Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu ameeleza kushangazwa kwake na hali mbaya ya umasikini unaowakumba Watanzania, huku taifa lao likiwa imejaa rasilimali nyingi zisizo na kifani.
Amesema, Tanzania ni nchi tajiri sana wa rasilimali, lakini wananchi wake bado wanakabiliwa na tatizo la umasikini, jambo ambalo amesema upo umuhimu zaidi wa uwezeshwaji wa wananchi, ili kuondoa tatizo hilo la umasikini katika ngazi ya kaya, mkoa hadi taifa.
Dk Nagu ameyasema hayo leo jijini Mwanza wakati akifungua Kongamano la siku mbili linaloratibiwa na TAPSEA lililo kutanisha Makatibu Muhtasi takribani 1500 wa mikoa mbalimbali nchini katika Hoteli ya Kimataifa ya Malaika iliyoko nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Pi amewataka makatibu muhtasi nchini kupitia fursa na nguvu waliyonayo kuanzisha Sacos ili kujikwamua kutoka katika hali duni za maisha licha ya watumishi hao kuwa na changamoto kubwa ya viwango vidogo vya mishahara.
Hata hivyo, alikwenda mbali zaidi na kuwaonya Watanzania kwamba, wasibweteke na hali waliyo nayo sasa, bali wachangamkie fursa zilizopo nchini za uwekezaji, ili wasije wakabaki watazamaji tu katika sekta hiyo muhimu na mkombozi mkubwa wa umasikini.
Katika hatua nyingine, mkuu wa mkoa wa Mwanza Erenest Ndikiro amewashukuru wadau wote wa TAPSEA kwa kuichagua Mwanza kuwa sehemu ya kufanyia Kongamano hilo huku akiamini kuwa kupitia ugeni huo basi ni fursa tosha kwa mkoa kuzitangaza zaidi raslimali za utalii zilizopo kanda ya ziwa.
Huu ndiyo ukumbi ulio lihusu Kongamano.
Mc wa Kongamano Efraim Kibonde ilikuwa ni zaidi ya 'Jahazi'.
Mwenyekiti wa TAPSEA akihutubia.
Zawadi hiyoo kwa mlezi mweshimiwa Waziri Nagu.
Kuna kitu cha ziada juu ya uonekano mahali hapa.
Nilipendezwa sana na mavazi rasmi ya vitenge yaliyotumika kwenye kusanyiko hili.
Mblogishaji maarufu nchini Otman Michuzi wa 'Mtaa kwa mtaa' naye nikamnasa katika flash na hapa akiniringishia kitu cha 7D.