WASANII Saida Karoli na mkali wa tungo za mashairi zilizojaa utajiri wa lugha fasaha ya Kiswahili Mrisho Mpoto al Maarufu 'Mjomba' wametajwa kuwa sehemu ya watumbuizaji watakaolipamba Tamasha la Urithi Festival litakalofanyika Kitaifa mkoani Mwanza kuanzia tarehe 31/10/2019 hadi 02/11/2019 katika viwanja vya Rock City Mall.
Likiwa limeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, na kusheheni vionjo kibao vya kuunadi utalii wa Tanzania, mgeni rasmi wa tamasha hilo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. kassim Majaliwa Majaliwa.
Akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa mikutano jijini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema kamati ya maandalizi imeandaa ratiba ya matukio, elimu na burudani zenye kuvutia zikihusisha pia wasanii maarufu wa muziki asili Kanda ya Ziwa , Muziki wa Bendi, Vyakula vya Asili, Mashindano ya Kwaya, Mieleka , Mbio za Baiskeli pamoja na mchezo wa bao, chini ya Kauli Mbiu:- URITHI WETU, FAHARI YETU.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.