ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 21, 2011

rOCK CITY LEO SINDIYO IMEFIKA SASA!!''

Ni katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza Leo tareha 21/05/2011. Kwa Kiingilio cha shilingi 3,000/= tu!
20%, Joe Makini, Linah, Barnaba, Sam wa ukweli, Mataluma, GodZilla, Mpoki, Wote hawa kutumbuiza.


Wataalam wa Sound toka Prime Times Promotion wakipata kitu cha supu' Mwanza..

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MAZISHI YA SHEKHE YAHAYA YALIYOFANYIKA LEO.

Baadhi ya wanafunzi wa Marehemu Shekhe Yahaya wakiwa Ibadani nyumbani leo asubuhi.

Makamu wa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal pamoja na baadhi ya viongozi wakiwa kwenye shughuli ya mazishi ya aliyekuwa mtabiri maarufu nchini Shekhe Yahaya Hussein aliyeaga dunia jana jijini Dar es sana kuzikwa leo tarehe 21 May 2011 katika makaburi ya Tambaza.

Friday, May 20, 2011

SHOO LAVU.

Ni mwimbaji mahiri toka nchini Tanzania mwanadada Mwasiti (shoto) na Doreen ambaye yu mtangazaji wa Clouds Tv, hapa walikuwa pande za Dom mwishoni mwa wiki iliyopita.

HUKU MVUA, HAPA CHECHE KULE 'MAJOTROO'

Wasaidizi wa maafa nchini Hispania wakiwa mtaani katika kijiji cha Cordoba kusini mwa nchi hiyo mbele ya magari yaliyopandiana mara kupitia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo.

Nako nchini marekani hali ni tete mvua kubwa kama za enzi za Nuhu zanyesha kiasi cha kusababisha watu kuhaha huku na kule kutafuta makazi, miji imejaa maji barabara hazipitiki kama hali inavyoonekana pichani jimboni Mississippi.

Wakati mvua kubwa zikiripotiwa kunyesha sehemu kadhaa hapa duniani hata kusababisha maafa huko nchini India kuna hali ya joto kali kinomanoma linalofikia nyuzi joto degree 49. Pichani kijana mmoja wa nchi hiyo akijipoza majini ndani ya ziwa Srinagar mara baada ya kutokota na joto hilo.

Radi mbaya kuliko inaripotiwa kutokea na kusambaratisha mnara mkuu wa mawasiliano ulioko katika vilima vya Petrin vilivyoko katika jiji la Prague, katika Jamhuri ya Czech.

Jijini Mwanza mvua isiyo na madhara imenyesha majira ya saa saba na nusu, na kudumu kwa muda wa nusu saa. Hali ya hewa kwa sasa imetulia yaani ni safiiiiii.

SHEKHE YAHAYA AFARIKI DUNIA:

Habari zilizotufikia sasa zinasema kuwa mtabiri mashuhuri nchini ambaye kwa kipindi kirefu amejizolea umaaarufu kupitia utendaji kazi wake Shekhe Yahaya Hussein amefariki dunia mapema leo, tayari familia imethibitisha juu ya taarifa hiyo ya msiba. Taarifa zaidi endelea kuangalia blogu hii.
@ g.sengo


Alizaliwa mwaka 1932 huko Bagamoyo kwa wazazi wakimanyema. Alipata elimu yake ya awali katika shule ya Al-Hassanain Muslim School jijini Dar-es-salaam. Baada ya hapo alikwenda visiwani Zanzibar alipojiunga na chuo kilichojulikana kama Muslim Academy kilichokuwa chini ya Sheikh Abdallah Swaleh Al-Farsy aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar wakati huo. Baada ya kuhitimu alielekea nchini Misri alipoendelea kusomea masuala ya dini katika chuo kikuu cha Al-Azhar kilichopo Cairo.

MWENYEZI MUNGU ILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU.

Thursday, May 19, 2011

MKUU WA IMF AJIUZULU KUTOKA WADHIFA WAKE, ULINZI WATAWALA MAFICHONI KWA MWANAMKE ANAYEDAI KUBAKWA ASIJEJIUA.

Mkuu wa shirika la fedha duniani, Dominique Strauss Kahn amejiuzulu, taarifa hiyo ikichapishwa katika wavuti wa shirika hilo ikisema amejiuzulu ili atumie muda uliobakia kujitetea katika kesi inayomkabili ya kujaribu kumbaka mwanamke mmoja mjini New York.

