ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 30, 2010

POLISI MWANZA WAINUSURU BENKI YA BOA NA UVAMIZI. WANASA MMOJA BAADA YA MWINGINE.

Jeshi la polisi mkoani Mwanza linafanikiwa kuwanasa watu wanne waliokuwa katika mpango wakufanya uvamizi katika benki ya BOA iliyopo mtaa wa Kaluta jijini hapa.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mwanza Simon Sirro amesema kuwa mara baada ya jeshi lake kupata taarifa kutoka kwa wasiri wake kuwa kuna watu wamejipanga kuvamia benki hiyo, waliweka mtego na hatimaye kufanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Donard Charles (28) mfanyakazi wa zamani wa benki hiyo aliyetimuliwa kazi.

Baada ya kuhojiwa na maafisa wa polisi, Charles alikiri kuhusika na mpango huo wa uvamizi na kusema kuwa kabla ya kukamatwa, yeye pamoja na wenzake wengine watatu walipanga uvamizi huo ufanyike mnamo tarehe 21 disemba 2010.

Ndani ya maelezo yake mtuhumiwa huyo amesimulia kuwa mara baada ya kufukuzwa kazi alifanya mpango wa kutafuta watu wengine watatu ili apate kushirikiana nao katika mpango huo haramu ambao nao tayari wamekwisha kamatwa.

Kamanda amewataja watu hao wanaoshikiliwa kuwa ni Henry Juma Salehe (32) ambaye ni shoe shine jijini Mwanza, Emanuel Masamilo (27) anayejihusisha na udalali pamoja na Wachu Kaloboka mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga ambaye ndiye mwenye siraha ambayo ilikuwa itumike kutekeleza uvamizi huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.