ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 29, 2019

MAN Utd YATHIBITISHA KUMSAJILI MLINZI WA Crystal Palace



Manchester United wamemsajiili beki wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka kwa mkataba wa pauni milioni 50.
Kiungo huyo wa miaka 21 amekubali kutia saini mkataba wa miaka mitano utakaomwezesha kulipwa hadi pauni 80,000 kwa wiki.
United tayari imelipa £45m kumnunua Wan-Bissaka amabye anatajwa kuwa mchezaji wa tano mkubwa kusainiw ana klabu hiyo baada yaPaul Pogba, Romelu Lukaku, Angel di Maria na Fred.
"Siamini nimejiunga na Ma Utd kwa kweli najivunia sana usajili huu," Wan-Bissaka alisema.
Manchester United imethibitisha usajili wake leo Jumamosi.
Kocha wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer amesema Wan-Bissaka ni "mmoja wa walinzi wakuu wanaoibuka katika ligi ya Premia".
Aliongeza kuwa: "Ana eshiku kazi yake, ana talanta kubwa inayomwezesha kuchezea Manchester United na ana vigezo vyote vya mchezaji tunayemtaka ajiunge na kikosi chetu na bila shaka atatusaidia kufikia malengo."
Mlinzi huyo ni ni wa pili kusajiliwa na klabu hiyo, baada ya usajili wa kiungo wa kimataifa wa Wales Daniel James, 21, ambao alijiunga na United kutoka Swansea kwa £15m.
United wana nafasi ya kurefusha mkataba wa miaka mitano wa Wan-Bissaka hadi miaka sita.

NGUMI KUPIGWA JULAI 7 CHANIKA MAGENGE MBEGU AHAIDI MAMBO MAKUBWA

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza bondia Ramadhani Mbegu 'Migwede' kupiga ngumi ya Mkunjo wa chini Upcut  wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Super D Coach shule ya Uhuru kariakoo Dar es salaam jana Mbegu anajiandaa na mpambano wake wa julai 7 utakaofanyika katika ukumbi wa manka pub Chanika Magenge


Na Mwandishi Wetu
Baada ya tamba mbalimbali za hapa na pale sasa mabondia Hussein Alli 'Gobosi' na Ramadhani Mbegu' Migwede' watazipiga julai 7 katika ukumbi wa Manka Pub Chanika Magenge mpambano wa raundi 8

Migwede amea wa ahidi mashabiki zake kuja kwa wingi kwani anacheza katika uwanja wa nyumbani na ato waangusha mashabiki zake ujue nimekuwa nikikimbiwa na mabondia mbalimbali hivyo bondia yoyote anaekuja katika anga zangu nakanyaga tu anakuwa kama ngazi

Mpambano uho ulio andaliwa na Rajabu Mhamila 'Super D' kupitia kampuni ya Super D boxing Promotion amesema kuwa pambano hili ndio litakalo amua nani zaidi bada ya mabondia hawo kuwa na viwango sawa kwa sawa  Ambapo katika viwango vya ubora nchini Tanzania Mbegu yeye ni nambari 10 wakati Hussein Ally yeye ni namba 14 katika ubora

Super D aliongeza kwa kusema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ambapo Hamidu Kwata atazipiga na Luckman Ramadhani na Salum Mandai 'Pacho' atazidunda na Waziri Rosta wakati Juma Zingiziwa ataoneshana umwamba na Alex Kachelewa juma Malenda atavaana na Ibrahimu Makubi na Hussein Shemdoe atazipiga na Juma Kadoda wakati Said Mbelwa atazidunda na Shabni Kaoneka na mapambano mengine mbalimbali ya vijana chipkizi

Super D aliendelea kwa kuseka kuwa siku hiyo ngumi zitaanza mapema sana kutokana na kuwa na mapambano mengi na makali hivyo kuwataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuwai kufika ukumbini ili ngumi zianze kwa wakati

usalamab wa mali zao ni wakutosha kabisa kwani mashabiki wanatakiwa waje na familia zao wapate burudani ya mchezo wa masumbwi

TACAIDS - "MSIDANGANYIKE, HAKUNA MBADALA WA ARV"

Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) imewataka watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutodanganyika na kuacha kutumia dawa kupunguza makali ya VVU kwani hakuna mbadala wa ARV.

DAR KUCHEZA NA MWANZA ROBO FAINALI SOKA WASICHANA UMITASHUMTA



Na Mathew Kwembe, Mtwara

Timu za soka za wasichana za mikoa ya Dar es salaam na Mwanza zimetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya UMITASHUMTA na zinatarajiwa kucheza leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.

