ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 1, 2019

VITENDO VILIVYOKATAZWA WAKATI WA KAMPENI NA WAKATI WA UCHAGUZI


Rushwa, Kukutwa na silaha wakati wa kampeni, dhihaka, Kutoa lugha zisizokuwa na staha, uchochezi, Kuteremsha bendera ya chama kingine, Ukabila na Udini ni moja kati ya vitendo vinavyokatazwa kwa wanasiasa na vyama vya siasa ima Wakati wa Kampeni au Wakati wa Uchaguzi.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Uchaguzi Serikali za Mitaa kwa mkoa wa Mwanza, bwana Matia Levi katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) ambapo pamoja na mambo mengine pia kikao hicho kilijadili uchaguzi Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika kote nchini Novemba 24 mwaka huu.

Aidha wadau wa vyama mbalimbali nao walipata fursa ya kuchangia mawazo.
Ukaguzi wa Maandalizi wilayani Sengerema.
Vifaa mbalimbali tayari kwa uchaguzi.
Vifaa mbalimbali tayari kwa uchaguzi
Vifaa mbalimbali tayari kwa uchaguzi

SERIKALI YAWATOA HOFU WANANCHI WA HANDENI

Serikali imewahakikishia wakazi wa Handeni, Mkoani Tanga uendelevu wa huduma ya maji licha ya kuharibika kwa miundombinu ya maji kulikosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ametoa kauli hiyo hapo juzi wilayani hapa wakati wa ziara yake iliyolenga kukagua athari ya mvua kwenye miundombinu ya maji sambamba na kupata ufumbuzi wa haraka kufuatia hali ya mvua zilizonyesha kwa takribani wiki mbili mfululizo. 
Mara baada ya kujionea hali halisi, Mhandisi Sanga aliwatoa hofu wananchi wa Handeni ambapo aliwataka kuwa watulivu na aliahidi kuwa Serikali itahakikisha huduma ya maji inarejea haraka iwezekanavyo.
"Ninawasihi wananchi kufanya subira na kuwa watulivu na kuzingatia maelekezo ya Serikali," alisisitiza Naibu Katibu Mkuu Sanga. 
Mhandisi Sanga alibainisha kuwa zoezi la tathmini ya athari ya mvua hizo kwenye miundombinu ya maji wanaloendelea nalo halitochukua zaidi ya siku tatu kama ilivyoagizwa na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa.
"Waziri wa Maji ametuagiza kuharakisha kukamilisha zoezi hili, nasi tutahakikisha linafanyika kwa kasi ikiwa ni pamoja na kutazama njia mbadala ili wananchi wapate huduma ya maji kwa haraka," alisema Mhandisi Sanga. 
Aliongeza kuwa Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli haipo tayari kuona wananchi wake wanataabika na kwamba hatua madhubuti na za haraka zinachukuliwa ili kuhakikisha wananchi wanapata maji.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela akielezea kwa ujumla athari za mvua hizo kwenye Mkoa wa Tanga, alisema kuwa zimeleta madhara kwenye miundombinu ya barabara na madaraja na kusababisha huduma ya usafiri katika maeneo mbalimbali kuathirika.
“Tulichokibaini katika mvua hizi zilizonyesha ni kuwa zimeharibu mabwawa ya maji na kusababisha maji yaliyotoka katika mabwawa hayo kuathiri miundondombinu mbalimbali ikiwemo ya maji na barabara,” alieleza Shigela.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akielezea athari za mvua hizo alisema ni pamoja na kuharibika kwa mabwawa 11 ya maji yanayotumiwa na wakazi wa Handeni na maeneo jirani na kati ya hayo yapo mabwawa makubwa matano ambayo aliyataja kuwa ni Kwenkambara, Mandera, Suwa, Msomera na Mkomba.
Aidha, Gondwe alipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna inavyotekeleza majukumu yake kwa wakati na kwa hatua mbalimbali za haraka zinazoendelea kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kurejesha mawasiliano ya miundombinu ya barabara na maji iliyoathirika.
Sambamba na hilo, Gondwe alimpongeza Mhandisi Sanga na timu ya wataalam aliyoambatana nayo kutoka Wizara ya Maji na taasisi zake kwa kufika Wilayani hapa mapema ili kufanya tathmini ya uharibifu wa miundombinu ya mabwawa ya maji ili kupata ufumbuzi.
“Kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Handeni tunatoa shukrani nyingi sana kwa Mheshimiwa Rais kwa kutujali na kuwatuma watendaji wa Serikali kufika hapa Handeni ili kutatua matatizo yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha,” alisema Gondwe.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), Mhandisi Clement Kivegalo ambaye ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Sanga alisema kuwa wanaendelea na tathmini ila kwa mabwawa yaliyopasuka wamebaini yalijengwa chini ya kiwango na pia hayakuwa yakitunzwa inavyostahili na hivyo kupelekea kuharibika wakati mvua hizo zilizonyesha.