Strauss Kahn ametuma taarifa yake kwa bodi ya shirika hilo. Amesema kuwa anakanusha mashtaka yote dhidi yake na amesikitishwa na kisa hicho kilichomkabili. Shirika hilo limesema kuwa litatangaza hivi karibuni utaratibu wa kumteua mkurugenzi mpya. Kwa sasa John Lipsky ataendelea kuwa kaimu Mkurugenzi mkuu wa IMF.


Dminique strauss-kahn mahakamani na Mwanasheria wake.
Awali waziri wa fedha wa Marekani amesema kuwa mkuu wa shirika la fedha duniani (IMF), Dominique Strauss-Kahn, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli, hawezi tena kuendesha shughuli za shirika hilo. Timothy Geithner ametoa wito kwa IMF kumteua rasmi kaimu mkuu wa shirika hilo.

Watu wakipita nje ya Hoteli iliyokumbwa na mkasa.
Bwana Strauss-Kahn anazuiliwa katika jela moja mjini New York baada ya kukamatwa hapo jumamosi kwa kosa la kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli moja.

Strauss-kahn ambaye amezuiliwa katika gereza la wafungwa sugu la Rikers Islands mjini New York yupo chini ya ulinzi mkali kuchunga asijiue. Hii ni baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Wakili wa mwanamke huyo kutoka Guinea, Afrika Magharibi, anayemtuhumu Strauss-Kahn, amesema mteja wake amepata mshutuko ambao sio wakawaida. Wakili huyo ameongeza kuwa kwa sasa yupo mafichoni na kwamba anajihisi ''Yuko pekee duniani''.

Strauss-Kahn, mwenye umri wa miaka 62, anakabiliwa na mashtaka saba dhidi yake na iwapo atapatikana na hatia, atahukumiwa kifungo cha hadi miaka 25 jela.


hisani ya bbc swahili

KAMA NI VIPAJI, PENYEWE SINDIYO HAPA!!

Taifa stars ya baadae.
Mwishoni mwa wiki nilipata fursa ya kutembelea viwanja vya shule ya msingi Igoma wilaya ya Ilemela jijini Mwanza, askwambie mtu nilikutana na watoto wadogo wanasukuma kandanda balaa, wakicheza mpira wa makaratasi aka cha ndimu huku wakizingatia sheria kadhaa za soka(ingawa siyo zote)


Mashambulizi yakiendelea kwa nyuma beki akipiga mahesabu ya kuuondosha katika hatari..

Mshambuliaji mara baada ya kuwatoka walinzi hapa akielekea langoni kuzifumania nyavu.

Kama ni suala la nidhamu na utii upo ...Wakubwa wakipita watoto hawa wana utaratibu wa kusimamisha mchezo (yaani pale pale ulipo) kisha wakisha pita mchezo unaendelea kama kawa...

Mwanza kuna timu nyingi sana za watoto (U14) tena zenye vipaji na walimu wazuri wa kujitolea wa soka, ukitembelea vituo hivyo matatizo ni yale yale 'uwezeshwaji'

Wednesday, May 18, 2011

'NI MJINI DASLAMU'

Wataalamu wa mambo wanasema........"

Asubuhi na mapema..na hekaheka za kusaka maji mtaani kwetu.

The house.

Ze ukutaz' barazani.

AJALI YA BASI YAUA 16 GEITA.


Na: Frederick Katulanda, Mwanza

ABIRIA 16 wamefariki dunia na wengine 120 wamenusurika baada ya mabasi mawili kugongana mkoani Mwanza. Mabasi hayo yaligongana jana asubuhi katika Kijiji cha Kibingo, Kata ya Nyamigota wilayani Geita, moja likitokea Musoma kwenda Bukoba na jingine Mwanza likielekea Biharamulo.

Kati ya abiria hao 120 walionusurika, zaidi ya 60 walipata majeraha. Taarifa zilizopatikana kutoka wilayani Geita na kuthibitishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Philemon Shelutete na Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Abdalah Dihenga zimeeleza kuwa ajali hiyo ilitokea saa 3:20 asubuhi.


