ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 25, 2012

TAARIFA KUHUSU DAWA BANDIA YA MALARIA

TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KUHUSU UWEPO WA DAWA BANDIA YA KUTIBU UGONJWA WA MALARIA IITWAYO ELOQUINE (Quinine Sulphate 300mg USP)

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni wakala wa Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti ubora, ufanisi na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii.

TFDA inapenda kuutaarifu umma kuwa imebaini kuwepo kwa dawa bandia ya kutibu ugonjwa wa Malaria katika soko. Dawa hiyo inaitwa Eloquine (Quinine Sulphate 300mg U.S.P) na ipo katika makopo ya vidonge 1000 (elfu moja) kila moja. Maelezo yaliyopo katika lebo yanaonesha kuwa dawa hiyo imetengenezwa na kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd cha nchini Kenya.

Hata hivyo, TFDA imebaini kuwa kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd hakitengenezi dawa yenye jina la biashara la ‘ELOQUINE’. Kiwanda hicho kimesajili Tanzania Quinine Sulphate 300mg B.P isiyo na jina la kibiashara. Aidha, kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd kimebainisha tofauti mbalimbali zilizopo katika lebo ya dawa bandia ikilinganishwa na dawa halisi inayotengenezwa na kiwanda hicho iliyosajiliwa na TFDA na hivyo kuthibitisha kuwa kiwanda hicho hakitengenezi dawa hiyo.

Katika kudhibiti usambazaji wa dawa hiyo hapa nchini, hadi sasa TFDA imekamata jumla ya makopo 155 ya dawa hiyo bandia ya Eloquine jijini Dar Es Salaam yaliyokuwa yakisubiri kusambazwa. Aidha, kopo moja lenye vidonge 115 limekamatwa Moshi, Kilimanjaro. Tayari mtuhumiwa mmoja amekwishafikishwa mahakamani na upelelezi wa chanzo na wasambazaji wa dawa hii unaendelea kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Uchunguzi wa dawa bandia katika maabara umebaini kuwa vidonge hivyo havina kiambato hai (active ingredient) cha Quinine Sulphate kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Malaria na hivyo matumizi yake ni hatari kwa afya ya binadamu.


Wafanyabiashara wote wa dawa na wananchi wanatahadharishwa kutozitumia dawa hizi na wale wote waliouziwa dawa hizi wanaelekezwa kuzirudisha dawa hizo katika ofisi za TFDA, vituo vya afya vya Serikali au vituo vya polisi vilivyo jirani nao.

TFDA inapenda pia kuwakumbusha wafanyabiashara wa dawa, wasafirishaji wa vifurushi na wananchi kutoa taarifa haraka iwezekanavyo pale wanapohisi kuuziwa dawa duni, bandia au zilizoisha muda wa matumizi. Taarifa zitolewe ofisi za TFDA makao makuu zilizopo Barabara ya Mandela, EPI Mabibo External, Dar es Salaam na Ofisi za Kanda zilizopo mtaa wa Nkurumah, Mwanza, Mtaa wa Sakina – Arusha, Hosptali ya mkoa ya Dodoma na Jengo la Ofisi ya Mifugo Mkoa wa Mbeya.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:-
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
EPI MABIBO EXTERNAL,
S.L.P 77150, DAR ES SALAAM

Simu: + 255 222 450512/450751/452108
Nukushi: + 255 222 450793
Barua pepe: info@tfda.or.tz
Tovuti: www.tfda.or.tz

MAMA ASIA IDAROUS KHAMSIN ASHEREKEA KUFIKISHA MAONYESHO 100

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Mama wa Mtindo Asia Idarous Khamsin akimkabidhi cheti cha shukrani kwa Gadner Habash ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa Nyumbani Lounge katika sherehe ya kusherehekea kutimiza maonyesho 100 iliyofanyika mgahawa wa Nyumbani Lounge jijini Dar es salaam.

Keki ya kutimiza shows 100 za Mitindo.

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Mama wa Mtindo Asia Idarous Khamsin akimkabidhi cheti cha shukrani kwa Victor Chashmir katika sherehe ya kusherehekea kutimiza maonyesho 100 iliyofanyika mgahawa wa Nyumbani Lounge jijini Dar es salaam.

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Mama wa Mtindo Asia Idarous Khamsin akimkabidhi cheti cha shukrani kwa mwandishi wa gazeti la Dimba, Jonathan Tito katika sherehe ya kusherehekea kutimiza maonyesho 100 iliyofanyika mgahawa wa Nyumbani Lounge jijini Dar es salaam.

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Mama wa Mtindo Asia Idarous Khamsin akimkabidhi cheti cha shukrani kwa Belina Mgeni katika sherehe ya kusherehekea kutimiza maonyesho 100 iliyofanyika mgahawa wa Nyumbani Lounge jijini Dar es salaam.