Dar es salaam imefikia hatua hiyo baada ya kuibuka kinara katika kundi A na hivyo itachuana na mshindi wa pili kundi C Mwanza katika hatua ya robo fainali. Pambano lingine la robo fainali litazikutanisha timu za mikoa ya Manyara ambao iliibuka mshindi wa kwanza kutoka kundi B watakaochuana na mshindi wa pili kundi D timu ya soka ya wasichana kutoka mkoa wa Mara.

Mshindi wa kwanza kutoka kundi C, timu ya soka wasichana kutoka mkoa wa Kagera imepangwa kuchuana na mshindi wa pili kundi B, Simiyu huku mshindi wa kwanza kundi D Morogoro watachuana na mshindi wa pili kundi A, Kilimanjaro.

Kwa upande wa soka maalum wavulana, michuano hiyo pia imefikia hatua ya robo fainali na inatarajiwa kuchezwa leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara ambapo mshindi wa kwanza kundi A Kilimanjaro atachuana na mshindi wa pili kundi C Dodoma. Mshindi wa kwanza kundi B Tabora atachuana na mshindi wa pili kundi D Ruvuma. Mchuano mwingine mkali utahusisha mshindi wa kwanza kundi C, Mtwara atachuana na mshindi wa pili kundi B, Kagera huku mshindi wa kwanza kundi D, Dar es salaam atachuana na mshindi wa pili kundi A, timu ya soka maalum wavulana kutoka mkoa wa Shinyanga.

Kwa upande wa soka wavulana, michuano hiyo bado inaendelea katika hatua ya makundi na inatarajiwa kuchezwa hatua ya robo fainali tarehe 1, julai, 2019 ambapo mshindi wa kwanza kundi A atacheza na mshindi wa pili kundi C, mshindi wa kwanza kundi B atachuana na mshindi wa pili kundi D, mshindi wa kwanza kundi C atacheza na mshindi wa pili kundi B na mshindi wa kwanza kundi D atachuana na mshindi wa pili kundi A.

Matokeo ya michezo iliyochezwa kundi A kuanzia tarehe 24 juni hadi tarehe 28 juni, 2019 katika soka wavulana inaonyesha kuwa Tanga imeifunga Singida 4-0, Dodoma wameichapa Mara 2-1, Dar es salam imetoka sare na Kilimanjaro 1-1, Singida imetoka suluhu na Kilimanjaro 0-0, Mara imefungwa na Dar es salaam 0-1, Tanga imeifunga Dodoma 2-1, na Dodoma imefungwa pia na Dar es salaam 2-3.

Kilimanjaro  iliifunga Tanga 1-0, Singida iliichapa Mara 2-0, Dodoma nayo iliifunga singida 2-1, Mara ikaichapa Kilimanjaro 2-1, Dar es salaam ikatoka suluhu na Tanga, Tanga ikaifunga Mara 3-0, Singida ikachapwa na Dar es salaam 0-3 na Kilimanjaro pia ikachapwa na Dodoma 0-3.

Matokeo ya kundi B soka wavulana, Mbeya ilichabangwa na mwanza 2-5, Pwani iliibugiza Iringa 4-0, Lindi nayo ikaichapa Mtwara 2-0, Mwanza ikaifunga Pwani 3-0, Simiyu ikaifunga Iringa 2-0, na Mbeya ikaichapa Mtwara 1-0, Lindi ikatoka suluhu na Simiyu, Mtwara ikafungwa na pwani 0-3, Iringa nayo ikabugizwa na Mwanza 1-5 na Mbeya ilipata kipigo kutoka Simiyu 0-1, Mwanza imeichapa Mtwara 4-0, Pwani ikatoka sare na Lindi 1-1, Iringa ikapata kipigo kutoka Mbeya 0-4, Mtwara nayo ikafungwa na Simiyu 1-3 na Mwanza ikatoka sare na Lindi 1-1.

Matokeo ya michezo ya kundi C yanaonyesha Geita iliichapa Kigoma 1-0, Manyara iliifunga Njombe 2-1, Shinyanga ilikubali kichapo kutoka kwa Ruvuma 0-2, Kigoma iliifunga Ruvuma 1-0, na Njombe ikaifunga Shinyanga 4-1. Pia Geita ikaifunga Manyara 2-0, Manyara ilikubali kipigo kutoka kwa Shinyanga 0-5, Ruvuma nayo ilifungwa na Geita 0-2, Kigoma ikaifunga Njombe 1-0, Manyara ikaichapa Kigoma 4-0, Njombe na Ruvuma zikatoka suluhu, Shinyanga ikafungwa na Geita 0-1, Geita ikaichapa Njombe 4-0, Kigoma ikatoka sare na Shinyanga 1-1 na Ruvuma ikakubali kichapo kutoka kwa Manyara 1-3.