Akizungumza kwa simu jana, Shelutete aliyataja mabasi hayo kuwa ni la Kampuni ya Mabasi ya Bunda lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Bukoba na basi la Sheratoni ambalo

lilikuwa likitokea Biharamulo kwenda Bukombe.Shelutete alidai kuwa ajali hiyo ilitokea kwa uzembe baada ya dereva wa basi la Sheratoni kulazimisha kulipita roli aina ya Fuso mali ya kampuni ya vinywaji baridi Nyanza Bottling Ltd ya jijini Mwanza, ndipo likagongana na basi la kampuni ya Bunda.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Nonosius Komba alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kwamba wakati huo alikuwa akielekea eneo la tukio. Dk Dihenga alisema awali walipokea maiti za watu wanane na kwamba hadi kufikia saa 7:00 mchana walikuwa na maiti 16.

"Mpaka sasa tuna idadi kubwa ya majeruhi wa ajali hiyo, wanaendelea kutibiwa na madaktari wetu, lakini kati yao majeruhi sita hali zao ni mbaya hivyo tumelazimika kuwakimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi na wengine tumewahamishia Hospitali Teule ya Sengerema kwa matibabu," alisema Dk Dihenga.

hisani ya Mwananchi.

HII NDIYO GHANDHI HALL MWANZA

Mahatma Gandhi (Mohands Garamchand Gandhi) Saint and Philosopher Prophet ao non violence father of the indian nation.

Mahatma Gandhi memorial hall Mwanza.

The foundation stone of this hall was laid on Wednesday 15 AUGUST 1951 (India Independence day) By Mrs. Gladys Ether Rowe wife of the provincial Commissioner and the opening ceremony was performed by his Excellency sir Edward Twining, K.C.M.G..M.B.E., on Sunday September 7 1952.

Gandhi Hall Mwanza
Kama unavyoona ni jengo lenye historia lililomilikishwa kwa halmashauri ya jiji la Mwanza, hivyo ndiyo wanao lisimamia, lakini kama ilivyoada kwa sisi watanzania - pamoja na jengo hili kuzalisha kupitia ukumbi wake kodishwa kwa wastani wa siku 3 kwa wiki, Jengo hili Kama limesahaulika vileeeee!!!...

Tuesday, May 17, 2011

MWANARIADHA WANJIRU AOMBOLEZWA

Wanariadha mashuhuri duniani pamoja na wapenzi wa riadha wamekuwa wakielezea masikitiko yao kufuatia kifo cha ghafla cha bingwa wa Olimpiki wa mbio za Marathon, Samuel Wanjiru wa Kenya.

Mwanariadha huyo wa Kenya alifariki dunia Jumapili usiku nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 24. Polisi wameeleza kuwa alianguka baada ya kuruka kutoka kwenye baraza la ghorofa ya kwanza nyumbani.

Wamesema mwanariadha huyo alikuja nyumbani usiku akiandamana na mwanamke mwingine, na baadaye mke wa Wanjiru- Triza Njeri alikuja akawakuta chumbani, na kwa hasira akafunga mlango wa chumba hicho huku akimwambia mumewe anakwenda kuwaarifu polisi..


Triza njeri (left), Ms Judy Wambui (centre) and international atlete Mary Wacera.
Haijabainika ikiwa Wanjiru aliruka nje kujiua, au kumfuata mkewe, au kwenda kufungua mlango wa chumbani. Polisi waliwahoji wanawake hao wawili kubaini kilichotokea.

Mwezi Desemba Wanjiru alishtakiwa kwa kutishia kumuua mkewe, kumiliki bunduki kinyume cha sheria na pia kumjeruhi mlinzi wa nyumbani.

Baada ya mkewe kuondolea mbali kesi inayomhusu walirudiana, na Wanjiru alitazamiwa kufika mahakamani kuhusiana na shtaka la kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Sammy Wanjiru alikuwa na umri wa miaka 21 aliposhinda medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 mjini Beijing , China, na akawa Mkenya wa kwanza kushinda dhahabu kwenye mbio za marathon za Olimpiki.

Chipukizi huyo aliibuka mwaka 2004 wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 , aliposhinda mbio za marathon za Fukuoka nchini Japan.

Baada ya kushinda taji la Olimpiki, mwaka uliofuatia alishinda mbio za London na pia Chicago. Mwaka jana alitetea taji la Chicago.

