Upigaji kura kumchagua rais kati ya Robert mugabe na hasimu wake Morgan Tsvangarai. |
Daftari hili lima majina ya wapiga kura waliofariki huku wengine wakiwa wamesajiliwa zaidi ya mara mbili na namba zao za vitambulisho zikiwa zimetofautiana. |
'Uchaguzi Zimbabwe ulikuwa huru'Obasanjo
Mkuu wa ujumbe wa
uangalizi kutoka Muungano wa Afrika nchini Zimbabwe, Olusegun Obasanjo amesema
uchaguzi mkuu wa hapo Jumatano ulikua huru na haki. Matokeo ya awali yanaoyesha
Rais Robert Mugabe na chama tawala cha Zanu PF wakiongoza kwa kura nyingi
Chama hicho tayari
kimedai ushindi. Msemaji wa chama hicho Rugare Gumbo alisema chama hicho
kilitarajiwa kushinda kiasi ya asilimia 70 ya kura hizo.
Lakini mpinzani wa
Mugabe, Morgan Tsvangirai, amesema uchaguzi huo ni wa uongo na kusema
udanganyifu uliofanyika una maana uchaguzi huo haukubaliki.
Waangalizi kutoka
Umoja wa Afrika na jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika wanatarajiwa kutoa
tamko rasmi hii leo kuhusu uchaguzi huo.
Bw. Obasanjo amesema
kulikua na visa kadhaa wakati wa shughuli ya kupiga kura. Hata hivyo amesema
visa hivyo haviwezi kutajwa kuwa na uzito wa kubatilisha au kufuta matokeo ya
kura.
Msimamo wa Muungano wa
Afrika unatofautiana na ule wa kundi la uangalizi la Zimbabwe Election Support
Network.
Kundi hilo ambalo
ndilo kubwa zaidi linalochunguza kura ya Zimbabwe limekashifu uchaguzi mkuu na
kusema ulikuwa na dosari nyingi. Hii ni kwa sababu watu milioni moja walizuiwa
kupiga kura.
Huku upande wa Rais
Mugabe ulitangaza kushinda uchaguzi na Morgan Tsvangirai akipinga ni dhahiri
kwamba Zimbabwe ingali na mgawanyiko mkubwa wa kisiasa..
SHUKURANI BBC Swahili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.