Katika michezo iliyochezwa kundi D soka wavulana, matokeo yanaonyesha Katavi ilifungwa na Kagera 1-2, Morogoro ilichapwa na Tabora 1-2, Rukwa ikaifunga Songwe 3-1, Morogoro ikatoka sare na Rukwa 1-1, Kagera ikaichapa Arusha 3-0, huku Katavi na Tabora zikitoka suluhu ya bila kufungana. Matokeo mengine Songwe ilichapwa na Kagera 0-2, Tabora na Rukwa zikatoka suluhu, Arusha ikachapwa na Morogoro 1-3, Arusha pia ilibugizwa na Songwe 1-7, Katavi ilifungwa na Rukwa 0-1, Morogoro ilifungwa na kagera 1-2, Arusha ilifungwa na katavi 0-2, Tabora ilichapwa na Kagera 0-3 na Morogoro na Songwe zilitoka suluhu ya bila kufungana.

Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea leo na kesho ili kukamilisha ratiba kwa timu za soka wavulana kutoka makundi A hadi D kwa soka wavulana ili kukamilisha ratiba ya michuano hiyo kabla ya kuchezwa hatua ya robo fainali kesho kutwa katika viwanja hivyo hivyo vya chuo cha ualimu Mtwara.

 Lidya Daudi wa timu ya soka ya wasichana Geita (mwenye jezi ya bluu) akichuana vikali kugombea mpira na mchezaji Eneck Daud wa Mbeya (jezi nyeusi) wakati timu hizo zilipocheza hivi karibuni.

Mshambuliaji hatari wa timu ya soka wavulana ya mkoa wa Lindi Omari Mohamed akifunga goli la pili kwa njia ya penati dhidi ya timu ya Mtwara huku golikipa wa timu hiyo Benard William  akijaribu kuchupa bila mafanikio wakati timu hizo zilipokutana hivi karibuni. Lindi iliifunga Mtwara 2-0.

MSIDANGANYIKE, HAKUNA MBADALA WA ARV - TACAIDS


Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) imewataka watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutodanganyika na kuacha kutumia dawa kupunguza makali ya VVU kwani hakuna mbadala wa ARV.


Rai hiyo imetolewa  na Mkurugenzi wa Uraghbishi na Habari wa TACAIDS, Bw. Jumanne Issango wakati akifunga Kambi ya Ariel 2019 iliyoandaliwa na asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI).

Akizungumza kwenye kambi hiyo iliyojumuisha watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mwanza na Mara Bw. Issango alisema kuwa inasikitisha kuona kuwa watu wengine wanaacha kutumia ARV na kisha kujikita kwenye dawa za kienyeji au maombi. “Matokeo yake ni VVU kuendelea kuwashambulia. Kinachosaidia kupunguza makali ya VVU mwilini ni ARV peke yake, hakuna mbadala,” alisisitiza.

Mkurugenzi huyo alisema, “Msidanganyike mkaacha kutumia dawa za ARV, mpaka sasa bado wanasayansi hawajapata dawa nyingine. Tunaamini ipo siku dawa itapatikana lakini kwa sasa wenye maambukizi ya VVU endeleeni kuwa wafuasi wazuri wa dawa na mtumie kwa usahihi.”

Akizungumzia vita dhidi ya maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kazi ambayo asasi ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) imekuwa ikiifanya tangu kuanzishwa kwake, Mkurugenzi huyo alisema kuwa hicho ni kipaumbele cha taifa hivyo hakina budi kufanyiwa kazi kwa juhudi.

Alisema kwa watoto na vijana wenye maambukizi, wataendelea kupata huduma za matunzo na tiba bila ubaguzi wowote ili kuhakikisha kuwa afya zao zinaendelea vizuri hivyo kuweza kufikia ndoto zao za baadaye.

“Kwa kazi zenu, AGPAHI mnagusa maisha ya Watanzania wengi. Kitendo cha kusaidia upatikanaji wa huduma za matunzo na tiba kwa wanaoishi na VVU ni cha utu. AGPAHI ni asasi ya kiutu na inajali Watanzania. Tunawashukuru kwa kuendelea kushirikiana na serikali kutoa huduma hizi muhimu,” alisema.

Aidha alikumbusha kwamba kuwa na maambukizi ya VVU siyo changamoto ya kumzuia mtu anayeishi na VVU kusonga mbele katika maisha yake na kutimiza ndoto zake, “Kinachotakiwa ni kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya,” alisema.

Friday, June 28, 2019

ILEMELA KUPIMA BURE SARATANI SHINGO YA KIZAZI.


Kuanzia tarehe 01 July 2019 hadi 05 July zoezi kufanyika katika vituo vya Afya Buzuruga na Sangabuye Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.

BONDE LAGEUZWA KUWA PANGO LA WABAKAJI NA VITENDO VYA ULAWITI WANAFUNZI WILAYANI KASULU.


