ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 7, 2025

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI YA KUMALIZA KABISA KERO YA MAJI NCHINI - NAIBU WAZIRI WA MAJI

 NAVICTOR MASANGU, PWANI 

Naibu waziri wa maji Mhandisi Kundo Mathew amesema kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassana  ni kuendelea  kuhakikisha kwamba inatatua kero na changamoto  ikiwa pamoja na kutafuta ufumbuzi   katika  suala zima la kuboresha  upatikanaji wa maji safi na salama  kwa wananchi bila vikwazo vyovyote.

Hayo ameyabaisha wakati akizungumza katika kikao kazi na wataalamu mbali mbali wa mamlaka za  maji wa Mkoa wa Pwani  ambapo amebasema kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha inafikisha huduma ya maji safi na salama kwa kiwango cha asilimi 85 katika maeneo ya vijijini na kwa upande wa maeneo ya mjini ni kwa kiwango cha silimia 95.

Monday, January 6, 2025

MNEC KASESELA,MWAKA 2025 NI MWAKA WA KUTENDA HAKI, UTU NA UPENDO

 

Mjumbe wa Halmshauri kuu ya chama cha Mapinduzi taifa MNEC Richard Kasesela amesema kuwa mwaka wa 2025 utakuwa mwaka wa kutenda haki kwa kila jambo na kwa kila mwananchi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi pamoja upendo na utu kwa kila mwananchi.

Na Fredy Mgunda

Mjumbe wa Halmshauri kuu ya chama cha Mapinduzi taifa MNEC Richard Kasesela amesema kuwa mwaka wa 2025 utakuwa mwaka wa kutenda haki kwa kila jambo na kwa kila mwananchi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi pamoja upendo na utu kwa kila mwananchi.


MNEC Kasesela alisema kuwa mwaka 2025 ni mwaka wa uchaguzi kwenye vyama vya siasa hadi uchaguzi mkuu wa kuwapata madiwani, wabunge hadi Rais hivyo ni bora ikatumika haki katika chaguzi zote.


Alisema kuwa vyombo vyote vya dola na wananchi wakitenda haki na wakitendewa haki hakutatokea vurugu kama ambavyo zinavyotokea nchi za jirani mara baada ya uchaguzi.


MNEC Kasesela alisema kuwa kila mwananchi akiwa na nidhamu kwenye maamuzi ya kutenda haki na nidhamu ya fedha na muda basi Tanzania itanufaika sana na mwaka 2025 kwa kutenda haki.


Alimalizia kwa kuwaomba viongozi wa dini nchi nzima kuwaombea viongozi wa serikali na vyama vya siasa kudumisha amani, utulivu katika uchaguzi za vyama na uchaguzi mkuu.

UONGOZI WA COREFA WAFANYA MAGEUZI MAKUBWA YA KUKUZA KABUMBU PWANI

 


NA VICTOR MASANGU,PWANI

Chama cha soko Mkoa wa Pwani (COREFA) katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita  Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya michezo hapa nchini imeamua kuweka mikakati kabambe ambayo itaweza kusaidia kuinua kiwango cha kabumbu kwa kuinua soka la vijana, wanawake, pamoja na soka la ufukweni  sambamba na  ujenzi wa  kiwanja cha kisasa cha mpira wa miguu.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa COREFA Robert Munisi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalumu ambao umefanyika  makao makuu ya ofisi za chama hicho kilichopo eneo la kwa Mathias Wilaya ya Kibaha na kuhudhuliwa na viongozi mbali  wakiwemo viongozi wa  soka la wanawake  kwa lengo la kujadili mambo mbali mbali ya maendeleo ya mchezo huo.

Mwenyekiti huyo amesema kwamba lengo kubwa la kukutana katika mkutano huo ni  kwa ajili ya kuweka mikakati na   mipango  madhubuti katika ya uongozi wa COREFA pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Pwani ili kuweza kuona namna nzuri ya kuripoti habari za mchezo wa soka, kusikiliza maoni, changamoto, pamoja na kuelezea mafanikio ambayo yamepatikana kwa Corefa.
Munisi amebaainisha  kwamba lengo lake kubwa ni kuweza kushirikiana na waandishi wote wa Mkoa wa Pwani katika kuhakikisha wanatangaza na kuhabarisha jamii mambo  mbali mbali ambayo ynafanywa na chama ikiwemo kuweka mipango ya kuripoti habari za mchezo wa soka la vijana, wanawake, na soka la ufukweni ikiwa sambamba na kushirikiana katika mambo mbali mbali ambayo yataweza kuletaa tija katika nyanja ya mchezo wa soka ndani ya Mkoa wa Pwani.

"Kimsingi mimi kama Mwenyekiti nimefarijika sana kukutana naa ndugu zangu waandishi w habari ambapo lengo kubwa ni kuzungumza mambo mbali mbali ikiwemo mafanikio ambayo tumeweza kuyapata tangu niweze kuingia madarakani na kitu kikubwa tumeweza kufanya mambo mengi ikiwemo kupata ofisi yetu  eneo la kwa mathiasi japo kwa sasa tumepanga lakini dhumuni etu kubwa ni kujenga ofisi yetu ya Corefa ambaayo itakuwa ni ya kudumu,"alisema Mwenyekiti Munisi.

Aidha alisema kwamba kwa sasa lengo lao kubwa ni kuwa ni uwanja mkubwa wa kisasa wa mpira wa miguu ambao utatarajiwa kujengwa katika kata ya viziwaziwa Wilaya ya Kibaha na kwamba tayari wameshapokea barua ya kupewa eneo kutoka kwa uongozi wa Halmashauri ya mji Kibaha kwa ajili ya kuweza kunegaa uwanja huo ambao kwa upande wao utakuwa ni moja katika ya vitega uchumi vya chama chao.

Kadhalika amesem kwamba  sasa wameshaanza kutekeleza maagizo ambayo yametolewa ba shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) ya kuanzisha ligi ya soka la ufukweni, ikiwa sambamba na kukuza soka la vijana pamoja na soka la wanawake amablo kwa sasa katika Mkoa wa Pwani linafanya vizuri ukilinganisha na miaka ya nyuma iliyopita.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo alitumia mkutano huo kudhamini kwa dhati juhudi za mwandishi wa habari za michezo Mkoa wa Pwani Abdalalah   Zalala kwa kumpogeza na kumkabidhi cheti na kiasi cha shilingi laki moja ikiwa kama ni moja ya motisha katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuandika na kuripoti habari za mchezo wa soka kwa kujitolea na weledi.

"COREFA inatambua mchango wa Mwandishi wa Habari za michezo Abdallah Zalala na leo tunamkabidhi zawadi ya fedha lakini tutaendelea kuwashika mkono Waandishi wote ambao watakuwa wanaandika zaidi habari za michezo za Mkoa wa Pwani,"amesema Munisi

Pia Munisi  amebainisha kwamba  Chama cha soka Mkoa wa Pwani  (COREFA)  kimejipanga na kujizatiti zaidi katika  kuhakikisha mpira unachezwa katika Wilaya zote  kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanunu, miongozo na katiba ya vyama ngazi ya Wilaya, Mkoa, pamoja na Taifa ili kuepusha migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza na kwamba wataendelea kushirikiana bega kwa bega  na wadau wa mchezo  wa soka  ndani ya Mkoa wa Pwani lengo ikiwa mashindano na ligi zote zifanyike kama ilivyopangwa kwa mujibu wa ratiba ya TFF.