo bila kutafuta ufumbuzi hawajui kuwa kadiri wanavyotumia muda mwingi kujadili matatizo wanafifisha uono wa kupata mawazo ya kufumbua matatizo.

Hivyo amewataka kubadilika.

SHARO WA KIHAYA NA BROTHER K WA FUTUHI WAJA NA SONGI LA KIRUGA RUGA - WAPI NI BOMBA


Washkaji wabee wanaotoka katika lile kundi la mchezo wa luninga Futuhi, linalofanya kazi zake ndani ya Star TV, kundi lililojikita katika uchekeshaji (comedy) Sharo wa Kihaya na Brother K hatimaye wameungana na wasanii wengine walio kwenye chain ya kushirikisha sanaa ya Uigizaji na sanaa ya Muziki kama vile akina Kitale, Masanja Mkandamizaji na wengineo.

Kwa mujibu wa msanii Sharo wa Kihaya amesema kuwa wameamua kulitoa songi hili katika kipindi hiki kwaajili ya mitego ya Tamasha kubwa la burudani nchini Tanzania lijulikanalo kama FIESTA wakiamini kuwa ndipo jukwaa kuu la wasanii kuainisha sanaa zao na kutoka.

Nao wanaamini kuwa wimbo wao utafanya vizuri kwa kuwakamata vilivyo wadau wa burudani.  Sikiliza songi hilo kwa KUBOFYA PYAY.   

RAIS KIWETE AFUTURISHA WASANII WA MUZIKI WA BONGO FLEVA, IKULU


Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii wa Bongofleva,Ally Kiba na mdogo wake Abdull Kiba.
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa bongofleva na muigizaji wa Filamu hapa nchini,atambulikae kwa jina la kisanii Zuwena Mohamed a.k.a. Shilole.
 
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongofleva mara baada ya kufturu.Kutoka kushoto, Snura, Keisha, Mwasiti, aliyechuchumaa ni Shilole, Dj Fetty, Mwanahawa Abdul a.k.a Quee Doreen.

Rais Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,TV,Mbwiga Mbwiguke.
 
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya pichani shoto Mwasiti Almas na kulia Zuwena Mohamed a.k.a Shilole wakiwa sambamba na Mtangazaji wa Clouds FM, Dj Fetty wakipakuafutari kufuatia mualiko wa Rais Kikwete kwenye viwanja vya Ikulu,jijini Dar jana.
 
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva wakipata futari kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar jana kufuatia mualiko wa Rais Kikwete.
 
Rais Kikwete akisalimiana na msanii wa bongofleva,Lawrence Malima a.k.a Marlow,kulia
kwake ni Ally Kiba pamoja na Abdul Kiba na kushoto ni Mtangazaji wa East Africa Radio, Sam Misango
 
Rais Kikwete akisalimiana na msanii wamuziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda na kulia kwake ni msanii wa bongofleva,Cassim Mganga,wakati wa kupata ftari jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar.
 
Rais Kikwete akiwasabahi baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya, mara baada ya kupata ftari mapema jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar, Rais Kikwete aliwaalika wasanii mbalimbali kupata ftari ya pamoja Ikulu jana jioni PICHA NA KAJUNA SON.
 

Friday, August 2, 2013

UCHAGUZI ZIMBABWE ULIKUWA HURU ASEMA OBASANJO

Upigaji kura kumchagua rais kati ya Robert mugabe na hasimu wake Morgan Tsvangarai.

Daftari hili lima majina ya wapiga kura waliofariki huku wengine wakiwa wamesajiliwa zaidi ya mara mbili na namba zao za vitambulisho zikiwa zimetofautiana.

Ingawa ni msimu wa baridi kali lakini nchini Zimbabwe lakini licha ya hayo wengi walijitokeza kupiga kura na pia kulikuwa namadai kuwa tayari kumetokea visa vya wizi wa kura hasa kwa daftari la wapiga kura lililotoka mkesha wa kupiga kura.

'Uchaguzi Zimbabwe ulikuwa huru'Obasanjo

Mkuu wa ujumbe wa uangalizi kutoka Muungano wa Afrika nchini Zimbabwe, Olusegun Obasanjo amesema uchaguzi mkuu wa hapo Jumatano ulikua huru na haki. Matokeo ya awali yanaoyesha Rais Robert Mugabe na chama tawala cha Zanu PF wakiongoza kwa kura nyingi
Chama hicho tayari kimedai ushindi. Msemaji wa chama hicho Rugare Gumbo alisema chama hicho kilitarajiwa kushinda kiasi ya asilimia 70 ya kura hizo.

Lakini mpinzani wa Mugabe, Morgan Tsvangirai, amesema uchaguzi huo ni wa uongo na kusema udanganyifu uliofanyika una maana uchaguzi huo haukubaliki.