CAPTIONS
1.   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati) akielekeza jambo wakati wa ziara ya kukagua athari ya mvua kwenye miundombinu ya maji Wilayani Handeni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), Mhandisi Clement Kivegalo

2.   Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), Mhandisi Clement Kivegalo (wa tatu kutshoto) akieleza jambo wakati wa ziara ya kukagua athari ya mvua kwenye miundombinu ya maji Wilayani Handeni. Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga.

3.   Athari ya mvua kwenye miundombinu ya maji Wilayani Handeni

4.   Timu ya wataalam kutoka Wizara ya Maji ikiendelea na ukaguzi wa athari ya mvua kwenye miundombinu ya maji Wilayani Handeni

5.   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe wakati wa ziara ya ukaguzi wa athari ya mvua kwenye miundombinu ya maji Wilayani humo.

6.   Timu ya wataalam kutoka Wizara ya Maji ikiendelea na ukaguzi wa athari ya mvua kwenye miundombinu ya maji Wilayani Handeni

HATIMAYE TUZO YA UBORA KWA KAMUNI YA MWANZA QUALITY WINES YATINGA OFIZI ZA MKOA WA MWANZA


HATIMAYE Kampuni ya Mwanza Quality Wines mapema hii leo imekabidhi rasmi tuzo yake ya ubora kwa ushindi wa kwanza kitaifa kwa makampuni ya kati  (mid size company) kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.

 Kampuni ya Mwanza Quality Wines inayozalisha mvinyo wa matunda jamii ya Power Banana imeibuka mshindi wa jumla wa tuzo za kampuni 100 bora (Top 100 Awards) mwaka 2019/20 zinazotolewa chini ya uratibu wa kampuni ya ukaguzi wa hesabu za fedha KPMG kwa kushirikiana na Mwananchi Communications Limited (MCL).

Tuzo hizo zilitolewa Oktoba 25, 2019 jijini Dar es salaam huku mapokezi ya tuzo ya mshindi wa jumla yakifanyika Oktoba 31, 2019 katika uwanja wa ndege wa Mwanza ambapo hiyo ni hatua kubwa kwa kampuni ya Mwanza Quality Wines ambayo tuzo za mwaka 2018/19 ilishika nafasi ya 30.

Naye mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema kuwa kampuni hiyo licha ya kuupa mkoa heshima kwa kuibuka washindi, bali pia imekuwa changamoto kuona matokeo chanya ya mapinduzi ya viwanda kwa mkoa wake naye amejipanga vyema kuona makampuni mengine yakisifika kwa uzalishaji bidhaa bora katika soko la ndani na nje ya nchi. 

BALAA! HARMONIZE AFANYA KUFURU MBAGALA SHANGWE KAMA LOTE


BALAA! HARMONIZE AFANYA KUFURU MBAGALA SHANGWE KAMA LOTE Msanii Anaetamba na Ngoma ya UNO Amefanya show katika viwanja vya Mbagala Zakheim kutambulisha Ngoma hiyo kwa mashabiki zake maeneo ya Mbagala

WANACHAMA CCM WATISHIA.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya mpanda Abel kimazi ameshindwa kutoa sababu za kutopitishwa jina  la mgombea aliyeshinda kwa madai kuwa  ni siri ya kikao cha chama.