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Mama wa Mtindo Asia Idarous Khamsin akimkabidhi cheti cha shukrani kwa Hamoup Lukelezi katika sherehe ya kusherehekea kutimiza maonyesho 100 iliyofanyika mgahawa wa Nyumbani Lounge jijini Dar es salaam.

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Mama wa Mtindo Asia Idarous Khamsin akimkabidhi cheti cha shukrani kwa mbunifu wa mavazi Falha Sultan katika sherehe ya kusherehekea kutimiza maonyesho 100 iliyofanyika mgahawa wa Nyumbani Lounge jijini Dar es salaam.

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Mama wa Mtindo Asia Idarous Khamsin akimkabidhi cheti cha shukrani kwa mbunifu wa mavazi katika sherehe ya kusherehekea kutimiza maonyesho 100 iliyofanyika mgahawa wa Nyumbani Lounge jijini Dar es salaam.

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Mama wa Mtindo Asia Idarous Khamsin akimkabidhi cheti cha shukrani kwa mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Kajuna katika sherehe ya kusherehekea kutimiza maonyesho 100 iliyofanyika mgahawa wa Nyumbani Lounge jijini Dar es salaam.

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Mama wa Mtindo Asia Idarous Khamsin akiwa katika picha ya pamoja na wabunifu wa mitindo pamoja na wanamitindo mara baada ya kumaliza kugawa vyeti katika sherehe ya kusherehekea kutimiza maonyesho 100 iliyofanyika mgahawa wa Nyumbani Lounge jijini Dar es salaam.

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Mama wa Mtindo Asia Idarous Khamsin akikata keki katika sherehe ya kusherehekea kutimiza maonyesho 100 iliyofanyika mgahawa wa Nyumbani Lounge jijini Dar es salaam. Wanaoshangilia ni wabunifu wa mavazi wenzake.

Friday, February 24, 2012

LAKAIRO HOTEL YAADHIMISHA MIAKA 10 KWA JAMII YATOA MISAADA VITUO VYA WATOTO YATIMA MWANZA

Mwenyekiti wa Makampuni ya Lakairo Investiment Mh. Lameck Airo ambaye ni mbunge wa Rolya akikabidhi msaada wa mchele, mafuta, sukari na mashuka kwa mwakilishi wa kituo cha watoto yatima cha Hisani toka wilaya ya Ilemela, Frednand Fredrick.

Mwenyekiti wa Makampuni ya Lakairo Investiment Mh. Lameck Airo ambaye ni mbunge wa Rolya akikabidhi msaada wa mchele, mafuta, sukari na mashuka kwa mwakilishi wa kituo cha watoto yatima cha Fonelisco toka wilaya ya Ilemela, John Makoye.

Hawa ndiyo wafanyakazi wa Lakairo Hotel ambao kwa siku ya leo wanasherehekea maadhimisho ya miaka 10 katika huduma ya hotelia.

Uongozi wa Lakairo Hotel marafiki na wafanyakazi.

Maandamano yalianzia Hotelini kupita barabara mbalimbali jijini Mwanza kufanya usafi.

"Hivyo basi sisi kama Lakairo Hotel katika miaka 10 tunayofuraha kufurahia ukuaji wetu uonaoendana na utoaji huduma bora jijini Mwanza."

Maandamano ya maadhimisho yakipita barabara ya Makongoro kushoto bro Six na Janet wa Airtel pale kati...

Dah wadau walipendeza ile kisawasawa...

Katikati ya jiji wakichaniza....

Katika kusherehekea miaka 10 ya utoaji huduma bora kama taasisi Lakairo Hotel imeamua kurejesha japo sehemu ya faida yake kwa kushiriki maandamano ya shughuli za usafi wa jiji kama ilivyo kwamba ni jukumu la kila mmoja vilevile kusaidia watoto yatima na waishio katika mazingira magumu.

Kila mdau alichukuwa mtoto mmoja na kukaa nae, kuzungumza nae kwa karibu almuradi kumpa malezi ya karibu kama mzazi.

"Si unaona picha tuliyopiga sasa naiweka kwenye face book"

Ni mmoja tu aliyestukia flash hii Dj Paty left.

Kisha muzikiiii....

Ulipigwa mpambano wa kudance kati ya watoto waishio mazingira magumu na wafanyakazi wa Lakairo Hotel viduku vilifumukajeee....

Mama mwenyekiti akiwa katika tabasamu na mtoto wake wa sherehe.

Kulia ni meneja Lakairo Hotel na kulia ni mkurugenzi Dany Lameck wakiwa na watoto wa sherehe, hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa watoto hawa yatima.