Waangalizi kutoka Umoja wa Afrika na jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika wanatarajiwa kutoa tamko rasmi hii leo kuhusu uchaguzi huo.

Bw. Obasanjo amesema kulikua na visa kadhaa wakati wa shughuli ya kupiga kura. Hata hivyo amesema visa hivyo haviwezi kutajwa kuwa na uzito wa kubatilisha au kufuta matokeo ya kura.
Msimamo wa Muungano wa Afrika unatofautiana na ule wa kundi la uangalizi la Zimbabwe Election Support Network.

Kundi hilo ambalo ndilo kubwa zaidi linalochunguza kura ya Zimbabwe limekashifu uchaguzi mkuu na kusema ulikuwa na dosari nyingi. Hii ni kwa sababu watu milioni moja walizuiwa kupiga kura.

Huku upande wa Rais Mugabe ulitangaza kushinda uchaguzi na Morgan Tsvangirai akipinga ni dhahiri kwamba Zimbabwe ingali na mgawanyiko mkubwa wa kisiasa..
SHUKURANI BBC Swahili.

WATEJA WAAIRTEL KUTUMA NA KUTOA PESA BURE

Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando, Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa , Meneja  masoko Airtel money Rwebu Mutahaba kwa pamoja wakionyesha Bango la hakatwi mtu wakati wa uzinduzi  wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini

Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando(katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini. Kushoto Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa (kulia) Meneja  masoko Airtel money Rwebu Mutahaba

Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa akiongea na wahandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure itakayo wawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure, pichani Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando, 


Tuma na kutoa pesa bure kupitia huduma ya  Airtel money
·         Wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure
·         hakuna makato yoyote kwenye huduma ya Airtel money – “Hakatwi Mtu Hapa”

Dar es Salaam, Tanzania, Alhamisi 1st Agosti 2013
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma za mawasilino leo imezindua ofa kabambe kwa watumiaji wa huduma ya kifedha ijulikanayo kama ‘Hakatwi mtu hapa’ inayowawezesha wateja wake nchi nzima  kutuma na kutoa pesa kupitia huduma ya Airtel money bila makato yoyote.

Promosheni ya Airtel money Bure itatoa unafuu wa kiuchumi kwa wateja wengi wanaotumia huduma ya Airtel money.

akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando alisema “Airtel inaongoza kwa huduma bora zenye gharama nafuu nchini, na tunaendelea kutoa huduma zenye ubunifu kwa  kuzindua promosheni mbalimbali kwa mwaka mzima.’Hakatwi mtu hapa’ promosheni tunayozindua leo ni mfano na mwendelezo wa dhamira yetu ya kufanya huduma ya Airtel money kuwa suluhisho na huduma bora ya  kifedha nchi nzima”.

Kwa upande wake Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa aliongeza  kwa kusema “ promosheni hii itawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma na kutoa pesa kwenye mtandao wowote bila makato.

“Tunayofuraha kuweza kutoa unafuu kwa wateja kufanya miamala ya pesa bila makato yoyote na kuwaondolea gharama za kutuma na kutoa fedha zillizokuwepo hapo awali.  Tumeamua kufanya hivyo ili kuwawezesha wateja wetu kupata kiasi chote cha pesa zao bila makato yoyote” aliongeza Singano.

Airtel kwa sasa inaendesha promosheni maalumu  kwa wateja  wake ya Airtel yatosha. promosheni ya ‘Hakatwi mtu hapa’  ni msisitizo unaoonyesha Airtel yatosha ambapo huduma zote ikiwa ni pamoja na  kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi, huduma za internet na sasa kwenye huduma ya Airtel money ambayo inakuwa promosheni kabambe , nafuu kuliko zote  nchini. Huduma ya Airtel money sasa  bila shaka Yatosha

Thursday, August 1, 2013

KARIBU ZuRii FASHION & BEAUTY BOUTIQUE ILIYOPO SINZA LEGHO DAR ES SALAAM.

HABARI NZURI KWA WALE WATEJA WETU VIBONGE aka PLUS SIZE NI KWAMBA MZIGO UMESHAFIKA DUKANI. 
KWA WALE KAKA ZETU MNAO TAKA RABA ZA MTOKO ORIGINAL CONVERSE, TOMS NA VANS PIA ZINAPATIKANA. 
WALE WA SIZE NDOGO PIA KUNA NGUO NZURI SANA ZINAPATIKANA.
WAZAZI WAPENDEZESHE PIA WATOTO WAKO NA ZuRii KIDS COLLECTION.
KARIBUNI MJIPATIE VITU VYA SIKUKUU, MAKAZINI, MITOKO NA KANISANI. 
NGUO NZURI, QUALITY NZURI NA BEI NAFUU. 
LOOK GOOD, FEEL GOOD WITH ZuRii FASHION & BEAUTY BOUTIQUE. 
TUNAPATIKANA SIZA LEGHO, NYUMA YA ROMBO GREEN VIEW HOTEL (KUNA KIBAO BARABARNAI PIA). TUPIGIE +255659189769 or WHATSAPP +447404332910 (BUSINESS ONLY). 
NGUO ZA PLUS SIZE ZINAZOPATIKANA NI SIZE 14-20 (UK).  NA SIZE NDOGO NI 8-14 (UK).
KARIBUNI SANA.