Hata hivyo amedai kuwa chama cha mapinduzi kinafuata katiba kanuni na taratibu katika kufanyia maamuzi hivyo kikao kinauwezo wa kutengua au kumpitisha mgombea aliyechaguliwa na sio kigezo cha kura.

Na Adelina Kapaya, Katavi

Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Irembo Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi wametishia kutokushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa madai ya kupitishwa mgombea wa ngazi ya mwenyekiti wa mtaa  ambaye  hakushinda kwenye kura za maoni .

Paskal kasomo ni mgombea aliyeshinda kwa kura 85 lakini jina  lililopitishwa  ni David sanganzila aliyepata kula 51na kupewa nafasi ya kugombea.

Kwa upande wake paskal kasomo ambaye  alistahili kutetea nafasi hio amesema kuwa hajui sababu zilizofanya jina lake kutopitishwa kwani amefuatilia ngazi ya wilaya na Mkoa lakin hajapewa majibu.

Baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamedai kuwa mgombea aliyepitishwa kutetea nafasi hio hana Sifa ndio maana hakushinda kwenye kura za maoni licha ya kupewa nafasi hivyo wameomba kurudishiwa mgombea waliomchagua.

JAFO AWATUNUKU TUZO WANAFUNZI4191

Nteghenjwa Hosseah OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amewatunuku wanafunzi 4191 tuzo za Astashahada ya awali, kati na Stashahada za chuo cha Serikali za Mitaa  mapema leo Tarehe 31/10/2019 katika viwanja vya Magufuli Square vilivyopo Hombolo chuoni hapo.


Akiwa katika Mahafali hiyo Waziri Jafo amewataka wanafunzi hao kwenda kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili waweze kutangaza sifa njema ya Chuo cha Serikali za Mitaa.

“Najua wengi hapa mtaajiriwa na mtaajiriwa katika Halmashauri zetu nataka muende mkazitendee haki halmashauri hizo, mkafanye kazi kwa bidii na kuleta mabadiliko chanya katika mamlaka zetu za Serikali za Mitaa”
Chuo hiki kinatoa maarifa stahiki kwa mahitaji ya soko la ajira la sasa,  napokea sifa nyingi za wahitimu wa chuo hiki wanapofanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini, naamini ninyi mnaohitumu leo mmeiva vyema kwenda kulitumika Taifa hili alisema Jafo.

Aliongeza kuwa Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma ukawe muongozo wenu katika utendaji kazi wenu wa kila siku, mkafanye kazi kwa umakini mkubwa ili tuzidi kuwa na wataalamu wenye weledi  ili maendeleo ya Taifa yaweze kufikiwa.


Wakati huo huo Waziri Jafo amezitaka  Halmashauri zote kuanza kutumia mfumo ulioboreshwa wa fursa na vikwanzo kwa maendeleo ambao umeandaliwa na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kwa kushirikiana na JICA.

“Mfumo huu ulioboreshwa utazisaidia Halmashauri zetu katika kupambana na vikwanzo vya maendeleo na kuona ni namna gani zinaweza kutumia fursa zinazopatikana katika maeneo hayo” Alisema Jafo.

Nikipongeze chuo hiki kwa kuwa wabobezi na mahiri katika maandiko yenye kutoa Dira na muelekeo  wa kupambana na changamoto zilizoko katika Mamlaka za Serikali za Mitaa alimalizia Jafo.

Naye Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Mpamila Madale amesema chuo hicho mbali na kutoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi pia wamejikita katika Tafiti, kutoa ushauri wa kitaalam pamoja na kuandaa machapisho ya kitaaluma.