Picha ya pamoja kila mdau na mtoto wake wa sherehe aliye mchaguwa.

Kisha chakula kizuri meza kwa kila mmoja...

Nilisahau kukwambia washindi katika kudansi mangoma walikuwa watoto yatima ambao waliifunika ile mbaya timu ya wafanyakazi Lakairo Hotel.

Thursday, February 23, 2012

MASAMAKI AONGOZA KURA ZA MAONI KIRUMBA.

Mchakato wa kura za maoni katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kumpata mgombea Udiwani wa Kata ya Kirumba wilayani Ilemela jijini Mwanza, umemalizika na Jackson Robert kuibuka kidedea.

Jackson ambaye ni maarufu kwa jina la Jack Masamaki, amepata ushindi wa kishindo baada ya kuzoa kura 528 na kuwabawa wagombea wenzake wanane akiwemo aliyewahi kuwa Diwani wa Kata hiyo Richard Rukambura aliyeambulia kura 191 na kushika nafasi ya pili.

Nurdin Mbaji aliyekuwa mgombea wa Chama katika uchaguzi Mkuu uliopita na kuangushwa na Novatus Manoko wa Chadema aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo kabla ya kifo chake, amepata kura 12 tu.

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa wilaya ya Ilemela Shahibu Akwilombe, zoezi la kupiga kura lilifanyika jana katika matawi yote ya Chama wilayani humo ambapo matokeo ya wagombea na kura zao kwenye mabano ni Hamidu Amir (153) na Frednand Tungu (70) Wengine ni Modestus Masige (55), Ally Mbaraka (48), Neema Mkindigire (33) na Nuru Ramadhani aliyeambulia kura mbili tu.

Akwilombe amesema kuwa, hatua inayofuatia sasa vikao vya Chama vya ngazi za Kata na wilaya ambavyo vitatoa mapendekezo kabla ya vikao vya mkoa vitakavyofanyika kati ya Februari 25 na 29 kupitisha mgombea wa Chama hicho.

Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Kirumba utafanyika Mei Mosi sambamba na Uchaguzi wa jimbo la Arumeru Mashariki, kufuatia kufariki dunia kwa Manoko aliyekuwa Diwani wa kata hiyo, Agosti 31 mwaka jana.

ALIYEKUWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA BLANDINA NYONI AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

Pichani kushoto ni marehemu bibi Ester Nyimbo Badi.
Kupitia matangazo ya vifo ya moja ya vituo hapa nchini taarifa zimesikika kuwa aliyekuwa katibu mkuu wizara ya afya Blandina Nyoni amefiwa na mama yake mzazi .

Sababu ya kifo cha mama huyo ni matatizo ya msukumo wa damu BP 'blood pressure'.

Blandina Nyoni pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Deo Mtasiwa hivi karibuni walisimamishwa kazi na Waziri Mkuu, Mh.Mizengo Pinda kutokana na kuonekana kuwa wao ndio kiini cha mgogoro wa madaktari ulioibuka na kumalizika hivi karibuni ambao ulisababisha matatizo makubwa kwa Taifa na kuigharimu nchi.

RIP BIBI.

MABADIRIKO YA RATIBA MSOND NGOMA KUTUMBUIZA MAX BAR ILALA JUMAPILI HII.....!!

BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya muziki’, inawaomba radhi mashabiki wao wa DDC Kariakoo kwa kuwakosa kwa wiki moja kwani kwa sasa wanapiga shoo Ya Jumapili hii watakua katika ukumbi wa Max Bar ya Ilala Bungoni Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila ‘Super D‘, alisema kuwa hawakupanga kuondoka Kariakoo lakini kutokana na muingiliano wa ratiba hawana budi kufanya hivyo ingawa wanaamini wiki zijazo mambo yatakuwa mazuri.

Alisema hata hivyo bado wanahitaji kuwa karibu na mashabiki wao kwani uwepo wao ndiyo kazi yao ya kuimba inakuwa inakamilika. “Wiki hii hatutapiga shoo hapa Kariakoo, na tutakuwa Max bar Ilala na hii imetokana na ratiba fulani ambayo tulipewa lakini naamini wiki ijayo kila kitu kitakuwa sawa, hivyo mashabiki wetu tunaomba radhi kwa usumbufu huo,” alisema Super D.

Wednesday, February 22, 2012

BABU WA LOLIONDO BADO ANA MVUTO, AHAMIA ROCK CITY?

Ngoma inapatikana Mwaloni Mwanza.

Kamera yako ilipomfuma Mzee mzima akikatisha katikati ya jiji la miamba toka kituo cha basi akitokea porini kuchimba dawa sijui unaitwa 'm-arovera' i think so...