KATIKA harakati zake za kuikwamua jamii toka katika lindi la umasikini unaosababishwa na vitendo vya ukatili, Shirika la KIVULINI limeendesha mdahalo wa majadiliano kuhusu namna ya kuzuia, kupunguza na kuondosha kabisa vitendo vya ukatili wilayani Kasulu huku ikibaini mapungufu makubwa yanayo sababishwa na baadhi ya viongozi wenye dhamana nayo jamii ikilaumiwa kushindwa kusimamia vyema majukumu yake.

“mtoto wa mwaka mmoja alawitiwa”

 Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI jana Juni 25, 2019 limeendesha mdahalo wa wazi katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma, ukilenga kutoa elimu kwa jamii kupinga hadharani aina zote za ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake.
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia) akifurahia na kumtuza mmoja wa wasanii waliokuwa wakitumbuiza kwenye mdahalo huo.
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kupata elimu kwenye mdahalo huo.
 Ujumbe.
 Ujumbe 2.
 Burudani.
 Wanaharakati wakitanabaisha majukumu yao.
 Chapa Kazi sio mkeo.
Afisa wa Dawati la Jinsia la Polisi wilayani Kasulu, Maimuna Abdul akitoa akizungumzia matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.

MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA BOSI WA JUKWAA LA WABUNGE WA SADC.


Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Veronica Nataniel Macamo Dihova.
Mkutano huo uliofanyika leo Ijumaa Juni 28,2019 Ikulu jijini Dar es Salaam, Tanzania na kuhudhuriwa pia Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Damas Ndumbaro na Katibu wa Jukwaa la wabunge la SADC, Boemo Sekgoma.
Dihova ambaye pia ni Spika wa Bunge la Msumbiji amewasilisha salamu za Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi pamoja na salamu za maspika wa SADC.
Pia Dihova ameeleza kwa kina kuhusu ushiriki wa jukwaa hilo katika mkutano wa 39 wa SADC unaotarajiwa kufanyika Tanzania  Agosti mwaka 2019.
Mwenyekiti huyo ameeleza Msumbiji na nchi nyingine za Afrika zinatambua mchango uliotolewa na Tanzania katika ukombozi wa mataifa mengi ya Afrika na uanzishaji wa nchi za mstari wa mbele na SADC.
Kwa upande wake, Rais Magufuli amemhakikishia Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zote wanachama wa SADC ikiwemo Msumbiji ambayo ina uhusiano wa kihistoria na kidugu na Tanzania. #CHANZO MWANANCHI

TANESCO KANDA YA KASKAZINI YAWAKUTANISHA WATEJA WAKUBWA NA WAWEKEZAJI KUJADILI CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA.

 Picha ikionyesha meneja wa shirika Tanesco  kanda ya kaskazini  Stella Hiza akiongea katika mkutano wa wa shirika hilo na wateja wakubwa wa nishati ya Umeme kanda ya kaskazini 
 Picha ikionyesha mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifungua mkutano washirika hilo na wateja wakubwa wa nishati ya Umeme kanda ya kaskazini 
Picha ikionyesha mkuu wa mkoa wa Arusha,Meneja wa Tanesco kanda katika picha ya pamoja na wateja wakubwa wa Nishati ya Umeme

Na Woinde Shizza ,Arusha 

Shirika la umeme Tanesco kanda ya kaskazini leo limewakutanisha wamiliki wa viwanda ,wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa wa mikoa ya kanda hiyo ili kuweza kujadili changamoto mbalimbali ambazo wafanya biashara hao wanakumbana nazo katika utendaji wao wa kazi ili kuimarisha  sekta ya nishati na ukuzaji wa viwanda nchini.

Akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Arusha katika kituo cha mikutano cha AICC mkoani hapa  meneja wa shirika hilo kanda ya kaskazini  Stella Hiza alisema kuwa mkutano huo utatengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuweza kupata kuwa na umeme wa uhakika kwa kila kanda.

Amesema  shirika la umeme Tanesco kanda ya kaskazini limepeleka mradi wa umeme kwa baadhi ya maeneo jijini Arusha ambapo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni mbili 2.6 mpaka kukamilika kwakwe.
Kwa upande wao baadhi ya mameneja kutoka kanda ya kaskazini wamesema kuwa shirika la umeme Tanesco wanaimarisha miundo mbinu ili kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi na kuondoa  na kutatua changamoto zinazowakabili wateja wao.