Alisema mpaka sasa chuo cha Serikali za Mitaa  kina jumla ya wanafunzi 7436 na ongezeko la wanafunzi hao kumepelekea uhaba wa madarasa ambapo kwa mwaka huu wameweza kujenga darasa moja lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 504 kwa kutumia mapato ya ndani na ujenzi huo umetumia  force account.

Mahafali haya ni mahafali ya kumi na moja na yamehudhurisha wahitimu wa Astashahada ya awali ya ugavi na manunuzi, menejiment ya rasilimali watu,utunzaji wa kumbukumbu, pamoja na maendeleo ya jamii.


Wanafunzi walohitimu kwenye Astashahada ya kati ni Utawala katika Serikali za Mitaa, Uhasibu na Fedha katika Serikali za Mitaa, Ugavi na manunuzi,menejiment ya rasilimali watu, utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka na Astashahada ya kati ya maendeleo ya jamii;


Wakati huo huo wanaofunzi waliohitimu katika ngazi ya Shahada ni Utawala katika Serikali za Mitaa, Uhasibu na Fedha katika Serikali za Mitaa, Menejiment ya Rasilimali watu, Maendeleo ya jamii, Ugavi na manunuzi pamoja na Stashahada ya Utunzaji wa Kumbukumbu 2019.

Tuesday, October 29, 2019

MAADHIMISHO YA SIKU YA AKIBA DUNIANI WANAFUNZI MSINGI NA SEKONDARI MWANZA WAPEWA DIRA


Benki ya Biashara Akiba (Akiba Commercial Bank- ACB) imeahidi kuendelea kutoa elimu kwa umma kuanzia ngazi ya chini yaani kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuhusu huduma za kifedha ikiwemo umuhimu wa kuweka akiba pamoja na manufaa ya kutumia vyombo vya fedha.

Mkuu wa Idara ya Masoko ya Benki ya Akiba, Dorah Saria ameyasema hayo Oktoba 26, 2019 kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo kwenye kilele cha Wiki ya Akiba Duniani 2019 iliyofanyika kwa Mkoa Mwanza katika uwanja wa Furahisha.
RWANDA YAZINDUA MAGARI YANAYOTUMIA UMEME

Rwanda ikishirikiana na kampuni ya Volkswagen na Siemens imezindua magari ya kwanza ya umeme nchini humo yatakayokuwa rafiki kwa mazingira .

Mradi huo ulioanza na magari 50 ambayo yametengenezwa kwa ajili ya majaribio hivyo yatakuwa yakitumiwa kama magari ya uchukuzi wa abiria jijini Kigali na kwingineko nchini humo.

Mkurugenzi mkuu wa Volkswagen Group ya Afrika kusini, Thomas Schäfer amebainisha kuwa magari haya yamo bado katika majaribio na kwamba yametengenezwa 40 aina ya e.Golf na kwamba malengo kwanza si kuuzwa ghali ingawa bei bado haijatangazwa.

''Magari haya hayana mpango wa kuuzwa kwa wateja kwa sasa. Tunalenga kwanza kuyafanyia majaribio na kujua yanafanya kazi vipi na ndipo tutakapowajulisha iwapo zitauzwa au la. Magari haya ni ghali ikilinganishwa na yale ya kawaida, kutokana na betri yake.

Betri peke yake ina gharimu kiasi cha dola 8000 za Kimarekani lakini umeme ukilinganishwa na mafuta ni bei nafuu.

Lakini iwapo serikali ikiwasaidia kwa kuweka sera mfano kwa kupata faida nafuu ,yamkini hali ikawa nzuri zaidi.

Angalia Uchina serikali iliazimia kwamba asilimia 25 ya magari yanayouzwa yawe yanayotumia umeme.''

Serge Iyakoze ni kiongozi wa madereva wa kampuni ya Valkswagen akihusika pia kutoa warsha kwa madereva wenza katika matumizi ta teknolojia ya magari hayo ambaye ameiambia BBC kuhusu wasiwasi au hofu kuhusu mwendo wa kimya wa magari hayo na iwapo hawatarajii kusababisha ajali za barabarani kwa watu waliozoea milio na honi za magari kuwashtua wanaotembea kwa miguu.