Ilitazamiwa na wengi kwamba mwanariadha huyo angeweza kuvunja rekodi ya dunia ya mbio za Marathon ambayo kwa sasa inashikiliwa na Haile Gebreselassie wa Ethiopia.

Haile ameelezea masikitiko yake kufuatia kifo hicho.

''Najiuliza ikiwa sisi kama jamii ya wanariadha tungeweza kusaidia kuepusha tukio hilo.'', alisema Haile kwenye mtandao wa Twitter.

Katibu mkuu wa chama cha riadha nchini Kenya David Okeyo amesema kifo cha Wanjiru ni pigo kubwa kwa Kenya.

'' Alikuwa mwenye furaha na tulitazamia angevunja rekodi ya dunia ya mbio za marathon hivi karibuni'', alisema Okeyo.

Bingwa wa zamani wa dunia Paul Tergat pia kutoka Kenya amesema nchi hiyo imepoteza mwanariadha chipukizi mwenye kipaji.

'' Ni habari za kusikitisha sana, na ni pigo. Alikuwa mwenye umri mdogo na alikuwa na nafasi ya kukimbia kwa miaka mingi. '' alisema Tergat.

Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amesema kifo cha Wanjiru ni pigo kubwa kwa matazamio ya Kenya ya kushinda medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao mjini London

EXEL WITH GRAND MALT NA ST. AGUSTINE MWANZA.

Wanafunzi wa Chuo kikuu cha St. Augustine cha Mwanza wakipata burudani wakati wa Tamasha la Excel with Grand Malt lililofanyika katika viwanja vya Chuo hicho mjini Mwanza juzi.

Katika hali inayoonekana kuwa ni kujipigia debe katika kinyang’anyiro cha tuzo za Excel with Grand Malt, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) cha Mwanza juzi walionyesha vipaji tofauti katika tamasha la uzinduzi wa promosheni ya tuzo hizo lililofanyika katika viwanja vya Chuo hicho mjini Mwanza.

Tamasha hilo lilishuhudia wanafunzi kutoka SAUT wakionyesha vipaji katika fani ya muziki, sanaa ya kuiga sauti ya viongozi mbalimbali na hatimaye kuonyesha mchezo wa soka kati ya wanafunzi wa kozi ya shahada ya juu ya sheria na wale shahada ya juu ya Elimu, ambapo sheria waliibuka kidedea kwa ushindi wa mikwaju ya penati.

Washindi walioshiriki katika kuonyesha vipaji vyao katika tamasha hili walizawadiwa zawadi mbalimbali zikiwemo mabegi ya kubebea kompyuta aina ya lap top, fulana za Grand Malt na kinywaji cha Granda Malt.

Tamasha hilo lilikuwa ni mwendelezo wa matamasha ya uzinduzi wa tuzo za Excel With Grand Malt ambayo yameishafanyika katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Morogoro na Iringa kama njia mojawapo ya kuhamasisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kushiriki katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo.

Excel with Grand Malt ni promosheni inayoendeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake ambacho hakina kilevi cha Grand Malt, yenye lengo la kutoa tuzo za aina mbalimbali kwa wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu hapa nchini.

Washindi watajinyakulia zawadi mbalimbali ambapo zawadi kubwa itakuwa hundi ya kununulia vitabu yenye thamani ya shilingi laki nne. Tuzo hizo zinashindaniwa katika makundi manne ambayo ni utamaduni na burudani, huduma za jamii na mazingira, ugunduzi na kipaji maalum.

Mbali na chuo cha SAUT, vyuo vingine vinavyoshiriki katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo ni Chuo cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara, Taasisi ya Jamii.

Vingine ni Chuo Kikuu Cha Elimu (DUCE), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa na Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa.

Washindi watapatikana kwa njia ya kutuma meseji kupitia simu ya mkononi kwenda namba 0658-517517, kupitia tovuti ya Grand Malt ambayo ni www.excelwithgranmalt.com. Pia kutakuwa viboksi vya kura katika maeneo mbalimbali ya vyuo vinavyoshiriki kama vile kwenye maduka, hosteli, kwenye migahawa .

KIM KARDASHIAN NA BRITNEY SPEARS WATINGA GAUNI MOJA KATIKA WEEKEND: NANI KAFUNIKA?

Britney Spears and Kim Kardashian were seen this weekend rockin the same dress. Brit Brit wore hers Saturday night at the KIIS FM’s 2011 Wango Tango Concert in LA and Kim Kardashian wore it while out on a date in Miami with her boo Kris Humphries.