"sisi kama shirika la tanesco tunawategemea sana wateja wetu wakubwa katika kukusanya mapato ya shirika  kwani zaidi ya asilimia 40% ya mapato yetu yanatoka kwa wawekezaji pamoja na wenye viwanda  na mapato haya yanatusaidia kuendesha huduma zetu pamoja na kukuza mapato ya nchi" Hiza 


Alisema kuwa  kwa upande wa Arusha wawekezaji wenye viwanda wapo 335 ambao ni sawa na asilimia 41%,Kilimanjaro ikiwa na wateja wakubwa 101 ambao wanachangia kwa asilimia 71% huku mkoa wa Tanga  117 ambao wanachangia kwa asilimia 64%.


Naye meneja wa Tanesco mkoa wa Kagera Fransis Martin aliwasihi wananchi ambao wanaiba umeme pamoja na wale wapoteza waache mara moja kwani kwakufanya hivyo wanapoteza mapato ya nchi

"katika jitiada za kupunguza wizi wa umeme tanesco imebadilisha teknolojia ya umeme katika hatua mbalimbali ikiwemo kubadilisha teknolojia   mita katika hatua mbalimbali yakwanza kuwabadilisha  wateja wa kawaida kutumia luku ,kutumia mita ambazo zinaakili yaani mita ambazo zinajitetea ambapo mtu akiigusa zinauwezo wa kutuma sms kwa watendaji wa shirika ili watendaji wafatilie"alisema Martin
Kwa upande wake mmoja wa wawekezaji kutoka SBC Peter Kalembo 
Aliipongeza sana Tanesco na kusema kuwa huduma inayotolewa na shirika hilo inakithi matarajia kwani changamoto ya umeme kukatika kwa sasa imepungua ,na hii imetokana na kutambua wajibu wao kwani kwa kipindi hichi huduma zao zinarizisha.

 Awali kulikuwa na shida kubwa kwa shirika hili kutoa huduma tarajio kwa wateja hivyo kufanya wawekezaji wengi kushindwa kuwekeza na wengine wakaona huduma ya umeme inawapa shida lakini kwa sasa wataweza kuwekeza maana tatizo hilo limeisha na katika  eneo la uwekezaji sera zinabadilika za kushawishi wawekezaji waweze kuja kuwekeza na kufanya biashara kwa pamoja .

Akifungua mkutano huo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema tangu kuanzishwa kwa nchi yetu shirika limeshazalisha mega wat 1500 na katika hilo hadi kufikia sasa megawat 1300ndio zinatumika tunauwiano wa zaidi wa megawat 200 ambazo azitumiki

Aidha aliwasihi Tanesco kutembelea maeneo ambayo yametegwa kwa ajili ya uwekezaji yaliopo katika cha Malula wilayani Arumeru ambapo kina ekari zaidi ya mia Tano nakuwekeza miundombinu ya umeme kwani  eneo hilo lina fursa mbalimbali za uwekezaji kwani katika eneo hilo kunatarajiwa kujegwa bandari kavu ya Tanga. 

Mkutano huo ambao umefunguliwa leo umeshirikisha mameneja  wa  Tanesco kanda ya kaskazini ,Wawekezaji,Wafanyabiashara wa Viwanda wakubwa ambao wametoka mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Tanga na Manyara.


MISA TANZANIA, ICNL WAJADILI NA WADAU CHANGAMOTO ZA KISHERIA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkurugenzi wa MISA Tanzania Gasirigwa Sengiyumva akichangia mada katika warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari. Geline Fuko (kushoto) akiwasilisha mada wakati wa siku ya pili ya warsha hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Network of Legal Aid Provider Christina Kamili (kulia) akiwasilisha mada wakati wa siku ya pili ya warsha hiyo. Na Mwandishi Wetu Katika kuendeleza hamasa na kutetea uhuru wa kujieleza katika jamii, MISA Tanzania na shirika la utetezi wa sheria na haki za kijamii la ICNL zimewakutanisha wadau mbali mbali katika warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari. Warsha hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya habari,asasi za utetezi wa haki za binadamu, wanasheria pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu. Warsha hiyo ya siku tatu iliyofanyika mjini Bagamoyo ambayo ni muendelezo wa warsha iliyofanyika mwezi Machi mwaka huu ililenga kuwakutanisha wadau hao kwa lengo la kujadili zaidi namna sheria za vyombo vya habari zinavyo athiri mazingira ya kazi za kiuandishi pamoja na uhuru wa kujieleza. Bw.Aloys Habimana kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL akiendesha warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari iliyoandaliwa na kuendeshwa na MISA kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL. Kadhalika akielezea umuhimu wa uwepo wa sheria rafiki katika kufanya mazingira yawe salama kwa tasnia ya habari,Bw.Aloys Habimana kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL lenye makao makuu yake nchini Marekani amesema changamoto ya sheria zisizo rafiki kwa taaluma ya habari na uhuru wa kujieleza ni changamoto sehemu nyingi duniani Afrika ikiwa na mifano halisi. "Pamoja na mazingira haya nawasihi msivunjike moyo wala kukata tamaa, masuala ya kisheria hayabadiliki kwa siku moja yanahitaji kupitia hatua kadhaa na kila jambo linaweza kupatiwa ufumbuzi hasa wadau wote watakaposhirikiana na kujenga hoja zenye ushawishi na tija kwa pande zote", alisisitiza Bw.Aloys. Bi.Lily Liu kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL akijadili jambo pamoja na wadau walioshiriki warsha hiyo. Sambamba na hilo Bi.Lily Liu mjumbe kutoka ICNL aliahidi kuwa shirika lao litaendelea kushirikiana na wadau husika katika nyanja zote ili kufanikisha na kutimiza adhma ya kuwa na jamii isiyo na sheria kandamizi zinazoathiri dhana nzima ya uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari. Warsha hiyo iliyojikita zaidi katika mfumo wa washiriki kubadilishana mawazo na uzoefu wao wa mazingira ya kazi pamoja na namna hali inavyobadilika na kubanwa kwa uwepo wa sheria zisizojitosheleza. Washiriki warsha hiyo wakijadili baadhi ya sheria na kanuni katika makundi. Mkurugenzi wa Highlands Fm Radio ya Mbeya Bi. Jacqueline Lawrence akiwasilisha mada kwa niaba ya washiriki wenzake Washiriki wa warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari iliyoandaliwa na kuendeshwa na MISA kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungwa kwa warsha hiyo.