''Unapoelekea kupata ajali kawaida huna budi kupiga honi kwani dereva ana uwezo kuangalia kwa upana mkubwa mbele yake,kwa muda mfupi.

Dereva huwa na hisia za kujua kinachoelekea kutokea kwa wakati mfupi. Unapomuona mtu akizubaa unaweza kumpigia honi. Lakini huwezi kwenda ukipiga honi ovyo ovyo,kwani hata mpita njia anao uwezo kuona gari na unaweza pia kumwashia mataa.''

Kampuni imeeleza kuwa inalenga kupanua wigo wa kazi zake katika mataifa mengi ya Afrika .

Baada ya Rwanda, Ghana ndiyo inatarajia kufuata na hatimae kwingineko.

Wakati mataifa ya Ulaya yanalenga kufikia mwaka 2030 kuwa yamekwisha achana na magari yanayotumia mafuta, Afrika ndiyo imeanza safari ambayo hatima yake haijawa wazi ila waliozungumza na BBC wameelezea kuwa hatimae wao pia watafika.

KUTOKA DIMBA LA ANFIELD: LIVERPOOL 2-1 SPURS | MATUKIO NYUMA YA PAZIA MPAKA USHINDI KWA LIVERPOOL


Go behind-the-scenes with this exclusive tunnel cam footage from LFC's 2-1 victory over Tottenham Hotspur at Anfield, thanks to goals from Jordan Henderson and Mo Salah, after Harry Kane put Spurs ahead.

KOMESHENI UBADHILIFU WA DAWA – Dkt. GWAJIMA.

 Dkt. Dorothy Gwajima, Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI (Afya), akifungua kikao cha Wataalam Wafamasia katika ukumbi wa Mikutano wa OR-TAMISEMI (Picha zote na Atley Kuni-TAMISEMI).
 Mkurugenzi wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Ntuli Kapologwe, akitoa maneno ya utangulizi juu ya kikao hicho kabla yakumkaribisha Naibu Katibu Mkuu kufungua kikaokazi hicho.

 Naibu Katibu Mkuu akifungua kikao hicho.
 Wafamasia wa Mikoa wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu hayupo pichani wakati wa kikao cha wataalam hao mjini Dodoma.

