ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 23, 2012

MASAMAKI AONGOZA KURA ZA MAONI KIRUMBA.

Mchakato wa kura za maoni katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kumpata mgombea Udiwani wa Kata ya Kirumba wilayani Ilemela jijini Mwanza, umemalizika na Jackson Robert kuibuka kidedea.

Jackson ambaye ni maarufu kwa jina la Jack Masamaki, amepata ushindi wa kishindo baada ya kuzoa kura 528 na kuwabawa wagombea wenzake wanane akiwemo aliyewahi kuwa Diwani wa Kata hiyo Richard Rukambura aliyeambulia kura 191 na kushika nafasi ya pili.

Nurdin Mbaji aliyekuwa mgombea wa Chama katika uchaguzi Mkuu uliopita na kuangushwa na Novatus Manoko wa Chadema aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo kabla ya kifo chake, amepata kura 12 tu.

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa wilaya ya Ilemela Shahibu Akwilombe, zoezi la kupiga kura lilifanyika jana katika matawi yote ya Chama wilayani humo ambapo matokeo ya wagombea na kura zao kwenye mabano ni Hamidu Amir (153) na Frednand Tungu (70) Wengine ni Modestus Masige (55), Ally Mbaraka (48), Neema Mkindigire (33) na Nuru Ramadhani aliyeambulia kura mbili tu.

Akwilombe amesema kuwa, hatua inayofuatia sasa vikao vya Chama vya ngazi za Kata na wilaya ambavyo vitatoa mapendekezo kabla ya vikao vya mkoa vitakavyofanyika kati ya Februari 25 na 29 kupitisha mgombea wa Chama hicho.

Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Kirumba utafanyika Mei Mosi sambamba na Uchaguzi wa jimbo la Arumeru Mashariki, kufuatia kufariki dunia kwa Manoko aliyekuwa Diwani wa kata hiyo, Agosti 31 mwaka jana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.