VITU ADIMU SOKO LA SAMAKI MWALONI KIRUMBA

UTALII TANZANIA SI MBUGA ZA WANYAMA TU..Samaki aina ya Sangara tayari kwa kukatwakatwa vipande soko la kimataifa Mwaloni kirumba jijini Mwanza.

Wafanyabiashara wakipanga vichwa vya samaki vilivyokaushwa almaarufu 'Mapanki' kwaajili ya kufungwa marobota kwa biashara nchi za afrika mashariki na kati.

Mapanki katika mpangilio madhubuti....

Kayabo ni samaki aina ya sangara aliyesindikwa kwa chumvi nyingi maarufu sana na soko kubwa liko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako ni chakula kinacholiwa na matajiri.

Kayabo uhamishaji toka sehemu moja hadi kwenye madaraja ya viwango.

Wafanyabiashara wakichambua makayabo yaliyokauka yenye ubora yanayopaswa kuingia kwenye hatua ta uwekwaji kwenye marobota njiani kwenda sokoni.

Mwananchi akigeuza vipande vya samaki vilivyokatwa almaarufu kama 'chips' kwaajili ya kukauka vizuri juani.

Maranyingi samaki wanaosafirishwa kwa soko la nje ni minofu tu iliyokatwa kiufundi ambayo huifadhiwa kwenye makasha maalum yenye barafu, vichwa, mifupa, mikia na mabaki mengine toka viwandani hukusanywa kwaajili ya kukaushwa kama hivi kwa chakula cha walaji wengine na masalia mengine yasiyohitajika hufanywa chakula kwa kuku.

Uanikaji soko la Mwaloni Kirumba Mwanza Tanzania.

Mabaki haya ya mifupa ya samaki anikoni kwaajili ya kuchanganywa na dagaa kisha husagwa kutengenezwa kama sehemu ya chakula cha kuku.

Oda maalum ya Mwanamuziki maarufu Kongo mkongwe mwenye bahati ya kupata mialiko mingi nchini...

Wanajulikana sana kwa jina la Ndege Mwarabu wakiranda kwa makundi katika meza zilizowazi za kuanikia samaki wa biashara sokoni Mwaloni Kirumba jijini Mwanza hakika ni utalii tosha.

Tuesday, February 21, 2012

ZIJUE SABABU 11 ZINAZOWAFANYA MABINTI WENGI WA SASA KUTOOLEWA, KAMA UNAZAKO ONGEZA..

1. The nice men are ugly.

2. The handsome men are not nice.

3. The handsome and nice men are Gay.

4. The handsome, nice and heterosexual men are married.

5. The men who are not so handsome, but are nice men,
have no money.

6. The men who are not so handsome, but are nice men
with money think ladies are only after their money.

7. The handsome men without money are after ladies money.

8. The handsome men, who are not so nice and somewhat
heterosexual, don't think ladies are beautiful enough.

9. The men who think ladies are beautiful, that are
heterosexual, somewhat nice and have money, are cowards.


10. The men who are somewhat handsome, somewhat nice
and have some money and thank God are heterosexual,
are shy and NEVER MAKE THE FIRST MOVE to ladies!!!!

11. The men who never make the first move, automatically
lose interest in us when we take the initiative.

NOW WHO THE HELL UNDERSTAND MAN?

" Men are like a fine wine. They all start out like grapes, and it's the ladies job to stomp on them and keep them in the dark until they mature into something you'd like to have dinner with."

PSPF YATOA MSAADA WA MATAWATI SHULE YA MSINGI BWILINGU CHALINZE MKOA WA PWANI

Kaimu MKurugenzi Ukaguzi wa Ndani wa Mfuko wa Pesheni wa Utumishi wa Umma PSPF. Bw. Godfrey Ngonyani (kushoto) akikabidhi msaada wa Madawati 60 yenye thamani ya milioni tatu walioutoa leo kwa Mjumbe wa Kamati ya Shule Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani, Bi. Jacklin Kitego kulia na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi. Anifa Kombo.

Kaimu MKurugenzi Ukaguzi wa Ndani wa Mfuko wa Pesheni wa Utumishi wa Umma PSPF. Bw. Godfrey Ngonyani (kulia) akizungumza na Wazazi na Wanafunzi pamoja na Bodi ya Shule ya Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani wakati walipokwenda kukabidhi msaada wa Madawati 60 yenye thamani ya milioni tatu kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Bi. Anifa Kombo na Mjumbe wa Bodi ya PSPF Bw. Ramadhani Maneno.

Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani wakigombania kukaa kwenye madawati mapya walioletewa na Mfuko wa Pesheni wa Utumishi wa Umma PSPF.
Haya tumalize utata...
(Picha na Mpigapicha Wetu)