WATOTO KUMENYANA NDANI YA TOTO PARTY, IDDI MOSI ART GALLERY MBEZI BEACH, DAR

KAMPUNI ya Glitz Entertainment imeandaa Toto Party kwa ajili ya watoto wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake linayotarajiwa kufanyika katika Art Gallery iliyopo Mbezi Beach siku ya Iddi Mosi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam muandaaji wa tamasha hilo, Deniss Ssebo alisema kuwa hii ni mara ya nne kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto, na wanatarajia kuanza kulipeleka na mikoani.
Katika Tamasha hilo, watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama soka, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi.
Aidha watoto hao pia wataweza kukutana na wenzao wanaoishi katika mazingira magumu.
Mbali na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.

Wednesday, July 31, 2013

MIKUTANO WA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA NA WANANCHI WA MTAA WA MALIMBE WATOA SULUHISHO KWA KERO ZAO

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza  ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani (wa pili kutoka kushoto) akisikiliza kero za wananchi wa mtaa wa Malimbe ikiwa ni sehemu ya utaratibu aliouweka kufanya mikutano ya kila mara katika maeneo ya kata yake, wengine katika picha kushoto kabisa ni Mwenyekiti wa Mtaa Bi Zenaida Musiba, Mtendaji wa kata ya Mkolani Evarist Mtaki, Afisa Ardhi Idara ya Urasimishaji Makazi holela jijila Mwanza Bw. Maduhu Kazi Ilanga, pamoja na Mhandisi wa barabara  halmashauri ya jiji la Mwanza Bw. Malulu.

Mwananchi ambaye ni mkazi wa mtaa wa Malimbe kata ya Mkolani mkoani Mwanza akitoa hoja ya kuitaka Halmashauri ya jiji iwapatie hati baadhi ya wananchi waliopimiwa viwanja na kufanikisha upimaji wa maeneo ambayo hayajapimwa ili kuwa na uhakika wa makazi yao.

Sehemu ya wananchi wa mtaa wa Malimbe kusanyikoni.

Afisa Ardhi Idara ya Urasimishaji Makazi holela jijila Mwanza Bw. Maduhu Kazi Ilanga, akijibu hoja motomoto za wananchi zilizowasilishwa.

Mhasibu wa Wananchi Mwalimu mstaafu Mzee Mahola aliwasilisha 

Akinamama.

Mwananchi akitoa hoja ya ukarabati wa barabara ya Malimbe - Saut - Mnangani hadi Mkolani Centre ili kupitika kiurahisi. 

Mwananchi huyu alimuomba Mstahiki Meya kuwasiliana na SUMATRA na kuwabana baadhi ya wamiliki wa vyombo vya Usafiri wanaokatiza ruti huku magari yao yakiwa yamesajiliwa kuihudumia njia yote.

Mwalimu Crecency Njogopa aliwakilisha akina mama kwa kulizungumzia suala la uhaba wa maji.

Mdau huyu alimuomba Mstahiki Meya kuwabana Tanesco kuongeza juhudi za kutandaza nguzo za umeme bila urasimu ambapo suala hilo limekuwa kero ya muda mrefu, suala ambalo limechangia kuwaficha wahalifu walioleta maafa ya ujambazi na ubakaji hasa kwa wakazi wapangao maeneo hayo wengi wakiwa ni wanafunzi wa Chuo cha SAUT.

Mhandisi wa barabara wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Bw. Malulu akijibu hoja na maswali yaliyojitokeza kwenye mkutano wa wananchi waishio mtaa wa Malimbe. 

Mstahiki Meya akitoa majibu na ufafanuzi kwa yaliyowasilishwa.

Kumalizika kwa mkutano eneo la mtaa wa Malimbe.

Wananchi wakimpongeza Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza mara baada ya mkutano kumalizika huku akitoa majibu mazuri yakitaalamu kupitia safu ya wataalamu alioongozana nao. 

Akina mama nao hawakuwa nyuma kutoa pongezi ambapo ndani yake waliahidi kutoa ushirikiano kwake na wataalamu hao wakati wa utekelezaji.