ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 20, 2011

SHEKHE YAHAYA AFARIKI DUNIA:

Habari zilizotufikia sasa zinasema kuwa mtabiri mashuhuri nchini ambaye kwa kipindi kirefu amejizolea umaaarufu kupitia utendaji kazi wake Shekhe Yahaya Hussein amefariki dunia mapema leo, tayari familia imethibitisha juu ya taarifa hiyo ya msiba. Taarifa zaidi endelea kuangalia blogu hii.
@ g.sengo


Alizaliwa mwaka 1932 huko Bagamoyo kwa wazazi wakimanyema. Alipata elimu yake ya awali katika shule ya Al-Hassanain Muslim School jijini Dar-es-salaam. Baada ya hapo alikwenda visiwani Zanzibar alipojiunga na chuo kilichojulikana kama Muslim Academy kilichokuwa chini ya Sheikh Abdallah Swaleh Al-Farsy aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar wakati huo. Baada ya kuhitimu alielekea nchini Misri alipoendelea kusomea masuala ya dini katika chuo kikuu cha Al-Azhar kilichopo Cairo.

MWENYEZI MUNGU ILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. hakika kifo cha huyu mjamaa kinafunga mlango wa kuongoza nchi kichawi, kwa ramli na maluweluwe na uwongo. kinafungua mlango wa nuru katika taifa jipya la tanzania

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.