Komesheni ubadhilifu wa Dawa – Dkt. Gwajima
Na Atley Kuni- TAMISEMI.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima, amewataka Wafamasia wa Mikoa kote nchini kupambana na kukomesha watu wanaofanya ubadhilifu wa dawa zinazotolewa na serikali kwenda kwenye sehemu za kutolea huduma za afya sambamba na kutafsiri falsafa ya hapa kazi tu kwa vitendo.
Akizungumza katika kikao kazi cha wataalam hao kinachofanyika mjini Dodoma, alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza vema ilani ya Chama cha Mapinduzi kwakuijali na kuipa kipaumbele sekta ya afya na ndio maana katika mwaka wa fedha 2019/20 serikali imepitisha bajeti ya Shilingi bilioni 57.4 ambapo katika mgawanyo eneo la dawa ni miongoni mwa vipaumbele vitatu vilivyo pewa umuhimu.
“Sasa tusimhujumu Mhe. Rais ambaye ameshafanya kazi kubwa na sisi tuliomo ndani ambao tumewekwa kusimamia tunaujuzi na utaalam sehemu ambayo yeye hawezi kuingia, watu wanaiba dawa tunawaangalia, wanaiba vitendanishi tunawaangalia, tutakuwa hatutimizi wajibu wetu kama matazamia yake naya wanachi yanavyotaka” alisema Gwajima.
Gwajima amewataka Wafamasia hao kutumia mfumo wa Ugavi wa dawa wa (elmis) ambao kimsingi taarifa zote za dawa zinaingizwa na kutumika kama muhtadha wa kuombea dawa kwa kila robo. Alisema mfamasia wa Mkoa atakuwa na wajibu wa kuhalalisha maombi ya dawa kwenda MSD kila mara, huku akiitaja mikoa ya kuanzia katika zoezi hilo ni pamoja na Singida, Dodoma, Manyara, Kagera na Geita.
“Tunataka kufanyika kwa Medicine Audit kila robo na taarifa yake kwa kila mkoa iwasilishwe OR-TAMISEMI” alisema Gwajima na kuongeza kuwa “lengo ni kuchakata taarifa za mifumo ya dawa ili kubaini kama kuna hazina ya dawa za kutosha au lah, ili kuweza kusaidia maeneo ambayo yanaupungufu wa dawa.” Alisisitiza Gwajima.
Katika hatua nyingine Gwajima alisema Serikali hivi sasa ipo katika maboresho makubwa ya mfumo wa uendeshaji wa shughuli za Afya (Government of Tanzania Health Management Information System-GoTHOMIS) ambao baada ya kukamilika kwake mfumo utatoa taarifa nyingi za makusanyo ya fedha za dawa mpaka ngazi ya mtumiaji wa mwisho.
Awali kabla yakumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii OR-TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe, alisema Sekta ya Afya imekuwa  miongoni mwa sekta zilizo pewa kipaumbele na Mhe. Rais hivyo kama wataalam lazima tuoneshe kwa vitendo kuwa Mhe. Rais hajakosea katika hili.
“Mtakumbuka ziara ya mwanzo kabisa Mhe. Rais, alijielekeza katika sekata hii muhimu kwa mustakabali wa maendeleo nchi hasa wakati huu tunapoelekea katika uchumi wa kati ifikapo 2025. Lakini hakuishia hapo toka ameingia madarakani imeendelea kutenga fedha kwaajili ya kujenga na kukarabati vituo vya kutolea huduma za afya, ambapo katika mwaka wa fedha 2017/18 vituo vya afya 352 zikiwepo Hospitali 9, Vituo vya Afya 304 na Zahanati 39 zilikarabatiwa, lakini hivi sasa vituo vinavyo jengwa na kukarabatiwa vimefikia 470 zikiwemo hospitali 67 mpya za Halmashauri ambazo zitakuwa na idara kamili ya dawa” alisema Kapologwe.
Kikao cha Wafamasia kimetayarishwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo, lengo likiwa nikuweka mipango ya kuhakikisha mianya ya ubadhilifu wa dawa inakomeshwa lakini pia kuweka mikakati endelevu ya upatikanaji wa dawa katika sehemu zote za kutolea huduma za afya.  

SAIDA KAROLI, MRISHO MPOTO NA WASANII NGOMA ASILI WATAJWA KILELE CHA URITHI FESTIVAL 2019 MWANZA


WASANII Saida Karoli na mkali wa tungo za mashairi zilizojaa utajiri wa lugha fasaha ya Kiswahili Mrisho Mpoto al Maarufu 'Mjomba' wametajwa kuwa sehemu ya watumbuizaji watakaolipamba Tamasha la Urithi Festival litakalofanyika Kitaifa mkoani Mwanza kuanzia tarehe 31/10/2019 hadi 02/11/2019 katika viwanja vya Rock City Mall.

Likiwa limeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, na kusheheni vionjo kibao vya kuunadi utalii wa Tanzania, mgeni rasmi wa tamasha hilo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. kassim Majaliwa Majaliwa.

Akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa mikutano jijini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema kamati ya maandalizi imeandaa ratiba ya matukio, elimu na burudani zenye kuvutia  zikihusisha pia wasanii maarufu wa muziki asili Kanda ya Ziwa , Muziki wa Bendi, Vyakula vya Asili, Mashindano ya Kwaya, Mieleka , Mbio za Baiskeli pamoja na mchezo wa bao, chini ya Kauli Mbiu:- URITHI WETU, FAHARI YETU.

HAPPY BIRTHDAY RAIS WA TANZANIA AWAMU YA 5 JPM 'JEMBE'


Barua kwa mh Rais.

