'Haya sasa ugomvi huo' na anaye utaka ni Mnyamwezi' Mr. Hills-So-GooD wa Passion fm ndani ya kitaa cha eneo la tukio.
Mwamba wa kaskazini Joe Makini juu ya Red Capet la Milipuko ya VODACOM.
Watu toka mataifa mbalimbali nao walijumuika kulipuka.
Ni wadada watatu wanaounda kundi linaloitwa 'FAGIO' kutoka nchini uganda, askwambie mtu watamu ile kinyama.
Hapa ngoma sambamba na dance zilipigwaaaaaa', kisha wakaganda hivi kwa style, then chezo likaendelea.
Wanadada wa kundi la FAGIO wakivuma kwao zaidi, Kundi hili Ni mara ya kwanza kufanya show Tanzania na kutokana na ubora waliouonesha wananchi hawakusita kuwapa shangwe.
Producer Q.toka MO Record akiwa na mkewe (walioketi) pamoja na ma-member wa MO Record, wakifuatilia show kwa umakini.
Juma Nature 'wacha awalipue watu'
Raha ya utamu!!
Burudani ilinogeshwa na mpambano baina ya vijana hawa wa VHT (Victoria House of Talent) kutoka Zoo' (Mwanza) pamoja nao THT (Tanzania House of Talent)ktoka Dizim' (Dar es salaam). "Mashabiki walijitenga"
Mavijana ya THT...
Street ili shine ile mbayaaaaaaa!!
THT...Take 2
Dj Chriss (kulia) along side meneja wa FAGIO toka nchini Uganda.
Inspector Haroun aka 'BABU' naye alikuwepo siyo kwa show bali kula maisha.
Watu walifunga mtaa kisha lkapigwa burudani NZURI isiyo kifani, Humo ndani kila kitu kikipatikana, kuanzia burudani, vinywaji, vyakula aina zote, Flowerz nzuri tena zenye kunukia, usalama full yaani kila kitu. aaaaaaaah MILIPUKooooooo!!
Thursday, December 30, 2010
HABARI
Jeshi la polisi mkoani Mwanza linafanikiwa kuwanasa watu wanne waliokuwa katika mpango wakufanya uvamizi katika benki ya BOA iliyopo mtaa wa Kaluta jijini hapa.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mwanza Simon Sirro amesema kuwa mara baada ya jeshi lake kupata taarifa kutoka kwa wasiri wake kuwa kuna watu wamejipanga kuvamia benki hiyo, waliweka mtego na hatimaye kufanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Donard Charles (28) mfanyakazi wa zamani wa benki hiyo aliyetimuliwa kazi.
Baada ya kuhojiwa na maafisa wa polisi, Charles alikiri kuhusika na mpango huo wa uvamizi na kusema kuwa kabla ya kukamatwa, yeye pamoja na wenzake wengine watatu walipanga uvamizi huo ufanyike mnamo tarehe 21 disemba 2010.
Ndani ya maelezo yake mtuhumiwa huyo amesimulia kuwa mara baada ya kufukuzwa kazi alifanya mpango wa kutafuta watu wengine watatu ili apate kushirikiana nao katika mpango huo haramu ambao nao tayari wamekwisha kamatwa.
Kamanda amewataja watu hao wanaoshikiliwa kuwa ni Henry Juma Salehe (32) ambaye ni shoe shine jijini Mwanza, Emanuel Masamilo (27) anayejihusisha na udalali pamoja na Wachu Kaloboka mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga ambaye ndiye mwenye siraha ambayo ilikuwa itumike kutekeleza uvamizi huo.
Thursday, December 30, 2010
HABARI
WAZIRI wa Uchukuzi, Omary Nundu amezindua safari ya treni ya pili inayosimamiwa na Kampuni ya Reli nchini (TRL) Kwenda Mkoa wa Kigoma kufuatia shida ya usafiri inayowakabili wakazi wa mkoa huo. Kuzinduliwa kwa treni hiyo kunatarajiwa kupunguza adha ya usafiri inayowakabili wakazi wa mkoa huo kwa kipindi kirefu sasa.