Wednesday, June 26, 2019

"KWIMBA TATIZO LENU NI NINI?"



Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella mwishoni mwa wiki amezungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kwimba na kubaini mengi madhaifu ambayo licha ya kwamba kila kuchwao afanyapo ziara wilayani humo amekuwa akikumbana nayo lakini mapungufu hayo yamekuwa yakijirudia, huku tatizo moja likizaa tatizo jingine jipya.

Kutokana na usugu huo amewataka wajiulize swali  'KWIMBA TATIZO LETU NINI' 








VIDEO: SERIKALI YATOA MSIMAMO KAULI YA MBUNGE WA KENYA


Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesimama Bungeni na kutoa msimamo wa serikali juu ya kauli iliyotolewa na Mbunge wa Starehe, Jaguar, ya kuwataka watanzania wanaofanya biashara nchini Kenya, kuondoka haraka la sivyo watawapiga mawe.

YANGA, AZAM FC NI UBABE TU...

Azam FC imesisitiza kwamba, kipa anayetajwa kumalizana na Yanga, Metacha Mnata, ataitumikia Azam FC msimu ujao na wala haendi sehemu nyingine.

Kauli ya Azam FC imekuja huku kukiwa na taarifa za Yanga kumalizana na kipa huyo ambaye yupo Misri na timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwenye michuano ya Afcon.

Metacha ambaye alikuwa kwa mkopo Mbao FC akitokea Azam FC, hivi sasa ni mchezaji huru kutokana na kumaliza mkataba ndani ya Azam FC.

Mtu wa kuaminika kutoka katika ofisi ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, ameliambia Championi kuwa kipa huyo hajasaini kwa mabingwa wa kihistoria Yanga na badala yake ataongeza mkataba wa kuendelea kuwatumika matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam.

“Siyo kweli kuwa Metacha amesaini Yanga, yupo kwenye mipango ya mwalimu na msimu ujao ataendelea kucheza Azam FC kwani ishu ya kumuongezea mkataba mpya tayari imeshafanyika kilichobaki ni kusaini tu,” alisema mtoa taarifa huyo.

SHAMRASHAMRA ZA BULABO 2019 MWENDELEZO WA HIFADHI YA UTALII TAMADUNI ZA WASUKUMA



 BULABO hufanyika kila mwaka mwezi wa sita kusherekea mavuno, tamasha hili limekuwa maarufu sana nchini Tanzania kutokana na matumizi ya kuenzi mila na tamaduni za watu wa kabila la Wasukuma chatu na fisi (zamani) katika ngoma jambo ambalo huwaduwaza wengi.

Ni wiki moja ya sherehe hizo imeanza ikiwa ni tangu mwishoni mwa wiki siku ya Jumapili na yakitaraji kuhitimishwa Jumapili ya tarehe 30 Juni 2019 ambapo huu ndiyo muonekano wake.