Miaka 60 iliyopita siku kama ya leo huko ardhi ilikuwa imetulia tuli huku miti ikichezacheza na kuzalisha hewa nzuri ya oksijeni. Ikasikika sauti za ndege na wanyama zikitoa nyimbo nzuri nzuri zilizonakshiwa zenye kuashiria jambo la kihistoria katika nchi hii. 

Wahenga wenye kun'gamua mambo wakapata ishara kuwa hii jambo halitokei aghalabu kutakuwa kuna jambo. Basi ndio mama mmoja kutoka huko chato akapata kujifungua mtoto ambaye leo hii amekuwa mkombozi wa watanzania pamoja na kuwa mfano mzuri wa nchi nyingine juu ya ufanisi wake wa kazi. Anaitwa Magufuli ila sisi tunamuita bulldozer, chuma , jiwe na kimbilio la watanzania ambao walikuwa walishakosa matumaini na nchi yao.

Mlimwengu mimi leo nimeamka na kidumu changu cha maji cha lita tano nipate kuelekea ikulu kusherehekea siku yako ya kuzaliwa na kukumwagia maji ikiwa ni ishara ya salamu kutoka mtaani kwetu maana ilikuwa ni miaka mingi watu wa Kibangu na Riverside hawana maji ila sasahivi maji ni kuanzia asubuhi mpaka jioni. Hivyo maji hayo yangeashiria kazi kubwa ambayo umeifanya kuhakikisha wananchi wako wanapata maji na unajua kuwa maji ni uhai.

Ila nimezuiliwa na wazee  kuwa siko serious ila hayo maji nitajimwagia mwenyewe kuridhisha moyo wangu.

Huku kwetu tuna msemo usemao kuwa ' Enkobe ekanyampira eibale norwo olatagamba wakahurila' kwamba nyani alijambia jiwe na kusema kuwa hata kama hujasema chochote ila habari imeipata. 

Point yangu ni kuwa kazi unayofanya wanaona ni kwamba wana macho ila wanajifanya wametia viboriti machoni wana masikio wanajifanya wameweka pamba ili wasisikie. 

Hii ni habari njema ambayo watanzania walikuwa wanaitaka na wapingaji hawajahi kukosekana. Hata mitume wa Mungu walipingwa na wengine wakauliwa sembuse hawa wachumia tumbo.

Vaa mkanda vaa buti wananchi tumeelewa mlimwengu mimi huwa nakaa na walimwengu na hao ndio wanaoiona kazi unayoifanya. Hizi kelele za chura hazina maana haziwezi kuzuia watu tusinywe maji.

Kazi hii unayopiga ni kubwa sana imefikia hatua hadi wananchi wanaona kipindi ulichopewa ni kidogo unahitaji kupata muda mrefu ila hawajui kuwa katiba ndio inayokuweka labda mpaka pale itakaporekebishwa. 

Mambo unayoyafanya siyo hadithi za abunwasi kama ni miundombinu imeonekana, sasa hivi tunapokea madege ambayo tulikuwa tunayaona kwenye mataifa ya wenzetu. Miradi mikubwa ya reli pamoja na barabara zinazojengwa kwa ufanisi wa hali ya juu. 

Nichukue nafasi hii utusamehe baadhi ya watu tunalalamika kuwa unaleta maendeleo ua vitu badala ya watu. Ila hawajui kuwa hayo ya vitu ndio yatakayopelekea kupata ya watu. Miundombinu unayoijenga taifa litakukumbuka maana kazi zitakuwa zimerahisishwa sana.

Ni mtu pekee ambaye umetujengea imani ya kutupa nguvu kwamba Tanzania inaweza kuwa nchi kubwa tukajitegemea pasipo kutegemea misaada kutoka nje na kweli matunda tunayaona sasahivi unatuletea madreamliner kwa uchumi wetu wa ndani. 

Hii ni imani kubwa ambayo umetujenga sasahivi vijana wengi wanawaza kuwa na viwanda vyao kwa sababu ya imani uliyotupa kuwa tanzania ya viwanda inawezekana.

