Barca walipata penalty, lakini Lionel Messi, licha ya maarifa yake na sifa nyingi katika ufundi wa penalty, aliishia kugonga mwamba.
Wakati wa muda wa majeruhi wa dakika tatu zilizoongezwa, Fernando Torres alionyesha utulivu wa hali ya juu sio tu kwa kushambulia ngome ya Barca ambayo kwa muda mrefu ilikuwa haiguswi, lakini vile vile kwa kumchenga hata kipa Valdes na kuutia mpira wavuni kwa makini. Mapema wiki hii, Torres alikuwa amenukuliwa akisema “sio siku zote timu bora hupata ushindi”, matamshi ambayo ni ndoto iliyotimia.
Klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza imefuzu kuingia fainali ya klabu bingwa barani Ulaya, licha ya nahodha John Terry kuonyeshwa kadi nyekundu dakika za mapema, ikisubiri kufahamu kama itacheza na timu ya kocha wao wa zamani, Jose Mourinho, akiwa mkufunzi wa Real Madrid, au pengine watakutana na Bayern Munich, ambao uwanja wao ndio utakaotumiwa kuandaa fainali ya ligi ya klabu bingwa. Real Madrid na Bayern zinapambana leo jioni, tarehe 25 Aprili 2012.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.