JE HUDUMA HII NI KWA SIKUKUU TU?
Akizungumza na baadhi ya abiria waliokuwa ndani ya treni hiyo jana,Waziri Nundu alisema kuzinduliwa kwa treni hiyo kutawasaidia wananchi kwenda kusheherekea sikukuu ya mwaka mpya ambapo Serikali imeamua kuruhusu treni hiyo ianze kazi ili kusafirisha abiria wanaopenda kwenda kula sikukuu ya mwaka mpya katika mikoa ambayo treni hiyo inapita.
STESHENI YA MWANZA, ZAIDI YA KUSAFIRISHA MIZIGO, KITUO HIKI HAKIJATOA HUDUMA YA USAFIRI KWA ABIRIA TANGU ZILIPOSITISHWA HUDUMA ZA TREN.
Hata hivyo wakati Nundu akizindua safari ya treni hiyo ilibainikia kwamba menejimenti ya Shirika la Reli nchini (TRL) inayongozwa na wawekezaji kutoka India hawakufurahishwa na hatua ya waziri huyo kuzindua safari hiyo. “Hii safari ni kiini macho kwa sababu wawekezaji hawaipendi na wameahidi kuisitisha baada ya sikukuu ya mwaka mpya” alisema mmoja wa wafanyakazi wa TRL huku akiomba jina lake lihifadhiwe.
Usafiri wa treni umezidi kudorora kila kukicha huku msongamano wa abiria ukizidi kuongezeka ndani ya treni kiasi cha kusababisha kero kwa abiria.
Wednesday, December 29, 2010
BANGO
Huu ndiyo mpango mzima!
Hawa ndiyo FAGIO kundi muziki wa ragga toka nchini Uganda wanaotegemewa kushuka, kukamua na kufanya mchuano FULANI HIVI kwani siku hiyo THT toka dar, VHT toka rock city wote watapanda stage HILO-HILO katika siku tutakapofunga mtaa wa posta na Nyamagana jijini Mwanza, na kisha pale kati MAKAMUZzzz ya BURUDANI zilizoshiba jicho lako likisaidiwa na KITU cha BIG SCREEN na maDVJ toka Uganda, INSHU NZIMA ni tarehe 31 mkesha wa kuuga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka mpya 2011.
Tumeisikia sana, tumeitamani sana na sasa twaenda... Kuiona Kupitia king'amuzi cha Star Times channel namba 8. "Ni kama kufungua mwaka na thamani mpya ndani ya nyumba"
ARUSHA - MWANZA - DODOMA
AAaaaaaaaa YUUUUUUUU REDeeeeeeeeee!!!....................!!!!!
!!...........................KITU HEWANI............................!!
Wednesday, December 29, 2010
BANGO
Kwa kutambua mchango unaotolewa na wasanii wetu katika tasnia ya filamu mtandao huu umeguswa na kazi za wasanii hawa na kuwatambua kwa kuwatangaza, kulingana na zoezi tulilokuwa tunaliendesha la BORA ZA 2010, wadau hawa wamechaguliwa na wapenzi wa filamu hapa nchini kupitia tovuti ya www.filamucentral.co.tz kuanzia mwanzo wa mwezi december katika mtandao huu wa habari za filamu kutoka Swahiliwood.
Tunawapongeza wale wote walioshinda na kuibuka washindi katika nafasi walizoshiriki, kila aliyeingia katika mtanange huu alikuwa ni bora lakini siku ya siku tuliitaji mshindi mmoja ambaye ndiye tunamtngaza leo hii, tumefarijika sana kwa ushirikiano mlioonyesha wadau wa tasnia hii toka mwazo wa zoezi hili hadi mwisho, tunapenda kuwatambua waliotikisa mwaka 2010 na kusema Hongera.