Mchawi mpe sifa zake na msema ukweli ni mpenzi wa mwenyezimungu viatu ulivyovivaa ni size yako wengine viliwapwelepweta ila leo hii vibaka wote umewabana, watu walikuwa wananeemeka peke yao huku wavuja jasho wanaumia. Ila sasahivi utakula chakula ulipopeleka mboga.

Una mengi umeyafanya siwezi kuyamaliza hapa ili nikutakie kheri katika siku yako ya kuzaliwa na kazi njema katika ujenzi wa nchi hii.

Wako
Mlimwengumimi
Mohamed Ismail
0762 07 03 61

Monday, October 28, 2019

WIKI YA 5, HAYA NDIYO MAENDELEO YA AHADI YA JPM UJENZI WA JENGO LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE MWANZA


IKIWA ni wiki ya 5 sasa kwa mara nyingine Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo hilo linalokadiriwa kugharimu Bilioni 12 hadi kukamilika kwake mwezi Aprili, 2020.

Kwa sasa hatua ya awali ya ujenzi wa msingi umefikia asilimia 60 ambapo kazi inafanyika usiku na mchana ili kufikia malengo ya kukamilika ndani ya miezi sita badala ya miezi 12 kama ilivyopangwa hapo awali.

Hatua ya ujenzi wa jengo hilo jipya na la kisasa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilolitoa Julai 15, 2019 wakazi akizindua miradi ya afya katika Hospitali ya Rufaa Bugando ambapo Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela nazo zinachangia shilingi bilioni nne kwenye ujenzi huo.

Mradi huo unasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na Wataalam kutoka Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kupitia mfumo wa "Force Account".
MISS WORLD KWA MWAKA 2018/2019 AITEMBELEA TANZANIA


Mrembo wa Dunia (Miss World) kwa mwaka 2018/2019 Vanessa Ponce De Leon akiwa katika picha ya pamoja na Mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2019/2020 Sylivia Bebwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, - Mrisho Gambo.

Vanessa ambaye ni Raia wa Mexico kwa sasa yuko mkoani Arusha, ambapo akiwa mkoani humo kwa kushirikiana Sylivia, watazindua mashine ya kutengeneza Taulo za kike zitakazojulikana kama Uhuru Pads.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mrembo anayeshikilia Taji la urembo la Dunia mwaka 2018/2019 kuitembelea Tanzania.

Vanessa anashikilia taji la Urembo la Dunia hadi hapo litakapofanyika shindano lingine la kumpata mrembo wa Dunia, shindano linalotarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu nchini Uingereza.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI. IKULU DSM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anapokea hati ya Utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule wafuatao- 1.Mhe. Riita Swan - Balozi Mteule wa Jamhuri ya Finlanda hapa Nchini 2.Mhe. Manfredo Fanti - Balozi Mteule wa Umoja wa Ulaya Nchini 3.Mhe. Meja Jeneral Charles Karamba- Balozi Mteule wa Jamhuri ya Rwanda Nchi Hafla ya Upokeaji wa Hati za utambulisho wa Mabalozi hawa zinafanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.

Sunday, October 27, 2019

MASHABIKI MWANZA WALIA NA KOCHA ZAHERA + MONGELLA ASEMA USHINDI UPO MISRI


Ushindi wa mabao 2-1 walioupata Pyramida FC katika dimba la CCM Kirumba dhidi ya wapinzani wao Yanga umeongeza mzigo mzito kwa wana Jangwani katika jitihada zao za kusonga mbele kwenye Michuano ya Kimataifa kwani sasa wawakilishi hao wa Tanzania watalazimika kushinda bao 2-0 pindi watakapokwenda ugenini wiki mbili zijazo kucheza mchezo wa marudiano.

Licha ya mashabiki wa nyumbani kushusha lawama kwa benchi la ufundi la timu hiyo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella bado ana matumaini na wawakilishi hao wa Tanzania akisema kuwa Yanga wana uwezo wa kupindua meza Misri.