Tuesday, June 25, 2019

WANANCHI MANISPAA YA IRINGA WAKUNWA NA UTENDAJI KAZI WA MADIWANI WA CCM


 Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Joseph Lyata ambae ni Diwani wa kata ya Kwakilosa akiwa pamoja na mwenyekiti wa umoja wa vijana manispaa ya Iringa Salvatory Ngerea,diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula pamoja na baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mkimbizi A wakiwa kwenye picha ya pamoja
 Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Joseph Lyata ambae ni Diwani wa kata ya Kwakilosa akiwa pamoja na mwenyekiti wa umoja wa vijana manispaa ya Iringa Salvatory Ngerea,diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula pamoja na baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mkimbizi A wakiwa kwenye picha ya pamoja

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

WANANCHI wa kata ya Mkombizi Manispaa ya Iringa wamekishukuru chama cha Mapinduzi ccm kupitia umoja wa madiwani wa chama hicho kwa kutatua kero yao ya ubovu wa miundombinu ya barabara iliyodumu kwa muda wa miaka saba.
Ni siku moja tu juni imepita   toka wananchi wa kata ya Mkimbizi Manispaa iliyopo chini ya upinzani wa chama cha demokrasia na Maendeleo chadema kutoa kero yao ya ubovu wa miundombinu ya barabara katika mkutano wa hadhara wa madiwani wa ccm wa Manispaa ya Iringa,uliofanyika juni 23 katika kata hiyo kuwaomba watengenezewe miundombinu barabara hiyo ambayo imenakwamisha shughuli za kiuchumi kutoka na ubovu wake.
Akizungumza wakati wa ukarabati wa barabara hizo Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Joseph Lyata ambae ni Diwani wa kata ya Kwakilosa ccm alisema kuwa lengo lao ni kutaka kuhakikisha barabara zote korofi zinakarabatiwa kupitia umoja wao kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
“Madiwani wa chama cha Mapinduzi ccm katika Manispaa ya Iringa tumeamua kwa umoja wetu katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kuangalia kero zilizopo katika kata zote 18 bila kujali iko ipinzania ua chama tawala’’Alisema
Alisema kuwa  lengo  lao ni kuhakikisha kero ndogondogo za wananchi katika kata  za madiwani wa ccm ndani ya Manispaa zinatanawatumikia wananchi wananchi wanatatuliwa kero zao.
Mpaka sasa jumla ya kata  5 tumeshakarabati miundombunu ya barabara ambazo ni kata ya Mwangata,Kihesa,Mtwivila, ,Kwakilosa ,Ipogolo na leo tupo kata ya Mkimbizi,tunataka maeneo ambayo ni korofi yanafanyiwa matengenezo;
Huu mpango ni endelefu,tutaendelea katika kata zote tukiwa na lengo kubwa la kuhakikisha kata ambazo zina changamoto ya miundombinu na kero zingine zinatuliwa kwa wakati katika kelekea uchaguzi wa serikali za mitaa’’Alisema
Diwani wa kata ya Mwangata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Nguvu Chengula alisema kuwa  umoja wa madiwani wa ccm wameamua kupita kila kata ya diwani anaetokana na chama hicho kuangalia kero na changamoto ambazo hazijatatuliwa wanashirikiana kwa pamoja na kutatua.
Chengula alisema kuwa umoja wa madiwani wa ccm kwa  kushirikiana na wadau wa maendeleo ndani ya manispaa ya Iringa tutahakikisha tunawafikia wananchi kila kata na kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi ili uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika nchini mwaka huu ccm iweze kushinda kwa kishindo.
‘’Mikakati tuliyojiwekea sisi kama Madiwani tunaotokana na chama cha mapinduzi ccm  ni kuhakikisha mapaka kufikia August 30 barabara zote korofi zilizopo katika kata na mitaa ya manispaa ya Iringa zinakarabatiwa ili wananchi waweze kufanya shughuli zao bila kikwazo’’Alisema
Nae mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwapongeza madiwani hao kwa kuisaidia serikali katika kutatua kero za wananchi kwa vitendo,huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wa madiwani hao ili kero zinazowakabili ziweze kutatuliwa.
''Tumemuomba mh.Rais atusaidie fedha kwa ajili ya kuweka rama katika barabara za manispaa ya Iringa zenye urefu wa kilomita 21,tunaamini mh.Rais atatusaidia,hivyo ninawaomba wadau wa maendeleo kujitoa waunge mkono juhudi hizi zinazofanywa na madiwani katika kuleta maendeleo ya manispaa ya Iringa''Alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mkimbizi A,Agata Kasisi alisema  kuwa barabara hizo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa wananchi hasa wafanyabiashara,bodaboda pamoja na wanafunzi ambao wamekuwa wakishindwa kwenda shule kutokana na miundombinu kutokana rafiki.
‘’Tunae diwani wa chadema aliyechaguliwa na wananchi,lakini ameshindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili katika kata yetu ikiwemo changamoto ya miundombinu.Tunawashukuru madiwani wa ccm pamoja na chama cha mapinduzi klwa ujumla kwa kututatulia kero hii na tunahidi kosa ambalo tulilifanya katika uchaguzi mkuu 2025 hatutalirudia  katika serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020’’Alisema