BORA ZA 2010
1. Msanii chipukizi bora za 2010 – HANIFA DAUDI (Jenifer)
2. Muigizaji bora wa kike — YVONNE CHERRYL (Monalisa)
3. Muigizaji bora wa kiume — STEVEN KANUMBA (The Great)
4. Mwandishi bora wa mswaada – ALI YAKUTI
5. Mchekeshaji bora – ATHUMAN MUSSA ( KING MWALUBADU)
6. Filamu yenye kava bora – DANGER ZONE
7. Mtayarishaji bora wa filamu – STEVEN KANUMBA
8. Kampuni bora ya utengenezaji filamu – RJ Company
9. Msambazaji bora – Game 1st Quality
10. Muongozaji bora – VICENT KIGOSI (Ray The Greatest)
Matokeo haya ni kwa mujibu wa watembeleaji wa mtandao huu ndani na nje ya nchi.
ZAIDI TEMBELEA filamucentral.co.tz
Wednesday, December 29, 2010
MICHEZO
Tuesday, December 28, 2010
BANGO
WELCOME KATIKA EVENT YA KUIKARIBISHA 'NYUIYA'
NI MAWE TU MA HIP HOP ZA UKWELI, BONGOFLAVA, HOUSE, RAGGA NA MA R&B FLANI HIVI.
HUKU TUKIOGA MASHAMPENI
Aaaaaah YA rahaaa!!..!!.
Hali iko hivi nje ya dimba la Emirates nyumbani kwa washika bunduki Arsenal ambao leo majira ya usiku wataumana na Chelsea kiwanjani hapa, kocha Arsene Wenger akikitaka kikosi chake kupata ushindi ili kujiweka ktk nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu .
Hali ya hewa ya baridi kali inaendelea kuleta bugudha kubwa katika michezo nchini Uingereza, hasa wakati huu wa sikukuu.
Jana Michezo ya Ligi Kuu ya soka ya England kati ya Blackpool na Liverpool na kati ya Everton na Birmingham ilifutwa.
Ipswich ambao walikuwa wawakaribishe nyumbani Watford katika mechi za Championship jana, mchezo huo nao umeahirishwa, wakati mechi ya Ligi Kuu ya Scotland kati ya Kilmarnock na Dundee United nao umeahirishwa.
Michezo ya rugby, pambano baina ya Gloucester na Northampton limeahirishwa kutokana na baridi kali. Pia michezo mingine ya rugby ya ligi kuu kati ya Bath na Exeter ilifutwa na ule mpambano baina ya Newcastle dhidi ya Leeds umesogezwa mbele, badala ya kufanyika Jumapili jana, sasa utachezwa leo Jumatatu.
Katika soka tena, michezo ya Championship ya Crystal Palace, Derby, Ipswich, Scunthorpe na Middlesbrough pia ilifutwa; michezo 22 ya Ligi daraja la kwanza na la pili pia iliahirishwa. Mechi ya ligi daraja la kwanza pekee iliyochezwa jana ni kati ya Huddersfield na Hartlepool, wakati ya ligi daraja la pili, kati ya Wycombe na Hereford ulinusurika kutochezwa na hatimaye ukachezwa kama ulivyopangwa.
Monday, December 27, 2010
BANGO
Mshindi wa Giraffe Unique Model, Asia Dachi (katikati) akiwa na furaha mara baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo (unique model of the year 2010). Kulia ni mshindi wa pili, Diana Mainanson na mshindi wa tatu Mariam Rabii. Shindano hilo lilidhaminiwa na Giraffe ocean view hotel, Channel ten, Magic fm, Global pubishers, Mohammed enterprises, Truworths, mtaakwamtaablog na uniqueentertz blog.
“Nawashukuru wote, vyombo vya habari, wadau na kila mmoja kwa ushirikiano mzuri na sapoti kubwa mliyonipa, Bwana CHARLES BEKON kwa UDHAMINI NA HATIMAYE NIMEFANIKIWA KUFIKISHA JAHAZI UKINGONI, kisha kufanikiwa zoezi la kuwatangaza wanamitindo kumi katika soko la mitindo Tanzania. Hakika ni fahari kubwa.” By Magese.