NA. VICTOR MASANGU, PWANI
Naibu waziri wa maji Mhandisi Kundo Mathew amesema kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassana ni kuendelea kuhakikisha kwamba inatatua kero na changamoto ikiwa pamoja na kutafuta ufumbuzi katika suala zima la kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi bila vikwazo vyovyote.
Hayo ameyabaisha wakati akizungumza katika kikao kazi na wataalamu mbali mbali wa mamlaka za maji wa Mkoa wa Pwani ambapo amebasema kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha inafikisha huduma ya maji safi na salama kwa kiwango cha asilimi 85 katika maeneo ya vijijini na kwa upande wa maeneo ya mjini ni kwa kiwango cha silimia 95.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.