I gotta ask, Who Rock'd It better?

Monday, May 16, 2011

RAHA YA SOKA LA MCHANGANI MAVETERANI WA IGOMA WAFUNGWA MDOMO NA KILIMO SPORTS CLUB.

Michuano ya YANGE CUP inayoshirikisha mitaa mitatu maarufu katika kata ya Igoma wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza imemalizika jana katika viwanja vya shule ya msingi Igoma kwa mchezo kati ya Maveterani wa Igoma waliokunjugwa bila ya huruma na watoto wao timu ya Kilimo Sport Club bao 6-1.Mchezo huo ulikuwa na vihusishi, vileta raha vyenye asili ya udiferenti vilivyonifanya nikodoe macho kuuangalia mchezo kwa dakika zote tisini.

Jiografia ya Uwanja wa shule ya msingi Igoma inadhihirisha kweli naam hapa ni Rock City kwani kuna vilima vya mawe vya hapa na pale tena vipo katikati ya dimba (cheki mishale) nachakufurahisha zaidi ni kwamba ingawa wachezaji wengine walikuwa wakicheza peku lakini hakuna hata mmoja aliye jikwaa

Bao pekee la maveterani liliwekwa kimiani kupitia mkwaju wa penati iliyopigwa kiufundi naye mzee Aboubakari Balinguna. Mawe kama kawa (tizama mshale)

Mzee Kazi Mashilingi alivunja rekodi kwani alikuwemo ndani ya mchezo kwa muda wa dk 50 yaani dk 45 kipindi cha kwanza na 5 kipindi cha pili bila kuugusa mpira, hapa akitoka kufanya mabadiliko kwa timu yake ya maveterani.

Katika mchezo huo wachezaji waliruhusiwa kutoka na kuingia bila kizuizi cha idadi maalum. Lengo la michuano hiyo ni kuhamasisha mazoezi kwa wazee ili kuimarisha afya.

GIGGS TOKA ENZI HIZO MPAKA SASA NA MATAJI ALIYOYATWAA AKIWA NA MASHETANI WEKUNDU.

Giggs na makombe yake.
Ngao - 8
Premier - 12
Euro - 2
FA - 4
Carling - 4
Na...ah Hizo nyingine sizijui wajameni (msaada kwenye tuta).

M-BLOGISHAJI MAARUFU AMBAYE PIA NI MSANII MKUBWA NCHINI JAPANI AJINYONGA.

Msanii mmoja mwenye jina kubwa nchini Japani, Miyui Uehara, mwenye miaka 24, amefariki dunia juzi alhamisi asubuhi baada ya yeye mwenyewe kujinyonga katika nyumba anayoishi katika eneo la Meguro jijini Tokyo.

Polisi amesema kuwa jirani yake aliuona mwili wake mlangoni kwake akiwa amejifunga skafu na kamba shingoni wkati wa saa nane usiku na ndipo tu aliita watu wa huduma za dharura. Uehara alikimbizwa hospitali ambako madakari walidhitisha kuwa alikwishakufa.

Kwa mujibu wa mtandao wa kihabari wa japantoday , Uehara ni mmoja wa watoto 10 waliozaliwa nyumba moja anayetokea mkoa wa Kagoshima, jambo ambalo si la kawaida sana nchini Japani (Watoto wengi katika familia moja) na kipaji chake kilijibainisha wakati akifanya kazi ya uhudumu katika klabu moja ya starehe, wakati huo alikuwa na miaka 18.


Moja ya picha katika mtandao wake www.oodunia.blogspot.com

Hapo alianza kuonekana kwenye majarida ya wanaume akiyapamba kwa picha zake zilizowafanya wanaume wengi hususan vijana kuyanunua kwa wingi na baadaye alifahamika kama “Malkia” miongoni mwa mashabiki wake.

Uehara anamiliki blogi yenye habari kemkem (www.oodunia.blogspot.com) ambamo aliweka picha zake 'Bila kificho', itembelee ujionee mwenyewe, na uchunguzi wa kipolisi unaonyesha kuwa aliutembelea mtandao huo mara ya mwisho saa 2 asubuhi siku ya jumanne ambapo alielezea huzuni kubwa aliyonayo kwa kutoweza kulipata penzi la Kweli.