Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Veronica Nataniel Macamo Dihova.
Mkutano huo uliofanyika leo Ijumaa Juni 28,2019 Ikulu jijini Dar es Salaam, Tanzania na kuhudhuriwa pia Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Damas Ndumbaro na Katibu wa Jukwaa la wabunge la SADC, Boemo Sekgoma.
Dihova ambaye pia ni Spika wa Bunge la Msumbiji amewasilisha salamu za Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi pamoja na salamu za maspika wa SADC.
Pia Dihova ameeleza kwa kina kuhusu ushiriki wa jukwaa hilo katika mkutano wa 39 wa SADC unaotarajiwa kufanyika Tanzania Agosti mwaka 2019.
Mwenyekiti huyo ameeleza Msumbiji na nchi nyingine za Afrika zinatambua mchango uliotolewa na Tanzania katika ukombozi wa mataifa mengi ya Afrika na uanzishaji wa nchi za mstari wa mbele na SADC.
Kwa upande wake, Rais Magufuli amemhakikishia Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zote wanachama wa SADC ikiwemo Msumbiji ambayo ina uhusiano wa kihistoria na kidugu na Tanzania. #CHANZO MWANANCHI
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.