MRADI WA MAJI LAMADI WAFIKIA HATUA ZA MWISHO

Washirika wa maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji Serikalini. Katikati waliokaa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo; kulia kwake ni Ofisa Mradi kutoka AFD, Katell Rivolet na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga na kushoto kwake ni Mkuu wa Msafara wa AFD, Claire Fargeaudou na Mratibu mradi kutoka EIB, Raoul Pedrazzani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo akisisitiza jambo wakati wa majadiliano ya utekelezaji wa miradi ya maji ya LV WATSAN. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga na Naibu Mkurugenzi, Idara ya Usambazaji Maji wa Wizara ya Maji, Mhandisi William Christian.
Ujumbe wa washirika wa maendeleo ulitembelea maeneo mbalimbali ya mradi. Pichani ni sehemu ya eneo la Tiba ya Maji.
Washiriki wa mkutano wakikagua miundombinu ya tiba ya maji kwenye mradi wa Maji wa Lamadi. Wa kwanza ni Mratibu mradi wa LV WATSAN kutoka EIB, Raoul Pedrazzani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga akizungumza jambo wakati wa mkutano. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo. Kushoto kwake ni Naibu Mkurugenzi, Idara ya Usambazaji Maji wa Wizara ya Maji, Mhandisi William Christian.
Muonekano wa baadhi ya maeneo ya mradi wa maji wa Lamadi ambao ulitembelewa na ujumbe wa washirika wa maendeleo.
Ujumbe wa washirika wa maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji kutoka Serikali kwenye eneo la chanzo cha maji cha maji mradi wa Lamadi.


Serikali imesema imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa maji wa Lamadi uliopo Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 93.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo alisema hayo hivi karibuni wakati wa ziara yake kwenye mradi huo.
Katika ziara hiyo Mhandisi Kalobelo alifuatana na washirika wa maendeleo wanaowezesha utekelezaji wa miradi ya maji kupitia Programu ya Uboreshaji wa Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ijulikanayo kama LV WATSAN ambao ni Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).
Mhandisi Kalobelo alisema amefarijika kushuhudia hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mradi na aliongeza kuwa hadi kufikia Agosti mwaka huu utakuwa umekamilika kwani shughuli iliyopo kwa sasa ni ya ufungaji wa pampu na baada ya hapo maji yataanza kutoka.
Kwa upande wake Mratibu mradi kutoka EIB, Raoul Pedrazzani alisema miradi inayotekelezwa chini ya Programu ya LV WATSAN imeonyesha mafanikio makubwa na aliipongeza Mamlaka ya Maji Mwanza (MWAUWASA) ambayo inajukumu la kusimamia miradi hiyo kwa niaba ya Wizara ya Maji kwa usimamizi mahiri wa utekelezaji wake.
Pedrazzani alisema EIB ina nia ya dhati ya kupanua ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika siku zijazo kwani imeridhishwa na namna ambavyo Serikali inatekeleza miradi maeneo mbalimbali kote nchini.
Naye Afisa Miradi kutoka AFD, Clement Kivegalo akizungumza kwa niaba ya ujumbe alioambatana nao, alisema wameridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi na kwamba AFD itaongeza udhamini kadri itakavyohitajika kufanya hivyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera ambaye alikuwa mwenyeji wa ugeni huo wilayani hapo, alisema mradi unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye wilaya na hususan katika mji wa Lamadi na alitoa wito kwa wawekezaji kujitokeza kwani maji ya yhakika yamepatikana na kwamba miundombinu mingine ipo vizuri ikiwemo barabara na umeme wa uhakika.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga akiuelezea mradi alisema unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia mia moja kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka EIB na AFD kwa gharama ya Shilingi Bilioni 12.83.
Mhandisi Sanga alisema mradi utazalisha lita Milioni 3.3 za maji kwa siku ambayo ni mara mbili ya mahitaji ya sasa ya wananchi wa Lamadi na maeneo jirani hasa ikizingatiwa kwamba mradi umebuniwa kuhudumia wananchi zaidi ya 60,000.
Aliongeza kuwa hatua ya kwanza ya maunganisho kwa wananchi; mradi utaunganisha kaya zipatazo 5000 na aliwataka wananchi kuchangamkia mradi ili kujiletea maendeleo.
Kabla ya ziara hiyo, washirika hao wa maendeleo walifanya mkutano Jijini Mwanza na watendaji kutoka Serikalini kwa ajili ya majadiliano na tathmni ya hatua za zilizofikiwa kwenye ujenzi wa miradi ya maji inayotekelezwa chini ya Program ya LV WATSAN.